SoC01 Kwanini nchi nyingine zinafanikiwa zaidi na zipo AFRICA?

Stories of Change - 2021 Competition

benny gilbert

Senior Member
Jul 4, 2018
110
65
Natumahi uko mzima wa afya.

Leo mitaongea kwa ufupi kuhusu TEKNOLOJIA...

Swali hili nimekuwa nikijiuliza sana kutokana na kusoma sana vitabu vya biashara na uchumi pamoja na teknolojia, nimefanya utafiti wa kina sana kwa nchi za africa especial EAST AFRICA & WEST AFRICA nimekuja kuona utofauti mkubwa sana kati na binti na anti ingawa wote wana matiti...

Niamua kujikita zaidi kwenye njia ya miamala ya mitandaoni nimeona Tanzania bado sana kwenye hii sector ukilinganisha na nchi zingine mfano, KENYA, UGANDA NA NIGERIA . Tanzania kwenye vyozo vingi vya biashara za mtandaoni hazipo, mfano kuna kampuni ambayo inaitwa CHIPPER CASH, hii kampuni ina dili na kutuma na kupokea pesa africa lakini Tanzania huduma hawatoi kwa ufupi huwezi kupokea pesa kutoka Kenya, Nigeria, Uganda na South Africa.


Kutuma pesa kutumia CHIPPER CASH ni bure kwa AFRICA...

UGANDA, NIGERIA , SOUTHAFRICA wanakula mterezo kutumiana pesa bure haijarishi upo mtandao gani ni BUREEE YAANI.


Paypal hatuwezi kupokea pesa, ila KENYA , UGANDA, NIGERIA, SOUTH AFRICA wanaweza. Kwann Tanzania?



SAFARICOM MPESA KENYA, unaweza kutuma na kupokea pesa kutoka PAYPAL NA SKRILL. Ukijisajiri kutoka Tanzania , hiyo options hupati. Sijajua kwanini Tanzania...



Ukienda kwenye cryptocurrency , Tanzania ndio tumesahaulika kabisa; nilijaribu kumtag CEO wa binance kuomba aweke TZS kwenye P2P BINANCE toka mwezi wa 3 , mwezi wa 7 nimeona kaweka lakini hakuna njia za malipo kama nchi zingine. Ukichagua KENYA SHILLING kwenye P2P BINANCE unaona kuna SAFARICOM MPESA, MPESA BILL, BANK TANSFER. Kwa Tanzania hiyo options hakuna...



++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++



Labda ningeomba nishauri serikali kupitia BOT, maana nchi nyingi nimesoma shida zinaanzia kwenye CENTRAL BANK. BOT ijaribu kuangalia sera zao kimataifa kama zinaweza kubadilishika ili kufungua mlango kwa financial institute kuweza ku integrate na mifumo ya Tanzania, mfano mzuri UGANDA; rais wao aliruhusu kampuni ya kichina ya cryptocurrencies kufunguliwa kwenye nchi yake, kampani hiyo inaitwa BINANCE. UGANDA imeweza ku integrate na mifumo mingi ya kimatifa na kutengeneza ajira kwa vijana kujiajiri wenyewe bila kutegemea serikali yao,

Kazi ya teknolojia ni kusaidia ufanisi na kupunguza GHARAMA ya maisha...

Omba langu ni kwa waziri husika wa teknolojia aweze kuliangalia ili swala kwa jicho la tofauti kupitia timu yake uku wakishirikiana na BOT.


Kuna teknolojia niliona NIGERIA & UGANDA niliipenda sana inaweza leta faida kwa nchi yetu, teknolojia hiyo ni NAMNA YA KUBADILISHA SALIO KUWA PESA TASLIMU(AIRTIME TO CASH).

Hii huduma inapatikana kwenye mtandao wa simu unaitwa MTN kwa UGANDA, NIGERIA NA SOUTH AFRICA.

Kwenye hizo nchi watu wanatumia salio la kawaida kama malipo na baadae wanatuma bank au kwenye akaunti zao kwenye simu mfano mpesa, tigopesa , halopesa na airtel money au bank transfer.

Unaweza kuuza bidhaa kwenye hizo nchi na kuchagua njia ya malipo ya "MOBILE TOP UP", nakutumiwa kwenye simu yako kama salio la kawaida.

Swali unatumia salio la 1M kupiga simu na kuchat?

Nadhani makampuni ya simu mje na hii huduma ili kutengeneza biashara nyingi kupitia njia hiyo kama njia ya malipo ya mtandaoni. Kwa kufanya hivyo mtafungua mlango mwingine wa ajira kwa vijana kwa waunganisha kwenye soko la dunia...


"BILA TEKNOLOJIA WATANZANIA WATAENDELEA KUILAUM SERIKALI, PIA BILA TEKNOLOJIA SERIKALI ITAENDELEA KUKOSA MAPATO".


Shukrani kwa wote mliosoma hadi mwisho.

Pamoja Tunaweza Kujenga Nchi Yetu!

 
Mfano na msaada bora kwa maendeleo ya taifa letu. Sasa tatizo ni kuwa ushauri wako hautafanyiwa kazi mkuu.
 
Inaniuma sana,
Kenya kuna option ya kutoa ela kutoka skrill kwenda Mpesa ila tz haipo yaani nashangaa hatujiongezi.
Tupo old schooled sana.
 
Back
Top Bottom