Legacy ya Malecela, Tanzania inaikaribia kwa mbali ya Mwalimu tu, na pia kitendo chake cha kuachia ngazi kwa hiari na kumuachia Msekwa, aliyemchagua mwenyewe, ni dalili tosha kuwa the man is a matured politician, na hata kitendo cha CCM kuweza kubalidilishana uongozi bila matatizo, nacho pia ni kikubwa sana, maana unaweza kuzama kwenye chuki za binafsi na Malecela, ukashindwa kuona mengi mazuri yaliyojiri, na kwa kuongeza tu ni kwamba, kwenye legacy yake,
1. Malecela ndiye aliyeitengenezea njia nchi yetu kwenye UN New York, OAU Adis, na EAC Nairobi/Arusha, leo wa-Tanznaia hatuna matatizo kabisa ya ku-deal na hivi vyombo muhimu duniani kutokan na mchango wake mzito huko, ambako zkiwa muwakilishi wetu aliweka sifa kubwa sana inyodumu mpaka leo, na kuwafungulia njia Salim, Mama Tibaijuka, Mama Mongella, Mama Migiro, ambao nao wameng'ara sana huko na Tanzania tunaendelea kunga'ara sana huko, kutokana na kazi nzito iliyofanywa na Malecela akiwa muwakilishi wetu huko na mwenye umri mdogo sana wa 20-30s.
2. Malecela, ndiye waziri wetu wa kwanza wa nje, kwa hiyo yeye ndiye aliyeitengenezea wizara hiyo mikakakti yake yote, ambayo sasa hivi ni moja ya wizara zinaheshimika sana duniani, kutokana na ufanisi wake kikazi, na kuweka standard za hali ya juu kwa wasomi wanaochukuliwa na wizara hiyo chini, leo wa-Tanznaia tunasifkiak kila kona ya dunia kwa diplomasia.
3. Malecela, was never a yes man, kitu kilicchomfanya kutoelewana na Mwalimu, hasa kipindi chake cha mambo ya nje, na ndipo walipoanza kufarakana, na tofauti zao zikawa in open alipokuwa waziri mkuu, ambapo Mwalimu alitaka nafasi hiyo apewe Mkapa, na hatimaye akpelekea kumshinikiza Mwinyi, kumuweka Msuya, na baadaye kumzuia asiwemo kwenye majina ya wagombea urais, na kumpitisha Mkapa ambaye alikuwa akimtayarisha kwa muda mrefu kama second choice after Salim,
Kwenye hii ishu Malecela, alifanya kosa kubwa moja nalo ni kumu-understimate Mwalimu, ambaye alikuwa ame-lay down akimsubiri tu, huku Mkapa na the likes kina Apiyo, wakienda back and forth Butiama kuwachongea Malecela na Mwinyi, almost kila siku. Malecela, alikosea one sheria ya siasa kuwa adui wako hawezi kuwa rafiki yako hata siku moja!
4. Malecela, kama kawaida aliposhika uamkamu kwa mara ya kwanza hicho cheo kikaanza kuwa a high profile position, maana Kawawa amekishika hicho cheo pia lakini hakuna anayekumbuka, yeye ni Mtanzania wa kwanza kukishika for 15 years mfululizo bila ya kupumzika, na baada ya uchaguzi wa mwisho wa rais alikuwa ameamua kupumzika nacho lakini akaombwa kuendelea mpaka uchaguzi huu na pia in the process kumtafuta mtu wa kum-replace, unless hujui siasa za bongo there is no way Kikwete angemchagua Msekwa kushika nafasi hiyo, leo cheo hicho kimekuwa a big deal ni kutokana na kushikwa na a true politician kwa muda mrefu, na sio siri kwamba ataendelea kukishika kwa pembeni, Msekwa anajua nini kuhusu siasa za CCM ya sasa? Maana hiii sio CCM ya 70s under Mwalimu, hii ni CCM ya wajanja na wenye mapesa, kama alivyosema Masatu, Msekwa mpenda raha ataweza kulala ndani ya madarasa ya shule za msingi vijijini wakati wa kampeni za uchaguzi?
Kwa kumaliza tu, ni kwamba Malecela anasimama kwenye standard ya peke yake, na anaiachia CCM njia nzito ya kufuata ili kuwa kongozi makini, na hasa uvumilivu na imani ya anything unachokiamini, Mkapa haishi kila wakati kumuomba ushauri what to do tuhuma anazoshutumiwa, Sumaye na Salim, wangeweza kuleta vioja vikubwa sana baada ya uchaguzi uliopita wa rais kama sio huyu mzee, Mtandao sasa ndio kabisa wamekwama kutokana na MMalecela kukataa kabisa kuwaruhusu kujiiingiza kwenye CCM, sasa hatimaye Mzee ameamua kupumzika, ndio hasa maana ya kuwa mwana siasa mzuri, Tanzania leo tunasumbuliwa na viongozi wezi na wafisadi, huwezi kumsikia humo kwenye wizi hata siku moja kama bin-adam amejitahidi kufanya mazuri aliyoweza na kuna mabaya machahce pia aliyofanya, lakini hakuna hata wakati mmoja hayo mabaya yake yalituletea matatizo ki-taifa, isipokuwa kuna waliokuwa na chuki naye ambao siku zote wako ready kumlaumu tu wakati wanajua kuwa hajawahi kuwa na madaraka ya kutoa uamuzi wa mwisho kwa taifa, maamuzi ambayo siku zote hutolewa na rais.
Anyways, nafikiri nimesema ya kutosha na tutaendelea kuelimishana, binafsi ninasubiri siku nitakapoweza kuandika vitabu at least vitano vya viongozi wetu waliowahi kushika nafasi za juu, ambazo right zake ninazo, lakini ninasubiri the right time waliyoiweka wao wenyewe walionipa hizo rights,
Kwa wale mliko London, New York, na DC, huyu mzee anaondoka mwishoni mwa wiki ijayo atakuwepo miji hiyo for at least miezi miwili, kwa hiyo inaweza kuwa nafasi muafaka ya kuweza kusema naye na kuchota siasa, na hata kumuuuliza maswali ambayo wengi hapa wanaoenkana kutokuwa na uhakika nayo.
Ahsante Wakuuu!