Kwanini Mzee Malecela alijulikana ghafla kama “Jumanne”?

Sasa umeeleza tu kuwa alivyolazimishwa kujitoa bila kueleza sababu ni nini.

Kosa kubwa kabisa la Malecela lilikuwa kushindwa kuitetea serikali bungeni hadi kukaibuka suala la OIC ; na suala la G55 ( Hoja ya Tanganyika na serikali tatu )wabunge walishamshinda hija PM malecela na ilibidi NEC Ya CCM iitwe haraka na mwalimu akaihutubia ndio wakafanikiwa kuuwa ile hija ya kina Njelu Kasaka
Suala hilo lilimkera sana nyerere ambaye aliona udhaifuu wa PM na kushindwa kumshauri Rais na kuchukulia upole wa Rais ali hassan mwinyi kwa faida yake ; kushindwa kumshauri rais ni kosa la kiapo hivyo alittakiwa kufukuzwa
Hilo ndio kosa lililofanya jina la Malecela kuingia kwenye Black Book kuwa asijekuwa Rais hata siku moja
 
OIC alitaka kutuingiza mkenge huyu jamaaa kama sio ukali wa mwalimu sote hapa tungekuwa na vibalagashia
Acha chuki dhidi ya waislamu.
Hizi ni baadhi ya nchi wanachama wa OIC:-
Benin, Burkina Faso, Cameroon, Cote d’Ivoire, Gabon, Guinea, Guinea-Bissau, Guyana, Mozambique, Nigeria, Senegal, Sierra Leone, Suriname , Togo na Uganda.
Je Nchi hizi zote wanavaa balaghashia?
Akili hamna hata macho basi hamuoni?
 
Katika historia tunaelezwa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. John Malecela aliitwa na mwalimu akamwambia anafaa kuwa Rais hivyo ajiandae. Inasemekana baada ya kuambiwa hivyo na mwalimu kwanza John alimweleza mkewe na alipofanya ziara nchini Iran alimweleza Mfalme kuwa anatarajia kuwa Rais wa Tanzania na hapohapo akapewa jina la Jumanne.

Kama mnavojua Iran ni nchi ya kiislam. Inasemekana baada ya kufika Tanzania kutoka ziara mwalimu alimfukuza akaenda kujificha kijijini kwao kongwa. Je, kuna ukweli wowote kuhusu hili?

Naamini hapa JF kuna watu wazima waliokuwepo kipindi hicho tunaomba mtueleze ukweli wa jambo hili. Je ni kweli?

Nawasilisha.
Zilikuwa propaganda za washindani,😄,iran hainaga mfalme..
 
Hujaelewa

Malecela alikuwa waziri wa kawaida wakati wa Nyerere ..
Nyerere alipanga kumpa uwaziri mkuu
Ndo inadaiwa akafanya Sherehe nyumbani kwake kabla ya kuteuliwa
Nyerere aka cancel uteuzi..

Hivyo hakufukuzwa cheo chochote
Ila alipewa uteuzi mwingine


Wakati Mwinyi anakuwa Rais ..
Wapambe wakamshauri Ampe Malecela uwaziri mkuu
Main reason watu walitaka wapate watu
Ambao sio vibaraka wa Nyerere

Nyerere bado alionekana anaingilia urais wa Mwinyi.. kwahiyo Kumteua Malecela kum replace Warioba ilikuwa ideal kuwa anaondoka kibaraka wa Nyerere (Warioba)
Anakuja mtu aliepishana na Nyerere huko zamani...

Jina la Jumanne alizushiwa wakati anataka kuwa Rais..alizushiwa na wapinzani wake kuwa kabadili dini ili Mwinyi ampendelee Urais na apate pesa za nchi za kiisalam zimsaidie kampeni..

Ukweli hakubadili dini..maadui zake walimpakazia..Ila alikuwa so powerful
Mpaka Nyerere akamlazimisha ajitoe kugombea urais ndo Mkapa akapita
Pia suala la kina Njeru kasaka lilichangia,,lile la kutaka serikali tatu,hili ndilo hasa lilimharibia malechela
 
Mkuu.....
Ebu soma kitabu kinaitwa "viongozi wetu na hatma ya Tanzania" kiliandikwa na hayati Baba wa Taifa, I'm sure majibu yote utayapata.
http://mallaba.org/UploadFile/20101011232236179.pdf
Niliacha zamani zana kusoma vitabu vya huyu Musa. Maana vinanichanganya tu, na wala havinifungulii njia ya maendeleo. Sana sana vinanirudisha nyuma tu. Kila anayevisoma vitabu vyake na kutekeleza yaliyomo ndani atalaumiwa na watanzania zaidi ya 75% na walimwengu 95%. Na mbaya zaidi ni kushuka kwa uchumi wa TZ na shilingi kila kukicha.

Nyie endeleeni kuvisoma vitabu vyake! Kama bado hamjachanganyikiwa!
 
Hatutaki kuwa mwanachama wa OIC
Acha chuki dhidi ya waislamu.
Hizi ni baadhi ya nchi wanachama wa OIC:-
Benin, Burkina Faso, Cameroon, Cote d’Ivoire, Gabon, Guinea, Guinea-Bissau, Guyana, Mozambique, Nigeria, Senegal, Sierra Leone, Suriname , Togo na Uganda.
Je Nchi hizi zote wanavaa balaghashia?
Akili hamna hata macho basi hamuoni?
 
Katika historia tunaelezwa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. John Malecela aliitwa na mwalimu akamwambia anafaa kuwa Rais hivyo ajiandae. Inasemekana baada ya kuambiwa hivyo na mwalimu kwanza John alimweleza mkewe na alipofanya ziara nchini Iran alimweleza Mfalme kuwa anatarajia kuwa Rais wa Tanzania na hapohapo akapewa jina la Jumanne.

Kama mnavojua Iran ni nchi ya kiislam. Inasemekana baada ya kufika Tanzania kutoka ziara mwalimu alimfukuza akaenda kujificha kijijini kwao kongwa. Je, kuna ukweli wowote kuhusu hili?

Naamini hapa JF kuna watu wazima waliokuwepo kipindi hicho tunaomba mtueleze ukweli wa jambo hili. Je ni kweli?

Nawasilisha.
Kwanza wewe ni fukunyuku kwani haya unayotaka kufukunyua yanakuhusu nini.Umri wako ukilinganisha na wa Mzee Malecela siyo wa kuanza kumletea mambo ya zamani ambayo hayana faida sio kwako tu hata kwa taifa kwa ujumla na utakuwa HUNA ADABU.Lakini jambo la pili wewe ni muongo na m-mbeya ambaye unafaa kuvalishwa DERA kwani kipindi kile Iran hapakuwa na mfalme. Mfalme alipinduliwa mwaka 1978 katika mapinduzi ya Kiislam yaliyomtoa Shah wa Iran,Mohamed Reza Pahlavi na kuanzishwa Jamhuri ya kiislam.Kwa hiyo achana na uzushi kwani hata hiyo ya kuitwa Jumanne haina ushahidi wowote bali ni maneno ya mtaani.
 
Kwanza Malecela kwao sio Kongwa acha uongo. Kwao ni Mvumi

Pili ni kweli "inasemekana" alisilimishwa na kuwa muislam ili apewe hela za kampeni na Jina alilopewa ni hill Jumanne

Tatu, katika uchaguzi wa 1995 hakuna aliyekua na nguvu kumshinda Malecele(Chigweyemisi) kwao ndo wanamuita hivyo kimeanguka mchana sijui kwanini

Nne, bila msuli wa mwalimu hata ule mpambano wa Mkapa na Kikwete usingetokea Malecela angeshinda mapema sana

Tano, Hakua na haiba wala uwezo wa kuwa Rais kwa mtazamo wangu. Na Nyerere alifanya vizuri sana kumblock
Ungemtaja first lady mtarajiwa Tatu Ntimizi
 
Back
Top Bottom