Kwanini Mwanasheria Mkuu anauza sheria ambazo Bunge limetunga?

Kitchener

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
13,833
Reaction score
27,749
Jana tukijiandaa kuingia mahakamani, tulibishana hoja kadhaa na mawakili wenzangu, kuna Revised Edition 2023 ambayo Rais Samia alizindua hapa juzi na tukaambiwa inauzwa milioni 4, sheria hizo zilizohuishwa tunaambiwa zitaanza kutumika July 2025.

AG Feleshi aliyepita alipohuisha R.E 2022 aliziweka zote kwenye website ya AG ili mawakili wadownload bure kwa sababu ni sheria zilizotungwa na bunge.

Hivi huyu AG wa sasa anapouza sheria hizo kwa milioni 4 na hataki kuweka kwenye mtandao kama PDF kama zilivyo zingine zote tunazozipata tanzlii na kwa AG, anafikiri mawakili wachanga ambao hawana hata uwezo kununua vitabu kwa milioni moja watafanyaje?

Au anataka revised edition hiyo itumiwe na wachache wenye uwezo tu? na je, sheria zikitungwa si zinakuwa wazi na kwa raia wa kawaida kabisa?

Yeye anawanyima raia wa kawaida kupata hiyo revised edition? mwenye majibu atuambie.
 
basi waweke kwenye mtandao zile PDF madogo wadownload, ila wanaotaka kununua hizi hardcopy ambao wengi naamini ni lawfirm kubwa pamoja na ofisi za umma, watanunua. raia wachache sana watanunua kwa bei hiyo, na kuweka bei hio wanawanyima raia haki ya kuaccess.
 
Ni bei fair, lakini kwa kweli mawakili wengi hawawezi mudu, ni vyema pdf iwepo pia.
 
Nunueni moja toeni copy nyingi...

Cc: Mahondaw
kwa nini tufanye hivyo wakati wao hawakuuziwa na bunge? kwani bunge lilipotunga liliwauzia? wanachotakiwa kufanya ni kuuza ila kwa upande mwingine, zile softcopy waweke mtandaoni watu wapate haki ya kuzipata, wawe wanasheria na wasio wanasheria, sheria zinapotungwa zinatugwa kwa ajili ya raia wote hadi wasio wanasheria, kuweka vizingiti vya kuzipata ni kuwanyima haki. Bunge lilitunga, likawapatia bila kuwauzia, wao wanatafuta kupata faida tena kwa pesa ya serikali, production ya vitabu hivyo ilitumia kodi zetu na wanatuuzia sisi wenyewe tena.
 
Ni bei fair, lakini kwa kweli mawakili wengi hawawezi mudu, ni vyema pdf iwepo pia.
ile 2022 R.E walisambaza mtandaoni bure, na ni lazima wafanye hivyo kwa sababu walipokuwa wanahuisha walikaa vikao wakilipwa posho za kodi zetu, wakaenda kuprint kwa kodi zetu, na wanataka kutuuzia sisi wenyewe. pamoja na kukubali ukweli kwamba production ya hardcopy imetumia pesa, lakini kwanini ufanyie biashara kodi yetu wakati hukutunga wewe hizo sheria? si wizi huo? au kuna pato anakula na mkuki na nyota kutoa hizo copy? hizo sheria kwenye hardcopy siku zote hata kama zipo wenye uwezo kununua huwa ni mashirika, ofisi za umma kama mahakama, DPP na lawfirms kubwa. raia na wanasheria wachanga wanazihitaji na hawatakiwi kunyimwa kwa kigezo cha pesa. kwa hiyo wakienda mahakamani watakuwa wanarefer wapi sasa? kwenye sheria ambazo hawajasambaziwa? kwani Bunge likitunga sheria si huwa linasambaza bure kwa raia wake? na kama hardcopy unachangia tu na wakati huo huo soft copy hawakunyimi.
 
Nakupata mkuu. Mimi mwenyewe nipo kwenye tasnia na bei hiyo siimudu.
 
sasa kwa fununu tu ni kwamba, baadhi ya sheria kuna replacement ya vifungu, hizo ulizozizoea sasaivi sivyo zitakavyokuwa, vifungu vimebadilika kwenye hiyo RE 2023. how can you make a reference in court unapofanya argument wakati wamekuficha? atakayekuwa anazo ni Mahakama, Mawakili wa serikali na wanasheria wakubwa kwa sababu walikuwa na uwezo kununua.
 
TLS chini ya Mwambukusi wasimame nalo hili.
 
Back
Top Bottom