Kwanini mwalimu hafanyiwi "certification" kama mhasibu (Certified Public Accountant) ilhali walimu ni wengi na elimu bora ndio msingi wa taifa imara?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
12,178
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Kwanini mwalimu hafanyiwi "certification" kama mhasibu (Certified Public Accountant) ilhali walimu ni wengi na elimu bora ndio msingi wa taifa imara??

Kwanini kuna "Certified Public Accountants (CPAs)" ila hakuna "Certified Public Teachers (CPTs)? Kwanini Maofisa Elimu hawathibitishwi kwa maana wao ndio uti wa mgongo wa taifa lolote imara?

Niliwahi kumuuliza binamu yangu mmoja hivi yeye ni accountant kwanini wakimaliza bachelor degree wanalazimika kufanya tena CPA papers ili watambulike na bodi yao ya uhasibu (National Board of Accountants and Auditors "NBAA") akasema ya kwamba baadhi ya vyuo huwa havifundishi vizuri wahasibu masuala ya kutosha pia baadhi ya wahasibu huwa wanafaulu kwa kupitia rushwa za ngono pamoja na rushwa za namna nyingine hivyo ni lazima kuwe na namna ya kuwadhibiti wahasibu vilaza.

Sasa nikajiuliza kama changamoto ni hizo katika vyuo that's means all students (let's say at the UDSM) go through the same circumstances, kwanini tusifanye "certification' kwa walimu/education officers ambao wao ndio wengi zaidi na ndio msingi wa taifa imara?

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
IMG_20191104_160143_172.jpg

 

BISECKO

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
539
1,000
Kuanzisha board na kufanya certification ni mambo mawili tofauti. Engineers wanayo board ila hawafanyiwi certification
Nafikiri Kuna vitu huelewi kuhusu 'professional certification'.

Kimsingi kila taaluma ina utaratibu wake wa kufanya certification, ifahamike kwamba, certification ni pale mwana taaluma anapokuwa approved to practice.

Mfano, wanasheria ili uweze kufanya practice ya kitaaluma ktk nyanja fulani ni lazma baada ya kumaliza shahada ukasome Post Graduate Diploma in Legal Practice, alimaarufu kama Law school huo ndo utaratibu wa certification yao.

Lakini taaluma nyingine, wao hutoa leseni, ukiwa licenced to practice ni kama uko certified...

Taratibu hutofautiana sasa usikariri ukafikiri wahasibu tu ndo wanakuwa certified ati kwakuwa they are exppresely termed 'Certified Public Accountant' na kwakuwa huwezi sikia 'Certified Public Architect' ukadhani kwamba hawa wakandarasi hawawi certified no.

Taratibu zinatofautiana na kuna uhusiano mkubwa kati ya uwepo wa chombo cha kitaaluma kama bodi na mchakato wa certification.

Certification ni jambo la kitaaluma kama hakuna chombo mahususi cha kitaaluma hiyo certification itafanyikaje ??

Kila taaluma iwe na utaratibu wake wa kufanya certification kwa kuzingatia vigezo vya kisayansi vya taaluma husika.
 

Giltami

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
750
1,000
Kwanza lekebisha sema your MOTTO and not our,cjui uzalendo upi? Nchi yangu naipenda ila kama utaona uovu na kunyamaza huo ni unafiki sio uzalendo maana kuna wazalendo mambo leo wachumia tumbo.Bahati nzuri au mbaya nimepitia coz zote mbili ualimu na Accountancy,Nchi yetu imepitia kipindi kigumu sana katika kuinua elimu nchini ikafikia hatua wakaajiliwa walimu wa upe watu walifaulu hadi maks 230 lakini hawakupata secondary hivyo bas huwezi kuweka mtihani huo ukijua wazi unahitaji wafanya kazi 50 na ulionao ni 15 mtihani wa nini,Polepole tutafika huko utakuwepo mtihani huo ila hakuna vyuo vinavyozalisha watu wenye nidhamu na maadili kama vyuo vya ualimu,tatizo ni kila mtu ana tabia zake.
 

double R

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,324
2,000
Hata taaluma zilizo na cerfication hazina weledi wala ubora wa huduma wazitoazo hauzingatiwi.

Nchi hii hakuna weledi kabisa.
 

hugo jr

JF-Expert Member
Jun 3, 2018
287
500
Nchi hii walimu wako nyuma sana, elimu yenyewe wanayopewa si nzuri sana, mfano voda fasta (crash program) ile ni kukurupuka sana, ukija mishahara ndo kabisaa. So poor ndo maana watoto wengi vilaza basi tu, mnasema elimu bure lkn serikali iboreshe elimu ya walim kwanza na stahiki zao then ndo mkianza kuwapitisha kwenye hiyo bord yenu watakua teachers atleast
Mm nilisoma crash program, ki ukweli tuliburuzwa tu ili nasi tukaburuze watoto na ndo kilichotokea, huwez fanya kaz kama hujafundishwa ethics za kazi,
Kuhusu bord ya walimu ni muhim sana lakin pasipo boreshwa stahiki za walimu na taaluma yao huko vyuon hiyo bodi itakua kazi bure
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom