Hardbody
JF-Expert Member
- Jan 25, 2017
- 3,551
- 3,803
Hujaeleweka
Nafikiri Kuna vitu huelewi kuhusu 'professional certification'.
Kimsingi kila taaluma ina utaratibu wake wa kufanya certification, ifahamike kwamba, certification ni pale mwana taaluma anapokuwa approved to practice.
Mfano, wanasheria ili uweze kufanya practice ya kitaaluma ktk nyanja fulani ni lazma baada ya kumaliza shahada ukasome Post Graduate Diploma in Legal Practice, alimaarufu kama Law school huo ndo utaratibu wa certification yao.
Lakini taaluma nyingine, wao hutoa leseni, ukiwa licenced to practice ni kama uko certified...
Taratibu hutofautiana sasa usikariri ukafikiri wahasibu tu ndo wanakuwa certified ati kwakuwa they are exppresely termed 'Certified Public Accountant' na kwakuwa huwezi sikia 'Certified Public Architect' ukadhani kwamba hawa wakandarasi hawawi certified no.
Taratibu zinatofautiana na kuna uhusiano mkubwa kati ya uwepo wa chombo cha kitaaluma kama bodi na mchakato wa certification.
Certification ni jambo la kitaaluma kama hakuna chombo mahususi cha kitaaluma hiyo certification itafanyikaje ??
Kila taaluma iwe na utaratibu wake wa kufanya certification kwa kuzingatia vigezo vya kisayansi vya taaluma husika.