Matusi na kejeli kwa walimu si suluhisho, tutafute njia bora za kukuza elimu Tanzania

Mugabonihela

JF-Expert Member
Dec 12, 2022
299
1,731
Habari za muda wapendwa,

Mara nyingi tumekua tukishuhudia matusi na kejeli kwa walimu hususani kwenye elimu zao na uwezo wa kiuchumi.kwenye miaka ya hivi karibuni yaan kuanzia 2012 na kuendelea kumekua kukizuka mijadala mingi mitaani na majukwaa mbalimbali wakidai uwezo wa walimu unachangia pia kushuka kwa elimu nchini.

Kutafuta tiba ya hili, hebu tujikumbushe kwa ufupi historia ya tasnia hii ya ualimu nchini.

Wakati Tanganyika inapata Uhuru mwaka 1961 na taarifa za sensa ya 1967 inakadiliwa watanzania walikua 12,313,469. Na asilimia 80% walikua wakiishi vijijini, kwa idadi hiyo tajwa hapo juu 70% ya wananchi walikua hawajui kusoma wala kuandika.

Hivyo basi kipaumbele cha kwanza kwa serikali ilikua ni kuongeza idadi ya wananchi wanaojua kusoma na kuandika.

Hivyo mwanzoni mwa miaka ya 1970's serikali ya Tanzania ilianzisha program maalumu (UPE) universal primary education lengo likiwa ni kupunguza illiteracy rate kwa kuongeza idadi ya walimu mashule.

Kupitia program ya UPE serikali ilichagua baadhi ya wahitimu wa darasa LA saba na kupewa mafunzo ya ualimu wakafundishe shule za msingi.
Hakukua na namna nyingine ya kupata walimu isipokua kuchagua best students waliomaliza shule za msingi ili wasaidie na wenzao kwa maana nchi haikua na wasomi kabisa.

Kwa tuliosoma miaka ya 1980's, 1990's na mwanzoni mwa miaka ya 2000's tunawajua walimu wa UPE. Baadae walimu hawa walistaafisha kwa kushindwa kuendana na mfumo wa elimu uliopo hivi sasa lakin jamii na serikali kwa ujumla zilitambua mchango wao.

THE CRASH PROGRAM OF 2001-2006
(PEDP 2001-2006) primary education development program.

Sasa hii ni program nyingine iliyofuata baada ya ile ya UPE, tofauti ya hii na ile ya UPE hii ya sasa ilichagua wanafunzi waliohitimu shule za secondary kujiunga na vyuo vya ualimu nchini ili kuendana na kasi ya uandikishwaji wa wanafunzi mashuleni. Na hapa ndipo matusi yalipoanzia.

Mwaka 2005 tumeshuhudia kuanzishwa kwa shule za kata nchini ambazo zimekua msaada mkubwa kwenye sekta ya elimu nchini.wengi wa wasomi wanao graduate vyuo vikuu miaka kuanzia 2015 walipata fursa kwenye shule hizi.

Sasa basi kwa wahitimu wa kidato cha nne wenye divisions kuanzia III na IV (ya 26 mwisho) kama walaka unavyosema walichaguliwa moja kwa moja kujiunga na vyuo vya ualimu grade A.
Sambamba na ngazi nyingine yaan wale wa advance mwenyewe walienda diploma pia kwa ajili ya shule za secondary.

Program hii ilianzishwa kuhakikisha Yale mashule yaliyoanzishwa yapate walimu hivyo serikali ilitoa fursa ya ajira kwa wale wasomi wachache waliopo mashuleni kwa wakati huo.

Kwa kua sekta ya elimu ilionekana pia kua ni biashara tukashuhudia kuanzishwa kwa vyuo vyingi vya ualimu nchini vikimilikiwa na sekta binafsi. Na serikali kwa kua demand ya walimu ilikua kubwa ilichukua walimu kwenye kila chuo kilichosajiliwa.

(PEDP) program hii ilitoa fursa kwa watoto wa maskini na wale ambao walishindwa kujiunga na taaluma nyingine kwani vyuo hivi vya walimu ada ilikua sawa na ile ya sekondari na ata treatment yao ilikua kama sekondari.

Apa liljengwa tabaka moja baya sana nchini, yaan unakuta mtu na div III 25 au IV 26 kwa kua mzazi ana pesa anamlipia aende TIA au CBE akasome certificate ya HR, PROCUREMENT au ACCOUNTANT na baadae anajiendeleza mpaka diploma. Alafu mtu huyu anakaa kwenye majukwaa ana mtukana mwenzie aliekwenda ualimu (utani tu)

MATUSI YALIPOANZIA

hii crash program haikua kwa walimu tu hata ma nurse walipelekwa kwa program hii. Matusi yalianza pale ambapo kila mtu alikua boss kwa mwalimu, yaani mtendaji wa kijiji na mtendaji kata hawa ni maboss wa mwalimu kwa kua shule ipo chini ya kata.

Hivyo hivyo na ngazi nyingine ikafikia nyakati DC ana amuru mwalimu apigwe kiboko.

UNYONGE WA WALIMU
walimu wengi ni watoto wa maskini kama tulivyoona walikimbilia crash program either kwa kukosa ada ya taaluma nyingine au kukimbilia ajira mapema wasaidie familia zao.

Wengi wao ni waoga wa kupoteza ajira wakifikira mzigo mkubwa wa familia zao maskini.

Leo hii wakati we upo mjini,unatoa matusi Kuna watu wapo vijijini shule ina walimu 3 wanatamani mwalimu atokee wakati wowote.

Wakati unamtukana huyu mwalimu kumbuka NYERERE ni mwalimu
MAGUFULI ni mwalimu (alinifundisha chemistry sengerema sekondari)
MAJALIWA.

Uzi utaendela........!
 
Professionalism ndiyo silaha pekoe ya kuwakomboa walimu.
Ni kweli lakin pia Sera ya kuruhusu vyuo binafsi kuzalisha walimu imepelekea kuwepo kwa walimu wasio na sifa. Pamoja na supply ya walimu kuzidi demand ya serikali na shule binafsi
 
Enzi za Kikwete tumepitisha kizazi cha ajabu sana kwenye ualimu na upolisi, yani failures wenye division four za kuelekea kwenye zero ndo walipelekwa ualimu.

Ndiomana ualimu na upolisi ndiyo sehemu zilizojaza MATUTUSA mno kuliko sekta nyingine hapa nchini, na ndio hao wamekuwa mtaji mkubwa sana wa CCM katika kutimiza ajenda zao nyingi chafu.
 
Ujinga na uzwazwa ni kipaji cha Watanzania walio wengi. Walimu ni sehemu tu ya jamii iliyojaa raia wajinga.
 
Ni taifa la watu wajinga tu linaloweza kukejeli na kudharau walimu. Kwenye maitaifa ya watu wenye akili walimu wanaheshimika sana.
Huko kwenye mataifa ambayo waalimu wanaheshikimika, utaratibu wa kuwapata waalimu sio wa kipumbavu kama huu wa Tz.

Division 4 ualimu & upolisi ni kuheshimu kwa kipi mkuu?
 
Huko kwenye mataifa ambayo waalimu wanaheshikimika, utaratibu wa kuwapata waalimu sio wa kipumbavu kama huu wa Tz.

Division 4 ualimu & upolisi ni kuheshimu kwa kipi mkuu?
Hakuna mtu anayetafuta heshima kutoka kwako. Wewe heshimu wazazi wako tu. Au tafuta watu waliopata Division one uwaheshimu.
 
Hakuna mtu anayetafuta heshima kutoka kwako. Wewe heshimu wazazi wako tu. Au tafuta watu waliopata Division one uwaheshimu.

Sasa mnajitetea nini? We uliona wapi heshima inaombwa?

Mfumo wa kuwapata waalimu kwa hapa Tz ni mbovu.
 
Sasa mnajitetea nini? We uliona wapi heshima inaombwa?

Mfumo wa kuwapata waalimu kwa hapa Tz ni mbovu.
Hebu nielezee kwa kifupi current directives and guideline of teachers preparation. Halafu fanya a short critical analysis tuone.
 
Kwa mawazo yangu, miaka ya nyuma walimu walidahiliwa kwa vigezo hafifu na vichache sababu ya uhitaji kwenye jamiii hivyo hakukua na namna.ile kwa tulipofikia serikali iangalie utaratibu mwingine pamoja na kuwaongezea salaries hawa jamaa.

Nadhani malipo duni yameathiriwa na namna ambavyo walikua wakidahiliwa vyuoni mwao.
 
Paragraph yako ya mwisho sijaelewa unamaanisha nini. Hebu soma tena alichoandika.
 
Ni kweli lakin pia Sera ya kuruhusu vyuo binafsi kuzalisha walimu imepelekea kuwepo kwa walimu wasio na sifa. Pamoja na supply ya walimu kuzidi demand ya serikali na shule binafsi
Iyo ni point ndogo sana.

PROFESSIONALISM NI MKUKI WA MOTO MKUU.

UNAMPELEKA KIJIJINI MWL. MWENYE UELEWA MPANA WA HAKI ZAKE KAMWE HUWEZI MSHINDA.
 
Kwa mawazo yangu, miaka ya nyuma walimu walidahiliwa kwa vigezo hafifu na vichache sababu ya uhitaji kwenye jamiii hivyo hakukua na namna.ile kwa tulipofikia serikali iangalie utaratibu mwingine pamoja na kuwaongezea salaries hawa jamaa.

Nadhani malipo duni yameathiriwa na namna ambavyo walikua wakidahiliwa vyuoni mwao.
Kwani mpwayungu village
Anasemaje

Ova
 
Back
Top Bottom