Kwanini mwalimu hafanyiwi "certification" kama mhasibu (Certified Public Accountant) ilhali walimu ni wengi na elimu bora ndio msingi wa taifa imara?

Mkuu Kuwa Mzalendo ipende Nchi yako,
Nami Nakuongezea swali Mkuu,
Kwanini wahasibu,Wagavi ili wawe Certified wanafanya Mitihani,kwanini wahandisi hawafanyi mitihani kuwe registered? Au wao kuna Special flani?
 
Marekani sehemu nyingi huwezi kuwa mwalimu kama huna certification, juu ya shahada kwenye fani yako.
Mkuu Kwani Kuwa certified ni Lazima Ufanye Mitihani au usome Kozi husika?
Fani kama Ugavi,Wahasibu wanafanya Mitihani,BT mbona Engineers hawafanyi Mitihani Kuwa Certified?
Wanaregistered tuu,baada ya miaka kadhaa ya Kazi kwenye fani hiyo anakuwa professional registered!
Provided tuu kasomea Engineering!
Any comments on that's or reference with developed countries?
 
Mkuu Kuwa Mzalendo ipende Nchi yako,
Nami Nakuongezea swali Mkuu,
Kwanini wahasibu,Wagavi ili wawe Certified wanafanya Mitihani,kwanini wahandisi hawafanyi mitihani kuwe registered? Au wao kuna Special flani?
Mimi sifahamu mkuu. Inaonekana CPA imelenga zaidi kutengeneza daraja la high-class pamoja na low class
 
Mwalimu analipwa 20 au 30 kusimamia mtihani hii si kukaribisha rushwa.Mfano anapewa hela na mmiliki wa shule 2milion arahisishe wanafunzi kucheat si anakubali?
Nchi hii walimu wako nyuma sana, elimu yenyewe wanayopewa si nzuri sana, mfano voda fasta (crash program) ile ni kukurupuka sana, ukija mishahara ndo kabisaa. So poor ndo maana watoto wengi vilaza basi tu, mnasema elimu bure lkn serikali iboreshe elimu ya walim kwanza na stahiki zao then ndo mkianza kuwapitisha kwenye hiyo bord yenu watakua teachers atleast
Mm nilisoma crash program, ki ukweli tuliburuzwa tu ili nasi tukaburuze watoto na ndo kilichotokea, huwez fanya kaz kama hujafundishwa ethics za kazi,
Kuhusu bord ya walimu ni muhim sana lakin pasipo boreshwa stahiki za walimu na taaluma yao huko vyuon hiyo bodi itakua kazi bure
Screenshot_20191107-163344.jpeg
 
Yatosha kusema ualimu sio consulting bureau ..hata huko kudhani unajitambua na kutaka walimu wawe certified ni kwasababu ulipitia mikononi mwa mwalimu huyo huyo! Tukishaanza kuhoji usajili wa walimu kama ilivyo kwa wahasibu na taaluma nyingine za ushauri na ukaguzi basi na elimu pia iwe huria ili mwenye kuhitaji elimu awe na hela ya kutosha auziwe elimu kisha agongewe mhuri maisha ya mwalimu yawe juu kama ya wahasibu,wahandisi,wasanifu majengo na maofisa ugavi na wengine ambao taaluma zao ni za ushauri!
 
Safi sana mkuu Infantry Soldier kwa swali makini sana. By the way huo ndio udhaifu mkuu wa cadre ya Ualimu nchi I. Ni profession ambayo haina professional board
Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Kwanini mwalimu hafanyiwi "certification" kama mhasibu (Certified Public Accountant) ilhali walimu ni wengi na elimu bora ndio msingi wa taifa imara??

Kwanini kuna "Certified Public Accountants (CPAs)" ila hakuna "Certified Public Teachers (CPTs)? Kwanini Maofisa Elimu hawathibitishwi kwa maana wao ndio uti wa mgongo wa taifa lolote imara?

Niliwahi kumuuliza binamu yangu mmoja hivi yeye ni accountant kwanini wakimaliza bachelor degree wanalazimika kufanya tena CPA papers ili watambulike na bodi yao ya uhasibu (National Board of Accountants and Auditors "NBAA") akasema ya kwamba baadhi ya vyuo huwa havifundishi vizuri wahasibu masuala ya kutosha pia baadhi ya wahasibu huwa wanafaulu kwa kupitia rushwa za ngono pamoja na rushwa za namna nyingine hivyo ni lazima kuwe na namna ya kuwadhibiti wahasibu vilaza.

Sasa nikajiuliza kama changamoto ni hizo katika vyuo that's means all students (let's say at the UDSM) go through the same circumstances, kwanini tusifanye "certification' kwa walimu/education officers ambao wao ndio wengi zaidi na ndio msingi wa taifa imara?

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
View attachment 1253892
 
Back
Top Bottom