Kwanini Mwabukusi(Mtanganyika) aigimbee Ubunge kutukomboa wananchi

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Kuliko kuwa na wabunge ambao wameonesha uwezo mdogo wa kupangua na kuchangia Hoja , Nina Kila sababu Mimi kama mtanzania Kuona haja ya kuwaondosha baadhi ya wabunge katika mjumba ule wa heshima na kusajili wabunge wapya wenye kaliba ya wakili mwakabusi na wengine wengi, kwani watatusaidia katika ukombozi wa nchi.
Kumekuwa na mvutano mkubwa juu ya muungano wa Zanzibar na Tanganyika huku Ismail Jusa bado akitaka kurejesha uhuru wa Zanzibar mikononi mwa Zanzibar na Wakili Mwakabusi akitaka pia kuikomboa Tanganyika kutoka katika Muungano huu ambao uliasisiwa na chama Cha mapinduzi na upo hai mpaka Sasa kwakuwa nguvu inatumika Ili Uwe hai.
Hivyo basi Tunamuombea wakili mwakabusi aje Kugombea Jimbo lolote ambalo Mbunge wake ni dhaifu, au hata ikiwezekana akagombee mbararali ambapo Jimbo lipo wazi kutokana na kufariki Kwa mgombea
 
Alishagombea huko Mbeya wakamuibia ule uchafuzi wa 2020, akataka kukata rufaa akakutana na kiasi cha pesa alichotakiwa kulipa, zaidi ya milioni 10 kama gharama ya kufungua kesi, kikamshinda, kwasababu wakati huo pia alikuwa anatakiwa kufanyiwa operation hospital, hivyo akaona bora aendelee na matibabu aachane na mambo ya kesi ya uchaguzi.

Naamini, 2025 anastahili kugombea tena, yule kichwa kinachotakiwa kwenda bungeni kwa lazima.
 
Kuliko kuwa na wabunge ambao wameonesha uwezo mdogo wa kupangua na kuchangia Hoja , Nina Kila sababu Mimi kama mtanzania Kuona haja ya kuwaondosha baadhi ya wabunge katika mjumba ule wa heshima na kusajili wabunge wapya wenye kaliba ya wakili mwakabusi na wengine wengi, kwani watatusaidia katika ukombozi wa nchi.
Kumekuwa na mvutano mkubwa juu ya muungano wa Zanzibar na Tanganyika huku Ismail Jusa bado akitaka kurejesha uhuru wa Zanzibar mikononi mwa Zanzibar na Wakili Mwakabusi akitaka pia kuikomboa Tanganyika kutoka katika Muungano huu ambao uliasisiwa na chama Cha mapinduzi na upo hai mpaka Sasa kwakuwa nguvu inatumika Ili Uwe hai.
Hivyo basi Tunamuombea wakili mwakabusi aje Kugombea Jimbo lolote ambalo Mbunge wake ni dhaifu, au hata ikiwezekana akagombee mbararali ambapo Jimbo lipo wazi kutokana na kufariki Kwa mgombea
Ni wazo zuri but agombee kupitia upinzani! Akipitia chama tawala hatokosoa tena hata ile IQ unayoiona itatoweka!!
 
Back
Top Bottom