Kwanini Mungu yupo?

Kwanini Mungu yupo?

Kuheshimiwa Kuna faida nyingi sana...Tena sio Kwa mwanangu TU, natamani niheshimiwe na kila mtu. Kuheshimiwa Kuna faida nyingi ila faida kuu, ni kuwa ukiheshimiwa huwezi kufanyiwa mambo mabaya kama
Kutukanwa,Kuibiwa,Kupigwa,kudharauliwa,Kutengwa,nk. Nk.
Kumbuka sisi binadamu ni social primates ..yani tunaishi Kwa kutegemeana sana.

Turudi Kwa Mungu, yeye anatutegemea sisi? Jibu ni nadhani utasema ni Hapana.
Na kama ukisema ndiyo, Bado swali litabaki kuwa "Je sisi binadamu na Mungu tunaotegemeana, tupo Ulimwenguni Kwa Nini?"

Sasa sidhani utajibu hiyo ndio.

Tuendelee...Kama hapana Mungu hatutegemei...Sasa sisi ametuumba wa Nini??

Mimi binadamu sitegemei Simu ili niishi, lakini nimeunda simu inayowaka,inayotumia chaji,inayotachi(kama binadamu anavyokula na kusali) ili niitumie Kwa faida zangu binafsi kama Kuwasiliana,Kutunza kumbukumbu nk.
Kama simu Haina hizo faida siwezi kuinunua/kuiunda.

Sasa Mungu aliyetuumba sisi wanadamu na hatutegemei, Je ni kwanini alituumba? Tuna faida Gani kwake?

Na most importantly, Je hiyo faida tunayompatia Ina uhusiano wowote na Sababu ya yeye mwenyewe kuwepo???
Kudharauliwa ni kinyume Cha kuheshimiwa...kutoheshimiwa si lazima utukanwe,bado hujaonesha faida ya kuheshimiwa na mwanao...na asipokuheshimu unapata hasara gani?..tuoneshe
 
Sasa mbona umesema Mungu yupo ili kumsimamia mwanadamu?

Nadhani ulikosea, Je kwanini sasa Unadhani Mungu yupo? Yeye ana Purpose Gani kuwepo?
Hapana sijakosea, mungu yupo ili kuwasimamia wanadamu ni mtazamo wa wanadamu juu ya uwepo wa mungu.

Nje ya mtazamo wa mwanadamu mungu yupo bila sababu maalum ni kama reality itself.

Nikikuuliza wewe kwanini upo hai utajibu nini?
 
.....Qur'an inasema tumeumbwa ili tuabudu.....

Basi imeishia hapo?
Maana hata hicho kiti kipo kwa ajili ya kukaliwa ila "sometimes" hutumiwa kama nyenzon ya kusimamia kufikia vitu vya juu.

Sometimes kiti hutumika kama kiegemeo mlango ili mlango usijifunge.

Hicho ni kiti kilichoundwa kukaliwa.

Kwahiyo sisi tunatakiwa kuabudu tuu?

#YNWA
 
Concept ya ibada ni Pana kwa muktadha wa uislam...na si swala/Sala tu!?
 
Unauliza kwanini Mungu yupo!!--- badala ya kwanza kujiuliza wewe mwenyewe kwanini upo na ukipata jibu ndipo uulize juu ya Kwanini Mungu yupo.
Tunayapiga yote Kwa mkupuo...Maana nikijua kwanini Mungu yupo ntajua na kwanini Mimi nipo
 
Hapana sijakosea, mungu yupo ili kuwasimamia wanadamu ni mtazamo wa wanadamu juu ya uwepo wa mungu.
Nje ya mtazamo wa mwanadamu mungu yupo bila sababu maalum ni kama reality itself.

Nikikuuliza wewe kwanini upo hai utajibu nini?
Kwahyo Mungu ni mtazamo tu wa Wanadamu
Nje ya Huu mtazamo Mungu Hana sababu?

Inamaana bila sisi, Mungu Hana maana yoyote?
 
Kudharauliwa ni kinyume Cha kuheshimiwa...kutoheshimiwa si lazima utukanwe,bado hujaonesha faida ya kuheshimiwa na mwanao...na asipokuheshimu unapata hasara gani?..tuoneshe
Okay umesema mwenyewe kutoheshimiwa sio lazima nitukanwe ..Inamaana unajua Kuna dalili zingine nyingi tu za kutoheshimiwa (ambazo nimetaja baadhi kama Kupigwa,kutukanwa,Kuibiwa,kusengenywa,kutosikilizwa,nk. Nk. Nk. Zipo nyingi sana.

Hizi zote dalili zote ni mbaya, na hakuna binadamu anayependa kufanyiwa hivyo...kwahyo hzio ni hasara za kutoheshimiwa ...Sasa faida ya kuheshimiwa ni kwamba utaepukana na hizo hasara.
 
Ukisengenywa unapoteza nini!?..bado hujaonesha faida ya kuheshimiwa!!...mwanao akikuheshimu unapata faida gani!?..tuoneshe
 
Tunayapiga yote Kwa mkupuo...Maana nikijua kwanini Mungu yupo ntajua na kwanini Mimi nipo

Wahenga walisema fimbo ya mbali haiui nyoka au hela iliyo mkononi ina thamani kuliko iliyopo kibindoni au hisani yaanzia nyumbani (charity starts at home) au ndege aliyekuwepo mkononi ni bora kule mia waliopo porini (a bird in hand worth hundred in bush).

Anza na wewe mwenyewe kujua kwanini upo duniani ??!!--- baada ya hapo you move a step further to ask other related questions.
 
Ukisengenywa unapoteza nini!?..bado hujaonesha faida ya kuheshimiwa!!...mwanao akikuheshimu unapata faida gani!?..tuoneshe
Pole pole TU ..nmeandika hasara nyingi mpaka Kupigwa Kuibiwa ila umeona ya kuulizia ni kusengenywa.

Sawa ..Sasa kusengenywa ni kubaya Kwa sababu Moja...Watu wakikusengenya wanakudharau, wakikudharau hawakupi nafasi, hawakusikilizi,hawakuamini,hawakusaidii ukiwa na shida,hawakukumbuki,.
Sasa kama wewe kwako hizo sio hasara basi wewe sio binadamu.

Na kama huoni shida ya kuishi na jamii inayokusengenya,inayokutukana,inayokudharau,isiyokuamini, isiyokulinda. (hata ukiumwa/ukifa haijali), isiyokujali, inayokunyanyapaa na kukutenga Basi utakuwa sahihi kusema hamna faida ya kuheshimiwa.

Na kama wewe huoni hasara ya kudharauliwa na mwanao na kufanyiwa yote hayo juu, Ntakushangaa siku nikikukuta unamlazimisha mwanao akuheshimu.
 
Wahenga walisema fimbo ya mbali haiui nyoka au hela iliyo mkononi ina thamani kuliko iliyopo kibindoni au hisani yaanzia nyumbani (charity starts at home) au ndege aliyekuwepo mkononi ni bora kule mia waliopo porini (a bird in hand worth hundred in bush).

Anza na wewe mwenyewe kujua kwanini upo duniani ??!!--- baada ya hapo you move a step further to ask other related questions.
Sawa basi, Ngoja niulize....Kwanini Binadamu tupo duniani?
 
NB: Huu mjadala sio wa kubishana kama mungu yupo au hayupo.
Hapa ninataka kuwauliza Kwa upole wale tunaoamini tayari kuwa Mungu yupo...Je, kwanini yupo?

Yaani siulizi mungu ametokea wapi/ametokanaje...
Hapa naulizia Kuna ulazima Gani wa yeye kuwepo? na kwanini yupo?

Mfano mtu akiuliza kwanini viti vya kukalia vipo, huwezi kujibu kwasababu mbao zikikatwa na kuchongwa vizuri zinatengeneza kiti, hapa utakuwa umejibu viti vinatokanaje....jibu zuri ni kwasababu vinatufanya binadamu tukae na kupumzika, hivyo tumevitengeneza...Inamaana bila kuwepo binadamu wenye shida ya kukaa basi viti visingekuwepo...

Kwahyo napouliza kwanini Mungu yupo? Siulizii chimbuko lake ametokana na Nini, ila naulizia ni sababu Gani iliyompelekea/iliyomlazimu yeye awepo.

Kuna wanaosema Mungu yupo ili auumbe ulimwengu, kwahyo function kubwa ya Mungu ni kuumba na kuendesha ulimwengu.

Hilo jibu kwangu halitoshelezi kwakuwa, Ningeuliza kwanini Huu ulimwengu upo?, Kwani Kuna ulazima ulimwengu uumbwe?

Kama Kuna ulazima wa ulimwengu kuwepo, basi Inamaana ulimwengu una thamani kuliko Mungu, kama binadamu tulivyo na thamani kuliko viti. Maana sisi ndo tumeleta viti, basi Ulimwengu umemleta Mungu.(yaani kama ni lazima ulimwengu uwepo, basi ulimwengu ndio umemlazimu Mungu awepo kama ambavyo Nyumba zinawalazimu mafundi ujenzi kuwepo,Simu zinawalazimu wauza simu kuwepo,Magari yanawalazimu madereva kuwepo, wahalifu wanalazimu polisi kuwepo nk.)

Lakini common sense inakataa.
Ingewezekana TU kusiwe na chochote, Hamna Dunia,hamna,Nyota,Hamna sayari, na Hakuna Mungu.

Sasa kwakuwa hivi vitu vipo, Je ni kwanini vipo?

Na kama ingewezekana kusiwepo kitu,Je ni Nini kililazimisha Mungu awepo?

Na kama mungu alikuwepo kabla ya Ulimwengu, na hakulazimishwa kuumba ulimwengu (angeamua angeacha na kubaki mwenyewe) Je yeye kwanini yupo? Nini kilipekea yeye kuwepo?

Kwanini Mungu yupo?
Mbina jibu ni rahisi tu? Mungu yupo ili tumwabudu... Simple and clear...
 
Ndugu yangu acha kusikiliza habari za walimwengu, Mungu yupo taka usitake anaonana na watu live siku ya umauti. Kwanzia leo habari hizi za kutaka kumkimbia zikome.
 
That is neither simple nor clear, Far from it.

Unaweza kusema Simu zipo ili tuzichaji??
Na kama ni hivyo, Ina maana kitendo cha kuchaji ni Cha muhimu kuliko simu yenyewe, maana unaweza kuchaji hata Kifaa kingine kama Laptop,Gari,Tv nk.

Useme gari lipo ili binadamu tuliwekee mafuta, Inamaana kitendo cha kuweka mafuta ndio Cha muhimu kuliko gari maana tunaweza kutafuta Kifaa kingine kama ndege tukaweka mafuta.

Sasa kama Mungu yupo ili tumuabudu Inamaana ibaada ni ya muhimu kuliko Mungu, Inamaana bila ibaada Mungu asingekuwepo...Na ibaada ni ya muhimu,binadamu tukiamua kuabudu mawe Haina haja ya kuwa na Mungu.

Kwanini Mungu yupo?
 
Ndugu yangu acha kusikiliza habari za walimwengu, Mungu yupo taka usitake anaonana na watu live siku ya umauti. Kwanzia leo habari hizi za kutaka kumkimbia zikome.
Mimi sijasema Mungu hayupo ndugu yangu...Ninaamini yupo...ila Nataka kujua kwanini amekuwepo??

Ni sawa na kuuliza kwanini nguo zipo, jibu ni ili zivaliwe.
Na mtu kuuliza kwanini nguo zipo, haimaanishi anaamini kuwa nguo hazipo.
 
Back
Top Bottom