Mbona hii mimi sikumbuki na wewe ndio unakumbuka ?, Huoni kwamba ni uonevu kunihukumu mimi bila kunipa kumbukumbu ya mimi kukumbuka kukubaliana na huu mkataba
Kwahio ningekataa kukubali na hilo hapo juu nisingeletwa duniani Au? na wale wanaokufa siku ya kwanza wakizaliwa huoni kwamba mtihani wao ni rahisi ?
Mababu zetu walioabudu mizimu na wao walipewa huu mtihani wakasahau au ?
Tusingehoji wala mababu zetu wasingehoji huenda mpaka leo sisi tungekuwa watumwa sababu tu ya ngozi ya babu yangu au sababu ya kuzaliwa na jina fulani...
Huna excuse....Jua kuwa tupo hapa duniani kwa ajili ya mtihani.
Maisha yetu yapo katika mfumo huu!!
Mungu kwa hekima,utashi na mapenzi yale aliamua kutuumba ili atufanyie mtihani! Viumbe vyote vilihudhurishwa mbele yake, akauliza nani yupo tayari kufanyiwa huu mtihani wa kupewa amana!! ?
Jua,milima,wanyama,bahari,malaika,mwezi,mbingu,nyota,miti na ardhi vyote vilikataa kuibeba hiyo amana badala yake mwanadamu alikubali kubeba hiyo amana.
Amana yenyewe ni hii kuwa atafanya aliyoamrishwa na ataacha aliyokatazwa kwa maana ya kuwa mtiifu. Viumbe wengine waliogopa kubeba kutokana na uzito wa suala hili ila mwanadamu ali underestimate uzito wa jambo hili akabeba majukumu. Ila aliambiwa kuwa akifaulu kutekeleza hayo atalipwa malipo makubwa ambayo ni Pepo na akishindwa basi ataadhibiwa kwa moto.
Viumbe vingine vilistaajabu kuona kiumbe dhaifu kama binadamu kukubali kubeba mzigo mzito.
Mwandamu yeye alichagua hiyari hivyo viumbe vingine havina hiyari ya kutenda kama mwanadamu.
Nafsi inapoletwa duniani huwa ineletwa kwa ajili ya mtihani hivyo ili kuwe na fair test kila nafsi huanza ikiwa haina kitu kichwani!! Ila humu duniani Mungu tayari ameshatanguliza kuweka uongofu kupitia vitabu vyake vitukufu,mitume na manabii (wa kweli).
Hivyo ni jukumu lako mwanadamu kuutafuta ukweli kama vile unavyohangaika kila siku kuutafuta mkate wako.
Mtihani huu una muda maalumu kwa kila mtahiniwa kuna ambao wamepewa muda mrefu na wengine mfupi. Mtoto toka anapozaliwa mpk kufikia baleghe huwa hana dhambi! Ila kalamu inaanza kuandika mema na mabaya yake mara baada tu ya kuwa ameshabaleghe kwa maana sasa anaelewa lipi jema na lipi ovu.