Kwanini Mungu hatufunulii tukaujua ukweli kama yupo na njia gani tufuate?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Sina shaka kuwa Kuumbwa au Uwepo wa dunia sio wa Nasibu, Vitu vingi nikiviangalia nauona uwepo wa Mtengenezaji au Muumbaji.

Mfano nawaangalia viumbe kama ndege jinsi Rangi zao zilizonakshiwa vema kwenye manyoya yao naona nguvu na utukufu wa yule aliyepanga viwe na vikawa, sauti zao tofauti za kuvutia ni kiekeleza tosha cha uwezo na utukufu wake:

SWALI: Ukweli ni upi juu ya Muumba?

Kwanini hatuletewi miujiza ya kutufanya tuwe na yakini kama hao waliopita ambao tumewasoma kwenye vitabu?

Kwanini Mungu asituletee Mwongozo mmoja ili tujue njia sahihi ya kufuata badala ya kila mmoja kujitapa na Kujiona yuko sahihi?? Tena huku wengine wakiua watu kwa vigezo vya dini? Ref. Kenya.
 
Hata kama asingeleta kitabu chochote, Uumbaji wake unatosha kushuhudia uwepo wake.
 
Tayari ulishapewa akili.....unaohitaji nini? Miujiza gani wakati Kila kitu na jinsi kilivyoumbwa ni miujiza tosha? Au Kwa kuwa umeshavizoea!
Kuna vitabu viwili bible na nature.
Mungu haitaji tena kukwambia yupo kazi zake zina mthibitisha
 
254


Qur'an 2:255. Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu. 255
 
Sababu hii hapa ishaelezwa!

Luka 16:29-31
[29]Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
.
[30]Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.

[31]Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
.
 
Ugali na mbuzi wa pale kwa meku unakuchanganya mpaka unashindwa kuelewa ? Subiri siku ukose ankara ndipo utajua kama hujui.
 
Mungu yupi unayemuongelea?
Wa waislamu?
Wa wakristo?
Wa wahindu?
Wa wabudha?
Wa baadhi ya tamaduni za kiafrika?

Ni yupi maana Mnaposema Mungu mjuwe kuwa dunia ina Miungu wengi na si mmoja, muogope mtu anaeyesema kuwa Mungu ni mmoja, huyo ni Muongo, maana kila dini ina Mungu wake na kila imani ina Mungu wake.

Mungu wa uislam ni tofaut na Mungu wa ukristo ndiomaana hizi dini zinapingana kwa mengi japo zinashare baadhi ya vitabu kutoka ktk dini ya uyahudi ambayo ndio imekuwa ikikopiwa na hizi dini mbili mpaka kuanzishwa kwake.

Kidogo ukristo unaweza kushahabiana Mungu wake na Mungu wa wayahudi maana wote wanamtaja Huyo aitwaye Yehova/elishadai, lkn pia bado ukristo unafeli kuforce yesu ni Mungu ijapokuwa ktk uyahudi huyo yesu hatambuliki kama ni Mungu wala kama amewai kuwepo, hapa utata unakuja.

Unapotafuta majibu ya maswali yako kuhusu jambo fulan basi hakikisha huyo unayesema Mungu, umjue na umaanishe ni Mungu yupi? Wa dini ipi?,

Ni ngumu hata kujibiwa maombi yako kama utaomba kwa kutomaanisha Mungu fulan, ambaye ndiye chanzo cha majibu yako kutokana na imani yako kwake.

Kuna baadhi ya dini zinaforce tuamini kuwa Mungu wa hiyo dini ndie sahihi, jambo ambalo si kweli, mfano huwezi kusema uislam ni dini sahihi wakati dini yenyewe imeanzishwa juzi tu kwa kukopi stori za imani zingine kutoka kwa myahudi na mroma, je kabla ya kuanzishwa kwa hii dini huyo Mungu aliabudiwa vipi?

Pia huwezi kusema ukristo ni dini sahihi wakati hii dini imenzishwa miaka ya 300A.D kutoka ktk imani ya warumi ambao kabla hawakuwa wakristo bali waumini wa imani ya kiyahudi ambayo haimtambui Yesu lkn baadae waliibadili imani hiyo kwa kuingiza stori za Yesu na ndipo sasa likaibuka vuguvugu la kuifuata imani mpya ya mafundisho yanayomuhusu huyo Yesu na waliofuata hayo mafundisho wakaitwa wanaYesu ama wakristo na hili halikuondoa utofauti na uroma/ukatoric, maana huwezi watenganisha na ukristo kwakuwa ni wao walioibua imani hii ya kumfuata kristo na wao kuitwa wakristo, ama waumini wa uyahudi walioamua kuamini ktk Imani ya Yesu ama imani ya kristo, na baada ya muda ktk migogoro ya hii imani ndipo sasa kukaibuka madhehebu mapya ambayo nayo yalikuwa sehemu ya huu ukristo ama uroma maana nao walitumia kanuni na sheria zile zile za mrumi kuunda madhehebu yao wanayoyatumia kumtukana mroma ama mkatoric kuwa anaabudu sanamu wakati huo wakiyatumia na maandiko ya biblia aliyoyaandika mkatoric ujinga huu.

Uyahudi nao huwezi kusema ni dini sahihi maana stori zake zimebase kuwa na jumla ya miaka 7000 tangu uumbaji mpaka leo hii, kuanzia story za wakina adamu mpka wakina musa n.k, je kabla ya hiyo miaka watu waliabudu nini? Ama tuamini kuwa dunia ina miaka hiyo hiyo isiyozidi 7000 kulingana na visa vya dini?.

Na wakati huo kisayansi na kihistoria kuna jamii ziliishi zaid ya maelfu ya miaka, mfano dini ya uhindu ina historia zaidi ya miaka 10000 kabla ya uwepo wa ukristo wala uislam, pia kuna tamaduni na imani za kiafrika ambazo zilikuwepo kabla hata ya uhindu na maelfu ya miaka.

Je hapo tuamini lipi?
Majibu mnayo kuwa hizi dini ni michezo ya watu tu kuicontrol dunia haswa afrika na Asia walipo vilaza wasiopenda kutumia akili zaidi ya hisia za kipumbavu.

Amkeni wajameni acheni kukalilishwa ujinga, haya mambo mbona ni mepesi sana hata hayahitaji akili kubwa.
 
Kwa kuwa unataka kujichosha soma vitabu vya dini zote,tafuta ushahidi wa kihistoria then utathibitisha Mungu wa Imani ipi ni wa kweli.

Ila kwa ambao tushapitia hizo process tunapokwambia Mungu wa kwenye Bible ndo Mungu wa kweli inabidi uelewe,hakuna haja ya kujichosha wakati utafiti ushafanywa ila kama unaona unadanganywa FANYA UTAFITI YOURSELF.
 
Mwenyezi Mungu alishatoa muongozo nao ni amri kumi alizompatia musa.Vilevile amekupatia akili unafahamu kutofautisha kati ya jema na baya
 
Kwa kuwa unataka kujichosha soma vitabu vya dini zote,tafuta ushahidi wa kihistoria then utathibitisha Mungu wa Imani ipi ni wa kweli.

Ila kwa ambao tushapitia hizo process tunapokwambia Mungu wa kwenye Bible ndo Mungu wa kweli inabidi uelewe,hakuna haja ya kujichosha wakati utafiti ushafanywa ila kama unaona unadanganywa FANYA UTAFITI YOURSELF.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Mambo ya dini bwana. Hongera kwa utafiti na hitimisho mkuu.
 
UKITAKA KUJUA MUNGU YUPO NGOJA YAJE YAKUKUTE MATATIZO MAKUBWA KUBWA HAPO NAKUAMBIA UTAJUA MUNGU YUPO MAANA UTAANZA MTAJA MUNGU BILA HATA MTU KUKUAMBIA.
 
Kuna dini kwa kujifagilia haijambo… waambie sasa walete aya au andiko kuthibitisha hoja yao… hola. Wakiletewa na dini ya mwenzao… wanageuka kisirani. Duh
 
Back
Top Bottom