Ni Hoja ya Kimantiki na kiakili kufikiri kwamba Mungu hafi na wakati huo huo kumkataa mtu uliyemsema hakufa kwamba sio Mungu?

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,664
Wataalamu wa Kufikiri:

Mada ya leo inatokana na fundisho kwamba kuna chanzo cha KILA KITU tunachokiona kwa macho,kusikia,kugusa, kuhisi au viwezavyo kuonjwa.Na kwamba sio tu vitu vinavyotambulishwa kwetu na ile milango mitano ya fahamu bali kwamba chanzo hicho cha kila KITU ni kwa vitu vingine ambavyo havionekani kwa macho ila uwepo wake tunaufahamu.Katika kundi hili ndipo kunapotokeza vitu kama UMEME,Hewa/Oxygen,Nafsi na kadhalika.

Chanzo cha vitu vyote hivyo kwa Wakristu na watu wengine huita chanzo hicho kikuu cha kila kitu (the Ultimate cause, the Uncreated Creator) kwamba ni MUNGU.

Kwa hiyo, unapohitimisha kwamba hakuna kitu au hali yoyote ile ambayo ipo juu ya Chanzo Kikuu ni dhahiri unakiri kwamba hata kifo sio au hakipo juu ya Chanzo cha Kila Kitu(MUNGU). Kwa lugha nyingine kwamba kifo hakina uwezo juu ya MUNGU.Ndio kusema kwamba Mungu hawezi kufa.Tafsiri ya kawaida ya kifo ni ile ya roho kutengana na mwili kama inavyotokea kwa mwanadamu na viumbe vingine vyenye uhai kama vile kenge, mende, Nguruwe, na viumbe vyote vyenye uhai.

MUNGU anao uwezo wote (Omnipotent).Mungu yuko mahali pote(Omnipresent-hafungwi na nafasi.Mungu anafahamu kila kitu (Omniscience)-anafahamu yaliyopita, yaliyopo na yajayo na kwamba yeye hafungwi na muda.

HOJA na IMANI kwamba Mungu ni muweza wa kila kitu na kila jambo, ni pamoja na uwezo wa kuwapo katika NAFSI TATU lakini akisalia Mungu mmoja(au Mungu yule yule bila kugawanyika).Uwezo huo ndio uliomfanya Nafsi yake ya Pili,YESU KRISTU kutwaa au kujiongezea mwili kama wetu sisi wanadamu na kisha akaa kati yetu na kufanya kila jambo tufanyalo wanadamu isipokuwa DHAMBI TU.

ILITOKEAJE MUNGU KUVAA MWILI?

Injili yaYohana 1: 1-18 inatusimulia na kutupatia wazo zima juu ya jinsi Mungu huyo alivyoweza kujivika mwili ili aweze kukaa na watu wake aliowaumba katika moja ya historia ya mwanadamu:

“1 Hapo mwanzo, Neno alikuwako; naye alikuwa na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno alikuwa na Mungu. 3 Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa; hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye. 4 Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu. 5 Na mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza kuushinda. 6 Mungu alimtuma mtu mmoja jina lake Yohane, 7 ambaye alikuja kuwaambia watu juu ya huo mwanga. Alikuja ili kwa ujumbe wake watu wote wapate kuamini. 8 Yeye hakuwa huo mwanga, ila alikuja tu kuwaambia watu juu ya huo mwanga. 9 Huu ndio mwanga halisi, mwanga unaokuja ulimwenguni, na kuwaangazia watu wote.10 Basi, Neno alikuwako ulimwenguni, na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua. 11 Alikuja katika nchi yake mwenyewe, nao walio wake hawakumpokea. 12 Lakini wale waliompokea, wale waliomwamini, aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu, 13 ambao walizaliwa si kwa maumbile ya kibinadamu, wala kwa nguvu za kimwili, wala mapenzi ya mtu, bali kutokana na Mungu mwenyewe. 14 Naye Neno akawa mwanadamu, akakaa kwetu. Nasi tumeuona utukufu wake, utukufu wake yeye aliye Mwana wa pekee wa Baba; amejaa neema na ukweli. 15 Yohane aliwaambia watu habari zake, akasema kwa sauti, “Huyu ndiye niliyemtaja wakati niliposema: ‘Anakuja mtu mmoja baada yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa.’” 16 Kutokana na ukamilifu wake sisi sote tumepokea neema kupita neema. 17 Maana Mungu alitoa sheria kwa njia ya Mose, nayo neema na kweli vimetujia kwa njia ya Yesu Kristo.18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu kamwe. Mwana wa pekee aliye sawa na Mungu ambaye ameungana na Baba, ndiye aliyetujulisha habari za Mungu.



JINSI MUNGU ALIUVYOONYESHA KWAMBA YEYE NI ZAIDI YA KANUNI ZINAZOTAWALA DUNIA NA ULIMWENGU

Katika kuonyesha Mungu ni muweza wa kila jambo na hakuna kinachomshinda aliamua kumtumia Mwanamke Bikra,jina lake Mariamu(Maria).Alimuomba kupitia kwake atwae Mwili wa Kibinadamu kama tusomavyo kutoka Injili ya LUKA 1:26-38:


“26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja bikira aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu, ewe uliyejaliwa neema na Mungu! Bwana yuko nawe!” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: Maneno hayo yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkubwa na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wakehautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. 36 Ujue pia kwamba hata Elisabeti, jamaa yako, naye amepata mimba ingawa ni mzee, na sasa ni mwezi wa sita kwake yeye ambaye watu walimfahamu kuwa tasa. 37 Kwa maana hakuna jambo lisilowezekana kwa Mungu.” 38 Maria akasema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema.” Kisha yule malaika akaenda zake”.

Nukuu hiyo niliyokupatia hapo juu ina mambo ya msingi makuu mawili, tunayoyapata katika aya ya 32: “Yeye atakuwa mkubwa na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu” na zile aya za 34 na 35: “34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu”.

Kama wewe ni Great thinker, utagundua kuwa tunapatiwa picha na Malaika kwamba:

MOSI, hiyo nafsi ya pili ya Mungu kwa sababu ya mwili itakaokuwa nao, itaitwa mwana wa Mungu.Maana yake, mzaliwa huyo (mtoto), ni moja ya nafsi tatu za Mungu,yaani (Mungu mmoja) na kwamba hatakuwa na Baba wa kibinadamu kama walivyo binadamu wengine.

PILI, uwezo wa Mungu kuzaliwa na mwanadamu itakuwa ni kwa muujiza.Muujiza kwa maana kwamba,njia ambayo ingalitumika kufanikisha au kuwezesha kile alichokuwa anakiongelea Malaika, ingalikuwa haitokani na uweza au nguvu za kimaumbile au nguvu za kiasili zinazofahamika na wanadamu.Kwa lugha nyingine, ni kwamba,ni jambo ambalo kwa uweza wa kibinadamu lingalionekana haliwezekani, lakini kwa Roho Mtakatifu lingalitokea hivyo bila matatizo na ndio maana Mama Bikra Maria anapotumia mantiki ya kibinadamu kutilia shaka suala hilo kutokea,Malaika anamuelewesha kuwa kutukia kwake ni nje ya mazoea ya kibinadamu(beyond natural LAWS).

Na kama ambavyo, ilivyofanyika wakati wa kuumbwa wanadamu na vitu vingine vyote ulimwenguni,Roho Mtakatifu(ile nafsi ya tatu ya Mungu iliyotulia juu ya vilindi vya maji) ndio ambayo ingalifanya kazi hiyo.

TATU,kwamba uweza wa Mungu hauna mipaka na lolote alitakalo anaweza kulifanya muda wowote kupita hata mantiki zetu.

Kwa hiyo, Mwinjili Luka anatuambia kwamba, Malaika Gabrieli alikuwa amemjulisha Bikra Maria kwamba mtoto ambaye angalimzaa angalikuwa na asili (nature) mbili: Umungu na ubinadamu.Ndiyo,kusema kwamba mtoto huyo, ambaye pia Bikra Maria alielekezwa kabisa na jina la kumuita (“31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu”), angalikuwa ni binadamu kamili na Mungu kweli.

YALIYOSEMWA NA MALAIKA GABRIEL YALITUMIA

Maneno yote na sifa za Kimungu ambazo ziliwekwa mbele ya Mama Bikra Maria, zote zilithibitika kwa wanadamu kwa njia ya milango ya fahamu kama ifuatavyo:


1. UMUNGU kwa Ujumla wake
Sifa mojawapo ya Mungu ni kutoa uzima wa Milele.Maisha yasiyo na mwisho.Maisha ambayo hayaamuliwi tena na Muda.Jambo hili Yesu baada ya kuzaliwa analisema waziwazi,kama Mwinjili Yohana 10:25-30 anavyotuhabarisha:

“25 Yesu akawajibu, “Nimewaambieni, lakini hamsadiki. Kazi ninazozifanya mimi kwa jina la Baba yangu zinanishuhudia.26 Lakini nyinyi hamsadiki kwa sababu nyinyi si kondoo wangu. 27 Kondoo wangu huisikia sauti yangu; mimi nawajua, nao hunifuata.28 Mimi nawapa uhai wa milele; nao hawatapotea milele, wala hakuna mtu atakayeweza kuwatoa mkononi mwangu. 29 Baba yangu ambaye ndiye aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote, wala hakuna awezaye kuwatoa mikononi mwake Baba.30 Mimi na Baba, tu mmoja.”

Uwezo wa Mungu kugawa UZIMA WA MILELE unaonekana tena kama tusomavyo katika Injili ya Yohana 10:28 na 17:1-2:

“28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.”

“1Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; 2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.” (Matayo 17:1-2).



2. Mungu na Ufahamu wa mambo Yaliyopita
Mungu ni uweza ujuayo yote yaliyopita.Ni uweza usioshindwa au hautawaliwi na muda.Uweza huu ulionyeshwa na Yesu kama tusomavyo kutoka Injili ya Yohana 8:56 hivi:

“56 Abrahamu, baba yenu, alishangilia aione siku yangu; naye aliiona, akafurahi.” 57 Basi, Wayahudi wakamwambia, “Wewe hujatimiza miaka hamsini bado, nawe umemwona Abrahamu?” 58 Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, kabla Abrahamu hajazaliwa, mimi niko.” 59 Hapo wakaokota mawe ili wamtupie, lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.”

3. MUNGU na Ufahamu wa mambo Yaliyopo Ulimwenguni.

Ukiwa unao uwezo wa kufahamu jambo ambalo linaendelea wakati fulani bila kuwepo sehemu ambako tukio linaendelea au kuambiwa, ina maana upo sehemu hiyo wakati jambo husika linapokuwa linatukia.Na kama ikiwa unafahamu jambo fulani kwamba linatukia mahali ihali haupo sehemu hiyo, ina maana kwamba unao uwezo wa kuwapo sehemu mbili tofauti kwa wakati mmoja(bilocation).Uwezo huu aliuonyesha Yesu Kristu wakati wa maisha yake hapa duniani kama tusomavyo kutoka Injili ya Mwinjili Yohana katika sura 1:47-48, kwamba Yesu alimfahamu Nathael bila kutambulishwa kwake na au kuambiwa na mtu yeyote mtu yoyote yule:

“47Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.48 Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesuakajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona.


Na MATAYO 16: 7-14 anatudokeza juu ya YESU alivyofahamu kifo cha rafikiye Lazaro kabla hata hajapewa taarifa za kifo na pia kwamba alifahamu kwamba Lazaro angalikufa baada ya kuugua kama tusomavyo:


"7Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena.8 Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena? 9 Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake.11 Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha.12 Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona.13 Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi.14 Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa.15 Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini; lakini na twendeni kwake.”


4. Mungu na UWEZO WA KUFAHAMU Mambo YAJAYO

Mungu lazima afahamu mambo yote yajayo. Umungu huo , ulithibitika katika Yesu kumfahamu Yuda kama mtu ambaye angalimsaliti kama tunavyosoma kutoka Injili ya Yohana 13:10-11:

“10Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote. 11 Kwa maana alimjua yeye atakayemsaliti; ndiyo maana alisema, Si nyote mlio safi.”

Kwa hapa nimalizie na uthibitisho mmoja kati ya matukio mengi ya Kimungu ya kufahamu mambo yajayo. Yesu kwa umungu wake, aliweza kusoma mawazo na mioyo ya watu,jambo ambalona mimi na wewe, hatuna uwezo nalo isipokuwa Mungu pekee.Tukio hilo ni lile la wayahudi kumjaribu kuhusu iwapo ni halali kulipa kodi au la,kama Matayo anavyotuhabarisha juu ya kisa hicho katika sura 22:17-18:

“17 Basi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, ama sivyo?18 Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema, Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki?”



5. MUNGU HUABUDIWA, HUTUKUZWA NA KUHESHIMIWA

Yesu kwa umungu wake, aliabudiwa: Iko mifano mingi sana ambako Yesu kwa umungu wake, aliabudiwa kama tunavyojulishwa na mwinjli Matayo 2:2,11:33 na 28:9.Ni Mungu peke yake anaabudiwa,kusifiwa,kutukuzwa na kusujudiwa.Hakuna kiumbe kiumbe kingine, nje ya Mungu mwenyezi, ambaye anapewa sifa kama hizo.Na sababu ziko wazi tu, kwamba tunamshukuru Mungu kwa kuamua kutuumba bila kushauriana nasi.Hakuna aliyemuomba Mungu azaliwe muda fulani,azaliwe na baba na mama fulani na au azaliwe katika sehemu fulani hapa duniani.Kumbe,watu waliokaa karibu na Yesu wakiisha kufahamu kwamba ni Mungu na kwa kufahamu makuu aliowatendea walimuabudu.Tunasoma habari za Yesu kuabudiwa kutoka injili ya Matayo: “Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.”

“Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.”( Matayo,28: 9)

SASA, MWANADAMU ANASEMAJE YESU SIO MUNGU NA KWA MAMLAKA YAPI?

Katika historia ya mwanadamu,kulitokea mwanadamu mmoja miaka 500 baada ya Yesu Kristu kuwa ameondoka hapa duniani kwa kifo na baada ya kufufuka,kudai kwamba Yesu kama Mungu hasingaliweza kufa.Katika Kurani (“maneno ya Mungu yuleyule ambaye sifa zake nimekwisha kuzibainisha kwa kina hapo juu") kwamba Yesu, Mwanaye Mungu na Mungu hakufa msalabani na kama ingalitokea hivyo basi huyo sio Mungu.Tunasoma hivyo kutoka Kurani An-Nisa(Sura 4) 156-157:

“156 Na pia kwa kufuru zao na kumsingizia kwao Maryamu uwongo mkubwa, 157. Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini. 158. Bali Mwenyezi Mungu alim- tukuza kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.”

Kwa Great thinker,Muhammad, mwandishi wa Kurani, (idhini ya Allah) anasema mambo yafuatayo:

1. Kwanza, Bikra Maria alisingiziwa kwamba yeye amemzaa Mungu.

2. Pili kwamba kama wakristo wanakomaa kwamba Yesu alikuwa Mungu na kwamba alikufa kweli basi huyo hakuwa Mungu.

3. Tatu,kwamba Yesu ambaye anafahamika na waislamu hakufa msalabani bali Allah(Mungu) alimtorosha kwa njia za “panya” (miujiza) na kumpeleka Mbinguni.

4.Kwamba kama Yesu hakufa mslabani na yuko Mbinguni basi yuko HAI hadi leo.


MASWALI YA KIMANTIKI NA KIAKILI

Kwa mantiki na akili za Mungu wa Muhammad tunajikuta tunang’amua mantiki nyingine ambazo naomba ziongoze mjadala wetu:

1. Kwamba ikiwa kutokufa ni ishara ya Umungu,ni kwa nini Muhammad na umma wa waislamu hawakubali kwamba Yesu ni Mungu?

2. Ikiwa Yesu hakufa, ishara ya kuonyesha kwamba ni Mungu hata sasa, ni kwa nini Kurani kupitia Muhammad inasema Bikra Maria alisingiziwa kumzaa Mwana wa Mungu na Mungu?

3. Aliyekuwa wa kwanza kuidhihirishia na kuisadikisha dunia kwamba Yesu alikuwa ni Mwana wa Mungu, alikuwa ni Malaika Gabrieli,Je,Muhammad anamaaanisha Malaika GABRIEL ni MUONGO na aliyekuwa amemtuma naye ni Muongo?

4.Je,Mungu anasema anaye Mwana na Mwanae Yesu Kristu anasema anaye Baba.Muhammad wote hao kwake ni waongo,je kwa kauli kama hiyo ya Muhammad, tuseme Muhammad anamfahamu sana Mungu kuliko MUNGU anavyojifahamu?

5.Je,ikiwa Muhammmad anamfahamu Mungu kuliko anavyojifahamu ina maana yeye Muhammad amechukua nafasi ya Mungu(amekuwa ULTIMATE CAUSE)?


BASI,kwa maswali haya na mengine ambayo ninyi ma-great thinker mtaongeza,naombeni sasa tuuanze mjadala.
 
Mungu hayupo.

Hayo mengine ni hadithi tu alinacha.

Eti mungu anajua kila kitu, akashindwa kujua kua shetani atakuja kuasi, maana angejua angesitisha kumuumba na hakuna ambae anemuuliza kwa nini hakumuumba.

Huyo anaeitwa mungu hajui chochote na hana uwezo na chochote, magonjwa yamemshinda, majanga, matatizo, vifo sasa yeye anaweza nini?

Mafundisho yote kuhusu mungu ni hadithi za kutunga.
 
(Nje ya mada) Mkuu uzi wako wa DOGMA mbona siupati?

Ulilalamika wewe na wenzio wakaufuta! Ni jambo la ajabu kuwa watu munataka tushirikiane kuutokomeza Ushoga na Usagaji lakini hamtaki tufanye hivyo kwa kuanzia kwenye vyanzo vya ushoga! Watu wanasema wanaye Mungu wanayemuabudu na aliyemtuma mtume wake Wa mwisho kabisa duniani lakini ni mungu gani huyo anayewatuma watu wake waogope mijadala juu yake na badala yake wawe wa kulialia na kukimbia mijadala?Mungu mwenye uweza wote bila shaka angaliwawezesha waumini wake AKILI na Mantiki za kujibu hoja zinazomhusu.Je,huyo mungu ni yupi hata aombe msaada Wa moderators katika kujinasua?
 
Mungu hayupo

1. Mungu hayupo wapi? Ulitarajia awepo wapi na lini na kwa muda gani?

2. Kusema hayupo maana yake humuoni. Je,kushindwa kwako kumuona ndio ushahidi unaopita mashaka kwamba hayupo?

3. Je,kutokumuona kwako,kumhisi ndio kigezo cha kumkataa kwamba hayupo? Je,Mungu na Umeme au mawimbi ya radio ni kipi kipo?
 
HII MADA ILIKUWA INATAKIWA IJADILIWE NA KKKT RC SDA TAG MOROVIAN NK ILI KUONDOA SINTOFAHAMU YENU KWANZA.
ANYWAY,
ILA SIHUWA MNASEMA ISSA WA QURAN SI YESU WA BIBLE?
OK, KWA UFUPI
1&2.KILA KIUMBE KITAONJA UMAUTI ISSA BIN MARIAM ATARUDI NA KISHA ATAKUFA (KASOME ZAIDI)
3.JE GABRIEL KUTHIBITISHA KUWA YESU NI MUNGU IPI KATKA QURAN AU BIBLE?
4.HAPA INAONESHA TUNAO MIUNGU WAWILI, MUNGU SENIOR NA MUNGU JUNIOR, HII NAYO IPO KWENYE KITABU KIPI?
5.JE MUHAMMAD ANAMFAHAMU MUNGU KWA KULIKO ANAVYO JIFAHAMU YEYE MWENYEWE, JE HILI AMELIONGEA WAPI?
 
Ulilalamika wewe na wenzio wakaufuta! Ni jambo la ajabu kuwa watu munataka tushirikiane kuutokomeza Ushoga na Usagaji lakini hamtaki tufanye hivyo kwa kuanzia kwenye vyanzo vya ushoga! Watu wanasema wanaye Mungu wanayemuabudu na aliyemtuma mtume wake Wa mwisho kabisa duniani lakini ni mungu gani huyo anayewatuma watu wake waogope mijadala juu yake na badala yake wawe wa kulialia na kukimbia mijadala?Mungu mwenye uweza wote bila shaka angaliwawezesha waumini wake AKILI na Mantiki za kujibu hoja zinazomhusu.Je,huyo mungu ni yupi hata aombe msaada Wa moderators katika kujinasua?
USIMSHUHUDIE JIRANI YAKO UONGO
JE UNAHAKIKA MIMI NI MIONGONI MWA WALIOLALAMIKA?
JE ALIYEOMBA UZI UFUTWE NI BINADAMU AU MUNGU? JE ULIIONA COMMENT YANGU YA MWISHO?
KWA HIYO VIPI TUNAWEZA KUKUTANA, ILA TUNAANZA NA BIBLE?
 
Pia kuacha huyo mwanadamu aliyezaliwa miaka 500 baada ya Kristo aliyepinga uungu wa Yesu, ....
pia yupo mwanadamu mwingine aliyezaliwa 1827(Ellen Gould White) na kuanzisha dini yake ya Seventh day Adventist alipinga Utatu Mtakatifu na Uungu wa Yesu...



Naendelea kufyonza

Unamaanisha yule aliyewakataza watu kutooga siku ya sabato na kutokula vyakula vya Protein kama Mayai?
 
&2.KILA KIUMBE KITAONJA UMAUTI ISSA BIN MARIAM ATARUDI NA KISHA ATAKUFA (KASOME ZAIDI)

1. Arudi kisha afe ili iweje?
2. Je,sababu zipi zilimfanya asife wakati ule na badala yake afe wakati huo unaoutaja?

3. Kwa hiyo,unashuhudia ukweli Muhammad alisema ukweli kwamba YESU,MUNGU hakufa Bali alitoroshwa msalabani?

4. Kwa hiyo unakubali kwamba Muhammad alikuwa sahihi kudai kwamba MUNGU ni MUONGO na mfanya Ghikiba?
 
USIMSHUHUDIE JIRANI YAKO UONGO
JE UNAHAKIKA MIMI NI MIONGONI MWA WALIOLALAMIKA?
JE ALIYEOMBA UZI UFUTWE NI BINADAMU AU MUNGU? JE ULIIONA COMMENT YANGU YA MWISHO?
KWA HIYO VIPI TUNAWEZA KUKUTANA, ILA TUNAANZA NA BIBLE?

Ulimwengu Wa Tekinolojia kama hii unahitaji uonane na mtu ndio ujenge hoja zako? Mungu mwenye uweza wote anaweza kushindwa kuwa na uweza Wa kukufanya ukawasilisha hoja zako na nikazifanyia Kazi?
 
Wapi huyo mtu kasema "Mimi Mungu"?

Bado macho yako yana tongotongo hata huoni vizuri au? Njia nzuri na ambayo imethibitika kwa mtu aliyesoma jambo na akashindwa kulielewa ni kurudia kusoma tena na tena. Basi,ikiwa umefikwa na hali hiyo rudia tena kusoma angalau mara tatu.
 
Hujasoma Uzi mzima umekimbilia tu ku-comment au?
NIMERUDI KUUSOMA TENA UZI VIZURI NILICHOONA UMETUMIA SANA MISTARI YA BIBLI KISHA UKAJA KUCHUKUA AYA HIZI Kurani An-Nisa(Sura 4) 156-157:



“156 Na pia kwa kufuru zao na kumsingizia kwao Maryamu uwongo mkubwa, 157. Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini. 158. Bali Mwenyezi Mungu alim- tukuza kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.”
UKIDAI NI MANENO YA MUNGU MWENYE SIFA ULIZOTAJA JUU. HIVYO BASI NAPENDA KUKUAMBIA KUWA HIZO SIFA ZA MUNGU ULIZOTAJA HAPO JUU SI SIFA ZA MUNGU MWENYE HAYO MANENO.
MUNGU MWENYE HAYO MANENO, HANA MWANA(YES) HANA MSHIRIKA(UTATU)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom