Kasumba ya ununuaji "Stabilizer" kama kifaa cha kulinda vifaa vya kielectronic na ukweli wake.

Transistor

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
970
1,461
Habari wanajamvi karibuni tena,

Leo nitazungumzia kuhusu kasumba ya ununuaji wa stabilizer kama kifaa cha kulinda vifaa vya kielectronics na ukweli wake katika dhana hiyo kitaalamu.

Mtu akinunua tu TV yake kitu cha kwanza ambacho hua anaamini kitalinda TV yake hua ni stabilizer.

Hata kama mtu hana tatizo la umeme mdogo amekuwa akifunga stabilizer kama ulinzi wa kulinda vifaa vyake visiungue.

Ukweli ni kwamba stabilizer hailsaidii kuzuia vifaa vyako visiungue.Kazi ya stabilizer ni kuongeza umeme ukishuka na kupunguza umeme ukipanda kazi ambayo vifaa vya kielectronics mfano TV,Laptop,Home theatre Ving’amuzi n.k vina mfumo huo tayari.

Vifaa vingi kwa sasa vinatumia mfumo wa PWM power supply ambao hauzuliki na Voltage flactuation (kupanda na kushuka kwa umeme).

Umeme hata ukishuka 100v vifaa hivi huendelea kufanya kazi na ukizidi 240 vifaa hivi hujizima.

Ukikuta kifaa chako kimeandikwa 100v-220v huna haja ya kutumia stabilizer na hata kama kimeandikwa 220 tu na wewe unapo ishi huna tatizo la low voltage huna haja ya kutumia stabilizer.

Kwasababu stabilizer haina uwezo wa kuzuia kifaa kisishambuliwe na tabia za umeme zinazo dhuru vifaa vifaa vya kielectronics tabia hizo zinapo tokea vifaa vyako vitaungua tu haijalishi umefunga stabilizer au laa.

Hivyo ukiona vifaa vyako haviungui haimaaniishi sababu umefunga stabilizer hapana sababu tu nikwamba tabia za umeme zenye madhara ya kuunguza vifaa vyako hazijatokea hapo kwako na si kwasababu umefunga stabilizer.

Na ukiona umefunga stabilizer na vifaa vyako vinaungua ungua,usije ukadhani stabilizer ni mbovu au feki,kazi yake si hiyo.

Kinacho unguza vifaa vya kielectronics haijarishi umefunga stabilizer au laa kinaitwa VOLTAGE SURGE,ni tukio ambalo stabilizer ya kawaida ile inayofanya kazi ya kupandisha na kushusha umeme haiwezi kuizuia.

NINI MAANA YA VOLTAGE SURGE

Voltage Surge pia hujulikana kama Transient Voltage.Ni tukio la ghafla la mabadiliko ya kiwango cha cha msukumo wa umeme (voltage) katika nyumba yako.

Kiasi cha msukumo wa umeme (voltage) ambacho kipo katika nyumba yako yaani 220 Voltage huongezeka ghafla na kufikia kiasi cha 20Kv (Sawa na Volt 20000 ) kwa kasi ya 10nanoseconds hadi 50uroseconds.

Surge pia huaribu frequency za umeme za kawaida ambazo ni 50/60Hz na kuwa kati ya katika mabadiliko kati ya 20Hz hadi kufikia 20Mhz. (Frequency ambazo ni za juu kiasi zinaweza toa sauti au mvumo).

tukio hili hutokea na kuishi katika mfumo wa umeme wa nyumba yako kwa muda wa 50 nanosecond hadi 2 miliseconds kwa mujibu wa IEEE Std C62.41 pamoja na ANSI C62.1991.

AINA ZA VOLTAGE SURGE

1. Disruptive surge
hii hasababisha kuharibu mifumo ya maamuzi na kumbukumbu za vifaa vya kielectronics vyenye mifumo ya logic, sababu huweza ku ingiza frequency chafu hivyo vifaa vikachakata taarifa zisizo sahihi na kusababisha vikashindwa kufanya kazi vile ilivyo kusudiwa.

2. Dissipative surge
hii ni tendo la kujirudia rudia la kupanda na kushuka kwa umeme kwa ghafla pia huweza kuambatana na aina ya kwanza ya surge na athari zake ni kuwa hufupisha maisha ya vifaa vya kielectronics.

3. Destructive surge
hii ni surge ambayo huaribu kila kitu on the spot.Surge hii mara nyingi husababishwa na radi.

Swali la kujiuliza ni Kwanini stabilizer ya kawaida haina uwezo wa kuzuia surge?

JIBU : Fahamu kasi ya surge ni kubwa kuliko kasi ya maamuzi ya kiutendaji ya stabilizer.

Kama tulivyo ona Surge hutokea kwa speed ya 10nanosecond hadi 2milisecond wakati stabilizer maamuzi yake hufanyika kwa speed ya 10milisecond.

Hivyo hadi stabilizer istuke kua kuna over voltage tayari surge inakua imesha piga na kuondoka.

Pia kwakua surge huambatana na electrical frequency distortion ya kuanzia 20Hz hadi 20Mhz husababisha stabilizer au PWM power supply kushindwa kufanya kazi yake katika utaratibu sahihi (Huchanganyikiwa) na kama surge itakua ni aina ya tatu basi hata stabilizer yenyewe itachomwa au kuharibika.

NINI CHANZO CHA VOLTAGE SURGE

Kwa mujibu wa ( IEEE Std C62.11 – Standard for Metal-Oxide Surge Arresters for AC Power Circuits voltage surge) vyanzo vya voltage surge vimegawanywa katika makundi mawili.

(a)Vyanzo vya nje ya nyumba

i.Radi.

Radi huweza kuongeza umeme wa ziada katika power line hivyo hupelekea kutokea kwa voltage surge katika nyumba za watumiaji wa umeme.

ii.Wasambazaji wa umeme (Kwa Tanzania mfano Tanesco)

Wazalishaji wa umeme huweza kusababisha voltage surge kutokana tendo la power source switching kwa mujibu wa (AIEE Committee Report [B1]6, IEEE Committee Report [B61], and IEEE Committee Report [B62]).

Tukio hili hutokea wakati wazalishaji wa umeme wanabadilisha chanzo cha uzalishaji umeme,kutoka chanzo kimoja kwenda kingine,tendo hili hufanywa kwa kufanya “switching” tukio hili hufanyika kwa haraka,unaweza kuliona tendo hilo pale umeme unapo katika na kurudi ndani ya sekunde kadhaa na hata mara nyingine umeme haukatiki ila unacheza kidogo.

Mara chache tendo hili hufanywa mchana,ili kuepusha madhara wasambazaji wa umeme hufanya jambo hili usiku wa manane kati ya saa saba usiku hadi saa nane usiku ambapo watu wengi wanakua wamezima vifaa vyao.

iii.Kulegea kwa waya katika viungio vya kwenye nguzo,au miti kugusa waya za umeme.

iv.Matumizi ya transformer moja zaidi ya nyumba moja.Kama itatokea mmoja wa watu waliounganishwa katika transformer hiyo akafanya vitendo ambavyo vinasababisha uzalishwaji wa transient voltage basi huathili wale wote wanao tumia transformer hiyo.

Vitendo hivyo ni kama vile Uchomeleaji,uendeshaji wa motor kubwa mfano mota za viwanda na mashine.

(b)Vyanzo vya ndani ya nyumba

i.Kulegea kwa viungo vya waya za wiring katika nyumba.

ii. Kuwasha na kuzima vifaa vya umeme (switching).

iii. Matumizi ya vifaa vifuatavyo katika nyumba yako-:

-Photocopiers (Mashine za photocopy)
-PC Power Supplies (Desktop computer)
-Laser Printers
-Mashine ya kuchomelea (welder machine)
-Power Factor Correction Equipment (capacitor bank)
-Motor Controllers (frequency motor control)
-Motor za za visima vya maji,pump,mashine za kufulia n.k
-Compressors (Vifaa vyote vinavyo tumia compressor mfano friji,Air condition,water dispenser n.k)

NINI MADHARA YA VOLTAGE SURGE.

1.Kuungua kwa taa mara kwa mara mfano taa aina ya Energy saver za CFLs pamoja na zile za LED.

Ukiona nyumba yako inaunguza taa mara kwa mara basi kuna uwezekano nyumba yako inazarisha surge kulingana na sababu nilizo zieleza au inawezekana line yako ya umeme inakabiliwa na vyanzo vya surge.

2.Vifaa vya kielectronic kama vile TV,Computer,projectors,na power supply kuungua mara kwa mara.

3.Kusababisha moto,uunguaji wa vifaa vya kielectroniks mara chache unaweza kupelekea kutokea kwa moto,ambao unaweza kuleta madhara zaidi katika nyumba.Hivyo vyanzo vya moto wa umeme si sababu tu ya wirering mbovu mara nyingine husababishwa na surge.

Kwa mujibu wa mtandao wa https://www.platinumelectricians.com.au/blog/what-is-a-power-surge/

NAMNA YA KUONDOA TATIZO LA VOLTAGE SURGE

Watu wengi wamekuwa wakiishi na tatizo hili bila kujijua katika nyumba zao,.

Tatizo la voltage surge lipo nchi nyingi,na imekua moja ya jambo linalo umiza vichwa wafanyabiashara wa vifaa vya electronics ambapo wengi sasa wameanza kutengeneza mifumo ya kuzuia vifaa vyao visiathilike na tatizo hili.Ndio maana unaweza kuona kifaa kimeandikwa "Volatage Surge protected”.

Zifuatazo ni njia za kuodoa voltage surge katika nyumba yako(Hii ni rahisi tu kwa yale matatizo yanayo tokea ndani ya nyumba na sio nje ya nyumba kwani kwa Tanzania mwenye kibali cha kushugulikia line za umeme nje ya nyumba ni TANESCO TU).

(A).Njia za kawaida za kujiadhari na power surge

1.Zima na uchomoe vifaa vyako wakati wa kipindi cha mvua
2.Ni vizuri Tanesco wakawa wanazima umeme wao kipindi cha mvua yenye radi nyingi kama eneo ambalo mvua hiyo inanyesha hawana surge arresters za kutosha.

3. Kama vifaa vyako vinaungua mara kwa mara Mwite mtaalamu wako wa umeme akague wiring yako kama ina chanzo chohote cha surge,na akushauri namna sahihi ya kukiondoa chanzo hicho.

4.Uwe na utaratibu wa kuwasha kwanza vifaa vitumiavyo umeme mkubwa kwanza ndipo ufate vile vidogo.

5.Kama mfumo wa umeme unaonekana upo sawa na bado unakabiliwa na surge Jaribu kukitambua kifaa kinacho sababisha surge katika nyumba yako.

6. Kama suge inasababishwa na loose connection katika nguzo waite Tanesco waje waondoe tatizo hilo.

7.Kama nyumba yako ina mfumo wa solar hakikisha pannel zako zimeungwa na earth wire,pia madishi ya ving’amuzi na satellite yafungwe earth wire

(B).Njia ya kuzuia surge kwa kufunga electronics surge arrestors katika nyumba yako au vifaa vyako hasa ya kielectronics.

Kwa mujibu wa (IEEE Std C62.11 – Standard for Metal-Oxide Surge Arresters) vifaa vya kielectronics ambavyo vimetengenezwa kwa ajiri ya kuvilinda vifaa dhidi ya surge ni vile ambavyo pamoja na tekinolojia nyingine ni lazima vihusishe kifaa kinacho itwa MOV ndani ya mfumo wa surge arresters hizo.

MOV ni kifaa maalamu ambacho kimethibitika kuweza kuondoa tatizo la Surge katika vifaa vya umeme.
MOV ni kifupi cha neno Metal-Oxide-Varistor.

UBORA WA SURGE ARRESTORS

Fahamu kuwa kuna surge arrestors za kufunga kwa ajili ya nyumba nzima na kwa ajiri ya kifaa kimoja kimoja.

Ubora wa surge arrestors unategemeana na tekinolojia iliyo tumika kuunda arrestor hiyo.

Ila kwa kifupi unapoenda kununua surge arrestor hakikisha unaulizia uwepo wa vifaa hivi katika arrestors hizo.

Surge arrestor bora ni ile ambayo imeundwa kwa vifaa hivi vifuatavyo.
1.Delay and control circuit

Hii ni saketi ambayo inasaidia kuchelewesha kifaa chako cha umeme ulicho kipachika kwenye umeme, kupokea umeme pale unavyo washa switch au umeme unapo rudi baada ya kukatika.

Kifaa hiki huzuia umeme huo kwa sekunde kadhaa ili kusubili umeme huo utulie kabisa ndipo kifaa hiki kita uruhusu umeme kuingia kwenye kifaa chako iwe simu,TV n.k.

Hivyo kamakuna surge yeyote ilikua imeambatana wakati umeme unarudi au wakati unawasha switch surge hiyo haita pata nafasi ya kukidhuru kifaa chako.

2. Varistor(Metal oxide varistor (MOV)

MOVs kazi yake ni kuondoa kiwango cha umeme ambacho kinazidi kiwango cha kawaida katika mfumo wa umeme.

Kama ikitokea umeme ukazidi kiwango cha kawaida MOVs huanza kutengeneza ukinzani ambao utaondoa excess voltage katika line ya umeme.

Kwakuwa Voltage surge ni kitendo cha kuongezeka kwa kiwango cha umeme

ghafla kunako sababishwa na kitu kama vile radi au loose connection na ambacho hutokea kwa sekunde kadhaa tu,MOVS kazi yake ni kuondoa ongezeko hilo la umeme kwenye line ili isifike kwenye kifaa chako na kuleta madhara.

3. Themistor

Thermistor;ni kifaa maalumu ambacho kazi yake ni kuzuia inrush currents mara tu umeme unavyo rudi au switch inapo washwa.

Tambua kuwa kila kifaa cha umeme kina mahitaji yake ya kiwango cha current,hivyo kuruhusu kiwango chote cha current kuingia katika kifaa husika mara nyingine huleta madhara ya kifaa hicho kuungua;ndio maana vifaa vingi vya umeme huungua wakati wa kuwashwa;hii inasababishwa na inrush currents.

Kuondoa tatizo hilo thermistor hutumika ambapo umeme huanza kuingia katika thermister ndipo huingia katika kifaa cha umeme.

Baadaya ya umeme kuwaka thermister huwa na ukinzani mkubwa sana hivyo kuzuia kiwango cha current kisiingie moja kwa moja katika kifaa chako,baada ya hapo kwa kuwa kifaa husika kitakua kinahitaji kiwango fulani cha current ili kifanye kazi,kitavuta kiasi cha current ambacho chenyewe kinahitaji;kwa kuwa thermistor imezuia current hizo kuvutwa kwa current na kifaa kutasababisha thermistor ipate moto;thermistor ikipata moto ukinzani wake hupungua hivyo kuruhusu kile kiwango tu cha current ambacho kimehitajika na kifaa ulicho kipachika wakati huo!

Hivyo kwa kutumia thermister kifaa kitapewa current kutokana na mahitaji yake bila kuzidishiwa!

4. Ceramic Capacitor Y Capacitors-DIP.(sparks killer).

Hii ni capacitor maalumu kwa ajili ya kuondoa Cheche zinazo tokea kwenye line ambazo zinaweza kupelekea surge.

Tambua kuwa unapowasha switch kuna cheche ambazo hutokea kutokana na kuungana kwa terminal mbili,au wakati mwingine kama line husika ina loose connection hupelekea kutokea kwa cheche,ambazo huweza kuleta surge;
hivyo kuhakikisha tunaendelea kuwa salama dhidi ya surge tunalazimika kuondoa sparks za aina yeyote kwenye line yetu ndo mana Ceramic Y Capacitor-DIP ikatumika.

5. Filter capacitor
Capacitor hizi hufungwa mbili sehemu ya mbele na nyuma ya ferrite transformer ndani ya surge arrestor.Kumbuka awali nilisema surge inaweza kuharibu mawimbi sahihi ya umeme hivyo kazi ya capacitors hizi kubwa mbili ni ku-smooth umeme unaoingia katika kifaa chako kuhakikisha hakuna mawimbi yasio hitajika yanajipenyeza katika kifaa chako cha umeme ambayo yanaweza kuleta madhara.

Pia kapacitor hizi zinasaidia kuhakikisha surge arrestor yenyewe haizalishi mawimbi yatakayo ingiliana na mifumo mingine kama vile mawimbi ya radio,TV n.k

6. Choke ferrite transformer

Kazi ya choke hii ni kuwa na sifa ya ku-Absorb excess voltage kwa kugeuza nguvu hiyo ya umeme iliyo zidi kuwa sumaku(electromagnetism).

7.Fuse

Kwa kifaa ambacho kinatimia MOVs,ni lazima kifaa hicho kiwe na fuse,kutokana na ufanyaji kazi wa MOVs.

inapotokea voltage surge inakuwa kubwa sana kawaida MOVs huzuia umeme kuingia kabisa katika saketi kwa kutengeneza short circuit ili fuse ikate.

Hivyo matumizi ya Fuse sehemu ambapo MOVs zimetumika hayakwepeki.

WAPI NITANUNUA SURGE ARRESTOR

Maduka ya vifaa vya umeme yanauza pia surge arrestors,wasiliana na mtaalamu wako akushauri arrestor ipi ni sahihi kulingana na mahitaji yako.

Pia unaweza kiwasiliana na sisi tukakufungia arrestor kwa ajili ya vifaa vyako pia
Unaweza bonyeza hapa kuona kifaa chetu cha surge arrestor kwa ajiri ya Tv,radio n.k ambacho ni toleo la mwaka 2015.

Video ya kifaa hii hapa

MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA KUHUSIANA NA SURGE.

1.Voltage stabilizer au Voltage regulator zinauwezo wa kuzuia surge?

JIBU: Inategemeana na mfumo wa stabilizer husika,ili stabilizer iwe na uwezo wa kuzuia surge ni lazima ndani yake uwekwe mfumo wa kielectronics unao husika na kuzuia surge.Kawaida stabilizer za namna hii huandikwa katika katika Menu yake kwamba zina mfumo wa surge protection.

Hakikisha unaenda na mtaalamu akusaidie kuthibitisha kama kweli stabilizer unayo nunua ndani yake wameongeza mfumo wa surge protection.

Na ufahamu kuwa stabilizer ambazo hufungwa surge protector mara nyingi hazitumii mfumo wa RELAY bali hutumia SERVO MOTOR.(ila si kila starbilizer yenye servo motor ina surge arrestor circuit ndani yake).

2.Earth wire inazuia surge?

JIBU. Ndiyo Earth wire inasaidia kulinda nyumba na vifaa vyako dhidi ya surge hasa kwa aina ya tatu ya surge kwa namna kuu mbili.

(i) Direct surge arrestor.Earth wire huweza kulinda nyumba yako kwa kukusanya umeme wote ulio zidi na kuupeleka katika ardhi.

(ii) Indirect surge arrestor,Earth wire husaidia vifaa vya kuondoa surge vifanye kazi kwa ufasaha hasa kwa kusaidia circuit breaker kujizima (hasa pale inapo tokea radi imepiga au kuna short imetokea).

Hakikisha nyumba yako ina mfumo bora wa earth wire,Na uhakikishe unakagua mara kwa mara.

3.Je kwanini wanao unda vifaa vya kielectronic mafano TV,Radio na Computer wasiweke mfumo wa surge arestors katika vifaa vyao kuepuka visiungue kuliko kusubiri kinunuliwe kama kifaa cha pembeni?

JIBU: Kuna baadhi ya kampuni chache zinafunga surge protector katika vifaa vyao hasa kwa vile vifaa vinavyo tumia “external power supply”.

Kampuni nyingi zinapotezea sababu ufahamu kuwa surge protectors ni kama mshumaa jinsi kinavyo pambana na surge ndiyo kinavyo kufa mapema MOVs hua na maisha mafupi na yasiyo tabirika kulingana na kiasi na idadi ya surge inazo kabiliana nazo.

Hivyo kampuni nyingi huepuka kufunga full surge arestors ndani ya vifaa sababu kama eneo ambalo mtumiaji litakua na surges nyingi mfumo wa surge ndani utakufa mapema tena labda kuliko ilivyotakiwa kuishi kwa kifaa hicho kwa ujumla.Hivyo wanaepuka kuonekana vifaa vyao vinaharibika mapema

4.Je ni lazima vifaa vyangu viwe vinaungua ndiyo nijue nina surge katika nyumba yangu.

HAPANA: Ukumbuke sio lazima uwepo wa surge katika nyumba yako uchome vifaa,bali uwepo wa surge husababisha maisha ya vifaa vyako vya kielectronics yakawa mafupi kuliko muda ambao kifaa icho kilitakiwa kuishi.

Aina ya tatu ya surge ndiyo mara nyingi huchoma vifaa “on the spot” ila hizi nyingine ni kama sumu inayo ua taratibu vifaa vyako hasa surge aina ya kwanza na ya pili.

Na ndiyo maana surge arrestors haziishi milele sababu kazi yake ni kukinga madhara yasifike kwenye kifaa hivyo surge arrestors ndiyo hufa badala ya TV yako au Computer yako.
5.Je ninunue Sabilizer yenye surge arrestor ndani au ninunue kifaa cha surge arrestor pekee.

JIBU: Vifaa vya kielectronics siku hizi vimetengenezwa kuhimili umeme mdogo hata ukifika 100 vinaendelea kufanya kazi,na umeme ukiwa mwingi vinajizima hivyo huna haja ya stabilizer kwa ajili ya TV yako kama tu voltage yake imeandikwa 100V-220v input voltage.

Unachotakiwa kununua ni Surge arrestors kwa ajiri ya TV,Music system, Simu au Computer.
Sababu gharama ya surge arrestor peke yake ni ndogo kuliko kununua stabilizer yenye surge arrestor
6.Nina stabilizer ila haina mfumo wa surge protector je vifaa vyangu vipo salama

JIBU: Hapana vifaa vyako havipo salama ikitokea surge aina ya tatu vitaungua au kama nyumba yako ina surge aina ya kwanza na ya pili itakua inashambulia vifaa vyako na vitaharibika kabla ya wakati wake,hivyo unatakiwa kufunga surge arrestor.
7.Nimefunga stabilizer ila vifaa vyangu vimeungua kwanini?
JIBU:Surge ndiyo huunguza vifaa vya umeme hata ukifunga stabilizer ya kawaida.

8.Kwanini sabilizer haina uwezo wa kuzuia surge?

Surge hutokea kwa speed ya 10nanosecond hadi 2milisecond wakati stabilizer maamuzi yake hufanyika kwa speed ya 10milisecond.Hivyo hadi stabilizer istuke kua kuna over voltage tayari surge inakua imesha piga na kuondoka.

Pia kwakua surge huambatana na electrical frequency distortion ya kuanzia 20Hz hadi 20Mhz husababisha stabilizer kushindwa kufanya kazi yake katika utaratibu sahihi (Huchanganyikiwa) na kama surge itakua ni aina ya tatu basi hata stabilizer yenyewe itachomwa au kuharibika.

ANGALIZO:

Kwakua vifaa vya Surge arrestor vinatumia MOVs hakikisha kabla ya kufunga mfumo wa surge protector katika nyumba yako mfumo wa vilinda circuit unafanya kazi vizuri.
Vilinda saketi hivyo vinapatikana pale katika distribution board (Main switch).

Vifaa hivyo ni Earth leakage circuit breaker pamoja na Residual circuit breaker.

Hakikisha kila laini ina uwezo wa kujizima automatic pale inapotokea short circuit.Pia hakikisha main Circuit breker ambayo ni earth leakage inauwezo wa kujizima pale inapo tokea leakage.

Kila kitu kikiwa sawa unaruhusiwa kufunga vifaa au kifaa cha surge arrestor katika nyumba yako.

WASILIANA NA FUNDI ANAYE TAMBULIKA ILI AKUSHUGULIKIE MATATIZO YA UMEME KATIKA NYUMBA YAKO.

KWA USHAURI KUHUSU MASWALA YA UMEME NA HUDUMA YA KUFUNGIWA MFUMO WA UMEME KATIKA NYUMBA ,KIWANDA N.K

HUDUMA YA KUKAGUA MFUMO WA UMEME KATIKA NYUMBA YAKO

HUDUMA YA KUBADILISHA WIRE RING KATIKA NYUMBA AU KIWANDA CHAKO

WASILIANA NASI 0629068815
Asante,
Imeandaliwa na Transistor

REFERENCE.
ANSI C62.22-1987, American National Standard Guide for the Application of Gapped Silicon-Carbide
Surge Arresters for AC Systems.1
ANSI C84.1-1989, American National Standard for Electric Power Systems and Equipment—Voltage Rat-
ings (60 Hertz).
IEC 34-15 (1995-01), Rotating Electrical Machines—Part 15: Impulse Voltage Withstand Levels of Rotating
A.C. Machines with Form Wound Stator Coils (draft revision).2
IEEE Std 18-1992, IEEE Standard for Shunt Power Capacitors.
IEEE Std 100-1996, The IEEE Standard Dictionary of Electrical and Electronics Terms, Sixth Edition.3
IEEE Std 824-1994, IEEE Standard for Series Capacitors in Power Systems.
IEEE Std 998-1996, IEEE Guide for Direct Lightning Stroke Shielding of Substations.
IEEE Std 1036-1992, IEEE Guide for Application of Shunt Power Capacitors.
 
Site ya mbele kabisa, nipo pembeni na Bakuli la popcorn juice saafi , nasubiria muda wa Iftari hapa.
 
Vp kuhusu hizi Fridge guard na Tv guard,je zinafanya kazi hiyo ya kuzuia Surge
Maranyingi hua na mfumo wa surge arrestor,ila si mara zote.

Kama nilivyo sema hakikisha kampuni iliyotengeneza hicho kifaa imeandika kuwa kina surge arrestor.

Kifaa kuwa guard kinaweza kikawa in high and low voltage ila sio voltage surge.

Ufahamu kuwa kma kifaa kina surge arrestor ni lazima katika menu yake watakushauri kuwa ukibadilishe baada ya muda flani.

Fahamu kuwa surge arrestors hazidumu zinakufa sababu kila siku zinapambana na surges na kila inavyo pambana na surge ndiyo inavyo zidi kubakiza muda mchache kama mshumaa tu.
 
Mfano wa surge arrestor zinazofungwa katika line nzima ya nyumba.

Zinafanana na circuit breaker za kawaida ila haina kidude cha kiwasha na kuzima.

Japo zipo za aina nyingi
images(3).jpeg
 
Maranyingi hua na mfumo wa surge arrestor,ila si mara zote.

Kama nilivyo sema hakikisha kampuni iliyotengeneza hicho kifaa imeandika kuwa kina surge arrestor.

Kifaa kuwa guard kinaweza kikawa in high and low voltage ila sio voltage surge.

Ufahamu kuwa kma kifaa kina surge arrestor ni lazima katika menu yake watakushauri kuwa ukibadilishe baada ya muda flani.

Fahamu kuwa surge arrestors hazidumu zinakufa sababu kila siku zinapambana na surges na kila inavyo pambana na surge ndiyo inavyo zidi kubakiza muda mchache kama mshumaa tu.
Shukran kwangu nina extension cable ambayo ubaya niliinunua kwa mtu hivyo sijui yapaswa niibadili baada ya muda gani ila imeandikwa Surge protection up to 2kv na mpaka sasa ina mwaka na haijawahi niletetea tatizo lolote vp ushauri wako kitaalam
 
Ni ngumu kusema ubadili kwa baada ya muda gani inategemeana na technolojia ambayo hiyo kampuni imetengeneza hicho kifaa.

Japo zipo za kisasa ambazo MOVs zake zikichoka kuna taa ya onyo inawaka ikihitaji replace ment.

Ugumu wa kusema lini kifaa cha surge kibadilishwe unatokana na mazingira ya tatizo kifaa hicho hicho kimoja chenye quality sawa kinaweza kwa mwingine kikaka miaka miwili kwa mwingine mitano.

Hii inasababishwa na nani hasa anapokea surge nyingi kwa siku kuliko mwingine.

Viwandani wao hujiwekea muda labda kila baada ya mwaka wanabadili.

Hivyo ni ngumu kusema hasa lini inabidi ubadili kama manufacturer hajasema na hakunda mfumo wa warning lamp.
 
Extension zenye mfumo wa surge arrestor mmfano hii japo nyingi za kichina ni feki wanaandika zina surge arrestor ukifungua ndani hukuti kitu chochote kinacho husiana na surge.
images(5).jpeg
 
Back
Top Bottom