Alichofanya Eliya Mtishbi na Tukipasacho Kufanya Dhidi ya Korona: Baada ya Kumwomba Mungu

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
1587138918224.png
Na. M. M. Mwanakijiji

Tunaweza kumwomba Mungu atusaidie kutuepusha na janga la ugonjwa wa korona. Kama binadamu na watu wenye imani tunaelewa wazi kuwa mwisho wa siku mambo yote yako mikononi mwa Mungu. Tunapojiachilia katika huruma na wema wake tunakiri uwezo na uwepo wake lakini pia tunakiri ubinadamu wetu. Kumwomba Mungu hakuwezi kuwa kosa. Nchi zote zilizoendelea ambazo nazo zimepigwa na majanga ya korona watu wake nao wanamwomba Mungu na kumlilia.

Kila siku hapa Marekani kuna watu wanakutana kwenye njia ya simu, Facetime, Skype na njia mbalimbali za mawasiliano kumwomba Mungu. Japo kwenye majimbo mengi ibada za hadhara zimesitishwa lakini siku ya Pasaka kwa mfano kwenye Jimbo Kuu Katoliki la Detroit Askofu Mkuu aliadhimisha Misa Takatifu akiwa na watu wachache tu kwenye Kanisa Kuu. Misa ile ilirushwa moja kwa moja na televisheni na kwenye Facebook na Youtube na sisi waumini tulifuatilia tukiwa majumbani mwetu. Mungu yupo mahali popote.

Kwa Wakristu kuna mstari unaosema kuwa “Wakutanapo wawili au watatu kwa Jina langu mimi nipo kati yao” (Mathayo 18:20). Mstari huu una maana kuwa uwepo wa Mungu katika ibada hauitaji wingi wa watu. Utendaji wake hauitaji mkusanyiko mkubwa wa watu. Katika maandiko tunakutana na mifano kadha wa kadha wa jinsi Mungu alivyoweza kutenda kwa kumtumia mtu mmoja au wawili tu au watu wachache lakini akafanya makubwa.

Mojawapo ya masimulizi makubwa yenye kusisimua katika Biblia ni kile kisa cha Elia Mtishbi. Baada ya watu wa Israeli kudanganywa na Manabii wa Baal, Elia akaamua kuwapa changamoto. Akawaambia kuwa yeye ni mtu mmoja tu aliyebakia akiwa ni Nabii wa BWANA na Baal alikuwa na “manabii” 450. Elia akataka kuwaonesha yupi ni Mungu wa kweli basi; yule mwenye Nabii mmoja aliyebakia au yule mwenye nabii 450 wenye mbwembwe nyingi. Simulizi hili linatuonesha kuwa Elia akawapa nafasi manabii wa Baali kumwomba Mungu wao atekekeze (aunguze) kwa moto sadaka walizoziandaa kwenye madhabahu.

Manabii wale 450 walianza kumwomba mungu Baal na kulia na kujichanja huku wakipiga kelele. Kwa kuwaangaliwa kwa nje unaweza kuamini walikuwa na imani zaidi, na kwa kelele na vilio vyao mungu wao angewasikiliza. Elia aliwadhihaki na kuwaambia labda waongeze sauti inawezekana mungu wao alikuwa amelala! Waliposhindwa ndipo Elia akaingia kazini yeye peke yake na bila sala ndefu tena katika jambo lisilowezekana (aliwaagiza waandalizi wake wamwagie maji zile sadaka mara tatu (alichimba na mfereji wa maji kuzizunguka kabisa). Na kwa sala fupi kabisa na yenye nguvu akamwita Yehova Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo. Alipomaliza tu sala yake na kabla ya kusema “Amina” Moto ulishuka toka mbinguni na kutetekeza sadaka zile na kuyakausha maji yale!

Ndipo watu wakajua kuwa Yehova ndiye Mungu. Unaweza kusoma kisa hiki kwenye 1 Wafalme 18:20-40.

Ndugu zangu, Rais Magufuli yuko sahihi kutaka Watanzania waliombee Taifa na hata bila yeye kutaka hivyo nina uhakika watu wenye imani wamekuwa wakiliinua taifa letu na watu wetu kwa dua na sala mbalimbali. Huu ni wajibu wetu; lakini siyo tu sisi dunia nzima inamlilia Mungu kumwomba. Hili haliwezi kuwa jambo baya wala la kudharau.

Na inawezekana Mungu ameshaanza kujibu sala na dua hizi. Mwanzoni mwa baa hili kulikuwa na hofu kuwa ugonjwa huu utaathiri zaidi Afrika labda kuliko bara nyingine lolote. Hata sasa maambukizi na vifo kwenye bara letu hayaendani na wingi na mtawanyiko wa watu wetu.

Pamoja na hayo bado Mungu anatupa nafasi ya kujiandaa zaidi. Haitoshi kumwomba Mungu na sisi bila kufanya au kuchukua hatua makini. Tayari taifa limechukua hatua mbalimbali ambazo naamini kwa kiasi kikubwa ni sahihi. Baadhi ya hatua zimechelewa sana na matokeo yake ndio tunaona maambukizi yakiongezeka badala ya kupungua. Na yameongezeka kwa haraka zaidi siku hizi za karibuni na tusipoangalia yanaweza kuongezeka zaidi ndani ya siku chache (kama tutafuata kama ilivyotokea nchi nyingine).

Lengo la Mikakati

Sasa hivi, lengo la mikakati yoyote inayochukuliwa na nchi ni kupunguza kasi ya maambukizi, kudhibiti wagonjwa wapya, na kuwalinda watu ambao bado hawajaambukizwa. Katika kupunguza kasi ya maambukizi ndipo panalala kazi kubwa ya kuidhibiti korona. Unaposoma habari mbalimbali duniani kwenye nchi zinazohangaika na ugonjwa huu sehemu kubwa ni kuwa kasi ya maambukizi mapya bado ni kubwa au ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba mifumo ya afya haikuweza kujiandaa nayo. Chukulia kwenye jimbo la Michigan ambako ninaishi.

Mgonjwa wa kwanza wa Corona alitangazwa Machi 10. Leo hii (mwezi mmoja na wiki moja baadaye) jimbo hili lina wagonjwa karibu 30,000 na vifo zaidi ya 2000! Na hapa ni pamoja na ukweli kuwa tumekuwa chini ya “lockdown” kwa karibu mwezi mzima! Watu wengi hawaendi kwenye makazini, michezo, hakuna ibada za hadhara n.k Na inadaiwa hatua zilizochukuliwa Michigan ni miongoni mwa hatua kali zaidi kuchukuliwa na jimbo lolote la Marekani.

Sasa, kama kwenye taifa hili lilioendelea hivi, lenye raslimali za kila namna watu wake wanaambukizwa kwa kasi hivi na kufa itakuwaje kwetu? Bila ya shaka kuna mambo (factors) ambazo zinafanya ugonjwa huu kuwa wa hatari zaidi kuliko nyumbani. Siyo kwamba watu wetu hawaupati ila inawezekana wanaupata kwa njia tofauti na labda kuna mambo ambayo bado hayajaeleweka vizuri kwanini haujaenea kwa kasi ile ile kama ilivyokuwa Hispania, Italia, Marekani, Uingereza, Ufaransa na China yenyewe ulikoanzia.

Kwa hiyo ni muhimu sana kuhakikisha kasi yake haiendi kwa kasi hivi. Binafsi nimeshtuka zaidi kuwa kwa siku mbili hizi idadi ya wagonjwa iliongezeka mara mbili. Nasubiria kuona namba mpya kutoka 88 zitatupeleka wapi. Kama ni kweli mtu mmoja aliyeambukizwa (ambaye hana dalili) anaweza kuambukiza karibu watu 40 basi namba yetu inaweza kuwa kubwa zaidi. Lakini pia kwa vile hata ambao hawaoneshi dalili baadaye wanaanza kuonesha dalili hizo basi wagonjwa wanaweza kuongezeka kwa kasi zaidi na kusumbua mifumo yetu ya afya.

Sasa tufanye nini?

Tayari hatua nyingi zilizochukuliwa zimesaidia lakini bado tunaona kuwa hata watu ambao wanatuambia tuchukua hatua wao wenyewe ni kama hawaelewi uzito wa janga hili na uwezekano wa tatizo hili kuendelea kwa muda. Nimesoma na kufuatilia maoni ya wadau mbalimbali na nimefuatilia hatua mbalimbali ambazo serikali imechukua hadi hivi sasa. Maoni yangu ni kuwa ni lazima tufikiri nje ya boksi; tufikirie nje ya boksi hilo kwa sababu mazingira yetu ni tofauti sana na nchi zilizoendelea. SIyo kwamba binadamu ni tofauti bali mazingira ni tofauti.

Hatuwezi Kuiga Yote Yanayofanywa na Nchi Tajiri

Mojawapo ya makosa makubwa ni wale wanaodhani kuwa wakiiga yanayofanyika hapa Marekani basi na sisi hali itakuwa hivyo hivyo. Mojawapo ya mapendekezo makubwa ni kuwa watu wanataka kila mtu akae nyumbani kwa angalau wiki mbili. Kwamba, tuiweke Tanzania nzima chini ya ‘lockdown’ kwa muda wa wiki mbili au zaidi. Hili ni rahisi kulisema kuliko kulifanya. Nitaeleza kwanini.
  • Nchi Tajiri zina uwezo wa kufunga nchi zao na wananchi wao bado wakawa salama. Hapa Marekani mojawapo ya hatua ambazo serikali imechukua kufanya maisha yawe rahisi kidogo ni kutoa fedha taslimu kwa raia wake wote (wenye kustahili). Kila mtu anapewa dola 1200 na mtoto anapewa dola 500. Huu ni mchango wa mara moja na unatarajiwa kurudiwa tena.
  • Mfumo wao wa mafao ye kukosa ajira (unemployment benefits) kwa kawaida ulikuwa unatoa karibu dola 360 hivi kwa kila mtu kwa wiki angalau 26. Lakini sasa hivi wameongeza dola 600 juu ya hilo. Hivyo, licha ya kupewa zile dola 1200 bado mtu aliyeomba fao la kukosa ajira atapata pia dola karibu 900 kila wiki kwa wiki angalau 26! Hii ni sawa na dola 24, 000 hivi kwa miezi sita!
  • Serikali imetoa pia mafao ya kusaidia biashara ndogo ndogo ambapo walipitisha kiasi cha dola bilioni 350 katika raundi hii ya kwanza. Fedha hizi makampuni yaliyoomba kama mkopo unaoweza kusamehewa inadaiwa kufikia jina zilikuwa zimeshakwisha na hakuna aliyepata kiasi chote alichoomba! Sasa hivi wanafikiria kuongeza kiasi cha fedha tena; sitashangaa kama haitofikia dola trilioni 1 ya kusisimua uchumi!
  • Kwa makampuni makubwa kuna fedha nyingi zaidi ambazo zinaenda kutolewa ili kusaidia yasianguke na kusababisha hali ya uchumi ambayo sasa ni mbaya kuwa mbaya zaidi.
  • Mataifa haya Makubwa yana mfumo mkubwa wa mahospitali ambayo yameongezewa uwezo mkubwa zaidi ikiwemo vifaa n.k.
  • Matumizi ya jeshi katika kusaidia kuongeza uwezo wa hospitali na vituo vya afya. Tumeona hili China na Marekani na nchi nyingine ambapo majeshi yao yameenda kuongeza nguvu kwenye taasisi za kiraia. Marekani kwa mfano Brigedi ya Uhandisi (Army Corps of Engineers) ambayo ndio msimamizi mkubwa wa ujenzi unashirikiana kujenga hospitali za medani (field hospitals) kwa haraka na kuwapa uwezo hospitali ambazo zimezidiwa wagonjwa.
Hiyo ni mifano michache tu ya kuonesha ni jinsi gani hatuwezi kumuiga tembo kwa kila kitu vinginevyo tutapasuka msamba. Na wazo la kuifunga nchi nzima kwa wiki hata tatu tu ni wazo linalohitaji kufikiriwa vizuri zaidi. Naamini katika hili Magufuli yuko sahihi. Hata hivyo, naamini kuna mambo mengine tunaweza kuyafanya.
  • Kwa vile virusi hivi vinaenezwa kwa haraka katika mikusanyiko mikubwa ya watu hasa kwa vile virusi vya koronoa vinaweza kukaa hewani kwa angalau dakika kadhaa kiasi kwamba mtu anaweza kupiga chafya akaondoka na mtu mwingine akapita pale pale na kupumua hewa ile. Haitoshi basi kukaa mita moja tu; tupunguze kabisa mikusanyiko. Makanisa na Misikiti yatangaze kusitisha ibada zao kwa angalau wiki mbili au tatu. Hii itapunguza kusambaa kwa haraka maana hadi hivi sasa hii ndio mikusanyiko mikubwa zaidi inayofanyika nchini. Watu wasali kama Elia Mtishbi! Uamuzi wa kusitisha ibada za hadhara si wa serikali ni wa taasisi za dini.
  • Ni wakati wa JWTZ kushiriki moja kwa moja kwenye kudhibiti wagonjwa na wale wanaofuatiliwa. Tuna kambi za jeshi nchi nzima, wakati umefika kwenye hizi kambi jeshi litengeneze “field hospitals” au kambi za mahema kwa ajili ya kuwahifadhi wale ambao wamekuwa karibu na watu wenye korona ili kuwaangalia kwa karibu na kukata uwezekano wa kuambukiza jamii. Wakati wasafiri tunawaweka karantini kwa sababu hatujui kama wameshaambukizwa au wamekutana na mtu mwenye ugonjwa ni vizuri familia za wagonjwa 88 na wale watu wao wa karibu waangaliwe kwenye kambi hizi za kijeshi ukizingatia pendekezo la tatu. Hadi hivi sasa hatujaona kuhusika kwa jeshi kunakofaa na kutosha.
  • Serikali badala ya kutoa mabilioni ya hela kwa kila mtu huku wakikaa nyumbani itenge kiasi cha fedha kwa ajili ya kuzilisha na kuhudumia familia ambazo zitakuwa kwenye uangalizi wa siku kumi na nne. Naamini hiki kitakuwa ni kiasi kidogo sana kulinganisha na gharama ya kuifunga nchi nzima. Uthubutu wa Rais Magufuli kujenga SGR, Nyerere Hydropower Dam na mengine unatudokeza kuwa hatosita kutenga kiasi cha fedha kwa jambo kama hili itakapolazimu na ninaamini inalazimu sasa. Jeshi na Mageresha (ambayo yapo kila wilaya na mkoa) wanaweza kutumika kuandaa vyakula na mahitaji mengine kwa familia hizi.
  • Wakati huo huo tuongeze uwezo wa kupima, kutenga/karantini na kutibu na kufuatilia maambukizi. Hii ndio kubwa ya kudhibiti. Bila kupima na kutenga itakuwa vigumu sana. Hatuwezi kuwaweka watu wote mahospitali, hizi nchi kubwa tu hazijaweza sisi inatubidi tufikirie nje ya hilo.
  • Kwa vile watoto wako majumbani badala ya mashuleni, Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Wizara ya Sayansi na Teknolojia na ile ya Mawasiliano (na nyingine husika) wafikirie namba ya kuanza kutoa masomo kwa njia ya radio na televisheni kwa ajili ya watoto. Vipindi vya TV na Radio viangaliwe ili watoto wasikae nyumbani tu. Hatuwezi kugawa laptop na kutoa elimu kwa kila shule nchi nzima (wenzetu matajiri wanaweza) sisi turudi kule kule kwenye radio na TV. Tusiwanyime watoto haki ya kupata elimu.
  • Tuwe wabunifu kukabiliana na janga hili tusifuate tu yaliyomo vitabuni. Tuangalie mazingira yetu.
Kwa vile tumeamua Watanzania waendelee kufanya kazi na maisha yao basi na serikali iwapunguzie mazingira ya kupata maambukizi hayo. Tusije kudhani tunaweza kufunga uchumi wetu na watu wakabaki salama na nchi ikawa salama. Sasa hivi huko tunakokwenda hakuna msaada wa wajomba zetu wala wakubwa zetu maana na wenyewe kwao kunaungua. Ni lazima tujiangalie sisi wenyewe na ikibidi tutumie nafasi hii kutengeneza bidhaa ambazo zinahitajika zaidi sasa duniani na kutoa nafasi kwa wajasiriamali wetu nao kunufaika huku jamii zao na familia zao zikiwa salama.

Nilisema mwanzoni katika Makala ya kwanza kuwa tukisubiri mgonjwa wa kwanza tutakuwa tumechelewa; ni kweli tumechelewa lakini hatujachelewa sana. Bado tunaweza kudhibiti. Tusizidi kuchelewa mwisho tutashindwa kabisa. Tusiende kuomba kwenye makundi kama manabii wa Baal! Tutaangamia huku tunalia! Nilisema kwenye Makala ya pili ya Bahati Nasibu ya Magufuli. Hadi hivi sasa bado hajaliwa; inaonekana inalipa lakini ni lazima ilipe kwa watu vinginevyo Watanzania watalipa kwa machozi.

Tunapoenda kumwomba Mungu kwa siku hizi tatu; tutumie siku hizi tatu pia kuja na mikakati mikubwa inayoonesha kweli imani yetu kwa Mungu inatufundisha kuwa Mungu ametupa nafasi ya kudhibiti. Tusije kufikirie Mungu atashusha moto toka mbinguni na kuiteketeza korona! Labda ni jukumu letu sisi kutengeneza mifereji ya maji, na kumwagia maji halafu tuache Mungu awe Mungu. Tukumbuke kuwa huyu Mungu hana upendeleo na wala hajali sura za watu na wala hapokei rushwa! (Rumi 2:11).

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Mzee kuchelewa ni kuchelewa tu acha kuuma na kupulizia! Serikali ya CCM ilileta kiburi tangu mwanzoni hadi kule Bungeni wakamzomea Mchungaji Msigwa aliyeleta hoja ya kujadili issue ya Corona kama dharura. Nilianzisha thread hio.

Tukubali tulifanya makosa hatukutaka kuwasikiliza waliokuwa na mawazo tofauti na sisi, tukiamini hawana akili na hawana uwezo wa kutuelekeza cha kufanya! Leo tuko wapi? Kiburi chetu kiko wapi?

Again, I call upon CCM regime, tuunganishe nguvu, tuweke siasa kando, tuweke majivuno kando, tuweke ukabila kando, tuitishe ule umoja wa kitaifa! Tuwasikilize wengine pia na tuyaheshiimu na mawazo yao pia. Kwa pamoja tutaweza.
 
Tupewe siku 3 tena tuombee malaria itoweke pia maana magonjwa yapo mengi Tu sio corona pekee.
Maombi yetu hayawezi kufika mbinguni kwasabb mioyo yetu watanzania ina manung'uniko na magufuli
 
Mkuu hakuna cha zaidi.., cha maana ni kufuata maelekezo ya wataalamu, kuepuka misongamano na social distancing...., hayo mengine yote ni ya mtu kujipa matumaini kwa imani zake (iwe mizimu, waganga, ramli au dini)...

Na mwisho wa siku kitakachotutoa kwenye hili janga (au kitakachowatoa binadamu as a whole sababu some individuals huenda tukawa tumekufa)..., ni nguvu ya mwili ku-fight against foreign invaders (virus n.k.) na kitakachodetermine namba ya watakaokufa ni umahili na kuendelea kwa wanasayansi kukesha usiku na mchana wakitafuta kinga...
 
Formula ya kufanya Maombi ya kitaifa iko Wazi, samehe, sahau, tubu. Leo hii tunataka tufunge kwa ajili ya Corona wakati wananchi wamejaa majeraha mioyoni mwao? Wamepoteza ndugu, wameondoshwa kazini isivyo haki, hakuna salary increments na mengineyo!

Unataka Wafunge? Kweli? Wakifunga kweli tutaambulia laana Maana Mungu hadhihakiwi, hao wa kwenye Bible wote walikua kitu kimoja!

Hivi wale ambao ndugu zao wako mahabusu kwa makosa ya uonevu leo hii ukiwaambia Wafunge, watakuelewa? Si watabadilisha Maombi yawe ya kulaani?

Tutubu kwanza, twende mbele za Mungu tukiwa na mikono misafi! Tutubu kwa uongo, uonevu, usengenyaji na vifo vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine tumehusika na Mungu wa Mbinguni atasikia Maombi na mafungo yetu, kinyume na hayo tutajipalia mkaa mikononi mwetu. Take it from me. Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Kiongozi wetu wa nchi
 
Duh....kipendacho roho, hula nyama mbichi! Matatizo matatu makubwa: (1) Kiburi (2) Kiburi (3) Kiburi

Na hayo yakiendelea, tutalipwa ujira wetu sawa sawa.
 
Wewe jamaa hujielewi kabisa!
Naomba uniwie radhi kwa kusema kuwa kuingiza fikra za siasa za kivyama katika mada zinazohusu maisha ya ndugu zetu Watanzania na sie wenyewe ni upumbavu ulio pitiliza.
Na bahati mbaya sana tabia hiyo imebobea kwako. Jirekebishe, mwanaccm yeyote lazima ana nduguze walioko Chadema au CUF. Na mwana Chadema yeyote anao wajomba,baba au mama walio CCM na huwezi kuta wanaombeana mabaya kwa sababu ya mavyama yenu hayo. Wewe ni wa ulimwengu huu kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndio Kibwetere mwenyewe anayetajwa na Salary slip?
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Tunaweza kumwomba Mungu atusaidie kutuepusha na janga la ugonjwa wa korona. Kama binadamu na watu wenye imani tunaelewa wazi kuwa mwisho wa siku mambo yote yako mikononi mwa Mungu. Tunapojiachilia katika huruma na wema wake tunakiri uwezo na uwepo wake lakini pia tunakiri ubinadamu wetu. Kumwomba Mungu hakuwezi kuwa kosa. Nchi zote zilizoendelea ambazo nazo zimepigwa na majanga ya korona watu wake nao wanamwomba Mungu na kumlilia.

Kila siku hapa Marekani kuna watu wanakutana kwenye njia ya simu, Facetime, Skype na njia mbalimbali za mawasiliano kumwomba Mungu. Japo kwenye majimbo mengi ibada za hadhara zimesitishwa lakini siku ya Pasaka kwa mfano kwenye Jimbo Kuu Katoliki la Detroit Askofu Mkuu aliadhimisha Misa Takatifu akiwa na watu wachache tu kwenye Kanisa Kuu. Misa ile ilirushwa moja kwa moja na televisheni na kwenye Facebook na Youtube na sisi waumini tulifuatilia tukiwa majumbani mwetu. Mungu yupo mahali popote.

Kwa Wakristu kuna mstari unaosema kuwa “Wakutanapo wawili au watatu kwa Jina langu mimi nipo kati yao” (Mathayo 18:20). Mstari huu una maana kuwa uwepo wa Mungu katika ibada hauitaji wingi wa watu. Utendaji wake hauitaji mkusanyiko mkubwa wa watu. Katika maandiko tunakutana na mifano kadha wa kadha wa jinsi Mungu alivyoweza kutenda kwa kumtumia mtu mmoja au wawili tu au watu wachache lakini akafanya makubwa.

Mojawapo ya masimulizi makubwa yenye kusisimua katika Biblia ni kile kisa cha Elia Mtishbi. Baada ya watu wa Israeli kudanganywa na Manabii wa Baal, Elia akaamua kuwapa changamoto. Akawaambia kuwa yeye ni mtu mmoja tu aliyebakia akiwa ni Nabii wa BWANA na Baal alikuwa na “manabii” 450. Elia akataka kuwaonesha yupi ni Mungu wa kweli basi; yule mwenye Nabii mmoja aliyebakia au yule mwenye nabii 450 wenye mbwembwe nyingi. Simulizi hili linatuonesha kuwa Elia akawapa nafasi manabii wa Baali kumwomba Mungu wao atekekeze (aunguze) kwa moto sadaka walizoziandaa kwenye madhabahu.

Manabii wale 450 walianza kumwomba mungu Baal na kulia na kujichanja huku wakipiga kelele. Kwa kuwaangaliwa kwa nje unaweza kuamini walikuwa na imani zaidi, na kwa kelele na vilio vyao mungu wao angewasikiliza. Elia aliwadhihaki na kuwaambia labda waongeze sauti inawezekana mungu wao alikuwa amelala! Waliposhindwa ndipo Elia akaingia kazini yeye peke yake na bila sala ndefu tena katika jambo lisilowezekana (aliwaagiza waandalizi wake wamwagie maji zile sadaka mara tatu (alichimba na mfereji wa maji kuzizunguka kabisa). Na kwa sala fupi kabisa na yenye nguvu akamwita Yehova Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo. Alipomaliza tu sala yake na kabla ya kusema “Amina” Moto ulishuka toka mbinguni na kutetekeza sadaka zile na kuyakausha maji yale!

Ndipo watu wakajua kuwa Yehova ndiye Mungu. Unaweza kusoma kisa hiki kwenye 1 Wafalme 18:20-40.

Ndugu zangu, Rais Magufuli yuko sahihi kutaka Watanzania waliombee Taifa na hata bila yeye kutaka hivyo nina uhakika watu wenye imani wamekuwa wakiliinua taifa letu na watu wetu kwa dua na sala mbalimbali. Huu ni wajibu wetu; lakini siyo tu sisi dunia nzima inamlilia Mungu kumwomba. Hili haliwezi kuwa jambo baya wala la kudharau.

Na inawezekana Mungu ameshaanza kujibu sala na dua hizi. Mwanzoni mwa baa hili kulikuwa na hofu kuwa ugonjwa huu utaathiri zaidi Afrika labda kuliko bara nyingine lolote. Hata sasa maambukizi na vifo kwenye bara letu hayaendani na wingi na mtawanyiko wa watu wetu.

Pamoja na hayo bado Mungu anatupa nafasi ya kujiandaa zaidi. Haitoshi kumwomba Mungu na sisi bila kufanya au kuchukua hatua makini. Tayari taifa limechukua hatua mbalimbali ambazo naamini kwa kiasi kikubwa ni sahihi. Baadhi ya hatua zimechelewa sana na matokeo yake ndio tunaona maambukizi yakiongezeka badala ya kupungua. Na yameongezeka kwa haraka zaidi siku hizi za karibuni na tusipoangalia yanaweza kuongezeka zaidi ndani ya siku chache (kama tutafuata kama ilivyotokea nchi nyingine).

Lengo la Mikakati

Sasa hivi, lengo la mikakati yoyote inayochukuliwa na nchi ni kupunguza kasi ya maambukizi, kudhibiti wagonjwa wapya, na kuwalinda watu ambao bado hawajaambukizwa. Katika kupunguza kasi ya maambukizi ndipo panalala kazi kubwa ya kuidhibiti korona. Unaposoma habari mbalimbali duniani kwenye nchi zinazohangaika na ugonjwa huu sehemu kubwa ni kuwa kasi ya maambukizi mapya bado ni kubwa au ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba mifumo ya afya haikuweza kujiandaa nayo. Chukulia kwenye jimbo la Michigan ambako ninaishi.

Mgonjwa wa kwanza wa Corona alitangazwa Machi 10. Leo hii (mwezi mmoja na wiki moja baadaye) jimbo hili lina wagonjwa karibu 30,000 na vifo zaidi ya 2000! Na hapa ni pamoja na ukweli kuwa tumekuwa chini ya “lockdown” kwa karibu mwezi mzima! Watu wengi hawaendi kwenye makazini, michezo, hakuna ibada za hadhara n.k Na inadaiwa hatua zilizochukuliwa Michigan ni miongoni mwa hatua kali zaidi kuchukuliwa na jimbo lolote la Marekani.

Sasa, kama kwenye taifa hili lilioendelea hivi, lenye raslimali za kila namna watu wake wanaambukizwa kwa kasi hivi na kufa itakuwaje kwetu? Bila ya shaka kuna mambo (factors) ambazo zinafanya ugonjwa huu kuwa wa hatari zaidi kuliko nyumbani. Siyo kwamba watu wetu hawaupati ila inawezekana wanaupata kwa njia tofauti na labda kuna mambo ambayo bado hayajaeleweka vizuri kwanini haujaenea kwa kasi ile ile kama ilivyokuwa Hispania, Italia, Marekani, Uingereza, Ufaransa na China yenyewe ulikoanzia.

Kwa hiyo ni muhimu sana kuhakikisha kasi yake haiendi kwa kasi hivi. Binafsi nimeshtuka zaidi kuwa kwa siku mbili hizi idadi ya wagonjwa iliongezeka mara mbili. Nasubiria kuona namba mpya kutoka 88 zitatupeleka wapi. Kama ni kweli mtu mmoja aliyeambukizwa (ambaye hana dalili) anaweza kuambukiza karibu watu 40 basi namba yetu inaweza kuwa kubwa zaidi. Lakini pia kwa vile hata ambao hawaoneshi dalili baadaye wanaanza kuonesha dalili hizo basi wagonjwa wanaweza kuongezeka kwa kasi zaidi na kusumbua mifumo yetu ya afya.

Sasa tufanye nini?

Tayari hatua nyingi zilizochukuliwa zimesaidia lakini bado tunaona kuwa hata watu ambao wanatuambia tuchukua hatua wao wenyewe ni kama hawaelewi uzito wa janga hili na uwezekano wa tatizo hili kuendelea kwa muda. Nimesoma na kufuatilia maoni ya wadau mbalimbali na nimefuatilia hatua mbalimbali ambazo serikali imechukua hadi hivi sasa. Maoni yangu ni kuwa ni lazima tufikiri nje ya boksi; tufikirie nje ya boksi hilo kwa sababu mazingira yetu ni tofauti sana na nchi zilizoendelea. SIyo kwamba binadamu ni tofauti bali mazingira ni tofauti.

Hatuwezi Kuiga Yote Yanayofanywa na Nchi Tajiri

Mojawapo ya makosa makubwa ni wale wanaodhani kuwa wakiiga yanayofanyika hapa Marekani basi na sisi hali itakuwa hivyo hivyo. Mojawapo ya mapendekezo makubwa ni kuwa watu wanataka kila mtu akae nyumbani kwa angalau wiki mbili. Kwamba, tuiweke Tanzania nzima chini ya ‘lockdown’ kwa muda wa wiki mbili au zaidi. Hili ni rahisi kulisema kuliko kulifanya. Nitaeleza kwanini.
  • Nchi Tajiri zina uwezo wa kufunga nchi zao na wananchi wao bado wakawa salama. Hapa Marekani mojawapo ya hatua ambazo serikali imechukua kufanya maisha yawe rahisi kidogo ni kutoa fedha taslimu kwa raia wake wote (wenye kustahili). Kila mtu anapewa dola 1200 na mtoto anapewa dola 500. Huu ni mchango wa mara moja na unatarajiwa kurudiwa tena.
  • Mfumo wao wa mafao ye kukosa ajira (unemployment benefits) kwa kawaida ulikuwa unatoa karibu dola 360 hivi kwa kila mtu kwa wiki angalau 26. Lakini sasa hivi wameongeza dola 600 juu ya hilo. Hivyo, licha ya kupewa zile dola 1200 bado mtu aliyeomba fao la kukosa ajira atapata pia dola karibu 900 kila wiki kwa wiki angalau 26! Hii ni sawa na dola 24, 000 hivi kwa miezi sita!
  • Serikali imetoa pia mafao ya kusaidia biashara ndogo ndogo ambapo walipitisha kiasi cha dola bilioni 350 katika raundi hii ya kwanza. Fedha hizi makampuni yaliyoomba kama mkopo unaoweza kusamehewa inadaiwa kufikia jina zilikuwa zimeshakwisha na hakuna aliyepata kiasi chote alichoomba! Sasa hivi wanafikiria kuongeza kiasi cha fedha tena; sitashangaa kama haitofikia dola trilioni 1 ya kusisimua uchumi!
  • Kwa makampuni makubwa kuna fedha nyingi zaidi ambazo zinaenda kutolewa ili kusaidia yasianguke na kusababisha hali ya uchumi ambayo sasa ni mbaya kuwa mbaya zaidi.
  • Mataifa haya Makubwa yana mfumo mkubwa wa mahospitali ambayo yameongezewa uwezo mkubwa zaidi ikiwemo vifaa n.k.
  • Matumizi ya jeshi katika kusaidia kuongeza uwezo wa hospitali na vituo vya afya. Tumeona hili China na Marekani na nchi nyingine ambapo majeshi yao yameenda kuongeza nguvu kwenye taasisi za kiraia. Marekani kwa mfano Brigedi ya Uhandisi (Army Corps of Engineers) ambayo ndio msimamizi mkubwa wa ujenzi unashirikiana kujenga hospitali za medani (field hospitals) kwa haraka na kuwapa uwezo hospitali ambazo zimezidiwa wagonjwa.
Hiyo ni mifano michache tu ya kuonesha ni jinsi gani hatuwezi kumuiga tembo kwa kila kitu vinginevyo tutapasuka msamba. Na wazo la kuifunga nchi nzima kwa wiki hata tatu tu ni wazo linalohitaji kufikiriwa vizuri zaidi. Naamini katika hili Magufuli yuko sahihi. Hata hivyo, naamini kuna mambo mengine tunaweza kuyafanya.
  • Kwa vile virusi hivi vinaenezwa kwa haraka katika mikusanyiko mikubwa ya watu hasa kwa vile virusi vya koronoa vinaweza kukaa hewani kwa angalau dakika kadhaa kiasi kwamba mtu anaweza kupiga chafya akaondoka na mtu mwingine akapita pale pale na kupumua hewa ile. Haitoshi basi kukaa mita moja tu; tupunguze kabisa mikusanyiko. Makanisa na Misikiti yatangaze kusitisha ibada zao kwa angalau wiki mbili au tatu. Hii itapunguza kusambaa kwa haraka maana hadi hivi sasa hii ndio mikusanyiko mikubwa zaidi inayofanyika nchini. Watu wasali kama Elia Mtishbi! Uamuzi wa kusitisha ibada za hadhara si wa serikali ni wa taasisi za dini.
  • Ni wakati wa JWTZ kushiriki moja kwa moja kwenye kudhibiti wagonjwa na wale wanaofuatiliwa. Tuna kambi za jeshi nchi nzima, wakati umefika kwenye hizi kambi jeshi litengeneze “field hospitals” au kambi za mahema kwa ajili ya kuwahifadhi wale ambao wamekuwa karibu na watu wenye korona ili kuwaangalia kwa karibu na kukata uwezekano wa kuambukiza jamii. Wakati wasafiri tunawaweka karantini kwa sababu hatujui kama wameshaambukizwa au wamekutana na mtu mwenye ugonjwa ni vizuri familia za wagonjwa 88 na wale watu wao wa karibu waangaliwe kwenye kambi hizi za kijeshi ukizingatia pendekezo la tatu. Hadi hivi sasa hatujaona kuhusika kwa jeshi kunakofaa na kutosha.
  • Serikali badala ya kutoa mabilioni ya hela kwa kila mtu huku wakikaa nyumbani itenge kiasi cha fedha kwa ajili ya kuzilisha na kuhudumia familia ambazo zitakuwa kwenye uangalizi wa siku kumi na nne. Naamini hiki kitakuwa ni kiasi kidogo sana kulinganisha na gharama ya kuifunga nchi nzima. Uthubutu wa Rais Magufuli kujenga SGR, Nyerere Hydropower Dam na mengine unatudokeza kuwa hatosita kutenga kiasi cha fedha kwa jambo kama hili itakapolazimu na ninaamini inalazimu sasa. Jeshi na Mageresha (ambayo yapo kila wilaya na mkoa) wanaweza kutumika kuandaa vyakula na mahitaji mengine kwa familia hizi.
  • Wakati huo huo tuongeze uwezo wa kupima, kutenga/karantini na kutibu na kufuatilia maambukizi. Hii ndio kubwa ya kudhibiti. Bila kupima na kutenga itakuwa vigumu sana. Hatuwezi kuwaweka watu wote mahospitali, hizi nchi kubwa tu hazijaweza sisi inatubidi tufikirie nje ya hilo.
  • Kwa vile watoto wako majumbani badala ya mashuleni, Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Wizara ya Sayansi na Teknolojia na ile ya Mawasiliano (na nyingine husika) wafikirie namba ya kuanza kutoa masomo kwa njia ya radio na televisheni kwa ajili ya watoto. Vipindi vya TV na Radio viangaliwe ili watoto wasikae nyumbani tu. Hatuwezi kugawa laptop na kutoa elimu kwa kila shule nchi nzima (wenzetu matajiri wanaweza) sisi turudi kule kule kwenye radio na TV. Tusiwanyime watoto haki ya kupata elimu.
  • Tuwe wabunifu kukabiliana na janga hili tusifuate tu yaliyomo vitabuni. Tuangalie mazingira yetu.
Kwa vile tumeamua Watanzania waendelee kufanya kazi na maisha yao basi na serikali iwapunguzie mazingira ya kupata maambukizi hayo. Tusije kudhani tunaweza kufunga uchumi wetu na watu wakabaki salama na nchi ikawa salama. Sasa hivi huko tunakokwenda hakuna msaada wa wajomba zetu wala wakubwa zetu maana na wenyewe kwao kunaungua. Ni lazima tujiangalie sisi wenyewe na ikibidi tutumie nafasi hii kutengeneza bidhaa ambazo zinahitajika zaidi sasa duniani na kutoa nafasi kwa wajasiriamali wetu nao kunufaika huku jamii zao na familia zao zikiwa salama.

Nilisema mwanzoni katika Makala ya kwanza kuwa tukisubiri mgonjwa wa kwanza tutakuwa tumechelewa; ni kweli tumechelewa lakini hatujachelewa sana. Bado tunaweza kudhibiti. Tusizidi kuchelewa mwisho tutashindwa kabisa. Tusiende kuomba kwenye makundi kama manabii wa Baal! Tutaangamia huku tunalia! Nilisema kwenye Makala ya pili ya Bahati Nasibu ya Magufuli. Hadi hivi sasa bado hajaliwa; inaonekana inalipa lakini ni lazima ilipe kwa watu vinginevyo Watanzania watalipa kwa machozi.

Tunapoenda kumwomba Mungu kwa siku hizi tatu; tutumie siku hizi tatu pia kuja na mikakati mikubwa inayoonesha kweli imani yetu kwa Mungu inatufundisha kuwa Mungu ametupa nafasi ya kudhibiti. Tusije kufikirie Mungu atashusha moto toka mbinguni na kuiteketeza korona! Labda ni jukumu letu sisi kutengeneza mifereji ya maji, na kumwagia maji halafu tuache Mungu awe Mungu. Tukumbuke kuwa huyu Mungu hana upendeleo na wala hajali sura za watu na wala hapokei rushwa! (Rumi 2:11).

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

TUSITISHANE WE MZEE.......tuache tuchape kazi, iwe kariakoo, feri, rangi tatu sie sio wavivu.
 
Mkuu umeandika porojo nyingi,sisi tunajijua ni hohehahe,huu uhohehahe wetu haujaanza ghafla,tumekuwa nao toka Uhuru.Serikali yenu ya awamu ya tano ikaona kuwekeza kwenye uongo na kiburi ndo itaonekana ni serikali special na inayoongozwa na kiongozi makini,mchapakazi na mwenye akili nyingi.kumbe walikuwa wanajidanganya wenyewe.Kwa kuwa tunajijua uhohehahe wetu ,tuliiomba serikali yetu ifunge mipaka ili tujaribu kuzuia huu ugonjwa usiingie nchini,serikali ikasema haiwezi ziwia watalii,baada ya ugonjwa kuingia nchini watu wakaomba ifungwe Dar wakiamini ni rahisi kuhudumia wakazi milioni tano sita wa Dar kuliko kuhudumia watanzania wote zaidi ya milioni 55,serikali bado ikagoma .Hii serikali lengo lake ni kuwa toa kafara watanzania and nothing ease.Acha tuombe Kama walivyotutaka but nahakika nao watafyekelewa mbali na hii corona
 
Na. M. M. Mwanakijiji
Kwa Wakristu kuna mstari unaosema kuwa “Wakutanapo wawili au watatu kwa Jina langu mimi nipo kati yao” (Mathayo 18:20). Mstari huu una maana kuwa uwepo wa Mungu katika ibada hauitaji wingi wa watu. Utendaji wake hauitaji mkusanyiko mkubwa wa watu.
Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Naunga mkono hoja
Mungu ni Omnipresent. Kufuatia Local Transmission ya Corona. Je, Sasa Tushinikize Watu Wasalie Majumbani Mwao, ila Sadaka Ndio Itumwe Kwa M-Pesa? - JamiiForums
P
 
Back
Top Bottom