Kwanini Mramba, na si Chenge, Lowassa, Tibaijuka na Muhongo?

Kwanini Mramba, na si Chenge, Lowassa, Tibaijuka na Muhongo?

Mimi sio ccm, lakini kuna wakati tuwe wakweli. Kwani muhongo ameiba nini? Au tibaijuka? Chenge, ngeleja sawa. Lakini hawa wawili ni nini? Maana muhongo hakutajwa popote, tibaijuka aliomba hela na akaikabidhi bodi ya shule

Jitahidi kuwa na uelewa mpana na kujua Mramba na Yona wamehukumiwa kwa kosa gani, hawa watu wamehukumiwa kwa kosa la kuisababishia hasara Serikali kwa kuruhusu misamaha ya Kodi je hawa waliohusika na masakata ya EPA, RADA,MEREMETA,KAGODA,RICHMOND na ESCROW wewe kama wewe unawaweka kundi gani? kwa nini hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa kuwatia hatiani? na cha ajabu wale wa EPA rais mwenyewe alitamka hadharani kuwa warudishe hizo fedha ingawa hatujui kama walirudisha na ni akina nani na je kwa nini Rais aliwaficha hawa watu na hawakutajwa hadharani?

 
Kwanza nieleweke mapema, kwamba siikosoi mahakama. Ila naweka mawazo yangu tu,ambayo katiba imeniruhusu kuwa huru kwayo

Nasema,kwa Daniel Yona,may be. . . Lakini kwa Mramba, nasikitika

Ktk utetezi wake, Mramba aliwahi sema,kwamba yeye,hakudharau ushauri wa TRA on Alex Stuat deal (hope nime spell vzr jina) alilipeleka swala husika mbele ya Cabinet

Na maamuzi juu ya swala hilo,yalitoka kwa Cabinet nzima. So kama ni dharau kwa ushauri wa TRA, iliyofanya dharau hiyo, ni Cabinet nzima

Ningeambiwa Mramba anaingia hatiani kwa kumshauri vibaya M/kiti wa Baraza la Mawaziri(ambae ni rais mwenyewe)hapo tungekuwa pamoja coz pengine alimshawishi mno President, kufanya maamuzi,ambayo President aliyaamini kwa kuaminishwa na Waziri wake kwamba yalikuwa sahihi

Either ways, congrats Mahakama kwa kuthubutu. Mmetuonyesha,kwamba kumbe hakuna mwenye exemption mbele ya sheria
 
1. Hii ni siasa ya uchaguzi wa rais 2015, not unexpected, inayomwonyesha Kikwete kama mpiga vita rushwa. Kwa upande wa pili ni kujaribu kumnyima ujasiri Ben Mkapa kumtetea mtu anayeamini anafaa kati ya wagombea waliojitokeza. Plan was kumtusi Mkapa left and right azire zoezi zima la kuchagua rais na yeye alijua hilo na kuchukua tahadhari. Hongera Ben kwa kuamua kutokuwa na roho ya kuku na kuamua kushiriki kwa maslahi ya Chama.

2. Zoezi hili la kufungwa ilikuwa limkumbe pia Prof. Costa Mahalu. Mungu wake kamwepushia kikombe. Wanaopigwa ni watu waliokuwa karibu na Ben Mkapa. Mambo yalivyo, hata Sumaye itamwathiri negatively katika urais huu. Ni mchezo wa aina ya siasa za Kikwete. Lakini kuna Mungu na kuna mwisho.

3. Niseme wala simtetei Mramba wala Yona, hata kidogo, wangestahili hata zaidi ya adhabu waliyopewa, ila nasema kuwe na fairness... Wezi wote wapate deserving treatment! Wawili hawa pamoja na Ben na Sumaye waliuza nmb kwa nguvu NMB na kuvunja board yake kwa madharau na kejeli. Walioathirika walimgeukia Mungu na jana amewajibia. Tujifunze kwamba mtetezi wa masikini wa Tanzania (kama NMB ilivyokuwa ya masikini) Mungu yuko kazini. Aibu gani hiyo sasa kwa Mramba na Yona? Isingewezekana mpate dunia nzima kama mlivyojaribu. Poleni lakini, tunajua kifungo ni kitu kibaya kwa mwanadamu lakini mjitathmini na wengine tujifunze. Poleni wanafamilia. Natambua madhali ya kuondokewa na Baba katika familia.
 
Kwanza kesi yenyewe imechukua muda mrefu sana, miaka 9! Halafu adhabu kiduchu.
Kwa mtu aliyewahi kushika nyadhifa za juu kama waziri, kufungwa miaka 3 ni mingi sana. Sema tu wengine hamjafika jela. Mtu kazoea kuendeshwa kwenye vx na kiyoyozi ndani, nyumba nzuri na kiyoyozi, nyumba ndogo za maana, halafu leo unanyea debe? Wee acha tu.
 
Kila siku watu wanalalalmika humu kuwa huko magerezani wamejaa wezi wa kuku lakini vigogo wanalindana; vigogo wanaposwekwa lupango pia wako wengine wanawaonea huruma kana vile hayo mabilioni wanayoiba huwa wanawagawia!!! Mramba ilibidi afungwe ili laana ya kuwaambia wananchi wale majani ihitimishwe!! Sasa yeye anakwenda kunyea ndoo hata akijapata msamaha atakuwa amenyooka.
Apewe msamaha na nani? Unajuwa december 9 tutakuwa na rais.
 
Kwa mtu aliyewahi kushika nyadhifa za juu kama waziri, kufungwa miaka 3 ni mingi sana. Sema tu wengine hamjafika jela. Mtu kazoea kuendeshwa kwenye vx na kiyoyozi ndani, nyumba nzuri na kiyoyozi, nyumba ndogo za maana, halafu leo unanyea debe? Wee acha tu.
Ndiyo maana yule mama alilia sana! Polisi wakamuonea huruma wakampa mramba kiti cha ofisini akalie. Mbona lipumba walimyima?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom