Kwanini Mramba, na si Chenge, Lowassa, Tibaijuka na Muhongo?

Kwanini Mramba, na si Chenge, Lowassa, Tibaijuka na Muhongo?

Kila siku watu wanalalalmika humu kuwa huko magerezani wamejaa wezi wa kuku lakini vigogo wanalindana; vigogo wanaposwekwa lupango pia wako wengine wanawaonea huruma kana vile hayo mabilioni wanayoiba huwa wanawagawia!!! Mramba ilibidi afungwe ili laana ya kuwaambia wananchi wale majani ihitimishwe!! Sasa yeye anakwenda kunyea ndoo hata akijapata msamaha atakuwa amenyooka.

Nilitegemea hukumu ilingane na muda wa miaka 8 tangu kesi ianze kuunguruma. Kwa mantic hiyo, kama kesi imekaa miaka 8 ndo imekwisha tar.06.7.2015 basi hukumu ilalie pale lupango miaka 8. Hakuna uwiano kabisa, sheria gani hizi.
 
Walioiba fedha za EPA walikamatwa wakawekwa mahabusu KEKO na hatimaye wakaachiwa! Wengine waliambiwa kuwa warudishe tu yakaisha. Naona Mramba na Yona wangeambiwa nao warudishe halafu yaishe. Si wote walichota toka serikalini?
 
Kibo10

hamuishi kutapatapa angeachiwa mngesema kafungwa mnasema sasa mnataka nini kama sio gubu kukuzidi we mtu.
TAKUKURU wamefanya kazi yao mmezoea kusema wanafunga vidagaa haya sasa papa huyo bado midomu juu sasa.
wewe sema ulitaka hii kesi iisheje .
jipange wewe
 
Last edited by a moderator:
Kibo10

Hawa hawawezi walikula ya mbuzi wakaota mapembe, bado kula ya mbogo wawe wanaturarua kila kuchapo.
 
Last edited by a moderator:
Watu wa kaskazini hasa wachagga tumekiona cha moto utawala huu wa Kikwete.

na alhamisi na ijumaa wana arusha " wamasai " mtakiona cha moto " tena kutoka kwa huyo huyo mkwere na mpaka anamaliza mtamkoma!
 
Jiulize mafisadi Idris Rashid, Mustafa Mkulo, Juma Kapuya na Ramadhan Dau hawaguswi

wengine kama wawili watatu hapo katika kikosi chako hicho "magonjwa" yao tu yanayowakabili ni "vifungo" tosha kwao kwani wanataabika mno.
 
Kwanza kesi yenyewe imechukua muda mrefu sana, miaka 9! Halafu adhabu kiduchu.

walikuwa wanaacha kwanza ili wamalize kuweka mambo sawa katika familia zao ili wao wakienda "korokoroni" basi wasitaabike kimaisha bongo.
 
Ramadhani Dau anastahili kupandishwa kizimbani kwa kosa la kutumia madaraka vibaya na kuifilisi NSSF!!! Nashangaa katika orodha ya yule YUDA Escariot ya wenye fedha nje ya nchi majina ya Chenge na Idris Rashid hayamo ili hali waingereza walizifichua account zao !!!! Zitto ni mnafiki na sio mkweli!

ni " mzito " hadi " kufikiri " kama lilivyo jina lake.
 
issue tunataka watu wajue ccm inapambana na ufisadi. Hiki ni kiini macho, na wameamua kuwatoa kafara kipindi hiki cha uchaguzi. Ni zuga tu na kuwahadaa watz.

100% precisely.
 
ccm ni zaidi ya uijuavyo....
Maajabu mengi yanaanzia tanzania. Labda ndio maana inaaminika hata binadamu wa kwanza aliishi tz kwani fuvu la binadamu wa kale kabisa liligunduliwa huku.
Baada ya miezi michache tutasikia wamebadirishiwa adhabu badala ya kuwa kifungo cha ndani watapewa kifungo cha nje!!!
HII INAWEZA KUWA HADAA YA CCM KWA AJIRI TU YA KUFANYIA KAMPENI KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI!!!
 
Kibo10

CCM ni zaidi ya uijuavyo mbona umeenda mbali sana?Vipi kina Werema ambao ni hivi majuzi tu waliingiza taifa ktk janga?Ukiwa na uswahiba na bwana mkubwa hutaguswa.

 
Last edited by a moderator:
Kwa afya aliyonayo lowasa sidhani km anaweza hata kukaa jera kwa angalau wiki moja. Mwacheni kwanza awaneemeshe watz kwa kurudisha kidogo pesa alizoiba ambazo anagawa km pipi
 
Kibo10

wewe ni mnafiki na inawezekana unatokea kasikazini ,na sikunhizi mumezidi kwa unafiki mkiongozwa na mengi wenu,
wangeachiwa mgesema wameshidwa,wamewachukulia hatua mnalalamika,tuwaeleweje?
 
Last edited by a moderator:
Kwa afya aliyonayo lowasa sidhani km anaweza hata kukaa jera kwa angalau wiki moja. Mwacheni kwanza awaneemeshe watz kwa kurudisha kidogo pesa alizoiba ambazo anagawa km pipi

najua wanalalamika watu wa kule kule walitaka waachiwe ili wapoke kama mashuja na mbwebwe nyingi maana ndo kawaida yao si uliona wakati wa mamvi alivyopokelewa,
 
hamuishi kutapatapa angeachiwa mngesema kafungwa mnasema sasa mnataka nini kama sio gubu kukuzidi we mtu.
TAKUKURU wamefanya kazi yao mmezoea kusema wanafunga vidagaa haya sasa papa huyo bado midomu juu sasa.
wewe sema ulitaka hii kesi iisheje .
jipange wewe
heko takukuru kwa kumaliza vitendo vya rushwa nchini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom