Kwanini Kikwete hakusimama na Lowassa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Kikwete hakusimama na Lowassa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 24, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kwanza ilikuwa ni Rais Bush na Michael Brown kule Lousianna wakati wa Katrina. Wakati kelele zinapigwa za kutaka kichwa cha Brown (mkuu wa FEMA) Bush alifunga safari kujionea na kwa jinsi anavyojua yeye alisimama mbele ya waandishi wa habari na kusema yale maneno ambayo yamebakia kama mwangwi "Brown you are doing a heck of a job".

  Bush alisimama na mtu wake aliyemteua licha ya kelele..

  Sasa wiki ile iliyopita hata leo hii kumekuwa na kelele za kutaka Waziri wa Fedha wa Marekani Bw. Geithner kujiuzulu. Mara tatu sasa Rais Obama amejitokeza pasipo woga kumtetea mteule wake na kusimama naye na kusema kama kuna mtu anataka wa kumlaumu basi wamlaumu yeye na kamwambia hata akileta barua ya kujizulu hatoikubali (basically asijisumbue).

  Obama amesimama na mtu wake aliyemteua!

  Ndiposa, nikabakia kujiuliza.. nini kilitokea Februari ile? Kwanini Kikwete hakusimama na mteule wake na kukubali kubeba lawama zote za Richmond yeye mwenyewe? Kwanini hakusimama na Karamagi, Chenge (ya Chenge labda haifai!) au Msabaha?

  Je kila watu walio chini yake wakilaumiwa yeye atawatosa tu? NI lini atakubali kubeba lawama na kusema kuwa "mnilaumu mimi"? Je yawezekana tunu hiyo ya kukubali kubeba mzigo kama kiongozi Rais wetu hana na badala yake ni bora watu watoswe ilimradi yeye anaendelea kuonekana ni msafi? Je kuna siku atasimama kuwatetea watu aliowateua au atawaacha wamomonyoke na hivyo kuthibitisha ni jinsi gani asivyo mwangalifu katika uteuzi (maana anashindwa hata kuwatetea!)!

  Ninaamini, hakuna wakati ambapo Kikwete alionesha udhaifu mkubwa kama kiongozi kama kushindwa kusimama na Waziri wake Mkuu au kupanga naye mkakati wa kujibu mashambulizi ya Bunge. Ndiyo maana ninaamini Lowassa hana sababu ya kumlaumu mtu mwingine yoyote (siyo Spika, CCM au Mwakyembe) kwa kujiuzulu kwake bali mtu mmoja tu ambaye alishindwa kuchukua msimamo mgumu!

  Lakini labda alijua maji yamemwagika? Je kama JK angesimama na Lowassa na kukubali uchafu na lawama zote za Richmond (as a matter of fact nakumbuka mkutano wake na waandishi wa habari nadhani alistahili kuubeba mzigo huo!).

  Kama mtu ukiteuliwa na Kikwete jua jambo moja.. you are on your own!!
   
 2. u

  urassa Member

  #2
  Mar 24, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu kiongozi yoyote yule lazima awe na strong elements zake za kuwa objective,hatupaswi kutetea wezi bali kukaa na kuongea ni lazima.
  Natumaini JK alikuwa na muda wa kuhold na kufuatilia hizo tuhuma kabla ya kuruhusu kuachia ngazi kwa PM wake.
   
 3. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Mwanakijiji kumbuka jambo moja muhimu sana,Kikwete asingeweza kugagamara na Lowasa ili abebe yeye lawama,kwani Lowasa ndiye aliyemwezesha kuingia Ikulu.Tena kabla mambo hayajapendeza tulimtonya pale Maelezo vipi huyo rafiki yako tumesikia utampa nafasi nzito katika serikali yako,Unajua alijibu nini,"Kwani kuna ubaya gani kama anazo sifa?"Kwa hiyo Kikwete alijua strength za EL kwamba alikuwa hata na uwezo wa kumu-over shadow huyu Kiranja Mkuu,Lakini sasa afanyeje?Kama siyo kumtosa?Kulikuwa na ukweli usopingika kabisa kwamba Bwana EL alikuwa na uwezo mkubwa wa maamuzi kuliko mwenyewe JK.Hata baada ya kumtosa amebakia kutapatapa tu bila kuwa na hoja kwani hajui EL anajipanga kumfanya nini.
   
 4. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Inzi wako kiboko... baada ya kumchafua Mh. Lowassa sasa anageuka kwa Mh. Rais... Endelea na vita yako mkuu ya kufanya nini tena? Hebu nikumbushe!!!
   
 5. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Aliogopa nguvu ya Bunge! Aliona alama ukutani na kama angesimama naye basi Bunge lingevunjwa, hivyo alimshauri kujiuzulu kwanza naye atalimalizia akiamini Idrisa atafanza kumalizia mpira wavuni kimyakimya na deni litakuwa limekwisha kiulaini halafu kifuatacho ingekuwa/itakuwa EL anasafishwa kwa nguvu zoooooote mpaka kusafishika na baadaye anateuliwa ubalozi Omaniiiiiii katika awamu ya lala salama
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  kwa nature ya taifa hili na sakata lenyewe asingeweza jk kusiama NA ELtatizo la JK ni kwamba kuna wakati huwa hafirii mbali(he cannot think beyond the next meal!!!)
  sasa ikitokea mtu wake aliyedhani anafaa akifanya madudu, Jk hukwepa lawama na kumtosa.tatizo ambalo humsumbua sana badae.
  kikubwa aache kusikiliza maneno ya watu, kuna watu wanamshauri vibaya sana, kama ambavyo aliwahi kukiri siku moja wakati anahojiwa na mwandishi mashuhuri wa sauti ta Amerika(shaka Sali), juu ya kumbadili msabaha alipokuwa waziri wa nishati na madini na kumfukuza kazi yule jamaa wa wizara ya elimu, JK alikiri kusikiliza maneno ya watu!!

  siku hz nakumbuka maneno ya baba yangu alisema (2005) kuwa huyu rais (JK) aliyechaguluwa nchi itamshinda maana ni Mtu wa fadhila.
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  53.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu
  atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.
  (2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya
  Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya
  Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu,
  watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli
  za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
  53A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 51 ya Katiba hii,
  Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na
  Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo na
  ikapitishwa kwa mujibuwa wa masharti ya ibara hii.
  (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
  yoyote ya kutaka kupitisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri
  Mkuu haitatolewa Bungeni endapo-
  (a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya Waziri
  Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 52 ya Katiba hii, wala
  hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja Sheria
  ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
  (b) haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa;
  (c) haijapita miezi tisa tangu hoja ya namna hiyo
  ilipotolewa Bungeni na Bunge likakataa kuipitisha.
  (3) Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu
  haitapitishwa na Bunge isipokuwa tu kama-
  (a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa
  mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
  Wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku angalau kumi
  na nne kabla ya siku inapokusudiwa kuwasilishwa
  Bungeni;
  (b) Spika atajiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili
  ya kuleta hoja yametimizwa.
  (4) Hoja iliyotimiza masharti ya ibara hii itawasilishwa Bungeni
  mapema iwezekanavyo kwa mujibu wa Kanuni za Bunge.
  (5) Hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa tu
  iwapo inaungwa mkono na Wabunge walio wengi.
  (6) Endapo hoja ya kura ya kutokuwa na imani kwa Waziri
  Mkuu itaungwa mkono na Wabunge wengi, Spika atawasilisha
  azimio hilo kwa Rais, na mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote
  vile ndani ya siku mbili tangu Bunge lilipopitisha azimio la hoja ya
  kura ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu
  atatakiwa ajiuzulu, na Rais atamteua Mbunge mwingine kuwa
  Waziri Mkuu.
   
 8. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  JK hakuweza na asingeweza kumtetea EL, NK wala IM katika sakata lile la RDC. Asingeweza kufanya hivyo kwasababu kashfa ile ilikuwa imeshaharibika sana mpaka ilipofikia kujadiliwa na Bunge. Na alieiharibu ni EL na kundi lake.

  Katika siasa za TZ, ukikosea kidogo tu katika kuchukua hatua, basi ni bora ijitenge na hatua zinazofuata ama ujitwike msalaba na kuanguka nao (uamuzi mbaya).

  EL alishaamini kuwa ameliweka Bunge zima (lililojaa wana CCM) katika hali ambayo isingeweza kujadili issues kama za Richmond. Alikuwa akiwakanya mara kwa mara kutojadili issue hizo na ilielekea kuwa waBunge walishakubali kuachana nayo. Hivyo, inawezekana kuwa alishamhakikishia Rais kuwa issue hiyo iko ndani ya uwezo wake. Ilipokuwa imefikia pabaya, Rais hakuona jinsi anavyoweza kujishughulisha nayo tena, kwani ingemgharimu sana kisiasa. Hivyo alimwachia afe nayo.

  Wakati mwingine kiongozi inabidi achukue maamuzi magumu kwa manufaa yake mwenyewe, taasisi anayoiongoza na wadau wengine. Kwa vyovyote vile, JK angejiingiza katika kutetea Mawaziri wake (katika kashfa ya RDC) hasa baada ya ushahidi wa kutosha kabisa kuthibitisha upotofu wa maadili, harufu ya rushwa na uvunjaji wa sheria angekuwa amejiingiza kwenye jambo la hatari sana na sijui leo tungekuwa tunaongea nini. Historia ya nchi hii ingeweza kuwa tofauti kabisa sasa. Si ajabu kwa mara ya kwanza Bunge lingevunjwa na maana ya hilo ni kuingia kwenye uchaguzi mpya wa Rais, Wabunge na madiwani.

  JK huwa ana tabia ya kuachia wateule wake ku-clean their mess. Sidhani kuwaa hiyo ni tabia mbaya. Ninaamini kuwa kila mtu akijenga tabia ya kusafisha maovu yake mwenyewe, tutakuwa makini katika matendo yetu. Kila uzembe una gharama yake. Uzembe wa mawaziri kwenye RDC uliwataka wao wemnyewe kuingia gharama zote zilizojitokeza. Wakitetewa kila mara watabweteka.
   
 9. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu msim-underestimate sana huyu mheshimiwa, anajua sana anachokifanya. Msisahau kabisa kuwa kulikuwa na mkakati wa nini kifanyike hadi yeye kuchukua ofisi. Mambo mengi hapo katikati yamefanyika.... EL hakuibuliwa tu hivi hivi kupewa u-PM. Kazi aliyoifanya kumwezesha mheshimiwa kufika pale inajulikana na lazima mzee angetoa hiyo fadhila. Ishu inakuwa kwamba, mahusiano yao ni ya kirafiki zaidi kuliko kazi, tena urafiki wa kijambazi. Nikiiba leo nikakuletea, kesho nikiiba kwa ajili yangu utanikemea je? Si lazima nitakuuliza mbona jana ulipokea na hukusema? Katika mazingira kama hayo ni vigumu mkuu kumchukulia mtu yeyote hatua maana yey pia sio msafi. Ndio maana ukipewa kazi na JK lolote likikutokea lazima uweze kupambana nalo mwenyewe na likikushinda uamue tu mwenyewe kuachia ngazi. Yeye hatakubebea mzigo wako na wala hatakutosa. lolote litakalokutokea, bado mtabaki marafiki maana yote uliamua mwenyewe - so huwezi kumlaumu directly!

  Kumtetea na kusimama na mteule wako inataka courage sana na hiyo itatokea tu iwapo kulikuwa na objectivity katika process nzima ya uteuzi. Hebu jiulize, kama tungekuwa na utaratibu wa bunge kupigia kura wateule wa raisi kabla hawajawa confirmed kwenye nafasi zao, ni wangapi wangekubalika??

  Kwa vile kwa wenzetu (Marekani) hakuna ugoro uliopo hapa, raisi ana uhakika akisimama na mtu wake hatam-let down wala watu hawatafikiri kuwa anamlinda kwa sababu binafsi. maana hazipo anyway. Hapa ukimlinda hivyo tukikupekua tutagundua alishiriki kuibia nchi ili kukuwezesha kupata uraisi, nyote mtakuwa matatani. So he'll never do it to anyone!!!
   
 10. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tanzania inahitaji utaratibu huo. Utaratibu wa wateule wa nafasi za juu nchini ni vyema ukawa unathibitishwa na Bunge (baada ya mjadala mrefu na kwa uhuru na busara zote). Hii ingeweza kuweka mising imara zaidi ya utawala bora. Kwa sasa Rais anaamua tu kubadilisha Baraza lake la Mawaziri kama anavyopenda na kuweka mtu yeyote kuwa Waziri bila kulazimika kujali maslahi ya Taifa. Viongozi hao ambao huwa na mamlaka ya kufanya maamuzi makubwa kwa Taifa, ni vyema wakawa wanaangaliwa kwa makini zaidi.

  Bunge pia linatakiwa kuwa na muda wa kutosha kujadili hoja za teuzi kuanzia wa PM (mbona muda hutosha kujadili Miswada, bajeti na mengineyo?), badala ya sasa ambapo jina likipendekezwa tu, wanaanza kupiga kura na hatimaye kutoa pongezi ambazo nyingi ni za uongo uongo tu ili kujiweka vizuri na muheshimiwa PM mpya kwa maslahi binafsi. Kama wangepata muda wa kujadili kabla, wangeweza kujiridhisha uwa uteuzi huo unafaa na ni wa maslahi ya Taifa na kuunga mkono kwa sababu za msingi zinazokuwa zimatolewa Bungeni.

  Ni lazima tubadilike kama tunataka kuendelea kwa kasi hasa tukizingatia tupo nyuma sana (kwa matakwa yetu wenyewe).
   
 11. A

  AMETHYST Senior Member

  #11
  Mar 24, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi nakubaliana na kuwa JK kumtetea Lowassa angefanya uamuzi mbovu kuliko hata hii zuga zuga anayofanya kwa sasa. Japo maswali magumu sana kujibu,Je Lowassa anamchukuliaje mshirika wake kwa sasa!
  (1) Ana kinyongo naye? na hivyo ana mpango wa kujibu mapigo kunako 2010
  (2) Bado wanawasiliana kirafiki zaidi na wana mipango ya baada ya 2010 kisiasa?
  (3) Amekubali yaishe kuwa nilivurunda mwenyewe na hana kinyongo na mkulu wa kaya?
   
 12. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa nini asimame nae. Ukijishika na mchafu nawe utachafuka na ingekuwa tatizo kwa serikali na taifa kwa ujumla. Mwache Edo afe nalo zigo lake
   
 13. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Amethyst; a, b na c yote sahihi!!!!
   
 14. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  No comment
   
 15. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi naomba nihisi nini kinachofikiriwa na EL baada ya kutokea yaliyotokea.

  Sidhani kuwa ana kinyongo nae. Hawezi kuwa na kinyongo na mtu ambae ameshamshinda kwa kila kitu hadi sasa. Rais wa nchi ana uwezo mkubwa sana, na siamini kuwa EL hatambui hivyo. Akiwa na kinyongo chochote, itabaki kumuumiza yeye mwenyewe kwa kuwa hana analoweza kumfanya Rais. Akifanya ujinga, kesi mbaya (Uhaini) inaweza kumkumba. Hivyo anachoweza kufanya ni kusikitika tu kwamba mwenzake amemuacha akiangamia. Na hasa akiangamia na kashfa kubwa zinazoendelea kumzonga kila siku kupitia wananchi, media n.k.

  EL hawezi kabisa kujibu mapigo yoyote 2010. Hawezi kwasababu hakutumia muda wake alipokuwa PM kujenga wigo wa kumfanya awe na nguvu ya kufanya lolote. Alikandamiza Wabunge wa CCM kutoa hoja ambazo aliona hazina maslahi kwake na serikali na hivyo wengi wao hawakuwa na mapenzi ya kisiasa kwake. Thibitisho la hili ni jinsi walivyomshindilia wakati sakata la RDC lilipomfikisha kujiuzuru.

  Nasikia kuwa bado wanawasiliana na kujadiliana mambo mbalimbali. Sijui kama mawasiliano yao ni ya kujipanga upya ama kibinafsi.

  Hisia zangu zinanituma kuamini kuwa baada ya 2010 na kama JK akichaguliwa tena, atajitahidi kumpa madaraka makubwa katika uongozi wake. Si ajabu akawa tena PM.

  Ni vigumu kwa EL kukubali yaishe. Nasikia tetesi kuwa bado anataka roadmap ya uongozi kama walivyopanga wanamtandao itekelezwe ambapo nae atapata nafasi ya kuliongoza Taifa hili (Kufungiwa kwa mwanahalisi kulitokana na tetesi hizi kutolewa nao). Kama nia hiyo bado iko "live" akilini mwake, basi atajitahidi kusafishika hadi roadmap iwe kweli na kama ilivyopangwa.

  Ili kufanikisha hili, hawezi kuwa na kimyongo na Mkulu wa kaya. Mkulu wa kaya ndie anaetarajiwa kutoa support ya nguvu kufanikisha ndoto za EL.
   
 16. J

  Jobo JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2009
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  JK ni mtu wa kusikiliza majungu! Hayuko empirical na nadhani huwa anogopa kivuli chake mwenyewe! Lowassa hakupata backing yoyote ya Rais wakati alipotuhumiwa bila ushahidi na happy go luck Mwakyembe! Mwakyembe a lawyer (ndivyo tunavyoambiwa) hakuona haja ya kumwita Lowassa ili ajibu tuhuma za ufisadi alizotupiwa. Kikwete alilijua hilo lakini hakujitokeza wazi kumtetea mteule wake. Alitaka tuamini kuwa wakati wa sakata hilo la umeme wa Richmond yeye hakuhusika hata kidogo! That would be true kama Waziri Mkuu ana mamlaka kamili ya utawala kama ilivyo kwa Uingereza au Kanada, but this is Tanzania... mtendaji ni Rais. Crisis ile ilimgusa pia na ni lazima alijua kilichokuwa kinaendelea. Alifahamu kuwa Lowasssa alikuwa innocent but akaamua aondoke kwani alishapata majungu kuwa lowassa alikuwa na nia ya kumpinga 2010 au kugombea Urais baada ya yeye kustaafu wakati yeye alikuwa anamtaka rafiki yake..!
   
 17. Makalangilo

  Makalangilo Senior Member

  #17
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Maji yakishmwagika hayazoleki,inabaki ..ahh majungu! Unataka kutwambia kuwa EL ni safi?
   
 18. k

  kananyayo Member

  #18
  Mar 24, 2009
  Joined: Dec 15, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK asingekuwa mjinga kumkingia kifua hasa baada ya kung'amua kuwa pamoja na kazi ya kumsaidia kuingia ikulu, kuna kazi nyingine pevu iliyokuwa imefanywa nyuma ya pazia na EL na kundi lake, la kujinufaisha binafsi na kundi lake, na la kutaka kufifisha madaraka ya presidency na kutaka wanamtandao ndio wawe kama un-official polit-buro, jambo ambalo halikubaliki
   
 19. J

  Jobo JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2009
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  huwezi kusema kuwa mtu ni mchafu hadi uwe na ushahidi! Hata kama ni mchafu kwa masuala mengine, hili lililomwondoa halikuwa na ushahidi. Mwakyembe alitaka kupitisha mambo yake mwenyewe. Ukiongeza na chuki za Sitta kuukosa uPM basi likazuliwa zengwe kuwa Lowassa ana nia ya kumwondoa JK 2010. Kikatafutwa kisingizio cha Richmond.
   
 20. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #20
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,916
  Trophy Points: 280
  1. Obama hakumtetea Tom Daschle, wala Bill Richardson, lakini alimtetea Treasury secretary wake.

  2. Bush hakumtetea Donald Rumsfield, lakini alimtetea Brown.

  3. Rais Kikwete, hakumtetea Waziri Mkuu wake wa kwanza E. Lowassa, lakini Masha ni waziri mpaka leo.

  Ahsante.

  William.
   
Loading...