Kwanini Mramba, na si Chenge, Lowassa, Tibaijuka na Muhongo?

Kwanini Mramba, na si Chenge, Lowassa, Tibaijuka na Muhongo?

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Bazil Pesambili Mramba na Jakaya Mrisho Kikwete ni watu walifanya kazi ofisi moja,Chini ya boss wao Benjamini Wiliam Mkapa.Ni watu walihudhuria vikao vya baraza la mawaziri pamoja chini ya mwenyekiti Rais Mkapa.

Sasa nimejiuliza Kwanini JK hakumwokoa Mramba kama alivyomwokoa Chenge Tibaijuka Na Lowassa?

Kama JK anapenda utawala wa sheria mbona Muhongo anapeta mtaani na urais anawania?

Vipi mama Anna Tibaijuka mbona hapandishwi kizimbani na alishatamka ni za mboga?

Tafakuri Please!
 
Hata kauli ya "mtakula nyasi " ilitoka wakati wa zama za zamani lakini zama hizi sisi tutakula tulichokula tangu oipindi hiko kwa utashi na umasikini wetu ila yeye atakula atachopewa.

Kila zama na kitabu chake, awali ni awali hakuna awali mbovu bora tu imeanza basi hakika hii ni awali.
 
Mimi sio ccm, lakini kuna wakati tuwe wakweli. Kwani muhongo ameiba nini? Au tibaijuka? Chenge, ngeleja sawa. Lakini hawa wawili ni nini? Maana muhongo hakutajwa popote, tibaijuka aliomba hela na akaikabidhi bodi ya shule
 
Kibo10

Kwa sababu hao uliowataja siyo Mramba.
 
Last edited by a moderator:
ivi unafikiri mahakama inaweza kutoa hukumu kufuata habari za kwenye kahawa
 
Msema kweli mpenzi wa Mungu. Wapo wengi ambao mazingira yanaonyesha wakijihusisha na ufisadi mkubwa au matumizi mabaya ya madaraka kipindi cha Mkapa.

Hii lazima ifanyiwe kazi.

Lakini ni ujinga kubeza jitihada zilizofanyika. JK safi kwa hilo.

Anyway imewah semwa jamaa ni jeuri alipingana dhahiri shahiri na vyombo vingine vya serikali.

Kwamba wengine nao walifanya madudu lakin hawakupelekwa mahakaman sio utetez wa maana mahakaman ndo maana nayeye hajawahi jitetea hivyo.

Nchi yetu inamalizwa na mambo kama haya. Tafadhalin tuwapinge wale wote wanaoyafanya - hata kama wanatoka vijiji tunakotoka.

Kuna watu wa ovyo kosa la jamaa wanaliona si kosa au anaonewa kisa anatoka jiran na wanakotoka.

Haya ni mawazo maovu. Kwahyo mimi nkitoka kwa kina chenge niunge mkono upuuz wake? Hii si sawa. Tutaharibu nchi kwa ubinafsi huu
.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom