Kwanini Mramba, na si Chenge, Lowassa, Tibaijuka na Muhongo?

Kwanini Mramba, na si Chenge, Lowassa, Tibaijuka na Muhongo?

Yote danganya toto wapate la kusema wakati huu wa uchaguzi kuwa wako serious kupambana na ufisadi. Wakati huo huo mapapa wa ufisadi wa Epa, escrow, rada n.k wanapeta na ndio watawateulie ccm mgombea urais.
 
Hawa hawakuwa wamejikiti katika uongozi wa chama walikuwa wanakula serekalini wakasahau serekali ipo hapo kwaajili ya chama na si wananchi.
 
Simiyu yetu atakuwa hajaona hii..nadhani akili yote ipo kwenye ya kesho.
 
Kibo10

Nashukuru serekali hii imetengeneza mfano wakufuatwa naserikali zijazo kwa kuwaburuza na kuwafunga hawa jamaa. Ikumbukwe kwamba Criminal liability haiishi, mtu anaweza kubuluzwa mahakamani kwa kosa alilolifanya miaka 20 iliyopita. Mbele ya safari tukipata uongozi bora, Cabinet km hii tuliyonayo yote itabuluzwa nakuswekwa segerea. Niswala namuda tu, hii nikitu watawala huwaga wanajidai hawaijui...kinachowalinda kina chenge, namafisadi wengine mnaowajua ni chama chao tu kuwa madarakani lasivyo mmeyaona yaliyotokea Zambia namalawi,. Tuvuteni subira maana kazi ya udhalimu haiishi milele.... Mungu anaendelea kuwavuruga wanguki
 
Last edited by a moderator:
Huyu Mramba alisema yuko tayari tule nyasi ndege ya raisi inunuliwe.
Afungwe tu.
 
Waliokosa ni wengi lakini Kikwete amepeleka na kuwafunga wale ambao alikuwa na Bifu nao shangaaa afisa utumishi wa bank kuu kufungwa kwa ujenzi wa bank kuu ...Waakati vote holder wa ujenzi bank Mkurugenzi wa Majengo ...hajafungwa

Then utashangaa watu kupelekwa mahakamani kwa ununuzi wa jengo la ubalozj ambalo aliyependekeza linafaa na linunuliwe hadji kwa ushahidi wa Hansard bungeni ni Jakaya Kikwete ...double standard
 
Mkuu mwanzisha mada...nini shida yako...say it?

Kwani Mramba hakufanya kosa? If yes na ushahidi wa kimahakama upo na umemtia hatiani, unataka nn tena?

JK asipofanya....ooohhh hafanyi....akifanya ooohh kafanya....

Au ndiyo ku.nya a.nye kuku, aki.nya bata kaharisha???
 
Lowasa anaingiaje hapa sasa??

Fikiri kabla ya kuandika na ku-post!!

CC: Kibo10

Watu tajwa hapo juu walitakiwa wawe magereza wanafanya nini uraiani?
Au ndani ya Ccm kuna wanaositail kupelekwa mahakamani wakastakiwe na kuhukumiwa na wengine wanatakiwa wakiiba na kulitia hasara taifa wajihuzulu na kuendelea kula bata?
 
Kibo10

Jamaa anaenda kufungumiwa kwenye kota za magereza tu..
 
Last edited by a moderator:
Huu ni mfumo wa uwajibishanaji wa Wawachina huu. Hata uwe fisadi vipi kama una Ngao juu jua hakuna wa kukuhoji, ila ngao ikianguka jua kitanzi kinakujia. Au ukiwa mchafu halafu sio msikivu kwa walioshika mpini jua unaangukia kwa akina "Prince Qing" (Zeng Qinghong) au akina Bo Xilai. Ngoja uingie uongozi mpya ndipo Muda utakapozungumza.
 
mmeanza tena.
kwa akili yako fupi, ana tiba utamfungulia mashitaka kwa kosa gani? kupewa pesa sio kosa ila kama kiongozi wa umma alitakiwa kutoa taarifa tu.
sasa hapo unamfungulia shitaka lipi zaidi ya kukosa maadili na kuwekwa nje ya uongozi kama alivyofanya? wapuuzi mna matatizo sana.
au umeanza kufikiria uchaga wake? mwizi ni mwizi tu hata kama ni mchaga.
Kibo10
 
Last edited by a moderator:
Salam mtoa mada,
Kwanza napenda kuweka wazi kwamba mimi ni mwanasheria na wakili na napenda kutoa mchango wangu hapa kwenye hii mada yako kama ifuatavyo ili tu tusaidiane kielimu na kimawazo. Na napenda kudeclare interest pia kuwa mie ni mtu ninayempenda na kumshabikia Prof Muhongo.

Napenda kuungana na wewe kwenye uzi wako kwa upande wa chenge kwa sababu kwa ushahidi ni maeneo mengi chenge aliingiza chaka serikali na kuisababishia hasara na hata kwa ushahidi unaoweza kujengwa kirushwa chenge anapatikana na hatia bila ya shaka.

Ila napenda nitofautiane na wewe kidogo kwa upande wa Tibaijuka na Lowassa. Kwa Tibaijuka najua utapata shida kuamini ila huu ndo ukweli kuwa, criminaly ni ngumu sana kusema kuwa ana hatia yeyote ile iwe either kuipa hasara serikali au kupokea rushwa, nakueleza kwa nini, Luge alimpa ile hela tibaijuka akiwa waziri wa ardhi,sasa ili uweze kucreate mazingira ya rushwa hapo ni lazima ujenge hoja kuwa kama waziri wa ardhi alimsaidia nini Luge? Na ukiangalia suala la escrow lilikuwa na Nishati na Madini, if Tibaijuka angekuwa waziri wa Nishati na Madini basi hapo mojamoja ingekuwa rahisi sana hata kutengeneza mazingira ya rushwa au kuitia hasara serikali. Kosa kubwa la Tibaijuka lilikuwa la kimaadili yaani kutodeclare pale alipopokea zile hela. Sasa hapa kama kosa la kimaadili lingekuwa na adhabu ya jela basi obvious Mama Tibaijuka nae angekuwa mtarajiwa wa Ukonga.

Niende kwa Lowassa, Mungu anisamehe, kusema kweli namchukia Lowassa na siamini kama ni kiongozi wa kulivusha hili taifa na kulipeleka linapotakiwa kuwa ila kwenye richmond kama mwanasheria lazima niseme ni ngumu kusema kuwa aliingizia hasara serikali kwa sababu records zinaonesha Richmond haikulipwa hata senti tano, if ingetokea Richmond imelipwa hela basi leo Lowassa nae angekuwa mtarajiwa ukonga, napo kwenye Rushwa hatukuonyeshwa ni wapi Lowassa alihongwa so hapo ndo utata unapokuja.

Tuje kwa Prof Muhongo sasa, hapo ndo sijui niseme umekosea au ulilishwa matango pori ndugu yangu kwa sababu hoja yako dhidi yake haina mashiko. Kwenye ripoti zote za uchunguzi no where wamesema Prof Muhongo ndo aliyetoa ruhusa au amri zile hela zitolewe. Ripoti zote zimemtaja Mwanasheria Mkuu kuwa ndo mtu aliyesema BOT ilipe zile pesa tena kwa maandishi na ndo aliyesema kuwa hata kodi isilipwe. Kwenye ripoti zote pia no where Muhongo ametajwa kupokea hata senti tano kutoka kwa mtu yeyote yule. Sasa hapo inaonesha kuwa umekosea kumuweka Muhongo hapa, labda kama ulimweka kinafki tu kwa sababu humpendi na unamchukia. Sasa kwenye hili suala kama hasara basi wa kushtakiwa atakuwa Werema na yeye ndo mtarajiwa wa Ukonga kwenye hili suala. Hata maswi ni ngumu sana kuwa na ushahidi wa kumfunga kwa sababu records zinaonesha in good faith alijibu sana kupata uhakika na uthibitisho makini tena kwa maandishi kama zile hela zilipwe au la.
Sasa kwenye kichwa chako cha habari ungewaweka chenge, Werema na labda kina Karamagi
 
Jiulize mafisadi Idris Rashid, Mustafa Mkulo, Juma Kapuya na Ramadhan Dau hawaguswi
nauona udini tu humu. Tutajie hao wamefisadi nini na wapi? hivi mtaacha lini hizi elementi zenu za udini? aliyekuwa anawabeba hayupo sasa hizi taifa ni letu sote. don't bother about udini wa mtu. hautatusaidia daima.
 
hivi kwani Kikwete alikuwa hakimu au jaji?
au mwendesha mashitaka?
mbona mko bize kumtetea mhalifu? hii ni ajabu ya aina yake. Da!

Tuhuma za hawa watu hazifanani tena za hawa wakina Mramba naweza kusema tuhuma na makosa yao ni madogo ukiringanisha kiwango cha fedha walichokitia kwa serikali kwani ni Billion 11, Siwatetei akina Mramba lakini ebu tuangalie viwango vingine vya fedha ambavyo serikali imepata hasara.
EPA - Billion 133
RICHMOND - Billion 122
ESCROW - Billion 312
CHENGE na Kashfa ya RADA
Kashfa ya VODACOM - Billion 700
na kuna nyingine za KAGODA, MEREMETA, ununuzi wa Mabehewa mabovu, Idara ya miundombinu Billion 256.

Zaidi ikumbukwe hadi sasa bado tunalipa Million 152 kwa siku IPTL.
Hawa wote waliohusika na kashfa hizi wengi wao waliishia kujiuzuru nyazifa zao au kuondolewa na Rais au kuhamishwa Wizara.

Ninachokiona mimi kwa hiki alichokifanya Kikwete ni kuingiza mgogolo wa kiuongozi kwani tutarajie Rais ajae na yeye lazima hawa wote wenye kashfa hizi nilizoziorodhesha hapa juu watashitakiwa na hii ndio itakuwa fedheha kubwa kwa Kikwete na utawala wake kwani kama alikuwa na nia njema ya kutoa hukumu kwa hawa watu haikutakiwa kuchukua miaka 9 eti mwaka anaomaliza uongozi wake ndio hukumu inatolewa.
 
Mimi sio ccm, lakini kuna wakati tuwe wakweli. Kwani muhongo ameiba nini? Au tibaijuka? Chenge, ngeleja sawa. Lakini hawa wawili ni nini? Maana muhongo hakutajwa popote, tibaijuka aliomba hela na akaikabidhi bodi ya shule

Fikiri kwa mapana zaidi usipende kukubali kila unachoambiwa! Una uhakika kwamba zile pay za Annie asili yake ilikuwa shule?
 
CCM ni zaidi ya uijuavyo mbona umeenda mbali sana?Vipi kina Werema ambao ni hivi majuzi tu waliingiza taifa ktk janga?Ukiwa na uswahiba na bwana mkubwa hutaguswa.


Kweli usipokuwa swahiba wa DHAIFU yatakukuta ya NGUZA!!! Utaozea lupango!!
 
Mimi sio ccm, lakini kuna wakati tuwe wakweli. Kwani muhongo ameiba nini? Au tibaijuka? Chenge, ngeleja sawa. Lakini hawa wawili ni nini? Maana muhongo hakutajwa popote, tibaijuka aliomba hela na akaikabidhi bodi ya shule
Sidhani kama Yona na Mramba waliiba, ila ninachofahamu waliisababishia serikali hasara ya bilioni 11.........kama walipata chochote kutokana na huo msamaha wanajua wenyewe.......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom