Kwanini mnawahukumu mno single mothers?

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
8,183
2,000
Masingle mazas wapo karne na karne,hata uimpose rules/sheria kali namna gani watakuwepo tu....

AND,yes tuwapongeze kwa ujasiri wao, despite being in the society full of hate and discimination wameweza kuwa Courageous kuchukua such responsibility...

By the way kutokuzaa sio ndio kipimo cha usichana....

Unaweza ukawa msichana hujawahi kuwa na mtoto,kwa nje, lakini ume'ua' watoto zaidi ya watano.....

Mheshimu yule anaye heshimu uhai.....

Pendekezeni njia wholly itakayowafanya vijana wasiingie kwenye ngono na wakiingia wachukue njia za kujikinga,mimba na maradhi....
Aaaa wapi... Sio kweli.....
 

mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
11,404
2,000
Kheri ya pasaka waungwana!

Ningeanza na kusema kwenye kila jambo kuna pande mbili za shillingi.

Katika pitapita zangu nyingi nimegundua kuna uzi nyingi katika jukwaa hili la MMU zinazowakandamiza na kuwaponda single mothers! Mnasahau kama hao walowatia mimba single mothers nao ni single fathers?
Nakubali katika maisha kuna kukosa na kukosoana lakini ningependa tuwekane sawa katika hili,haimaanishi kwasababu BAADHI ya single mothers hawana msimamo na vigeugeu basi wote wapo hivo.
Na kingine kama mtu ni single mum lazima uelewe kuna sababu ilopelekea hilo sidhani kama kuna mtu anaependa kulea mtoto peke yake bila ya sababu ya msingi.Au ukiachilia mbali hilo kuna baadhi wanaoamua kulea mwenyewe kwasababu the other part is not the right father figure for their child!Naamini si kila anayeweza kumimbisha mtu anapaswa kuwa baba!

Ningependa tuwekane sawa kuwa kuna single mother wa aina nyingi:

1. Kuna wadada wengi wanaoamua kujizalia tu kwasababu hakuna wanaume wanaoeleweka ambao wanakidhi viwango vyao na umri umeshatupa mkono mtu anaona ajizalie tu apate mrithi,wa aina hii naamini wanaweza kujimudu na kuhudumia watoto wao bila msaada wa mtu na ni watu wanaojielewa.

2. Kuna walopewa mimba ambazo wawili hao walikubaliana kuzaa pamoja na wakatengana kwasababu tofauti.Hawa mara nyingi wapo mguu ndani,mguu nje kwasababu kulikuwa na mapenzi na makubaliano kati yao kwahio ni rahisi kukumbushiana

3. Kuna walobeba ujauzito kibahati mbaya na mwanaume hayupo tayari kubeba majukumu.Wanawake wa kundi hili hawatakagi mahusiano na maex zao kiujumla kwasababu wanakuwa wameumizwa vyakutosha na wakishasonga mbele wamesonga.

4. Kuna walojibebesha mimba kwa matumaini ya kuolewa au kupata mwenza wa maisha au mteremko wa maisha(hawa ni wale ambao wanazaa hata na wanaume za watu).Hawa ni kundi jingine ambalo pia ni mguu ndani,mguu nje yaani anytime anarudiwa na kuachwa madhali yake yanamuendea.

But all in all mwishoni mwa siku kuna mwanaume alihusika katika hili kwa njia moja au nyingine.Kama ni kinga wanapaswa kutumia wote kujikinga na ujauzito usotarajiwa sasa ikiwa wewe unaenda kulala na mwanamke ambaye huna future nae kila kinga yoyote(kondom au uzazi wa mpango) unategemea nini hasa?

Tusihukumu single mothers kama wakosaji ni wao tu na wanaume ndo malaika mbona hamwahukumu single fathers?Au mnataka kusema wao ni tofauti kwasababu hawajabeba ujauzito.
Mtoto siku zote ni wamama ndio maana wamama ndio wanapata jukumu la kulea lakini tukipiga tathimini ya wanaume au ambao wamezaa tu ni single fathers naamini imepiku idadi ya wanawake.
Single fathers pia wanaweza kwenda kwa ex zao na kubinjuana so hakuna tofauti ya kusema ni single mothers tu sio Wife material kwasababu mnahofia wataliwa.Then tunaweza kusema Single fathers nao sio Husband material.This goes both ways kwa jinsia zote.

La muhimu ni kujuana vyema huyo single mum/ dad kabla ya kuanzisha mahusiano naye na mahusiano alokuwa nayo na ex wake lakini sio kuhukumiana!
uzuri wako umekubali kuwa single mother na single father wote hawako fit kuingia kwenye ndoa. Hiyo ndio point kuu.
 

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
9,104
2,000
Masingle mazas wapo karne na karne,hata uimpose rules/sheria kali namna gani watakuwepo tu....

AND,yes tuwapongeze kwa ujasiri wao, despite being in the society full of hate and discimination wameweza kuwa Courageous kuchukua such responsibility...

By the way kutokuzaa sio ndio kipimo cha usichana....

Unaweza ukawa msichana hujawahi kuwa na mtoto,kwa nje, lakini ume'ua' watoto zaidi ya watano.....

Mheshimu yule anaye heshimu uhai.....

Pendekezeni njia wholly itakayowafanya vijana wasiingie kwenye ngono na wakiingia wachukue njia za kujikinga,mimba na maradhi....
Yaani umeongea bonge la pointi Rebeca 83!Salute to that madam!
Wao sijui wanataka hizo mimba wanazowajaza watu wakazitoe baadala ya watu kufundishwa njia mbadala za kujikinga.Hivi katika mashule Tanzania watoto wanafundishwa jinsi ya kujikinga na mimba zisizotarajiwa?

And since wanaume wanahalalisha uzinzi ni vyema mabinti wafundishwe jinsi ya kujikinga na uzazi wa mpango!Nchi nyingine vidonge vya uzazi wa mpango ni bure kwa mabinti!Serekali inatambua katika umri fulani mshawasha unaongezeka na ili kuepuka mimba zisizotarajiwa hao mabinti wana option ya kuchagua ya njia ya uzazi wa mpango!
 

C Programming

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,011
2,000
Katika pitapita zangu mitandaoni kuna mdada nilikutana nae anatafuta mchumba serious badae aje kuwa mume basi nikajikuta naanzisha mahusiano nae.

Baada ya kudate nae zaidi ya miezi minne nimekuja kugundua kumbe ni single mother alizaaga na mume wa mtu ambaye anadai kipindi cha uchumba alimzalisha akamkimbia akaoa mtu mwingine hivyo alimtelekeza . Na kuhusu mtoto yupo wake kwa sasa yupo mama yake Kibaha anamlea.

Kiukweli huyu binti hajanikosea chochote ila mimi kama sipo tiyali kuoa single mother staki kumdanganya kama nitamuoa wakati moyoni najua siwezi kumuoa hivyo naombeni njia ya kusitisha huu uhusiano bila kumuumiza huyu mdada
 

Hechinodemata

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
1,061
2,000
Njia ya muongo ni fupi sana, mara upo na singo mother miezi 4 mara mara upo kwa baba mkubwa miezi 4 umepewa siku 30 uondoke, Chai sana aisee
 

Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
2,524
2,000
Katika pitapita zangu mitandaoni kuna mdada nilikutana nae anatafuta mchumba serious badae aje kuwa mume basi nikajikuta naanzisha mahusiano nae baada ya kudate nae zaidi ya miezi minne nimekuja kugundua kumbe ni single mother alizaaga na mume wa mtu ambaye anadai kipindi cha uchumba alimzalisha akamkimbia akaoa mtu mwingine hivyo alimtelekeza . Na kuhusu mtoto yupo wake kwa sasa yupo mama yake Kibaha anamlea .

Kiukweli huyu binti hajanikosea chochote ila Mimi kama sipo tiyali kuoa single mother staki kumdanganya kama nitamuoa wakati moyoni najua siwezi kumuoa hivyo naombeni ya kusitisha huu uhusiano bila kumuumiza huyu mdada
Wewe dogo unazingua sana. Wewe jana si ulianzisha sredi (thread) kwamba baba mkubwa amekupa notice ya siku 30 uondoke kwake? Umeshatoka na tayari kabla ya muda na kukamata single maza? Una laana wewe. Ukute ndio kitu ya baba mkubwa, utakula jeuri yako mjaa laana wewe .
Kama single maza anakukosha, kamatia hapo hapo kama mtu aliyesombwa na maji akakamata mzizi
 

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Aug 23, 2010
4,679
2,000
Ushasepa home??

Huyu ameshazaa??

Vipi ushapata kibarua cha kuendesha maisha?

Unatuomba ushauri wakati hapa ulituelekeza namna ya kuacha mwanamke? Pitia desa zako au mganga hajigangi?


Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu....
 

luckyline

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
12,034
2,000
Kesi nyingi zilizoko mahakamani ni viwanja vyenye mgogoro. Yaani hata zikiisha utasikia kuna mwanafamilia kakata rufaa, mara yule kaleta bill of cost. Mara yule kaleta zuio, Etc etc......

Ndo maana tukakubaliana kabla viwanja vyenye mgogoro havijanunuliwa, kwanza mnunue hivi visivyo na mgogoro.

Bi shost hawezi kuolewa kirahisi hivo wakati kuna wadada wamejitunza wakajinyima starehe sasa yeye ni nani? Kwamba ana bahati zaidi ya wengine?
Kwamba yeye anajuamulia tu kwamba yeye hawezi kula pipi kwenye ganda leo aolewa tena kirahisi? Hapana.!!

Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake.😆
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom