moi wa kitaa
JF-Expert Member
- May 3, 2015
- 1,016
- 1,016
Marehem ndio alisema cku akifatulewe kwanza sasa kosa letu nini
Sio wote wenye ujasiri wa kwenda msibani wakavu bila kunywa chochote.Habarini wanajf I hope mko good kabisa.
Niende kwenye key point direct bila kupoteza wakati hii issue ikoje watu mnaenda msibani kuzika then mnatoroka na kwenda kunywa pombe baa za jirani hatimaye mnalewa hovyo na kuonyesha picha mbaya kwa wafiwa.
Acheni hiyo tabia sio nzuri hata kidogo.
Hivi ni kwanini mnaenda kulewa wakati wa msiba unaendelea ni kwamba ni stress za msiba au mnasherekea kifo cha mwendazake?
Asanteni!!
Tatizo wanajiovadozi alcohol then inakuwa sio msiba tena ni fujo tupuSio wote wenye ujasiri wa kwenda msibani wakavu bila kunywa chochote.
Hata hivyo msiba ni kama sehemu ya ibada,hivyo sio vibaya kutumia chakula au kilevi Kwa kiasi.
Nitabia ya ajabu
Sasa wakisha lewa wengine huanza kulia hovyo kama watoto
huku wakimtaja marehemu na vituko walivyokuwa wakifanya pamoja enzi za uhai wake
Okay okayBinafsi sipendi na situmii kilevi ila sioni tatizo watu kunywa. Tatizo huja pale wanapofanya fujo. Lakini mbona fujo zijawahi zishuhudia kwasababu ya pombe?
Ama kwa hakika kwetu hakunaga shughuli ndogo, iwe msiba, kipaimara, ndoa, etc.ukiwa huna pombe unawakosesha watu furaha. Munasogezaje muda kama hakuna issue ya kuwasindikiza na baridi lote hilo?
Kwetu wanakesha. Yaani hata matanga watu wanakeshaga. Safarini na msiba lazima wazimue aisee.
Babu yangu alifariki 2019, msiba ulikaa wiki nzima dar. Watu wanakuja kunywa na kula tu. Mpaka boss wangu alikua haamini tuna msiba lkn mwenhekiti wake wa jumuiya akamuhakikishia kuna msiba jirani anaenda kunywa hapo pombe kwa mzee fulan. Safari same thing, gari ya maiti ikapata hitilafu kila mtu akarudi bar anasema naendaje nyumbani bila ya baba ama babu yangu? Nutawajibu nini mimi nimemwacha baba/babu porini huko kumbe ni hapo rockhill hotel tu? Ama kwa hakika rock hill waliuza ile siku usiku maana tulikua na gari nyingi sana. Coaster zaidi ya 15 ukiachilia mbali watu walikua na makreti ya bia kbs kwenye magari yao na katoni za vinywaji vingine. Kiukweli uchungu ulipungua sana tukishukuru kwa maisha yake maana aliumwa muda mrefu hivyo pombe ilikua sehem ya faraja kwa walevi.
Ila niwaase tu ndugu zaguni pombe si nzuri kwa afya zetu. Pia alosto ya pombe inatufanya tushuke thamani zetu maana mtu anasubiria msiba wa mtu anayejihimu ama familia hake ndo akanywe pombe za kumdhalilisha. Kunyweni kwa kiasi na tuepuke utumwa wa vilevi.
Tabia inakera kweli kweli, wengine wanaanza kufanya fujo msibani au kuropoka hovyo tu, Mara ugomvi kugombea simu ya marehemu.Sio majonzi hiyo tabia inakera sana
Hii ni fedhehaTulienda kweny matanga ndgu walienda kulewa wakarudi kama saa sita usiku halafu walipigana kweny msiba ,ukiangaliavwote ndugu.