Experience yangu jinsi ngono zinavyotokea wakati wa kusafirisha misiba

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,186
9,287
habari wakuu

naam mimi mimi si mgeni humu ila ningependa kushare some little experience juu ya usafirishaji misiba
habari wakuu

naam mimi mimi si mgeni humu ila ningependa kushare some little experience juu ya usafirishaji misiba

mimi ni mfanyabiashara,ambapo nilianza na biashara hizi juakali tangu miaka ya 2009 baada ya kustop chuo nilikokua nasomea bachelor of human resources kutokana na sababu za ujana zaidi.

Basi baada ya kufanya biashara hizi za juakali huku nikijihusisha na shughuli zingine za hapa napale njee ya Tanzania katika kitongoji kidogo kinachoitwa falcon hatimaye nikapata mtaji kidogo
ulionirudisha bongo kufungua biashara

basi nilipofika bongo nikaona ngoja nichukue coaster moja niifanye kwa shughuli za kukodisha.
Basi moja kwa moja niende kwenye mada sasa mana sipo kutoa historia mwisho mniokote mabwe pande.
Nikaanza rasmi kazi hii ya kukodiasha gari yangu aina ya coaster wakati huo ninayo moja nasafari yangu ya kwanza ilikuwa kwenda marangu.
Hapa sasa ndio penye mambo safari inaanza pale upanga ndugu wameaga wamemaliza huku mimi na kijana wangu tukiwa tumekaa kwenye gari tukiwaacha wamalize taratibu zao tupakize mwili (kiroba) tuanze safari kuelekea kilimanjaro. Basi wakati tumejilalia kwenye gari wakaanza kuingia wadada wazuri wasafi wanaonekana wana pesa wakaingia kuwahi siti na wengine wanabadilisha nguo na sisi tukiwa humo. zikaingizwa katoni za bia na na pombe kali nyingi. mara kiroba kilikuwa tayari kuingizwa kwenyw gari tukasaidiana na wafiwa kuingiza mwili ndani ya gari. baadae waendaji wakaingia kwenye gari mlango ukafungwa ac ikawashwa na gafla story zikabadilika kwenye gari huku wale wa nje wakitupungia mkono kama ishara ya kututakia safari njema. Story zilizokuwa zinapigwa ndani ndizo zilizonishangaza kwani ni sikuwa na uzoefu na ni siku chache tangu ninunue hii gari,basi wakaanza kuuliza Jack Daniel yangu iko wapi mwingine anaeuliza konyagi yaani ilikuwa kila mtu na kiburudisho chake huku gospel zikiendela kwenye tv tatu za ndani ya gari.

Hatimaye bagamoyo wakaomba kuchimba dawa sheli huku wengine wakiwa tayari wamelewa basi tukashuka wote hapo nje full kukumbatiwa mnapewa sifa sijui za uongo na kweli, mwingine anakuganda mpige story na yeye tu huku akikuona unaongea na mwingine anakununia flani hv.
Safari inaendelea hadi tunafika hotelin sasa pale ndio pombe ndio zinanyweka in large scale na watu kulewa hoi.hapa sasa ndio kuna vioja mwingine anapete mkononi anakuja anakukumbatia kimahaba na busu juu huku anakuuliza unakunywa nini nikununulie(wadada mkisafirishaga misiba sijui mnapataga wapi rundo la hela namna ile) basi ikifika saa tano usiku tunaendelea na safari kuelekea njia panda himo ambapo ndio kituo kikuu cha kupumzika. basi baada ya kutoka hotelin unajikuta tayari ushadendeka na wawili bila hata kujijua na mbaya zaidi wengi wanaofanya hivi ni wananafasi nzuri kimaisha, wengine ni maafisa wa jeshi wengine unaona kabisa msibani aliletwa na shangingi la kifahari. basi pale tumiendelea na safari taa za ndani zinazimwa na hakuna anaekumbuka kama ndani kuna maiti tena maana utakuta wale wamelaliana hawa wanadendeka mimi mwenyewe naongeleshwa na jinsia za kike tatu tofauti. hadi tukafika njia panda tukapumzika baadae saa moja asubuhi tukaanza safari ya kupanda marangu,maajabu tulipofika pale msibaa ukaanza tena vilio kwenye gari hatari.basi mnashusha maiti mnatulia pale kama robo saa hapa sasa ndio kila mtu anachukua namba zenu eti wakimaliza kuzika mje kuwafuata wakalale sehem nzuri. Wakimaliza kuchukua namba sisi tunashuka njia panda himo kutafuta vyumba vya kulala pale double M lodge.

Basi tukifika double M tunachukua vyumba huku tukiwawekea booking baadhi ya wafiwa waliotuambia tuwaweke vyumba

Naama saa tisa imefika wafiwa wanaanza kupiga simu tuwafuate baadhi waje kulala kwenyw lodge, hapa sasa ndio patamu, tunawafuata kisha tunarudi nao njia panda himo bia zinanyweka kupoteza mawazo ya kufiwa huku wengine wakiwaponda waume zao waliowaacha dar kuwa hawawatoshelezi kimapenzi, nadhan mnaeza kuvuta picha wadada wakikutana pamoja huku wakiwa tayari wameshalewa hapa nakwambia mnakuwa na wadada wengine wenye majina makubwa mjini lakini hapa hutaamini kama ni yeye ndio yanayomtoka maneno hayo mdomoni. basi sikukaa mda mrefu mwenzangu akaambiwa amsindikize mfiwa mmoja kubeba katoni za vinywaji kumbe wameenda kumalizana hukohuko, basi sasa hapa nimebakiwa peke yangu na sijui niongee na yupi nimuache yupi maana unakuta wengi wako kwenye ndoa na tayari wote wameingia kingi.


nadhani leo niishie hapa
ila visa ni vingi kuna siku mwenzangu alienda kulala na mtoto wa marehem masaa mawili baada ya kumzika baba yake kule mafinga.
pia hii tabia ya ngono wakati wa kusagirisha misiba iko kwa mikoa yote ya Tanzania ukienda mbeya musoma bukoba... na hakuna msiba nilioshuhudia warembo wengi kama msiba wa yule dada aliyeungua gorofani na mpenzi wake kwenye apartment yake mikocheni tukamsafirisha kibosho.

Pia nilichojifunza mabint wengi wa mikoani hawajawahi kufika dar hivyo wakijua mmetoka dar ni kama wanakuwa na kichaa fulani kuhakikisha mnalala wote

karibuni tusikilize bambi bambi ya jidena
 
Back
Top Bottom