Ndugu
voicer, nimekusoma na nimegundua vitu viwili au vitatu hivi juu ya ufahamu wako;
1. Unasumbuliwa na ushabiki tu wa siasa usiojengwa juu ya reasoning ktk msingi wa uelewa na maarifa..!
2. Huna basics za kisheria in connection na mahakama
3. Hujui michezo ya siasa za CCM dhidi ya wapinzani wake. Bahati mbaya hata hujui ni kwanini kesi hii imefunguliwa. Na hujui kuwa CHADEMA are smarter than CCM na serikali yote..!
4. Hujaisoma hati ya madai/mashitaka (affidavit) ya Halima Mdee. Hujui ni nani anashitakiwa. Ndiyo maana unashangaa CHADEMA walikuwa wanafanya nini mahakamani...!!
## Ngoja nikujibu hoja moja baada ya nyingine
Nimekuuliza wanaizuiaje, lakini sijaona jibu la maana..
Unasema nini hapa? Wewe unataka wajibu nini kwani? Unaweza kwenda kuwafundisha wajibu nini..!
Hujaeleweka. Fafanua, una maana gani.
Wewe ni MWONGO. Unless useme "wanashinda mahakamani kuwavizia kina Halima Mdee" kwa maana ipi..?
Lakini, kama una maana ya ule uhuni wa mahakama wakishirikiana na CCM na wahuni wengine ndani ya serikali kutengeneza njama za kutaka kesi ile isikilizwe upande mmoja, then mawakili wa CHADEMA walikuwa very right kuzuia uhuni huo...
Na walifanikiwa na kuvuruga mpango mzima wakishirikisha mpaka bunge. Si unakumbuka uongo wa Spika Dr Tulia Ackson..?
Anatangaza saa 3asb kuwa ana Injuctoion ya mahakama kutochukua hatua yoyote juu ya wabunge hao baada ya kupoteza uanachama wao. Halafu mahakama inasikilizwa shauri saa 8mchana na Injuction inatoka saa 9alasiri..!
Unaweza kueleza ni kwa Spika Dr Tulia aliamua kudanganya umma na kuvunja katiba ya JMT? Unadhani tungejuaje haya iwapo mawakili wa CHADEMA wasingehakikisha wanawepo mahakamani siku hiyo..?
Ndiyo maana nakuambia CHADEMA are smarter than you, CCM na washirika wenu...!
Unajichanganya sana ndugu
voicer. Shauri tayari liko mahakamani na mawakili walikuwepo mahakamani kwa sababu hiyo. Shida yako nini kwani..?
Huna taarifa za kutosha. Unapiga kelele tu..
Kesi hii haina kosa la forgery ya nyaraka. Kina Halima wanapigania ubunge wao tu...!
Hujui chanzo cha mgogoro huo ni nini?
In case kama umesahau, acha nikukumbushe..
Mgogoro wa kina Halima Mdee na wenzake dhidi ya chama chao hata kufika mahakamani leo ni matokeo ya uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na urais wa mwaka 2020 ulioharibiwa na Mwendazake Magufuli na CCM..!
Kwa hiyo, katika kujadili hali ya kisiasa hapa nchini katika vikao vya maridhiano, hilo automatic litaingia huko na lazima lijadiliwe..
Wewe kama linakupa shida kwa sababu zako binafsi, basi unahitaji kusaidiwa kwa kuelimishwa tu...!
Unaelewa circumstance ya "kutoongelea swala lililo mahakamani". Hakuna tatizo ili mradi haliongelewi ktk namna ya kuingilia maamuzi ya mahakama..
After all, elewa nguvu na mamlaka ya Rais katika mambo haya. Na ishu ya kina Halima Mdee, is pure political inayohitaji political intervention. Hiyo kwa taarifa yako haitatuliwi mahakamani sawasawa na ilivyokuwa kesi ya ugaidi wa Freeman Mbowe...!
Una maana gani?
Nimekuambia hivi, agenda ya maridhiano CHADEMA wanayo tangu mara baada ya uchaguzi mkuu 2020 hata kabla baba yenu Magufuli hajafa. Hujaelewa nini hapo? Haya ya kina Halima Mdee ni matokeo tu..!
Kama wameliongelea ni vyema, maana ni sehemu ya matatizo. Wewe unaona shida kwani..?
Uliye na ufinyu wa tafakari na maarifa + ufahamu ni wewe. Kaa na utafakari kwa makini utagundua tatizo lako...!