Honestly, ndugu
voicer mimi sijakuelewa. Sijui unahoji usichokielewa kweli au umeamua kujitoa ufahamu ili ignorantly ufanye blind propaganda (spinning)... Anyway. Hebu twende hoja moja baada ya nyingine;
Si wameshasema kuwa hawajawahi kupeleka jina lolote kwa kutumia nyaraka yoyote? Watakaopaswa kuthibitisha uhalali wa ubunge wa hawa kinamama ni NEC na Bunge. Hata hiyo "temporary injuction" ya uhalali wa ubunge wao hadi 13/6/2022 hawajapewa CHADEMA. Amepewa Dr Tulia na Bunge lake...
Huu ni uthibitisho namba moja kuwa, CHADEMA hawana tatizo na hawa kinamama. Wao wamemaliza kazi yao kwa mujibu wa taratibu za chama/taasisi yao..!
Walipaswa wao wenyewe hao kinamama 19 waliopewa baraka hizo waseme na kuthibitisha ukweli huu mbele ya vikao halali vya kikatiba vya chama/taasisi yao yaani CC na Baraza Kuu vilivyoamua kuwa hawafai tena kuwa wanachama wa CHADEMA. Hawakufanya wala kusema lolote kujitetea..!
Kuumbuana kulipaswa kufanyike ndani ya vikao halali vya chama sio nje ya hapo. Hawakufanya hivyo. Maana yake hawana lolote la kuiumbua CHADEMA..!
Wamekutana face to face kwenye CC na BK lakini, Halima na wenzake hawajawahi ku reveal uhuni wowote. Mahakamani wameenda kujiegemeza ili ubunge wao uendelee labda mpaka hiyo 2025. Sijui kama watatibiwa...!
Two facts zishuke;
1. It's true, CHADEMA haina ushirika na hao wanawake 19 tena. Imewafuta uanachama..!
2. Si wao ndio wameshitaki mahakamani? CHADEMA si ni mmoja wa washitakiwa? Sasa mantiki ya hoja yako kuwa CHADEMA imehamishia nguvu mahakamani ili kuzuia kesi ya hawa kina mama inatoka wapi? Unaijenga ktk msingi upi? Au hujui unaandika nini?
Wamekuambia hawaandai? Ni moja ya washitakiwa huko mahakamani. So, it's obviously, wanaandaa majibu na ushahidi wao kulingana na hoja za mdai (Halima Mdee)
By the way, umeiona hati ya mashitaka/madai ya Halima Mdee?
Utacheka!
Ni ubabaishaji mtupu. Ni kuhaha kwa kwenda mbele..!
Unadanganya. Unajichanganya mno. Kwa kifupi wewe ni MWONGO na umetekwa na UKADA WA CCM na kuacha ufahamu kwenye kiuno chako. Aidha, wewe huna "basic facts" za sakata hili ndiyo maana unajichangaya
"Intetion" ya vikao vya maridhiano kati ya serikali/CCM na CHADEMA ilikuwepo hata kabla hawa hawajafungua kesi mahakamani. Ilikuwepo tangu uhai wa mwasisi wa matatizo haya mwendazake Magufuli hajafa mwaka jana 2021..
Kwa hiyo, vikao vinavyoendelea havijasababishwa na sakata hili bali ni matokeo ya mfumo mbaya wa utawala, katiba na sheria uliozaa matatizo...
Kama linajadiliwa, basi it's just by the way na ofcoz limechochea zaidi umuhimu wa kuwepo vikao vya majadiliano na maridhiano kama hivyo...!!
Hili swali umeuliza na unapaswa ujijibu mwenyewe..!!
Umejibiwa kikamilifu. Hakuna matusi hapo. Ila kama kuna sehemu nimekuita mjinga ama mpumbavu, basi haiwezi kuwa matusi hayo, bali ni ukweli wa sifa na tabia yako..!
Au unaweza KUJIKANA mwenyewe? Unaweza kuikana tabia yako..?