Ukiona umependwa na Shangazi saana! ujue huna Bright Future, Darasani wa mwisho, huna fani, so Mko Level moja na shangazi yako au chini yake, kufa na kuzikana, wewe wa hapo hapo kijijini. Lkn kuna vitoto kwenye Mapaji ya nyuso zao vinaonekana wazi Nyota zinawaka si kawaida, Mashangazi wana zi ng'amuaga mapema. hapo sasa... tatizo ni Nyota yako!
Wafanya Biashara kubwa za kimataifa, Maprofessor,ma- Rais, Mawaziri, yaani wata kaao kwenda mbali kimaisha kuliko hata watoto wa shangazio, wanao kulia pamoja!
Wasomi watoto wa Safari za mbali, Ma-Diaspora, Katu hawatakaa wapendwe, utasikia ''Litoto hili halisikii, limechukua majina ya wapi sijui! linasema mimi mchawi'' hapo anakwepa asikuchinjie kuku km wanae wanavo kula! utaondoka na njaa!
Alafu lina Kiburi, kama mama ake! angalia linavonitazama! utakufa hivohivo! huendi popote! lione kwanza linavokula, linajiretereta hapa mchana woote huu mimi niko shambani nije kulipikia, likikosa likaseme umbea! Msomi utakuwa wewe? ukae ofisi ya nani? thubutu!!!!
Shangazi mpole Mnyenyekevu Utamsikia anawatangazia watoto wote pale ''kwa nini msijibidishe kama Bwire? atawashinda wote hapa ndani na Bwire amesha kuwa msomi wa hali ya juu, Kabisaaa! atafika mbali'' fanyeni mchezo na shule. ....na kweli inakuwa hivohivo