Kwanini Mashangazi wengi wana roho mbaya?

Kwanini Mashangazi wengi wana roho mbaya?

Shangazi zangu hunisaidia baada ya mzee Abdul-like figure kujikuta kapatia sana maisha wala hana haja na mimi.

Ila naona wanakuwepo wenye chuki lakini mara nyingi hutegemea na familia, sipingi hoja yako. Hasa ukikuta familia mzee wako ana pesa sana ila kajikataa kwako, hapo usitegemee sana shangazi kukupenda maana watakosa fursa kwa ndugu yao. Kama mzee wako anaenda nao sambamba kiuchumi hapo tegemea wanaweza kwenda kinyume naye na kuonesha true colours.

Pia wenye elimu ndogo sana huwa na tabia za kichawi kiasi. Kwanini anafaulu lakini wanangu wanafeli? Kwanini mdogo wangu amlipie huyu wakati kaka yetu hataki, hiyo hela si wangelipiwa wanangu?

Umaskini nao uko directly proportional na chuki, husda, wivu, tamaa za kijinga na roho ya kwanini.

Sasa ole wako uwe wa ukoo unaoamini kupuliza ndo utakoma. Wenye imani zao wako peace lakini zisiwe imani hybrids kama makanisa ya wahuni.

Mwisho, watu wasipinge tu wakati hawana encounters kama hizi. Mtu anadai sio mwizi wakati hajwahi kuwa na fursa ya kuiba. Hapa nadhani ulilenga scenario ya nyumbani pesa hamna au baba kaingia mitini. Wanaokataa kwa kuchukulia kisa wao kwao maisha safi na ndugu zao huja sikukuu na kwenye sherehe hawajakutana na uhalisia wao. Mbona wazazi wakifa ndugu wengine ndo wanauza mali na kuachia umaskini akina junior waliokuwa wanafake kuwapenda?
 
mkuu sijasema wote.
Mkuu kama sio wote basi tambua kuwa hiyo ni hali tu ya kimaisha kuna Mama wenye roho mbaya kuna baba wenye roho bibi wenye roho mbaya etc.

Cuz hata watu wenye roho mbaya nao huzaa na kuitwa mama/kaka zao huzaa na wao kuitwa shangazi. Dada zao huzaa na wao kuitwa mamkubwa au mamdogo etc.

Kwa hiyo mkuu hiyo ni hali ya kawaida katika jamii watu wote hatuwezi kuwa katika Category 1. Na kwa experience yangu ya maisha niliyonayo sipingi kuwa kuna mashangazi wenye hizo tabia ulizoziongea but most of them tabia hizo huwa sizo zao Ila wana pachikwa ubaya wa bandia na mawifi zao Kwa sababu ya conflict ambazo huwa wanakuwa nazo.
 
T14 Armata umeongea kweli tupu, ubarikiwe sana.
 
yuzazifu,

Huyo shangazi hana hela na pengine watoto wake hawana akili. Mimi shangazi zangu wapo poa japo hawana hela pia. ni roho ya mtu tu na sio wote.
 
Mkuu kama sio wote basi tambua kuwa hiyo ni hali tu ya kimaisha kuna Mama wenye roho mbaya kuna baba wenye roho bibi wenye roho mbaya etc

Cuz hata watu wenye roho mbaya nao huzaa na kuitwa mama/kaka zao huzaa na wao kuitwa shangazi . Dada zao huzaa na wao kuitwa mamkubwa au mamdogo etc

Kwa hiyo mkuu hiyo ni hali ya kawaida katika jamii watu wote hatuwezi kuwa katika Category 1 ... Na kwa experience yangu ya maisha niliyonayo sipingi kuwa kuna mashangazi wenye hizo tabia ulizoziongea but most of them tabia hizo huwa sizo zao Ila wana pachikwa ubaya wa bandia na mawifi zao Kwa sababu ya conflict ambazo huwa wanakuwa nazo
maelezo mazuri bt umeconclude kishabiki sana, laiti ungewahi lelewa na aunt ndo ungeupata uhalisia wa nachokisema.
 
Huyo shangazi hana hela na pengine watoto wake hawana akili. Mimi shangazi zangu wapo poa japo hawana hela pia. ni roho ya mtu tu na sio wote
Ndo maana nikasema wengi nikimaanisha si wote, mi nina mashangaz 3 bt mwenye roho ya kwanini ni huyo 1
 
maelezo mazuri bt umeconclude kishabiki sana, laiti ungewahi lelewa na aunt ndo ungeupata uhalisia wa nachokisema.
Eehh aunt yangu Mimi /baba yangu mimi /mama yangu mimi akiwa ana roho mbaya Hiyo haimaanishi kwamba Wazazi wa watanzania wengine pia nao wako hivyo+ mkuu
 
ndo maana nikasema wengi nikimaanisha si wote, mi nina mashangaz 3 bt mwenye roho ya kwanini ni huyo 1
Basi kwa mnajili huu hii thread yako ilipaswa kuwa na heading inayouliza kwanini shangazi yangu ana roho mbaya. Na sio kwanini mashangazi wengi wana roho mbaya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom