Kwanini Marekani ameshindwa kuimaliza Iran haraka?

Tukisema jamaa kapuyanga anatumind. Taifa dogo ambalo hata China mwenye alihofia??? Jamaa hapa kazingua.
Comrade Bazazi Bin Dunya hebu tulia.

Japan is a Chihuahua with a memory of a lion....

Japan aliweza kumuonea Uchina pale tu ambapo Uchina alikuwa chini ya utawala wa mataifa ya Ulaya.

Kihistoria Uchina na India ndiyo mataifa makongwe na yaliyowahi kuwa na nguvu sana Mashariki ya Mbali kwa miaka zaidi ya 5000. Kiufupi Uchina limewahi kuwa taifa tajiri zaidi duniani kwa vipindi vitatu tofauti ndani ya miaka 2000. Huyo Japan amenza kuwa na nguvu karne ya 19 baada ya Mapinduzi ya kisayansi ya Mfalme Meiji. Ila Japan aseme ajidanganye amvimbie Uchina, nakwambia itakula kwake. Taifa lenye watu zaidi ya Bilioni moja, tena majirani zako, utapambanaje nao labda ???
​
 
Muda huwa ni mwalimu mzuri sana.
Mkuu 'Malcom Lumumba', umeandika mengi; najuwa maandishi marefu ya aina hii huwa ni kikwazo kwa wengi humu JF

Nimejitahidi nikakusoma mzima. Mara zote huwa nipo upande unaoonewa, (underdog) na hasa kama anayeonewa hafanyiwi haki. Sikuwa upande wa Ukraine kwa sababu alikubali kuwa chambo cha kutumiwa na wakubwa.

Lakini hasa lililonifanya nirudi na kukusoma mada nzima, baada ya kukaribishwa kwenye mada yako hii, ni kuhusu swali lako hilo ulilowasilisha kama kichwa cha mada yako:

"---kwa nini Marekani ameshindwa kumaliza Iran haraka"

Kwani ulikuwa na matarajio ya Iran kumalizwa haraka katika muda gani?

Kumalizwa kwa Iran ulitegemea kuweje?

Kuna mifano yoyote ambayo nchi ilimalizwa haraka? Unaweza kusemalabda Venezuela ilimalizwa haraka?

Umetoa mfano wa Afghanistan kumalizwa haraka, jambo ambalo siyo kweli, kwa sababu sote tunajuwa walivyokimbia na kuacha silaha huko

Hakuna nchi hata moja iliyomalizwa haraka; mara zote wanaoshambuliwa wakiweka ngumu kazi ya kumalizwa huwa haipo; isipokuwa misukule kama tulivyo sisi sasa hivi.

Ningependa kuingia kwenye sababu za hawa wakubwa kuwa na tabia hizi za uonevu hasa kwa sasa. Bila ya kueleza kwa undani, nakurejesha tu kwenye shughuli iliyofanyika mwaka jana Uchina ikiwahusisha akina Putin, Xi Jinping, Kim Jong Un, na waziri mkuu wa India. 'Optics' hizo na yaliyozungumzwa hapo usifikiri yalienda bila kutiliwa maanani na hawa wakubwa.

Ngoja niishie hapa kwa sasa.
 
Hapo kwa ndugu zetu katika imani🤣🤣
 
EEEEnHEEEE!

Mwambie Waingereza wapeleke "opium war" wakati huu huko China!

Hii miamvuli wanayoitegemea akina Japan na wengineo imeanza kuwa na matundu ya kutisha sana.
 
Myahudi wa kibosho likimwaga madini kama lipo uwanja wa vita Iran kumbe pumbavu tu
waga
 
Mzee unaogopa kuwa na record mbaya kwa mafaili ya jamaa wa Msasani pale Mwai Kibaki?
Unaogopa kunyimwa ruhusa kujivinjari nchini kwao 😃
Mambo ya kugongewa muhuri kwenye mkoba au siyo?
 
CIA na MOSSAD zikae chini for years waje na suluhisho halafu mtu uje tu uone US na Israel zimekosea, HAPANA.
Katika vita ya siku 12 , PM Netanyahu alikiri kwamba MOSAD walikosea kwa kutoa data zisizosahihi kuhusu uwezo wa Iran kwa ku under estimate nguvu ya Iran. CIA wamekiri kukosea Libya na hata Syria ya leo

MALCOM LUMUMBA amerudia sana mfano wa Viet Nam . CIA ilifeli kama ilivyofeli kule Afghanistan
 
Sijui kwa nini Trump kawa mtumwa wa Netanyahu wakati Biden hakua ivyo
Hapana! Marekani ni watumwa wa Israel. Kuna lobbying group inaitwa AIPAC( America-Israel PUBLIC Affairs Committee)! imefanikiwa kuweka viongozi katika Congress na White house. Senators na Reps wanafadhiliwa na AIPAC inayoundwa na Wayahudi wenye pesa

Biden alisadia vita ya Gaza na kuzuia UN resolutions zote. In fact Biden ameburuzwa sana na Israel
 
Ukishachagua TU upande
Uchambuzi wako unakosa mantiki na credibility

Unalinganisha vita ya Marekani aliyepigana chini ya wiki mbili na Urusi ambaye anapigana miaka mitatu Hadi sasa na taifa jirani hapo
 
Wewe nikikumbuka ulivyokuwa unatuaminisha mwanzoni mwa vita vya Urusi

Wewe jamaa tangu uandike uongo uongo kule kwenye uzi wa mgogoro wa Urusi na Ukraine, inahitaji kusoma mara mbili mbili unachoandika.
Kwa hiyo nyinyi mnafurahi taifa moja kuua political leadership ya taifa jingine kisa vita???Hiyo ni sign ya weakness sio nguvu.Nguvu inatambulika kwenye utiifu wa sheria za kimataifa, sio kulipua watu na nchi kisa una jeshi kubwa, nguvu kubwa etc.
Pili mlitaka Urus wamle kichwa Zelensky ili tu awafurahishe watu kama nyinyi et ndo nguvu hizo au sio???Umesahau Putin alimuhakikishia waziri mkuu wa Israel kipindi kile kuwa hatomgusa Zelensky???Uo ndo uongozi...
Vita sio betting, au Simba na Yanga, kwamba mna-prove ubishi wenu kwa kutembea na roho za watu.
Et Urusi hatawali anga, mosi hujui kuwa kuna vijeba vimejichimbia pale -NATO na air defenses za Kutosha, utalinganisha na Iran??
Pili Urusi anawezapiga popote kwa missiles akitokea kwake, kwa nini ahangaike kuweka rehani maisha ya airforce yake wakati ana alternative??Makombora tu na drones zinagusa kila kona..

US atashinda pambano pale Iran lakini hatshinda vita...BATTLES yes, atawatwanga kwelikweli lkn kushinda vita sio rahisi pale, nchi kubwa ile, milima na mapango kama yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…