Kwanini Marekani ameshindwa kuimaliza Iran haraka?

Ushabiki.
Unasema israel wanazui watu kutoa habari ila wewe uko namtumbo unajua kwamba inapigwa kama Gaza!

Iran kwa sasa anarusha drones na makombora kwa kuvizia, maana mwanzo alirusha kwa kupupa mara israel mara kwa waarabu wenzie, wakati anarusha kwa pupa Israel alikuwa anawinda lounchers na maghala kisha kulipua.

Irani sasa hivi anatepeta ila anatembelea kiburi cha waislamu wote duniani kwamba ni bora kufa kuliko ku surrender

Kitakwimu inaonesha makombora na drones zinazorushwa toka Iran imepungua kwa 90%
 
Your English has improved exponentially. Hongera Sana....

I hope next time we meet, the edges of your brain power would pace geometrically as well....
 
Usiwape hizi taarifa, waache watafute wenyewe.....
Sijui kama wanajua watafutie wapi. Taarifa ya kendy itawasaidia sana vijana wa Kenya na Uganda wanaosoma JF. Hawa wakwetu lugha ni tatizo, kutafuta habari tatizo !
Hapa atakuja kusema chanzo chako hakiaminiki, hivyo usipoteze muda......
Sidhani kama watahoji chanzo! kwani wameelewa kilichoandikwa!

Some people will always be committed to misunderstanding you no matter how hard you explain....
Nawatetea Vijana hakuna misunderstanding kuna ignorance ya hali ya juu sana Tanzania.
Wengi wanasoma ili kujibu kilichoandikwa, hawasomi kuelewa kilichoandikwa ndio maana wanabisha tu katika mabandiko. Hawana uwezo wa ku rebuttal hoja. Ujinga umekolezwa na DINI. Yaani hawana muda wa kuangali jambo kutoka angle tofauti! huku Wayahudi kule Waarabu! hawajishughulishi hata kutafuta facts

Mfano, nimewauliza kosa la Iran ni lipi hadi ashambuliwe? Hakuna anayejibu, wapo bize, apigwe !
 
Hayo huwa ni mahesabu ya mdomoni kwa watu ila field huwa wanajua kabisa hapa lolote inatokea.

Hata Putin alienda akifikiria siku tatu tu Ukrain itakuwa imeanguka ila mpaka leo mwaka wa nne ana hangaika.

Putin anaanglia faida ya miaka 50 mpaka 100 ijayo.

Hapo Iran USA atapoteza pesa lakin in long run hizo hela si kitu
 
Hiii chai %90 haaaaa wangepishana vikumbo kuondosha Wananchi wao Middle East!!!!!!! Iran

ndio kwanza yupo kwenye %0 . 0 ndiomana Yemen bado kanyuti kaambiwa tulia kwanza tupungeze zagazaga za miaka ileeeee..

ngoma bado Asubui sn.

Tela Aviv wanakufa kwa presha tu usiku mnene kwao.
 
Kwa hiyo ulitegemea Iran itapigwa ndani ya siku ngapi?
Iran ni nchi kubwa sana na ina jeshi kubwa (kwa idadi ya wanajeshi na silaha)
 
Boeing KC-135 siyo tu ndege, bali ni alama (A Symbol) ya nguvu ya kijeshi ya jeshi la anga la Marekani na ubunifu wa kiteknolojia. Leo hii moja imeanguka na kusababisha vifo vya askari 6, huku nyingine imepata hitilafu na kukimbilia Israel. Hitilafu zimetokea Iraq na wao wanadai ni matatizo ya kiufundi.

Hizi ndege zilitengenezwa mwaka 1955, kipindi cha utawala wa Raisi Dwight Eisenhower na mpaka leo hii zipo tu. Kiufupi hizi ndege ni vituo vya mafuta vinavyopaa (Flying Gas Station). Hizi ndege ni za kipindi cha vita baridi na zina miaka zaidi ya 60, jambo ambalo linazifanya zitumia gharama kubwa mno kwenye ukarabati (Maintenance).

Taarifa zinasema kwamba hizi ndege kwa safari moja tu hutumia zaidi ya dola za Kimarekani 11,000 ambazo ni sawa na milioni 23 hadi 24 za kitanzania. Jumla ndege zote hugharimu dola za Kimarekani bilioni 5 kwa mwaka kufanyiwa matengenezo. Miaka ya 2003 baada ya kuonekana hizi ndege ni kongwe na zitahitaji gharama kubwa kuzifanyia marekebisho ilibidi watengeneze ndege nyingine jambo ambalo halikufanikiwa mpaka leo hii. Inasemekana mbali na marekebisho mengi, hizi ndege haziwezi kuvuka 2030.

KIUFUPI SASA: Operesheni nzima ya Marekani na Israel inategemea Boeing KC-135. Ndege-vita kama F-35 zinazoshambulia, au B-2 Spirit(Ambazo zinategemewa kutumiwa hivi punde) na ndege nyingine zinazofanya shughuli za ujasusi zinategemea sana hizi Boeing KC-135 katika kufanya mashambulio. Tatizo linakuja hapa sasa:

Mosi, hizi ndege zinahitaji matengenezo makubwa ya gharama ili kuweza kuruka juu na kufanya kazi vizuri. Hii vita ikiendelea, sidhani kama Marekani atakuwa na uwezo wa kuzifanyia marekebisho ndani ya muda mfupi ndege zenye miaka zaidi ya 60, kongwe kuliko hata TANGANYIKA. Rushwa ndiyo chanzo kikubwa kufanya serikali ya Marekani ishindwe kupitisha zabuni ya kutengeneza aina nyingine ya ndege zenye uwezo wa kujaza mafuta kama KC-135. Kiufupi, kinachomkuta Marekani kipindi hiki, ndicho kilichomkuta Urusi miaka ya 90's (Zingatia the Sinking of the Kursk/Crash of Antonov A-24)ambapo ndege zake kongwe na manowari zilikuwa zinapata ajali tu kwasababu za kiufundi.

Pili, hizi ndege zina udhaifu mkubwa mno. Zinapojaza mafuta huwa zinaenda taratibu mno angani jambo ambalo kwa vita kama hii ya Iran, itazifanya kuwa shabaha rahisi mno. Kiusalama inabidi hizi ndege za F-35 na zingine zijazie mafuta Iraq ili zishambulie Iran. Lakini bahati mbaya, Iraq imejaa wanamgambo wa kishia ambao wanaweza kuzitungua. Ukizingatia pia kwamba itakuwa ngumu kwa hizi ndege kutua sehemu kama Saudi Arabia, UAE, Bahrain au Qatar kwasababu kambi za Marekani hazifanyi kazi kwasasa.

UKWELI NI KWAMBA, kipindi hiki Marekani ameyatimba....

 
Unajua bajeti ya ulinzi wa Marekani Kwa mwaka ukilinganisha na bajeti ya Iran na nchi zingine??
Umechagua upande ambao utakutesa sana kwenye chambuzi zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…