barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,917
Nakumbuka enzi Mzee kanitoa bush kuja kuishi na mama wa kambo town.. Darasani nikawa moto zaidi ya watoto wake. Haikumfurahisha, siku tukifunga shule na kuleta matokeo, nipo juu with flying colours. Sasa dingi hawezi nisifia mbele za Mke wake (my stepmother) tukiitwa sebuleni kutoa report za matokeo mi yangu ni "excellent" na "Very Good"... Kwenye tabia pameandikwa "Best Conduct"..
Mama wa kambo si masimango hayo, kuwa nafanya vizuri sababu nakula bure, nalala bure kwenye umeme na kutumia choo cha kuflash...Asijue hizo ni haki zangu za "kikatiba" mana huyo ni baba yangu, nastahili hayo yote.. Sasa mzee kwa kumuogopa mkewe akawa hawezi kunipongeza kwa zawadi, zaidi ataniita pembeni na kuninunulia zawadi ambayo ni "Perishable" - yaani msosii au chochote ambacho sitafika nacho nyumbani ili wale wadogo zangu wasione wivu.
Ugomvi mwingine ulikuwa ni wa kuongea "kilugha" na baba mzazi, kwa kukulia kwangu kijijini nilikuwa mahiri sana wa lugha ya kikwetu, na nililelewa kuamini kuwa mtu wa heshima kama mzee lugha sahihi ya mawasilino si Kiswahili. Mama hakupenda akihisi namteta (maana hakuwa wa kabila moja na baba). Mzee alipenda sbb ilimkumbusha asili yake, na pia alijifunza kupitia mimi misamiati mingine ya ndani ambayo mi niliichota kwa babu yangu..
Kuna wakati tulizama katika maongezi na baba alicheka sana katikati ya maongezi sababu ya utamu wa lugha...maana story za kilugha zina utamu wake, ilimuudhi mama wa kambo akahisi ninajenga ukaribu na baba kuliko wanae.
Nilipokuwa wa pili darasani, aliniuliza unataka nini? Nikamwambia nipeleke jando, maana nilikuja mjini nikiwa bado nina "mkono wa sweta", hali hii ilinipotezea sana kujiamini mbele ya watoto wenzangu mana walinicheka sana kwa kuwa wengi kama si wote wa umri wangu washakuwa wamekata.
Mbaya zaidi na watoto wa kike mtaani walijua kuwa nina "mzula" kutokana na nilivyokuwa nataniwa. Muhula huo zawadi ya kupelekwa jando ikafa, maana baba alinambia natakiwa kwenda kijijini kwa babu na bibi. Babu alinipenda sana sasa alikuwa kaomba niende, nikapewa ahadi ya likizo ijayo kama nitafanya vizuri basi ntaenda Jando maana pia utakuwa ni msimu wa baridi kwa kidonda kupona haraka.....Muhula ujao nilikaza msuli sana lakin nikaishia nafasi ya pili darasani.
Wakati ukafika nikaenda Jando baada ya kurudi kwa babu mana nilimpa story babu za mjini navopata tabu na kuchekwa halafu dingi ananipiga kalenda. Babu yangu hakupenda sana, alipenda niende jando la porini, aliamini kutibu kidonda cha Jando kwa mitishamba ambayo huongeza nguvu za kiume, mara kidonda kikipona, aliamini kuna namna ya ufanisi kwa mwanaume aliyeenda Jando la porini na yule wa Hospitali kwa kuitibu mishipa ya fahamu kwenye kichwa cha "mjomba".
Pia, Jando la porini vijana hukaa na wazee na kufundishwa miiko na namna ya kuwa baba wa familia. Kwa kufanyiwa Tohara mjini, basi mi ningekosa hizo "fursa".
Mbaya zaidi babu alipata story za jinsi wadogo zangu wale wa mjini jinsi vidonda vyao vilikuwa vinasafishwa na nesi wa kike, jambo lililomuuzi babu, maana mila haziruhusu.. Kwetu vijana walioenda jando huitwa "Wanyamlusi". Hupewa vifimbo vidogo "sungururu" ili kujikoa kwenye "enka" ili kumtuliza "mjomba" anaposimama.
Hali ya kutailiwa iliniongezea kujiamini, nilitamani nirudi mjini haraka, hata wengi wajue kuwa hali iliyonipa unyonge wa ndani haipo tena.
Maisha kwa mama wa kambo yaliendelea, alijaribu kutengeneza ukuta kati yangu na wadogo zangu aliozaa yeye. Huku upande wa shule hali ilikuwa nzuri, nilifaulu Kidato cha Kwanza kwenda Tabora Wavulana, enzi za Tabora ya Jeshi, Afande Chacha mzee wa mwendo legeza. Nilipokuwa narudi likizo niliwafundisha wadogo zangu..
Wakakua nami nikakua, nilichaguliwa tena Tabora wavulana kwa kidato cha tano na sita, nikawa mwalimu mzuri wa tuition kwa wadogo zangu walioanza nao elimu ya upili, hawakutamani tuition za walimu wa mtaani...walinielewa...kupitia nondo zangu na mbinu za kusoma wakafanya vizuri sana..
Mwingine nilimkazania ku-reseat mpaka akaenda SHY-BUSH, Wakagundua mi ni ndugu yao mwenye upendo... Sasa wakaanza kujaribu kunipenda japo mama yao alikuwa hajawatoa kwenye minyororo ya chuki dhidi yangu.
Baba hakuwa tayari kunisifia hadharani na kunitia moyo mbele za mke wake kwa kuogopa kumuudhi. Mahali nilipofanya vizuri aliniita faragha na kunipa moyo, aliona kitu cha pekee ndani yangu, lakini kimvuli cha mama wa kambo kilimtisha!
Maisha yakaenda, wadogo zangu wakakua nami nakakua...upendo na harakati zangu zikawasogeza, walichopewa kwa siri na mama yao ili mimi nisifaidi nao wakanipa kwa siri.. Walianza kung'amua kuwa mie ni ndugu yao ninayewapenda.
Nikawa mkaka, nikaenda chuo...Nikawa sasa kama kiongozi wao, wao wakajua tofauti yetu ni mama tu lakini baba yetu ni wa wote. Ukiingia sebuleni tulipokaa pamoja na mzee huwezi jiuliza.. Maana nilifanana nae kama jezi za timu ya mpira tofauti namba tu, wakaanza kuniita kaka, tofauti ya mwanzo walipokuwa wananiita jina langu la kijijini Madeha.
Sasa tumekuwa wakubwa. Ukitukuta huwezi jua kama tumechangia baba tu, tunapendana na kuheshimiana sana. Mama(my step mother, maana sasa huwezi jua kama si mama yangu jinsi anavyonipenda) amekuwa rafiki, mambo mengine hunambia mimi badala ya watoto aliozaa, hunitumia pia kuwashauri wanae wanapoteleza...Mimi ndio muitisha vikao vya familia na kuwa katibu wa kikao cha Mwenyekiti Baba..
Haya ni maisha niliyojifunza kwa Mama wa kambo. Wakati mwingine wamama wa kambo hawana ulazima wa kuwashurutisha watoto wao kuwachukia watoto wa kambo..Kuna namna ya kuwalea na kuwaelewesha kuwa watoto wote ni ndugu. Hata Wababa pia, wawe na ujasiri wa kuwakanya wamama wanaowasumbua watoto wao wa kambo.
Hivi ni jadi Wamama wa Kambo kuwatendea sivyo watoto wasio wao? KWANINI Wababa hukosa sauti mbele ya mama wa Kambo? Na Mbona wababa wa kambo huwa hawana visa kama mama wa Kambo?