Kwanini mali za watumishi wa wananchi zinafanywa siri?

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,015
12,281
Wabunge kutoa taarifa ya mali Sheria ya 1995 Na.12 ib.12 70.-(1) Kila Mbunge atatakiwa kuwasilisha kwa Spika nakala mbili za taarifa rasmi ya maelezo ya mali yake na kadri itakavyokuwa, mali ya mke au mume wake.

Taarifa itatolewa kwa kutumia fomu maalum itakayowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge na itatolewa mara kwa mara kama itakavyoagizwa na Sheria hiyo.

(2) Spika atawasilisha kwa Kamishna wa Maadili nakala moja ya kila taarifa rasmi iliyowasilishwa kwake kwa mujibu wa masharti ya ibra hii.

(3) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka masharti kwa makusudi ya kusimamia hifadhi ya taarifa ya mali iliyowasilishwa na Mbunge kwa mujibu wa masharti ya ibara hii, na kuhakikisha kwamba watu wasioruhusiwa au wasiohusika hawapati nafasi ya kuona taarifa ya mali wala kujua yaliyomo katika taarifa ya mali.
 
Kwa sababu over 90% wako kimaslahi zaidi. Kula kwanza, utumishi baadaye, ndivyo wao wasemavyo.

Kama akipewa hamsini na 5 ya umma, tano ni ya maendeleo ya wananchi ili kuwapumbaza na kuandaa mazingira ya kura, wakati 50 inadumbukizwa akaunti binafsi.
 
Mdr kmmmk
jose-mourinho.jpg
 
Hili laweza kuwa halisi pale ambapo wabunge ni watu wa kujitolea, walioridhika kuliko ilivyo sasa ambapo ubunge ni njia ya kujitafutia maslahi zaidi.
Utamaduni uliojengeka ni kwamba ubunge, uwaziri na hata urais ni ulaji (Kuongeza na kujilimbikizia mali). Sababu kubwa ni umasikini wa jamii kwa ujumla (fikra na mali).
Hata hivyo, tunahitaji viongozi walioridhika, wasio na tamaa na waliostaarabika ambacho ndiyo changamoto.
 
Hii inaondoa maana ya kutaja mali za mtumishi, kwasababu sisi tunapswa kuzifahamu kabla hatujamkabidhi ofisi ya umma. Ili akiiba au akiondoka na mali zaidi ya kiasi tulichomlipa tumuulize kazitoa wapi.
 
Back
Top Bottom