Hapo ndo waislamu mnafeli kujitetea, kama maana yake ni Amani iwe nanyi, kwa nini asiongee kiswahili hadi aongee kiarabu. Je, wote watanzania wanajua kiarabu?Asalamu alaykum ni salamu na maamkizi kwa maana ni amani iwe juu yenu, haijalishi anayesalimiwa ni muislamu au siyo, lakini tumsifu Yesu Kristo au Bwana Yesu asifiwe siyo maamkizi kwani hata Yesu mwenyewe aliwafundisha wanafunzi wake waseme amani iwe kwenu Mat. 10:12 na Yesu mwenyewe alisema amani iwe kwenu John 20:19-21. Hivyo kuombeana amani kwa anayetaka amani ndiyo salamu na maamkizi bora hususan kwenye jamii ya watu wa imani tofauti.
Sijasema kwa maana ya hoja iliyopo. Ilo ni Tatizo kubwa kwa Waislamu, waislamu wengi unakutana nao utasikia Asalaam Alaykum, bila kujali huyu mtu anajua kiarabu au hajui.
Tumieni lugha kulingana na mazingira, linaweza likawa neno la kawaida ila kwa vile halipo kwenye lugha inayoeleweka kwa wengi katika jamii ya kitanzania inaleta mkanganyiko.
Mfano ukitumia lugha ya kiswahili ukawakuta watu, ukasema Amani iwe nanyi, hapo awe wa dini yoyote hadi mpangani ataitikia vizuri bila kua na maswali maswali.
Tutumie lugha kulingana na mazingira