Kwanini Makamu wa Rais hasemi "Bwana Asifiwe"?

Kwanini Makamu wa Rais hasemi "Bwana Asifiwe"?

Ndo tabia za Waislam wengi. Ukikutana nae, anataka akusalimie Asalam Aleykum, Wakati wewe ukimsalimia Shalom au mwana kondoo ameshinda, haitikii.

Binafsi mtu akinisalimia kiislam, siitikii.
Though, kwa Sudan hata kanisani huwa tunasalimiana Asalam Aleykum na haina shida.
Unakataa salam alaikum unakubari Shalom! Unaijua maana ya Sharom?
 
Kwa nini anatumia lugha ya kiarabu kwa watu wanaotumia lugha ya kiswahili na lugha zao nyingine za asili?
Mkuu mpaka hapo tu nawewe umetumia baadhi ya maneno ya kiarabu LUGHA.
 
Hapa ni kuwahi beche tu.

But mbona kakobe ni mkristo na hapotezi muda kwenye kufungisha ndoa ?
Ndoa za wakristo zina complication nying Sana mkuu , mpak mchungaji anakufungisha ndoa ushalipa charges kibao umempa mpak na hela ya mafuta ya gari ....kwenye mazishi ndo usiseme , mtu anakufa Leo maiti inakaa wiki nzima anasubiriwa sjui nani nani yupo ulaya na usenge usenge mwingi tuu....aaah, waislam hawana hzo aisee ukifa leo wakikustahi Sana utazikwa kesho ila ikiwezekana unazikwa Leo hii hii
 
Na kwny kutoa roho, ni kujilipua tu BOOM, kisha yalaaah...!!!

Wamemaliza kazi Mtu anaenda kupokea bikira zake 72 akhera

Takibiiir
Maneno tu na mawazo ya wajinga, uislamu hauruhusu jambo hilo ndugu.
 
Badala ya kutumia kiarabu basi awe anayatamka hayo maneno kwa Kiswahili
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mkichoma nyumba za wapemba zikimalizika mtaanza kujiuliza mbona za wachaga hatuchomi.
Mlifanya kila aina ya figisu kuondoa upinzani kwenye gemu, sasa hakuna wakumshambulia mmeanza kutafutana wenyewe kwa wenyewe.
Tukija kwenye hoja yako, kwanza ungeangalia maana halisi ya hizo ulizoita salamu kuu za kidini.
"Tumsifu yesu kristo au Bwana yesu asifiwe" kwa muislamu sio salamu bali ni kumtukuza yesu. Na salamu anayoikubali muislamu ni ile ya yesu mwenyewe alipo watokea wanafunzi na kuwaambia "Amani ya bwana iwe nanyi" na hii ndio maana ya neno Assalaamu alaykum.
Kwa maana hiyo hakuna picha yoyote mbaya anayoijenga makamu wa rais.
 
Hata Tulia juzi alisema Bwana Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristu na hakusema Asalam Alaykum
 
Watanzania karibia wote wanajua Kiswahili na wengi wanajua Kingereza ukilinganisha na Kiarabu, waliopitia madrasa ndio wanajua Kiarabu.Ukitumia lugha ya Kiarabu utaelewaka zaidi na wenzako mliopitia madrasa ila wengine utawaacha gizani.
Kusalimiana ni sehemu ya utamaduni wetu. Lakini kwa vile udini umetutawala basi maneno yoyote ya kiarabu tunayaona ya kiislamu. Mtu akisema "inshallah " tunamuona mdini lakini akisema " thank God" tunaona ni kawaida tu.

Amandla...
 
Ndoa za wakristo zina complication nying Sana mkuu , mpak mchungaji anakufungisha ndoa ushalipa charges kibao umempa mpak na hela ya mafuta ya gari ....kwenye mazishi ndo usiseme , mtu anakufa Leo maiti inakaa wiki nzima anasubiriwa sjui nani nani yupo ulaya na usenge usenge mwingi tuu....aaah, waislam hawana hzo aisee ukifa leo wakikustahi Sana utazikwa kesho ila ikiwezekana unazikwa Leo hii hii
UONGO HUO.

Hakuna Mtu au Mtumishi yeyote anayekulazimisha uweke maiti yako muda mrefu.

Hakuna Mtu/ Mtumishi wa kanisa lolote anayekulazimisha ufanye sherehe yoyote iwe ya nafuu au ya gharama, yeye atakuambia tu ufunge NDOA ambayo ipo kibiblia, ni agizo la Mungu.

KWAHIYO, kuweka maiti sana au kuweka kamati ya muda mrefu na kufanya sherehe ni makusudio ya Wanandoa wenyewe na ndugu zao na sio UKRISTO.

Ndugu yako akifa leo jioni muite mchungaji/Padri aje kuzika kesho asubuhi uone kama atakataa.

Ukiwa na mchumba wako nendeni kanisani mkiwa na Wazazi wenu kama mashahidi uone kama ndoa haijafungwa.

UKRISTO auhusiki hapo ni mipango yenu wenyewe.
 
Maneno tu na mawazo ya wajinga, uislamu hauruhusu jambo hilo ndugu.
...
images%20-%202020-12-27T014026.218.jpg
 
Assalam alaykum, ina maana ya Amani ya Bwana iwe pamoja nawe. Na ndio salam sahihi tokea enzi za manabii. Hivyo kama wakristo wangekuwa wanasalimiana kwa kusema Amani ya bwana iwe pamoja nanyi,basi hata kwa makamo wa rais isingekuwa shida. Lkn ukisema bwana Yesu asifiwe imekaa kiimani zaidi kwa upande wa kikristo sio ki salam.
 
Haya mambo ya Dini ukiwaza sana unaweza ukajikuta unapotea zaidi, hayahitaji complications sana ki hivyo.

Hizi salamu ni lugha tu imebadilika, lakini ukute hata hazina impact kihivyo. Mfano Asaalm Alaykum ni kiarabu ambacho tafsiri yake kiswahili ni "Nakusalimu". Kwa hiyo hata Mkristo ukisema Asalam Alaykum unakua umesema Nakusalimu ila tu katika Lugha ya Kiarabu (Sio Kiislam) .

Au mfano salam kama "Bwana Yesu Asifiwe", kama Muislam unaamini kua katika Binadamu Waliotumwa (Mitume) na Mungu kuja kueneza dini yake na Yesu pia Yumo basi hakuna shida akipewa sifa, sawa tu akipewa sifa Mussa, Daudi, etc. Yaan Mungu alitutumia wanadamu Mitume Mbalimbali hivyo kusema fulani kati ya hao apewe sifa sio kosa au tatizo.
usijaribu kuipaka paka batil rang iwe haki.haki ipo waz batil ipo waz.zitakuja zama za mwisho watu watatafutia majina mazuri dhamb mfano pombe zitaitwa majina mengine mengine na vitu kama hivyo.
kila din ina misimamo yake.ukimforce mtu atoe salam ambayo inakwenda ku jeopardize iman yake entirely hawez kuitoa na elim kwel kwel niliona pale.nakushauri tulia em chimba uliza hata kwa watu wa karibu unaoamin wamesoma kwa nin salam hio uliyotaka itolewe ina jeopardize iman.completely inakutoa nje ya reli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu, heshima kwenu!

Ukifuatilia hafla nyingi za awamu hii ya 5, viongozi wamejijengea tabia ya kuanza hotuba zao kwa kutoa salamu kuu za kidini kama "Asalaam Aleiykum", " Tumsifu Yesu Kristo", "Bwana Yesu Asifiwe" nk

Imekuwa hivi sana kwa Mh. Rais Magufuli, Waziri Mkuu na pia kwa mawaziri na viongozi wengi wa juu.

Lakini hali ni tofauti kwa Makamu wa Rais, mama Samia. Ukifuatilia ufunguzi wa hotuba zake, huishia tu kusema "Asalaam Aleykum". Hasemi zile salamu nyingine za Wakristo.

Hii inajenga picha gani, wakuu?
We ndiyo bwege kabisa yaani bado unatukuza ukoloni kwa salamu za kiarabu na kizungu walizokukaritisha kupitia kuruan na biblia,badilika kwani Iafrika hausmini ktk hayo masalam mzee
 
Inajenga picha kwamba sio mnafiq.

Huyo mama kwanza sio muongo muongo maana kama mnakumbuka alivyosema kipindi kile cha kampeni kwamba hata mkimpgia kura mgombea mwingine lakini wa CCM ndio atakayeshinda. Kwani aliongopa?
Acha uchozi unataka kusema mlishinda mkaibiwa kura?

Hakuna upinzani wa kiasa Tz mmekalia majungu,umbea,roho mbaya,uchochezi,nk
 
Salam za kinafiki tu. Kwanza mimi nashangaa mtu kusema Tumsifu Yesu Kristo alafu tena Bwana Yesu asifiwe! Hapa tu ni unafiki kwa salamu hizi! Kama ukitumia salamu mojawapo hapo kuna shida gani?

Alafu salamu za kidini za nini? Hii imeanzia utawala wa JK alafu awamu hii ndio imepamba moto!!
 
Samia namuunga mkono! Kwanini aseme salamu asizoamini? Salamu za kidini ni ibada! Ni unafiki kusema salamu za dini zote!
 
Hapo ndo waislamu mnafeli kujitetea, kama maana yake ni Amani iwe nanyi, kwa nini asiongee kiswahili hadi aongee kiarabu. Je, wote watanzania wanajua kiarabu?
Sijasema kwa maana ya hoja iliyopo. Ilo ni Tatizo kubwa kwa Waislamu, waislamu wengi unakutana nao utasikia Asalaam Alaykum, bila kujali huyu mtu anajua kiarabu au hajui.
Tumieni lugha kulingana na mazingira, linaweza likawa neno la kawaida ila kwa vile halipo kwenye lugha inayoeleweka kwa wengi katika jamii ya kitanzania inaleta mkanganyiko.
Mfano ukitumia lugha ya kiswahili ukawakuta watu, ukasema Amani iwe nanyi, hapo awe wa dini yoyote hadi mpangani ataitikia vizuri bila kua na maswali maswali.
Tutumie lugha kulingana na mazingira
Payrol, haya ni maamkizi ambayo waswahili wameshayazoea kuamkiana nayo, kwa kuwa uswahili una athari ya uarabu ndiyo maana ukakuta kuna maneno mengi ya kiarabu tunayoyatumia katika kiswahili ambayo hayana mjadala wowote lakini kwa kuwa kuna watu wamekuwa programmed kuuchukia uislamu na uarabu wanaona utumiaji wa asalamu alaikum ni udini hiyo ndiyo shida. Siku kama Alkahmis na Ijumaa mbona tunazitumia katika kiswahili sijasikia watu wakisema tunatumia kiarabu? Maneno kama dini, sala, ibada ,imani, hukumu, siasa , maisha, raha, salama n.k yote haya ni asili yake kiarabu na ni maneno ya kiswahili fasaha mbona watu hawasemi yabadilishwe? Kuna neno la kadamnasi (kidaam-un-naas) ni neno la kiarabu lenye maana ya mbele ya watu mbona linatumika sana? Hivyo asalam alaikum ni maamkizi kama maamkizi mengine yanayotumika kwenye lugha ya kiswahili mfano "shikamoo", "cheichei" , "habari yako" na bila kusahau maamkizi ya kisasa "mambo?"
Kama kweli utakuwa huna dhana mbaya basi utaelewa matumizi ya lugha kutokana na mazingira, hivi kweli kusema bwana Yesu asifiwe au tumsifu Yesu Kristo ni maamkizi ya kutumiwa na waswahili? Kama kusema asalamu alaykum kunaleta ukakasi basi tuwaombe wanasiasa wasisalimie watumie maamkizi ambayo unaweza ukayapendekeza wayatumie ambayo unahisi hayatoelemea katika imani ya dini yoyote. Kumbuka hata Yesu alisema "shalom alaichem".
 
Back
Top Bottom