Kwanini Makamu wa Rais hasemi "Bwana Asifiwe"?

Kwanini Makamu wa Rais hasemi "Bwana Asifiwe"?

Ubaguzi wake umetoka wapi????? Yeye ni muislamu na uislamu umetutaka tusalimiane salam yetu "Assalaam alaikum=iwe juu yenu amani" , na sio shikamoo, bwana yesu asifiwe n.k.
Kwani Waarabu Wakristo wanasalimianaje?
 
Salam za kinafiki tu. Kwanza mimi nashangaa mtu kusema Tumsifu Yesu Kristo alafu tena Bwana Yesu asifiwe! Hapa tu ni unafiki kwa salamu hizi! Kama ukitumia salamu mojawapo hapo kuna shida gani?

Alafu salamu za kidini za nini? Hii imeanzia utawala wa JK alafu awamu hii ndio imepamba moto!!

..ni kweli salama za kidini zilianza ktk awamu ya JK.

..lakini mimi sikumbuki kumsikia JK akitumia salamu hizo.

..ukichunguza utakuta wanaotumia salamu hizo ni wale wenye uwezo mdogo wa kuzungumza na kujenga hoja majukwaani.

..kwa maoni yangu, ni vizuri tukatumia salamu zinazotuunganisha waTz wote, au hata tukatumia salamu za vyama vya siasa.
 
Asalaam aleikum ni salamu zinazotumiwa sana na watu wa pwani na visiwani. Ni kama vile visiwani hawasemi "shikamoo" kama tulivyozoea sis watu wa bara. Kwa vile mhusika ni mtu wa visiwani aachiwe asalimie kwa namna alivyozoea. Ni kiswahili cha unguja, tusiwalazimishe watumie cha kwetu. Kama vile ambavyo wanavyotumia maneno kama tungule, mfereji, buku n.k. hili nalo tuwaache waendelee kutumia. Tusiingize udini kwenye hili.

Amandla...

..wanaotumia salamu hizi ktk shughuli za kisiasa wamelenga UDINI.

..wanaamini wakisalimia "asaramareko" na "bwana yesu asifiwe" wanaleta usawa wa kidini.

..Sasa VP Samia Suluhu kutumia salamu ya upande mmoja uliolengwa na waanzilishi wa salamu hizo ndio kunaleta mgogoro huu unaouona hapa.
 
Kwani kabla ya Mtume (SAW), Waarabu walikuwa hawasalimiani?
Unaijua salamu ya waarabu wasiokuwa waislamu wewe? Hata "marhaba" ni salamu ya waarabu pia, "A'salaam Alaykum" imekuja mara ya kwanza katika qur'an.
 
Unaijua salamu ya waarabu wasiokuwa waislamu wewe? Hata "marhaba" ni salamu ya waarabu pia, "A'salaam Alaykum" imekuja mara ya kwanza katika qur'an.
..unayosema ni kweli.

..lakini wanasiasa wanaotumia "a'salaam aleikum", "asarama-reko," hapa Tz wamewalenga Waislamu.

..Ni vyema tukaachana na salamu za Kidini tukawa na salamu za KITAIFA/KITANZANIA.
 
Wakuu, heshima kwenu!

Ukifuatilia hafla nyingi za awamu hii ya 5, viongozi wamejijengea tabia ya kuanza hotuba zao kwa kutoa salamu kuu za kidini kama "Asalaam Aleiykum", " Tumsifu Yesu Kristo", "Bwana Yesu Asifiwe" nk

Imekuwa hivi sana kwa Mh. Rais Magufuli, Waziri Mkuu na pia kwa mawaziri na viongozi wengi wa juu.

Lakini hali ni tofauti kwa Makamu wa Rais, mama Samia. Ukifuatilia ufunguzi wa hotuba zake, huishia tu kusema "Asalaam Aleykum". Hasemi zile salamu nyingine za Wakristo.

Hii inajenga picha gani, wakuu?
Acha uboya..
Kwanza ungejiuliza nini maana ya hiyo salam alafu ujiuluze inamhusu nani katika hao anaowasalimia.je Angesema gudimoningi ungeuliza anamsalimia nani? Acheni uzwazwa wenu..
 
..unayosema ni kweli.

..lakini wanasiasa wanaotumia "a'salaam aleikum", "asarama-reko," hapa Tz wamewalenga Waislamu.

..Ni vyema tukaachana na salamu za Kidini tukawa na salamu za KITAIFA/KITANZANIA.
Salam ya kitaifa ndo ile Tumsifu Yesu😂😂
 
Ana ijua imani yake. Hata wewe Mkristo unae sema Asalaam aleikum una kosea maana sio imani yako
Wewe ndo unakosea maana ungejua maana ya hiyo salam usingepumbaa akili na ubongo
 
Picha anayoijenga kuwa nyinyi mna imani zenu na yeye ana yake, maneno maneni ya nini?
 
Waislam nawakubali kwenye mazishi na ndoa, no wastage of time ....
Hapo kwenye mazishi napenda sanaaaa😆 siyo wakiristo watakuacha ulie had machozi yakukauke😆😆 ila sasa kama ulikuwa unabipu haujafa, ndugu yangu utafufuka huku ukisikia tope jekundu likipga juu😅😅😅
 
Back
Top Bottom