Kwanini maisha ni Ubatili?

Kwanini maisha ni Ubatili?

Hakika huu ni ubatili Mkuu, anashukuru kwa kutokufa wakati lazima tu atakufa. Anavyoshukuru ni kama hatokuja kufa tena.
Kuna muda ukitafuta maana halisi ya haya maisha unagundua hata maana yenyewe haina maana kwasababu hiyo maana haitodumu kwamaana utakufa na kuiacha,so hakuna maana.
Angalia tu ile ajali ya ndege ,ndoto nyingi zimepotea ,yaani ujujua mwingi binadamu ila hajui hata sekunde moja mbele atakuwa wapi.

Honestly ,mimi tangu nitambue sina mipango ya muda mrefu japo nina mafanikio sijawahi kuhofia mbele sana ila najua nitakufa .
 
Ili uchelewe kukufa
Ila mwisho wa yote utakufa tu,nini maana ya kuhangaika au kuhofia kifo ambacho hujui kitakukutia wapi na saa ngapi.

Mwaka 2018 nilikua namuuguza jamaa yangu wa karibu,usiku mmoja alikuja mgonjwa yuko mahututi sana. Madaktari na wataalamu mbalimbali wa afya walijitahidi mpaka yule jamaa akawa sana kabisa mpaka inafika asubuhi.
Kuliookucha jamaa alikua fit kiasi ukilinganisha na hali aliyokua nayo,basi jamaa aliamka pale akaenda toilet,akanywa uji,n.k na kuanza kutupigisha story mle wodini. Zaidi alimshukuru sana Mungu kwa kumuepusha na umati kwasababu bado ana mipango mingi na tegemezi wengi sana.

Tulipiga story kama nusu saa hivi,jamaa akarudi zake kulala hapo kitanda. Na alipolala hakuamka tena ikawa ndio bye! bye! (R.I.P).

So unaona jinsi maisha yanavyopoteza maana.
 
YESU alikuwa na mambo ya chini chini sana ila chakula chake kikuu ilikuwa samaki na mikate na divai mara moja moja. Yumkini ameacha mali nyibgi sana ambazo ndugu zake hawana taarifa nazo
Yule mwanamke kisimani hajamuachia watoto kweli? Au Mariam Magdalena, usikute kuna ambayo tulifichwa.
 
Ila mwisho wa yote utakufa tu,nini maana ya kuhangaika au kuhofia kifo ambacho hujui kitakukutia wapi na saa ngapi.

Mwaka 2018 nilikua namuuguza jamaa yangu wa karibu,usiku mmoja alikuja mgonjwa yuko mahututi sana. Madaktari na wataalamu mbalimbali wa afya walijitahidi mpaka yule jamaa akawa sana kabisa mpaka inafika asubuhi.
Kuliookucha jamaa alikua fit kiasi ukilinganisha na hali aliyokua nayo,basi jamaa aliamka pale akaenda toilet,akanywa uji,n.k na kuanza kutupigisha story mle wodini. Zaidi alimshukuru sana Mungu kwa kumuepusha na umati kwasababu bado ana mipango mingi na tegemezi wengi sana.

Tulipiga story kama nusu saa hivi,jamaa akarudi zake kulala hapo kitanda. Na alipolala hakuamka tena ikawa ndio bye! bye! (R.I.P).

So unaona jinsi maisha yanavyopoteza maana.

Duu, it's sad story, but alikufa kifo kizuri sana. Alikufa huku anaongea na bila kuwasumbua watu wake kumuuguza
 
Unapambana na kujinyima ili kujenga kitegauchumi chako baada ya kuzeeka na kufariki watoto wanakiuzilia mbali na kutumia pesa yote kwenye starehe:
Ukiwa duniani mche Mungu na tafuta mali ili ikuwezeshe kuishi maisha yako wewe mwenyewe ukiwa hapa duniani:

Watoto haki yao ni kuwapa elimu tu, ili iwawezeshe kujitegemea kama ilivyo kwako:
 
Hatari Sana ndugu😁..wanadai Kuna peponi ambako hakuna dhiki Wala njaa,na ili ufike Kuna sheria tena wamekupangia na kukuwekea usimamizi wa sheikh & padri.ushenzi mtupu😓
 
“Kwa nini maisha ni ubatili” ni la kina sana—ni swali ambalo watu wengi mashuhuri wa falsafa, dini, na roho wamejiuliza kwa maelfu ya miaka. Hapa kuna majibu kwa mitazamo mbalimbali:

1. Mtazamo wa Biblia – Kitabu cha Mhubiri

Katika Biblia, hasa kwenye Mhubiri 1:2, inasema:


Maana yake ni nini?

Maisha ya mwanadamu huwa mafupi, yenye tabu, na vitu vyote tunavyofanya vinaonekana kuwa havina maana ya kudumu.

Mali, heshima, furaha za muda – vyote huisha.

Mwanadamu huzaliwa, huteseka, hufa – na dunia huendelea kama vile hakuwahi kuwepo.

Lakini mwisho wa kitabu hicho, Mhubiri anasema:


(Mhubiri 12:13)

Hii ina maana: Maisha yanapata maana yake ya kweli pale tu yanapomrudia Muumba.

2. Mtazamo wa Falsafa ya Kifalsafa (Existentialism)

Wanafalsafa kama Jean-Paul Sartre na Albert Camus walisema: maisha hayana maana ya asili – ni mwanadamu anayepaswa kuyapa maana.

Camus alisema maisha yanaonekana kuwa ubatili kwa sababu ya mateso, mauti, na kutokueleweka, lakini mwanadamu anaweza kuishi kwa ujasiri kwa kuyakubali hayo na kuumba maana ndani yake.

3. Mtazamo wa Kiroho wa Kina (Metaphysical)

Maisha ya duniani yanaweza kuonekana kuwa ubatili kwa sababu ni kivuli cha maisha ya kweli ya kiroho.

Sisi si miili tu – bali roho zilizotumwa duniani kwa muda mfupi.

Maisha ya kimwili ni somo, mtihani, au hatua ya mabadiliko ya nafsi kuelekea kwenye nuru au uzima wa milele.


4. Kwa Nini Maisha Yanaonekana Ubatili?

Kwa sababu:

Hakuna kitu cha kudumu (kila kitu huchakaa na hufa)

Maumivu, magonjwa, kifo haviwezi kuzuiliwa kabisa

Mali na heshima haviwezi kutufanya kuwa na amani ya kweli

Binadamu hawezi kuelewa kila kitu kwa akili yake ndogo


Lakini:



Twende sawa vichwa vigumu vinahitaji hapana.
Ni kweli maisha haya ni ubatili mtupu kwa mtu asiye na Kristo Yesu moyoni mwake. Wenye Yesu mioyoni mwao wana kitu kinachoitwa AHADI YA UZIMA WA SASA NA ULE UTAKAOFUNULIWA BAADAE.
Kila nikifikiria ubatili wa maisha haya,ndipo nazidi kumshukuru Yesu kwa kuja.

Ndio maana siku zote namwomba anisaidie niyafanye mapenzi yake kwa muda alionipa wa kukaa hapa duniani nikijua kwamba Mimi ni mvuke tu!
 
Naona wengi tunapata tabu sana kuhsu kufahamu lengo halisi la sisi kuletwa duniani,ila ndg zangu kwa yeyote anaehtaji kufahamu lengo la kuletwa kwake Hapa Duniani Basi namsihi atenge muda asome kitabu Cha Quran tukufu,kitabu kinachosomwa na waislam.
Quran imetoa majibu yote Khs Kwann sisi tupo Hapa duniani.
Moja ya mistari inayoelezea Hilo ni Hapa Mungu muumbaji aliposema ktk Quran kwamba "HATUKUUMBA MAJINI NA WATU ILA WAPATE KUNIABUDU"....Hapa Kwenye "KUNIABUDU" ndipo unahitajika kuipata elimu yake na hapo ndipo lilipo jibu la Haya yote tunayojadili hapa ikiwemo Hili neno "PUMBAO LA DUNIA"
Someni Quran ndg zangu Mungu ameweka majbu yote hapo.
Ni kweli kwamba kwenye hicho kitabu kuna ahadi ya mabikra 72 peponi?
 
Back
Top Bottom