Kwanini maeneo ya jeshi kama Lugalo na External kumejengwa bar na frame nyingi sana?

Wakuu ikipita barabara ya external kwenda maji chumvi unapita eneo la jeshi, limejaa bar na frame.

Hali iko hivyo ukipita Lugalo, kumefunguliwa frames nyingi sana kwenye eneo la jeshi.

Swali, je, jeshi letu limeona uwekezaji pekee wanaweza kufanya kwenye maeneo yao ni kufungua bar na frame tu?

Jeshi letu lina maeneo potential sana, mazuri ambayo wangeweza kualika wawekezaji wakubwa wa kujenga shopping centres ama malls, recreational centers, na uwekezaji mkubwa kuliko huu wa bar na frame.

Je jeshi letu limekosa washauri wazuri wa uwekezaji wa ndani ama hata wa nje hadi kuwekeza kwenye bar na frame?


Naunga mkono na miguu hoja ya Recreational centers.

Hali ya maisha ya watu wa Dar inaziitaji sana hizo kusaidia kupambana na Tatizo la maradhi ya akili/fahamu.


Maajabu ni kwamba wanatumia Bar Kama mbadala wake.
 
Wamewekeza kwenye sekta nyingi nyingi tu mpaka usafi, afya, ujenzi ulinzi kupitia kitengo chao cha SUMA JKT
Fremu hizo pia zimejengwa Kigamboni ferry
Wanastahili pongezi kwa mafanikio haya na kuongeza ajira kwa vijana na wataalamu wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia hata kilimo mfano makotopola dodoma wanamashamba makubwa ya zazibu

Ukienda ruvu wanafunga sana

Mlale songea wanalima sana mahindi n.k
 
Kuna Uzi humu Jf unalaumu vitambi Kwa baadhi ya maofisa wa jeshi na hii ndio sababu.Karibu mikoa yte nliyozurura iwe Kambi ya FFU,jeshi,au polisi Kuna bar ambazo zimepewa majina mazuri mazuri kama police mess n.k.Na Kuna nyama choma na bia za bei ya punguzo na ukiwa polisi unaruhusiwa Kukopa.
Sasa vitambi vitaachaje kuchomoza?
 
Naunga mkono na miguu hoja ya Recreational centers.

Hali ya maisha ya watu wa Dar inaziitaji sana hizo kusaidia kupambana na Tatizo la maradhi ya akili/fahamu.


Maajabu ni kwamba wanatumia Bar Kama mbadala wake.
Kwa maeneo ya jesho, wajenge hata residential complex na watapata hela nyingi sana.

Ama wawape NHC ama TBA hayo maeneo waingie ubia na watu wajenge residential complex zenye maduka na recreational centers za kueleweka kuliko hizi bar na frames.
 
Kwa maeneo ya jesho, wajenge hata residential complex na watapata hela nyingi sana.

Ama wawape NHC ama TBA hayo maeneo waingie ubia na watu wajenge residential complex zenye maduka na recreational centers za kueleweka kuliko hizi bar na frames.

Tatizo hayo maeneo. Wanajeshi wanapewa kipaumbele wenyewe kwa kuuziwa kwa bei nafuu. Imagine ubungo ya leo hii mwanajeshi anauziwa kiwanja kilichopimwa kwa milioni 10

Hao wanajeshi wakishauziwa na wao wanauza
 
Kipindi majeshi mengine duniani yana ongoza kwa kufanya tafiti za silaha mpya na mambo mengine ya kijamii huku kuna jeshi liko "bize" kujenga maduka, kuonea raia, kuvunja matofali na kuiba wake za watu, kupanga ni kuchagua
 
Ofcourse zilitangulia na miaka hiyo zilikuwa ziko nje ya jiji. Lakini bila shaka kutangulia siyo kigezo cha kuziacha ziendelee kukaa wakati mazingira yamebadilika.


Sio lazima wahame, wanaweza kubadili matumizi na kuweka kitu chenye manufaa kwa wote jeshi na wananchi Kama vocational training centers, vyuo vidogo vya tafiti na gunduzi mbali mbali, hospitals etc.
 
Back
Top Bottom