Zee la Nyeti
JF-Expert Member
- Aug 5, 2014
- 702
- 470
Wengi wanalia kwa sababu trip za kuonana na michepuko yao zinapigwa pin,
Kulia kunatokana na kwamba..binti amelelewa tangu udogoni na familia yk..na ameizoea..kile kitendo cha kuondoka nyumbani ni cha huzuni..sababu anaenda anza maisha mapya na mtu ambaye mmejuana ukubwani....
Nimependa ulivyoandika. Una umri gani? (najua wadada hampendi hili swali)
yeah..muda wa sadaka..mi sina sadaka..nimeamua nijiupdate kidogoDah jf hadi chach?
hhahahaah!!! yani umenifanya nitoke church ili nikaangue kicheko nje
mkuu misa ishaisha..next tym ntakushtua kama vipiKiongozi umesali wapi nije nijiunge?
Analia kwa furaha kwamba anakwenda kumiliki dushelele kihalali
Na ndio maana nikakuuliza coz nimehisi origin yake, japo hata mimi sijui lina maana gani..!hata sijui maana yake lakini najua ni jina zuri la kipare. Nandera ni mtoto flani kule arusha nilikuwa nampenda sana enzi hizo.
1. Furaha
2. Kuacha familia, sio siri nikiwatazama wadogo na kaka zangu na ndugu niliokuwa naishi nao nyumbani, utani, ucheshi, furaha aisee lazima nilie, kaka zangu huwa wanatabia ya kunibeba juu mara kwa mara hafu wananizungusha aisee lazima nilie, huwa tunafungua muziki na kucheza pale sebuleni huku mama akituona anacheka sana aisee lazima nilie, kaka zangu wana vituko hadi raha aisee lazima nilie. Kubwa zaidi mimi ndio pekee binti nyumbani wengine wote madume aisee lazima nilie, nikimcheki mama lazima nilie. Sorry kwa maneno mengi lakini umenifanya nilie hata kabla sijafikia kuolewa, oh shit! lakini lazima niolewe.
Bwana Harusi, kwanza hongera kwa kutekeleza wajibu wako kwa jamii, wazazi na kwa Mungu kwa kufunga Ndoa!
Ni mara chache sana siku hizi kuona Bibi Harusi akitoa machozi siku ya Harusi. Wengi wao macho makavu kuangalia zawadi gani imetoka na nani ametoa - kibiashara zaidi!
Kwa maoni yangu hakuna atakayekuja na jibu moja kuhusu kwa nini Bibi Harusi atoe machozi siku ya Harusi.
Vilevile kwa maoni yangu usimuulize Mkeo sababu ya kutoa machozi. Tunza hiyo kumbukumbu ikufariji katika kila utakapopitia katika vipindi vigumu huko mbele. Just treasure the memory - it is unique!
Mpende na kumuheshimu Mkeo. Fanya kazi halali kwa bidii ili utunze familia yako. Siku za Ibada (bila kujali imani yenu) nendeni kusali - pamoja! Mtangulizeni MUNGU katika maisha yenu - A Family Which Prays Together, Stays Together!
Mungu abariki kazi za mikono na akili zenu na awajalie kila lililo la heri katika maisha yenu. Awajalie maisha marefu ya furaha na ya mafanikio - muishi kuona na kufurahia mafanikio ya wajukuu ma vitukuu wenu! Amina.
Wataalamu watakuja na majibu zaidi!
Na mimi hadi nimelia baada ya kusoma uzi wako,nakuomba nikuoe aisee,hebu kuja pm.