Lee Cho in
JF-Expert Member
- Apr 13, 2015
- 941
- 693
Bwana Harusi, kwanza hongera kwa kutekeleza wajibu wako kwa jamii, wazazi na kwa Mungu kwa kufunga Ndoa!
Ni mara chache sana siku hizi kuona Bibi Harusi akitoa machozi siku ya Harusi. Wengi wao macho makavu kuangalia zawadi gani imetoka na nani ametoa - kibiashara zaidi!
Kwa maoni yangu hakuna atakayekuja na jibu moja kuhusu kwa nini Bibi Harusi atoe machozi siku ya Harusi.
Vilevile kwa maoni yangu usimuulize Mkeo sababu ya kutoa machozi. Tunza hiyo kumbukumbu ikufariji katika kila utakapopitia katika vipindi vigumu huko mbele. Just treasure the memory - it is unique!
Mpende na kumuheshimu Mkeo. Fanya kazi halali kwa bidii ili utunze familia yako. Siku za Ibada (bila kujali imani yenu) nendeni kusali - pamoja! Mtangulizeni MUNGU katika maisha yenu - A Family Which Prays Together, Stays Together!
Mungu abariki kazi za mikono na akili zenu na awajalie kila lililo la heri katika maisha yenu. Awajalie maisha marefu ya furaha na ya mafanikio - muishi kuona na kufurahia mafanikio ya wajukuu ma vitukuu wenu! Amina.
Wataalamu watakuja na majibu zaidi!
nimejifunza ktu kutoka kwako asante xana mkuu