Kwanini mabibi harusi wengi wanapenda kulia siku ya ndoa?

Kwanini mabibi harusi wengi wanapenda kulia siku ya ndoa?

Hahaha unaguna? ?? Ndio hivyo...kwangu mimi nililia nikiwaza hapo tu....nilivyokuwa najaliwa na kupendwa home na kupewa hitaji lolote..je mume atafanya km kwetu...especially km mimi ni lastborn naondoka uwiii...upweke wanaobakinao lol
Ok.hapo sawa.
 
Tafsiri zaidi ya moja:-

Familia alioizoea (Baba, Mama, Dada, Kaka, Ndugu, Watu wa karibu) kuiacha na kwenda kuanza maisha mapya.

Furaha iliyopitiliza kikomo.

Kutokuamini kama kweli anaolewa siku hiyo, pengine alishakutana na vikwazo tele kuhusiana na kuolewa na ikashindikana.

Pengine hakuwa tayari kuolewa ila alilazimishwa na wazazi wake.

Kwa kweli kama nilivyosema hapo juu, kuna mengi na haya niliorodhesha ni machache tu
 
Hodi wanajamvi wakuu wa JF,

Najitokeza hapa kwa mara ya kwanza, kwanza nitoe shukrani kwa jinsi mnavyodadavua mada husika, Nimeoa hivi Karibuni, hivo siku ile ya harusi tulipotoka tu kanisani na kujumuika katika ukumbi wa BZ HOTEL basi bibi arusi alikuwa akitoa matone ya chozi moja, moja, huku wazee wa hekima wakitoa neno.

Ulikuwa wakati mgumu sana kwangu kuona mwenzi akibubujikwa na machozi hali ambayo ilinipa nafasi ya kufikiri mengi sana. Sasa nimekukutana na hilo la kulia kwa bibi arusi siku ya harusi, hivi maana yake ni nini?

Naomba kufafanuliwa nanyi wanajamvi...
Mwanamke ni kiumbe wa ajabu sana na kujua kilichopo kichwani kwake ni mtihani mkubwa ambao Mwenyezi Mungu ametutega.
Wewe akilini Kwako unaweza kufikiria analia Yale maneno ya wosia kutoka kwa mzazi, kumbe amemuona Ex wake aliyemtoa bikra pale ukumbini halafu Kaja na mwanamke mpya. Mambo ni mengi kwa kweli. Usijiulize sana mambo ya mwanamke, Jifunze kumpenda na kumhudumia hayo mengine waachie wana saikolojia kijana.
 
Mkuu siungemuuliza mkeo?? sasa kaishu kadogo haka kakulia mpaka ukalete hapa!!!.mkeo ndo alilia badala ya kumuuliza kwanini ulilia wewe unakuja hapa kutuuliza,au unataka kutujulisha kuwa umeoa??.
 
Back
Top Bottom