GE2025 Kwanini maandamano ya 29 October yatafeli vibaya sana

GE2025 Kwanini maandamano ya 29 October yatafeli vibaya sana

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Risasi tatu zitatosha kusambaratisha hayo maandamano kama yakitokea. Hakuna kitu Watanzania wanaogopa kama kufa. Hasa wa mijini. Ugali mtamu aisee.
 
Dadeki!
Hizi sifa duuuu! Hapo kutoboa ni ngumu hasa ukizingatia unapambana na mtu mwenye nguvu ya dola au uchumi u akili. Huwezi kutoboa
CCM kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 60 si ajali.

Hakuna sehemu ingine duniani ambako CCM ingeweza kutawala kwa muda wote huo bila kung’olewa madarakani.

Wameweza kufanya hivyo kutokana na aina ya watu wanaowatawala.
 
Maandamano ya kutaka kuisimamisha Serikali huwa hayapangwi na vikao ndugu. Mtazolewa wote na kupewa uhaini.

Yaani maandamano siku ikifika unatoka ndani, starting point na destination utazikuta huko huko mbeleni. Hapo ushajitoa riho yako yaani liwaloo na likawe.
 
Maelekezo Maalum kuhusu tarehe 29 Oktoba.

Siku hiyo kazi ni rahisi sana

Viongozi wa CCM tunaishi nao mitaani; Nyumba zao zipo mitaani kwetu, mali zao zipo mitaani kwetu.

Ofisi za CCM zipo mitaani kwetu. Ofisi za Umma nazo zipo mitaani kwetu

VItuo vya kupigia kura vipo mitaani kwetu

Mawaziri, Wabunge na Madiwani tunaishi nao mitaani kwetu, familia zao na ndugu zao tunaishi nao mitaani kwetu. Machawa na mali zao tunaishi nao mitaani kwetu.

Ndugu watanzania, mafuta ya taa, petroli na viberiti havijawahi kuwa adimu.

Tukafanye kazi iliyotukuka hiyo Oktoba 29 hadi hawa Mafisadi watuheshimu na wakome kutuchezea na kutuua.

Share na mwenzako
Wewe unayo sema maneno haya upo wapi?
Upotanzania.?
Maana wan CCM wataka kimya huku wakiona nyumba zawo na zinateketea kwa moto.
Au ndio unataka wa Tanzania wauwane wenyewe kwa wenyewe.
Katika watu millioni 60 wanao ipenda CCM wamo humoi. Unadahani wataka kimya tuu. Kuna jeshi kuna polisi kuna dola
 
Wewe unayo sema maneno haya upo wapi?
Upotanzania.?
Maana wan CCM wataka kimya huku wakiona nyumba zawo na zinateketea kwa moto.
Au ndio unataka wa Tanzania wauwane wenyewe kwa wenyewe.
Katika watu millioni 60 wanao ipenda CCM wamo humoi. Unadahani wataka kimya tuu. Kuna jeshi kuna polisi kuna dola
Niwepo wapi zaidi ya hapa hapa bongo?
 
Maandamano ya kutaka kuisimamisha Serikali huwa hayapangwi na vikao ndugu. Mtazolewa wote na kupewa uhaini.

Yaani maandamano siku ikifika unatoka ndani, starting point na destination utazikuta huko huko mbeleni. Hapo ushajitoa riho yako yaani liwaloo na likawe.
So maandamano ni kuitoa serikali ya samia na ccm madaraka au kuzuia uchaguzi?
 
Maandamano hayatakuwepo kwasababu ya unyumbu na usaliti walionao wa Tz
 
Wewe unayo sema maneno haya upo wapi?
Upotanzania.?
Maana wan CCM wataka kimya huku wakiona nyumba zawo na zinateketea kwa moto.
Au ndio unataka wa Tanzania wauwane wenyewe kwa wenyewe.
Katika watu millioni 60 wanao ipenda CCM wamo humoi. Unadahani wataka kimya tuu. Kuna jeshi kuna polisi kuna dola
Wengine wanatumwa kuja kuharibu maandamano ya AMANI, hebu fikiria polisi wakisoma haya mambo anayoyaandika watapiga marufuku fasta kwa madai kuwa kunaviashiria vya uvunjifu wa Amani.
 
Umenijibu na hujanielewa
Anyway, wenye pesa wazitunze,wente chakula mkitunze
Nawahakikishia mnaenda kuona ambayo hamkuyategemea kwa hawahawa watz wanaoonekana waoga

Ndo mtakapojua watz wa ss sio wale ,na hawana uoga tena
It's going to start km utani ila ndo hivyo
Tanzania mpya imeshazaliwa...
kiti kishachukuliwa muda spiritually...
Nilikua naku support kumjibu jamaa na maandishi yake meeengiii ambayo hayana tija .Tupo pamoja nchi tunaikomboa!
 
Yatafanyika lakini yatafanikiwa? Sio maandamano ya dakika kumi tuu alafu malengo yasitimizwe
Bro hata kama yamiwa maandamano ya sekunde 10 ni ujasiri na hayataishia hapo huo ni mwanzo..kwaiyo unataka tuvumilie kutawaliwa na mzanzibari asokua na utu kwa muda wa miaka mi 5 tukae kimya kama mandezi?haiwezekani hioo
 
MAANDAMANAO YA 29OCT YATAFELI VIBAYA MAPEMA SANA KUTOKANA NA SABABU KUU ZIFUATAZO;


Anaandika, Robert Ng'apos Heriel
Mtibeli


1️⃣ Ukosefu wa Miundombinu ya Kiufanisi.


Maandamano makubwa yenye lengo la mabadiliko ya utawala yanahitaji:


a) Kamati za mipango (planning committees)
Hizi kamati naona hazipo. Ukimfuatilia Mange Kimambi na Maria Sarungi ambao ndio vinara wa maandamano haya unagundua hawana kamati zozote zaidi ya vikao vyote vinafanyika mitandaoni na inakuwa live.
Kamati ndio msingi mkuu wa goo organization na mobilization ya maandamano haya. Kama hazipo atafanikiwa vipi? Embu msaidieni Mtibeli aelewe.


b) Mfumo wa mawasiliano ulio salama,
Udukuzi, kufuatiliwa kuliko kupitiliza, usaliti wa mawasiliano ndani ya wenye nia ya kuandamana. Hayo yote yatakwamisha maandamano.


c) Mpangilio wa uongozi wa ngazi mbalimbali (national → regional → district → ward).
Unaweza kujiuliza kama wewe ni muandamanaji. Kwenye kata au mtaa wako kuna mfumo wowote wa kuyaratibu ili yatokee. Au ndio upo pekeako kwenye actual ground lakini mtandaoni ndio upo na na wenzako?
Tumia hiyo kama scale yako.


Mazingira ya Tanzania ya sasa, upinzani au wanaharakati wengi hawana mtandao thabiti wa ndani (grassroot network).
Hii inamaanisha hawana uwezo wa kuunganisha watu hata Laki moja kwa wakati mmoja bila kutambulika mapema.
Serikali inamiliki taasisi zote za mawasiliano, usalama, na inafanya doria usiku na mchana katika mitandao ya kijamii, hivyo hufahamu mipango kabla haijatekelezwa.
Kwa mantiki ya kiintelijensia, maandamano hayo yatakufa kabla hayajaanza, kwa sababu mpangilio wake utavujishwa na kusambaratishwa mapema.


2️⃣ Ukosefu wa Uratibu wa Malengo.


Maandamano yenye mafanikio lazima yawe na lengo moja linaloeleweka na kukubalika kitaifa.
Lakini maandamano haya yana malengo zaidivya moja yanayokinzana, mfano;


a). Kupinga uchaguzi,
b). Kuiondoa serikali iliyoko madarakani kumaanisha kuindoa CCM
c) Kupinga utekaji na mauaji. Wasiojulikana. Na sababu zingine.


Lengo la kwanza ni la kisiasa (kupinga uchaguzi)
lakini la pili ni la mapinduzi (kuiondoa serikali ya Samia madarakani) ambalo kisheria na kiusalama linachukuliwa kama uhaini au uasi.
Lengo la tatu ni la kijamii na haki za binadamu za msingi yaani haki ya kuishi. (Hili lingeunganisha watu wengi zaidi).


Hivyo, wapo wanaoamini wanapigania haki za uchaguzi, na wapo wanaoamini ni vita dhidi ya serikali. Na wapo wanaoamini wanatetea haki za binadamu za kuishi kwa waliotekwa na kuuawa na kutojulikana walipo.
Kukosekana kwa umoja wa tafsiri ya malengo kunafanya maandamano hayo yasifanane kihoja, kimkakati, wala kiitikadi, hivyo yatakosa mwelekeo mapema.


3️⃣ Udhaifu wa Uongozi wa Harakati.


Harakati yoyote ya kisiasa inahitaji:


a) Kiongozi mwenye karisma,
Najaribu kuangalia nani ni kiongozi aliyenyuma ya haya maandamano mwenye ushawishi. Kama ni Tundu Lisu yupo zake gerezani anapambana na kesi yake ya mchongo.


b) Mtu anayeaminika na umma,
Mwenye uwezo wa kujenga hadithi ya matumaini, hadithi zenye kuchochea chuki ya wananchi kwa serikali. Humphrey Polepole naye alitoa matumaini lakini amekamatwa dakika ya sabini ya mchezo kipindi cha pili.


Tanzania kwa sasa, licha ya kuwa na wanasiasa wa upinzani, hakuna kiongozi mmoja anayekubalika kitaifa kama sauti ya mabadiliko ya kweli.
Wengi wamechoka, wamegawanyika au wamo katika mikakati ya kisiasa ya muda mfupi. Na serikali inajaribu kila njia kuwavunja vunja na kuwagawanya kadiri inavyowezekana. Jana mumemwona Ezekiel Wenje. Ni kwamba wanawakatisha tamaa na kuwavunja moyo watanzania.


Bila kiongozi thabiti mwenye command structure, watu wanakuwa kama kundi lisilo na kichwa. Yaani kundi linajiendea endea bila mwelekeo. Hayatakuwa na tofauti na vuguvugu la Luddism kwa wale mliosoma Advance History 2.
Ndiyo maana kwa kitaalamu, maandamano kama haya huanza kwa makelele mitandaoni na kufa siku ya tukio. Haitakuwa mara ya kwanza.


4️⃣ Udhibiti Mkali wa Vyombo vya Usalama.


Kitaalamu, Tanzania ni nchi yenye mfumo wa ulinzi na usalama ulio wa kiintelijensia zaidi kuliko wa nguvu.
Taasisi kama:


I). TISS (Usalama wa Taifa),


ii) Jeshi la Polisi,


Iii) JWTZ (Jeshi la Wananchi)
Na vitengo vya cyber intelligence
vina uwezo mkubwa wa kutambua, kuvuruga, au kuzuia matukio kabla hayajafanyika.


Kwa mfano:


a) Mawasiliano ya Wapanga maandamano hufikiwa kupitia “surveillance”,


b) Viongozi wa maandamano hufuatiliwa kimyakimya,


c) Wengine huchukuliwa “preventive custody” kabla ya siku ya tukio.
Ndio hao unasikia kila siku wanakamatwa mara leo huyu kesho yule.
Wahamasisha maandamano mtandaoni au watu wenye mrengo huo nao huchukuliwa mapema kabisa kabla ya siku husika.
Mtu kama John Heche, John Mnyika, na wenzake hawawezi kuwa uraiani kufikia tarehe 29.


Watahifadhiwa kwa muda huku wakipewa usumbufu kidola mpaka upepo utakapotulia wataachiwa.


Hii inaondoa uwezekano wa maandamano kuanza kwa wingi au kwa ufanisi.
Kitaalamu, tunaita hii “preemptive disruption model” njia ambayo huzima uasi kabla haujaanza.


5️⃣ Hofu ya Kijamii.


Wengi wetu Watanzania ni watu wa amani tusiopenda vurugu, na tumelelewa kwenye misingi ya “amani ni bora kuliko vurugu, au funika kombe mwanaharamu. Apite".
Kisaikolojia, jamii imejengwa kuwa risk-averse (uepukaji wa hatari).
Hivyo, hata kama wanakubaliana kimoyomoyo na hoja za maandamano, wengi hawatashiriki hadharani.


a) Mfumo wa kiutamaduni, kiimani (dini), na kijamii unahimiza utii kwa mamlaka.
Wengi wataishia kusema “Mungu ataingilia” "Mungu atajibu", "tumuachie Mungu" au “Tusubiri uchaguzi mwingine”, hivyo kuua nguvu ya umoja wa kuandamana.


Kwa hivyo, uungwaji mkono utakuwa wa moyoni na mitandaoni lakini si wa miguu kwa mguu sako kwa bako. Watu wanakubaliana mtandaoni, lakini hawatokei barabarani.


6️⃣ Udhibiti wa Habari na Mitandao.


Serikali ina uwezo wa:


a) Kufunga mitandao ya kijamii.
Ikifunga mitandao wananchi wangapi wanauelewa wa kutumia VPN na mambo ya kidijitali. Wangapi?


b) Kudhibiti vyombo vya habari,
Media zote, redio zote, na wenye followers wengi watadhibitiwa iwe kinguvu au kwa kupewa pesa kuwatuliza
Si ndio yale mtaishia kumlaumu Millard Ayo wa watu. Atafanya nini?


c) Kuendesha kampeni za kupotosha


Vitengo vya propaganda kwa sasa vipo kazini: hakuna wakati vinatakiwa kufanya kazi kama wakati huu. Propaganda za kupotosha jamii mfano
“Maandamano yamehairishwa,”
“Viongozi wamekamatwa,”
“Maeneo fulani ni hatari.”
" Wanataka kuchafua nchi"
"Wanavuruga amani"
" Wanatumiwa na mabeberu"
" Watanzania ni waoga sana" hii pia ni. Propaganda iliyofanikiwa sana na ambayo kwa sasa watawala huipigia msumari ili iwe ni kama culture ya watanzania


Hii hufanya hata waliokuwa tayari kushiriki wakose maelekezo sahihi na motisha ya pamoja. Kwa mtazamo wa psychological operations (PSYOPS), hii ni silaha ya kisaikolojia inayotawanya umoja wa wanaharakati. Niliwaambia Saikolojia na soshiolojia ni msingi mkuu wa serikali kutawala watu.


Matokeo yake, maandamano hufa kabla ya saa sita mchana, na wale wachache waliotoka hukamatwa bila upinzani. Kisha baadaye watu huanza kulaumiana. Hoo hamjatoka. Nyie waoga n.k.


Kufikia hapa TaikonMaster sina la ziada. Nimejaribu kujadili. Kwa uhalisia na kwa kuzingatia siasa za nchi yetu, Saikolojia ambayo ninaifahamu kwa sehemu, intelijensia ambayo naifahamu kidunchu, na kwa kutumia falsafa (mantiki na hoja).
So kama utakuja kichwa kichwa na kutoa matusi yako sitaingilia uhuru wako na jinsi unavyoelewa mambo.


Nawatakia sikukuu njema ya Nyerere day.


Acha nipumzike sasa.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Ikitokea leo maamdamano yakafamikiwa

1. Ni rahisi aliyekataliwa akarejea kwasababu uchaguzi usipofanyika lazima jeshi lishikilie madaraka kwa muda. Je huko juu jeshini waliopo ni nje ya mfumo?

2. Hawajaandaa mtu atakayeshikilia madaraka baada ya hapo. Badala yake wanasiasa walewale wataanza kurejea kwa chama che ushawishi na kupewa madaraka. Failure.

3. ?????
 
Unazungumzia porojo mkuu. Wenzako wapo serious wanahitaji msaada
Ninachokiona mimi watu wataogopa kutoka kupiga kura kuhofia polisi walioandaliwa kupambana na waandamanaji.

Mnavyowaambia na kuwambusha wapiga kuwa kuna watu wamepanga kuandamana na serikali inasema imeandaa kuwavunja waandamanaji, tayari hapo mpiga kura umemkosa. Hafa mimi na familia yangu wametukosa maana polisi hawachagui. Tutaumia tusiohusika na tutachanganywa na wanaosema wataandamana.

Siku hiyo ni kukaa nyumbani hata kazi hazitafanyika za kutoka.....

Ushauri wangu, serikali na vyombo vyake iache kuyapaisha haya madai ya wanaosema wataandamana maana kwa kufanya hivyo inawaogopesha wapiga kura
 
Ninachokiona mimi watu wataogopa kutoka kupiga kura kuhofia polisi walioandaliwa kupambana na waandamanaji.

Mnavyowaambia na kuwambusha wapiga kuwa kuna watu wamepanga kuandamana na serikali inasema imeandaa kuwavunja waandamanaji, tayari hapo mpiga kura umemkosa. Hafa mimi na familia yangu wametukosa maana polisi hawachagui. Tutaumia tusiohusika na tutachanganywa na wanaosema wataandamana.

Siku hiyo ni kukaa nyumbani hata kazi hazitafanyika za kutoka.....

Ushauri wangu, serikali na vyombo vyake iache kuyapaisha haya madai ya wanaosema wataandamana maana kwa kufanya hivyo inawaogopesha wapiga kura

Watakaoenda kupiga kura ni ccm kindaki Ndaki
Wajumbe wa nyumba kumi kazi zao nafikiri huzijui kipindi cha uchaguzi.

Wanapita nyumba kwa nyumba kwa wanachama wao wanaelekea kupiga kura
 
Back
Top Bottom