Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,645
- 134,355
Mimi ni wa longi, halafu nikawa sipendi kabisa kuitwa Mzee, hadi my 1st born na 2nd born walipopata watoto, na kuitwa babu!.Ha ha umetisha Kaka....
Prof . shivji huyu huyu ninayemheshimu aliongea kauli dhaifu kama hiyo? Au alikuwa anamaanisha nini kuhusu saga hiyo labda sikuelewa??!!
Hawa Punch hawakuwa na adabu kabisa. Nakumbuka waliwahi kumpanchi hata mkuu wa nchi mwaka wa 1995. "It was so embarrassing!" :embarassed2:
Kwa hiyo Prof Shivji naye alikuwa ana entertain huo uhuni wa PUNCH!
No wonder Prof Kabudi kapaita pale UDSM kuwa ni jalalani.
Usishangae wakawa wanafikiri kuwa ni achievementHata mie nimejiuliza, huyu Victor na Saloti wana amani kweli kujua walisababisha kifo kisichokuwa a hatia?
Usisahau wengine hawajui asili ya daladala,chai maharage, hata matriculation tuliyofanya udsm wanaisikia tu,wananifanya sometimes nakosa nyuzi za kusoma wanaandika chips mayai tu.Una cheti changu cha kuzaliwa ama?
Kila masika na mbuu wake mkuu! Hizo zama 'primitive era' zimeshapita.Usisahau wengine hawajui asili ya daladala,chai maharage, hata matriculation tuliyofanya udsm wanaisikia tu,wananifanya sometimes nakosa nyuzi za kisoma wanaandika chips mayai tu.
Nakumbuka nilisoma shule moja ina genge la wahuni, bweni lao hata walimu wahaingii, hawa wahuni hawaogi, chakula wanabebea ndoo, na bangi ni kama chai, hawa wana harassments za ajabu. Wkt ule ukiangalia mikoa ya kaskazini walikuwa hivyo, kusini, nyanda za juu, kila shule ilikuwa na tabia hizi. Tambaza kilichonishinda ni genge la wahuni wale.
Watoto wengi wa 2000 hawajui haya madude. Hata Punch walimchora Nani siasa za wakati ule hawajui.
MkuuWale wahandisi waliokuwa wanafanya haya wako wapi? Lazima wawe na matatizo makubwa sana. Kufanya haya ni kukosa utu. Kuna baadhi ya dhambi ukishazifanya, Huwezi kubaki salama.
RIP Levina
Mimi nilisoma Tambaza ile ya wahuni, ni kweli walivuta sana bangi kule summit ila wengi walitoka na Div. 1 na sasa they are successful wana maisha mazuri.Tambaza kilichonishinda ni genge la wahuni wale.
Wengine wanachomekea hizo comment ilikupotosha ukweli, wengi wao wanajua uelekeo wa hizi nyuzi ni wao kuja kutambulikaNimesoma uzi wote kwa masikitiko but niliposoma comment kua levina alichanganya wakaka wawili ata once na masikitiko yangu yakaishia hapo
Wote washakufa mbwa haoTukuulize wewe na hao marafiki zako, huyo saroti nae bado yupo? Na Huyo Victor nini kilimua?
Maelezo mengi lakini porojo tu.
Are you Shivji's lapdog? Nukuu iko clear kabisa alikuwa anapingana na Mongela cha ajabu unaibuka na blah blah kibao na utetezi dhaifu kabisa.
Namkumbuka sana huyu dada yangu, Levina Mukasa. Alikuwa Mtanzania kutoka maeneo ya Kyaka, Misenyi. Alikuwa anachukua shahada ya Ualmu. Alikuwa mtulivu sana kwa aiba na kwa matendo.
Nakumbuka siku aliyofika Getruda Mongela akahutubia akiwa amesimama juu ya HIGH TABLE, meza iliyokuwa katika cafeteria ya Manzese, na ilioyotumiwa exclusively na wanafunzi wa Engineering mwaka wa nne. Mama Mongela alisema kuwa alikuwa amekuja kuizika PUNCH.
Jioni yake Profesa Shivji aliweka mdahalo usiokuwa rasmi nje ya cafeteria ya Manzese na kupinga kauli ya Getruda na kumbeza kwamba " You can't declare resolution of what you didn't establish" Wiki iliyofuata PUNCH akatoa toleo lingine likimtukana Getruda matusi yote.
Ndipo baada ya hapo serikali ikatangaza kitita cha Sh Mil 10 kwa yeyote atakayempata mshirika yeyote wa PUNCH. Baada ya hapo ilitoka makala ndogo ya PUNCH iliyotundikwa Hall One. Kisha PUNCH ikafifia kabisa.
EMT umenikumbusha mbali sana.