Victor aliishatangulia kitambo mbele ya haki, lakini hata hivo mimi nilihusika ktk tukio hilo, Victor was my friend, Habari ina upotoshaji. Ni kweli mimi na Victor wakati huo tukiwa 4th year eng. alikuwa na mahusiano na huyo marehemu Levina, wakati huohuo ana mahusiano na Saloti wa 1st year.Hata mie nimejiuliza, huyu Victor na Saloti wana amani kweli kujua walisababisha kifo kisichokuwa a hatia?
Levina alienda na Victor Silver sand, kuna picha zilipigwa zikionyesha Victor na Levina wakiwa na vinywaji na wenyefuraha hukohuko silver sand. Yupo pia mhadhiri wa B. Com alionekana akiwa nao akishuhudia hali ya upendo huo, jina nalihifadhi, na mimi nilikuwepo. Ugonvi ulizuka kidogo pale Saroti na kundi lake walipojaribu kuingilia furaha ya wawili hao. Huyu Saroti wa msoma alikuwa Kijana wa vurugu sana, nadhani alikuwa anavuta bangi. Alim-harasi sana huyo binti baada ya siku hiyo.
Kwa uelewa wangu Harassment za Saroti kwa Levina nadhani ndizo zilipelekea Mzee Punch kuingilia kati na kumuingiza Levina ktk orodha ya watakao punchiwa kama mwandishi anavyosema. Binafsi namtetea marehemu Victor, Yeye na Marehemu Levina walishawishiana kwa njia za kawaida. Lakini suala la kunyanyasa akina mama pale chuo, ni kweli walinyanyaswa kwa msaada wa mzee Punch! Hivi bado punch yuko?