Kwanini kodi ya magari mapya ni kubwa kuliko kodi ya magari ya miaka ya zamani? 2)

Pantosha

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
349
464
Habari wana JF,

Mimi naomba kuuliza:

1). Hivi ni kwanini kodi ya magari mapya ni kubwa kuliko kodi ya magari ya miaka ya zamani?

2). Inakuaje kodi ikawa kubwa kuliko bei ya kununua+kusafirisha hadi linafika bandarini Dar es Salaam?
 
Habari wana JF,

Mimi naomba kuuliza: 1). Hivi ni kwa nini kodi ya magari mapya ni kubwa kuliko kodi ya magari ya miaka ya zamani? 2). Inakuaje kodi ikawa kubwa kuliko bei ya kununua+kusafirisha hadi linafika bandarini Dar es salaam?
Serikali yenyewe hailipi kodi kwa magari inayoingiza
 
Mtoa mada usitumie hisia pitia mada ya Taxation O-level ujue sababu za kuweka kodi kubwa kwenye imported goods.
 
Kuna kitu kinaitwa TRAB NA TRAT yani ndo huwa kina kina kinaaa kinaaa............................kinaaaa.................
Hahahaaaaaa…….serikali iangalie hizo kodi. Inasababisha wananchi wasiendeshe magari ya kisasa. Impacts ya magari ya kisasa ni nyingi:

1). Kupunguza ajali zinazosababishwa na gari kuwa limechoka

2). Kupunguza uchafuzi wa mazingira

3). Kuokoa pesa za matengenezo ya mara kwa mara

4) kuokoa pesa ya mafuta

5) kuwafanya wananchi waipende nchi yao.

Ushauri: Serikali ibadilishe sheria ya kodi ya magari ambayo ukiangalia ni kama inataka nchi iwe dampo. Watu wanaagiza magari ya miaka ya nyuma sana kwa sababu ya kodi.
 
Kodi watu wamepiga kelele hatuoni mabadilio yeyote zaidi zaidi wanaongeza kodi kimya kimya...

Bara bara nzuri zinajengwa kwa ajili ya matumizi ya kupeleka magari mazuri Nchi jirani maana wao kodi zao zinalipika..

Tanzania hizi Toyota za 2015 kuja juu ni gari ya Zamani ila Tanzania ni jipya kabisa kodi yake haishikiki unaona lengo la Serikali sio kupunguza ajali na kuwafanya raia wake watumie vitu bora wao lengo lao ni kodi hao Wananchi watajua wenyewe hiyo imepelekea Wananchi wengi kuwa na chaguo la magari ya chini sana na yenye kinga ndogo pindi likipata ajali hata ndogo linaweza kugharimu maisha ya abiria na dereva...

Hizo pick up au Malori ambayo ndio kiungo kikubwa cha kukuza Uchumi ndio balaa hilo Fusso Tiper dogo linafika kuanzia 75m kuendelea ni kama tumerogwa imepelekea Japan wanauza kutokana na soko letu sio mwaka wa gari hata kama gari ni ya 1998 watauza bei juu kwa sababu Watanzania tunanunua kwa kuangalia TRA wanasemaje sio kwamba unalipenda hilo gari...
 
Habari wana JF,

Mimi naomba kuuliza: 1). Hivi ni kwa nini kodi ya magari mapya ni kubwa kuliko kodi ya magari ya miaka ya zamani? 2). Inakuaje kodi ikawa kubwa kuliko bei ya kununua+kusafirisha hadi linafika bandarini Dar es salaam?
Wakati tulitegemea siye wenye Bandari kupata unafuu mkubwa kuliko walioikosa, lakini mambo ni kinyume kabisa!

Nadhani ndipo kiwango cha mawazo ya viongozi wetu kilipokomea!

Na sasa ndiyo wameamua kumuuzia bandari mwarabu!
 
Kodi watu wamepiga kelele hatuoni mabadilio yeyote zaidi zaidi wanaongeza kodi kimya kimya...

Bara bara nzuri zinajengwa kwa ajili ya matumizi ya kupeleka magari mazuri Nchi jirani maana wao kodi zao zinalipika....
Umeongea ukweli. Hii sheria ibadilike.
 
Si yelezee hapa tujue sababu? Halafu kuna nchi wanatoza kodi ndogo kwenye bidhaa mfano Uganda , wao hawajaisoma hiyo topic ya Taxation?
Hahaha vimo (viwango) kutofautiana ni kawaida. Mliozaliwa siku moja leo hii tukiwapima leo hii hamuwezi kulingana urefu na uzito.

Ishu ya Uganda ni hiyo hiyo Kodi zipo ila tofauti ni viwango.
 
Si uelezee hapa tujue sababu? Halafu kuna nchi wanatoza kodi ndogo kwenye bidhaa mfano Uganda , wao hawajaisoma hiyo topic ya Taxation?
Hao wa Topic achana nao Mkuu wanaingia kwenye Test ya Taxation muda si mrefu...
 
Hahaha vimo (viwango) kutofautiana ni kawaida. Mliozaliwa siku moja leo hii tukiwapima leo hii hamuwezi kulingana urefu na uzito.

Ishu ya Uganda ni hiyo hiyo Kodi zipo ila tofauti ni viwango.
Bidhaa nyingi zinapita bandari yetu ila Watanzania wanafata hiyo bidhaa Uganda ilikolipiwa kodi na kuja kuuza Kariakoo kama mashuka na bidhaa zingine kuingiza magari na nguo Uganda sio kodi kubwa kama Tanganyika...
 
Nashukuru kwa kuelewa.
 
Mtoa mada usitumie hisia pitia mada ya Taxation O-level ujue sababu za kuweka kodi kubwa kwenye imported goods.
Unawekaji tax kubwa kwa bidhaa ambazo hata huzalishi? Weka tax kwa bidhaa ambazo unazalisha ili kudiscourage watu kuimport bidhaa kama hizo toka nje ili ulinde viwanda.

Unaweka kodi kubwa kwenye magari halafu majority ya raia wako wana mishahara chini ya milioni... Je, lengo ni kwamba wasinumue magari maisha yao yote au?
 
Back
Top Bottom