miss strong
JF-Expert Member
- Jul 4, 2012
- 7,011
- 3,708
Mmmmhhhh
Huyo ni trilionea. Anamiliki kanisa lenye aelfu ya waumini, kituo cha TV na benki. Hao kina Pengo wao ni watumishi wasio na mshara mali zote ni za waumini katika makanisa wanayoyaongoza. Watu kama akina Mzee wa upako, Gwajima, Kakobe, na manabii, wachungaji na mitume wengi walioanzisha makanisa yao ni kama wakurugenzi wa makanisa hayo kwa hiyo kimsingi wao ndio wamiliki. Niliwahi kumsikia mzee wa upako akisema eti watu wanahoji kwanini michango anayoitisha ipitie kwenye akaunti yake binafsi badala ya kanisa. Akasema yeye ndiye mwanzilishi na kuwa akifa yeye na huduma inaishia hapo. Kuna waumini walimfungulia Kakobe kesi eti anatumia ovyo mali za kanisa. Mahakama ilisema Kakobe hana kosa kwani kanisa ni lake na yeye ndiye mwanzilishi hivyo ni mali yake wao walijiunga wakati limeashaanzishwa na kuwa kama hawaridhiki waende na wao wakaanzishe la kwao
Ni kwl kabisa hata mimi simuamini kbsa huyu mwingira akifuatiwa na mzee wa upako na mlima wa moto hao sitaki kabisa kuwasikiliza..kwangu ninaelewa mafundisho yake ni mwalimu mwakesege peke yake na the late mosses kulola..over
Kwa walokole, adui wa kiroho tunajilinda na kupambana naye kwenye maombi. Adui katika mwili tunajilinda kwa ulinzi wa kimwili (bodyguards) kama unajihisi hauko salama.
Huwezi jua wanaomzunguka Pengo au sheikh mkuu ni akina nani, au kwa vile hawavai combat au miwani myeusi ndiyo maana unasema hawana walinzi? Jaribu siku moja uwasogelee uone mambo!
Nina uhakika maana sijawahi sikia sehemu ambapo wanasema Kardinari Pengo amebaka ama anatembea na mke wa mtu hata kwa kusingiziwa.Ila kwa Mwingira na Gwajima nimeshawahi kusikia hata kama watakuwa walisingiziwa ila nimeshawahi kusikia tena zaidi ya mara mojaMmmhhh
Mkuu una uhakika?
Jiulize kwanza kwa nini vatican city ina jeshi kabisa na kwa nini baba mtakatifu analindwa?Kardinali Pengo hana walinzi kwa kuwa anakula halali lakini Gwajima na Mwingila wanahitaji walinzi kwa kuwa wamezoea kula haramu
Unafukua makaburiKhaaaa
Sio kila ulinzi ni kuogopa maadui. Mungu pia anao malaika walinzi, je anamuogopa nani? ULINZI NI UFAHARI PIA. Na ni TABIA YA MUNGU MWENYEZIHalaf wakitoa mahubirii utawasikiaa kua na amani ya bwana, Mungu yupo pamoja nawe usiogope chochote"" wakati kwanza wao wanatembea na walinzii haa uongo huuu
Kwa hiyo Mungu hana uwezo wa kukulinda dhidi ya maadui wa kimwili??? Binafsi haya makanisa yatanipita tu kushoto. Ni bora niziishi zile amri za Mungu zilizopo kwenye Biblia, Kuliko madudu yanayoendelea kwenye haya makanisa. Badala ya kutoa sadaka yangu kwa waganga njaa kama hawa. Kuna ubaya gani nikienda kuitoa sadaka hiyo kwa wale wasiokua nacho na wenye uhitaji??? Tunaangamia kwa kukosa maarifa. Mungu atusaidieMungu anawalinda dhidi ya maadui wakiroho mabodigadi dhidi ya maadui wa kimwili
Acha uongo mbwa wee tukikudaka utaweza thibitisha kauli yako.Hao wachungaji wajasiriamali wenuNani kakwambia Pengo Hana walinzi. Kwa taarifa yako, pengo safari zake zote yupo na masister . Wale masister ni balaa, ukiwakagua mifukoni utakimbia. Wanavifaa vyote. Huwa wanatembea na silaha. Fanya uchunguzi umuone Pengo, Masister wapo nae sambamba. Tena masister wawili, inavyosemekana hao masister wamepitia jeshi na usalama wa taifa.
biblia inaseema wanangamizwa, kumbe kuna ambaye anawangamizaMtumishi wa Mungu analindwa na mabodigadi?
Kwa kigezo hicho huyo hafai kuitwa mtumishi wa Mungu.
Ama kweli watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.