Kwanini hela ya Kenya ina thamani zaidi, tena mbali kuliko ya Tanzania wakati tumebarikiwa kila kitu?

Kwa hivyo hapo tuseme shilingi ya Uganda ndiyo yenye nguvu?
 
Ukiwa na shiling elfu kumi Tanzania utanunua vitu vingi lakini ukichukua hiyohiyo elfu kumi ukaenda nayo kenya hautonunua vitu vingi kama ulivyonunua Tz so thamani ya shiling ikiwa ndogo kuna faida saana (hasa kwa nchi zinazozalisha bidhaa nyingi)
Mzee unaongelea thamani gani wakati vitu vingi unategemea ku import? Usichukue hesabu za kiuchumi za china ukazileta Tz. Huku ukitaka kununua kitu una convert pesa yako kwenye pesa ya kigeni, and you wish thamani ya pesa yetu iwe ndogo!! Kama umeshawahi kufanya biashara utaelewa, unauelewa mfumuko wa bei?
 
Na mimi nikukumbushe 1966 wakati tulipoachana na matumizi ya East Africa Schilling na kila nchi kuanza kutumia fedha zake Shilingi ya Tanzania na Shilingi ya Kenya zilikuwa sawa(1TSh=1KSh) iweje leo iwe mara 20?

Shilingi ya kenya inaimalika sana zaidi ya shilingi ya tanzania, ndani ya mwaka mmoja imeimalika zaidi ya shilingi mbili zidi ya tanzania. Tukija na na reasoning za kijinga tutakuja after few years na rate ya 1:40. Hatutaki kuamini kuwa Tsh ina decline
 
Kanuni ni very simple, ukiwa na kiwango kizuri cha mauzo ya huduma na bidhaa nje ya nchi na kupata foreign currency ya kutosha especially dollar, pesa yako inakuwa na thamani na nguvu kubwa.

Kwasababu utakuwa umejiimarisha kiuchumi na hali yako ya kifedha na uwezo wa watu wako unaimarika.

Kenya wanafanya export nyingi sana tena mbaya zaidi 80% ya source ya hizo exports ni mali na rasilimali za tanzania.

Walikuwa wana export huduma za utalii kwa kutumia mbuga zetu, mazao mengi wanayo export yanalimwa na kuzalishwa hapa katika ardhi ya Tanzania. Wanatumia majina ya rasilimali mali zetu kujitangaza kuwa zipo kenya na hivyo walikuwa wanapata watalii wengi sana kupitia rasilimali zetu na wao kunufaisha makampuni ya kenya na kutunisha hazina yao ya foreign currency kule Kenya.

So sisi ugonjwa wetu ni m'moja, tupo nyuma sana katika kufanya exports..... Tukiweza kuuza sana bidhaa nje baada ya muda fedha yetu utaanza kupanda thamani na kuwa juu.
 
Kanuni ni very simple, ukiwa na kiwango kizuri cha mauzo ya huduma na bidhaa nje ya nchi na kupata foreign currency ya kutosha especially dollar, pesa yako inakuwa na thamani na nguvu kubwa...
Yaani umeongea kwa usahihi kabisa wakenya wanaexport rasilimali zetu yaani wanapata fedha ya kigeni kwa mgongo wa ujinga wetu.
 
Mtoa mada nikukumbushe tu kua hela ya japani (japaneese
Yen) ina thamani almost sawa na hiyo shilingi ya kenya lakini hiyo haimaanishi uchumi wa japani na Kenya zinakaribiana.
Ina maana thamani ya fedha sio moja ya sababu ya kuwa na uchumi mkubwa? Uhusiano wa hivi vitu viwili ukoje?
 
Kama Nchi mbili mnauchumi unaofanana mwenye sarafu yenye thamani ndogo anapata advantantes kwenye Import wakati export inakuwa chache..

This how China does kwenye Issue ya Currency manipulation

Shillings 2500 ya Kenya ni sawa shillings 50000 ya TZ, lakini Chakula cha 2500 Kenya ni 5000 TZS (250KSH) Hapa Tanzania, ama kwa namna nyingine tukiuziana bidhaa sisi tunapata competitive adavantage cause we will sell a lot at cheaper price, wao hawawezi kutuuzia kwa sababu bidhaa zao zile zile zitakuwa ghali.
 
Kwahiyo na bidhaa zinazonunuliwa kwa wingi China kuja TANZANIA na wao China hela yao Ina Thamani ndogo kushinda TANZANIA shilingi?


Daah Kuna viazi humu.
 
Exchange rate na thamani ya pesa ni vitu viwili tofauti kabisa; exchange rate inategemea sana decimalization ya pesa yenu wakati thamani ya pesa inategemea foreign reserve mlizonazo na uchumi wa nchi yenu.

Kwa Tanzania tulifanya makosa sana miaka 1980 tulipoanza devaluation ya shillingi huku tukipandisha mishahara ya wafanyakazi kila mwaka bila kuangalia productivity. Effect ya process hiyo ilikuwa kupunguza decimalization units za shillingi ya Tanzania mpaka ikafikia hatuhesebu hela kwa centi tena bali tunahesbau kwa elfu elfu elfu. Noti kubwa tuliyokuwa nayo wakati huo ilikuwa Shillingi mia, lakini leo tunazungumzia elfu 10. Process hiyo huwa ni one way, hairudi nyuma; kwa hiyo hata kama tutakuwa na uchumi imara sana duniani leo, bado shilingi haitarudi kuwa ya daladala tena (dola kwa shilingi tano).
 
Sawa sawa hapo ndipo tuliponasa kwenye umeme wa DC,ukiangalia hata Somalia vita ndio kula yao.
Pa kuangalia ni hapo pa kuifanya process irudi na hapo ndio kwenye kina kirefu,irudi senti tano unnue ice cream ,naona tuendako sio mbali tena karibu itatoka noti ya 50,000/
 
Ni kwa sababu Kenya ni nchi Masikini sana. Lakini Tanzania ni nchi Tajiri sana na Tanzania imeingia "Uchu" wa Kati, hivyo hulazimika kutumia Shilingi ya Tanzania nyingi kununua Shilingi chache ya Kenya πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜…πŸ˜„
 
Ukiwa na shiling elfu kumi Tanzania utanunua vitu vingi lakini ukichukua hiyohiyo elfu kumi ukaenda nayo kenya hautonunua vitu vingi kama ulivyonunua Tz so thamani ya shiling ikiwa ndogo kuna faida saana (hasa kwa nchi zinazozalisha bidhaa nyingi)
Ndugu yangu, thamani 'halisi' humtegemea zaidi muhitaji wa pesa yako, ili akapate 'vile' anavyohitaji yeye kwa wakati huo.
Kuna wakati BAADA ya uhuru nchi zetu EA (Ke,Tz,Ug) zilitumia hela moja, SHILLING.
Hata baada ya kutengana kwa muda mfupi hali ilikuwa muzuri, Ushs =Kshs =Tshs. Soko letu kuu kwa nchi zetu lilikuwa moja. Viwanda katika nchi zetu vilianzishwa kimikakati ya kuimarisha umoja/ushirikiano na sio migongano/mipambano.
Migogoro mingi ambayo baadae ilikua na kukuzwa sana, hatimae ilikuja sababisha kuvunjika kwa EAC na ndio iliyotufikisha hapa.
Kutokana na historia viwanda vingi vya mahitaji muhimu ya kila siku kama sabuni, dawa ya meno, mafuta ya kupikia etc vilikuwa Kenya. Hivyo basi Kshs ikawa ndo yahitajika zaidi kwetu na hata kwa Uganda, ili kupata hayo mahitaji (muhimu).
Pamoja na Tz kuamua kufunga mipaka na kukimbizana kuanzisha viwanda mbadala na kuingiza baadhi ya bidhaa hasa kutokea China, ili kuziba mapengo, bado biashara ya kuingiza mahitaji kutoka Kenya kimagendo ilishamiri na kuifikisha thamani ya Tsh hapa ilipo.
 
huyo ni jasusi CIA amekuja kutafuta taarifa
 
Kwahiyo na bidhaa zinazonunuliwa kwa wingi China kuja TANZANIA na wao China hela yao Ina Thamani ndogo kushinda TANZANIA shilingi?


Daah Kuna viazi humu.
Hujaelewa nini, sisi na mataifa mengi tunanunua vitu vingi kutoka China kwa sababu pesa yao ina thamani ndogo kuliko US.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…