Kwanini Dr. Slaa anawakosesha raha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Dr. Slaa anawakosesha raha?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 11, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mwitikio wa CCM, makada wake na wapenzi wake dhidi ya Dr. Slaa umenishangaza sana. Toka alipotangazwa zimetumika mbinu mbalimbali za kumharibu kisiasa hata kibinafsi na nusura kidogo zifanikiwelakini zilipojibiwa kimahiri ikawa ni kama wao CCM wanamtengeneza shujaa mbele ya macho yetu. Ka nzi kalikopita sehemu mbalimbali mwishoni mwa juma kamejikuta kanashindwa kutoa taarifa ya sababu ya mwitikio huu.

  Hata hivyo kanadokeza kuwa kati ya vitu vyote vinavyowatisha ni masuala ya EPA na Meremeta. Masuala haya mawili hawataki kabisa yaangukie chini ya mtu kama Dr. Slaa ambaye tayari amejionesha kuwa licha ya kwamba hana madaraka kuwatolea uvivu watuhumiwa wa uhalifu bila woga jambo ambalo limemshinda mtu aliyeko madarakani.

  Lakini japo hilo linaelezea kutishwa kwa waliko madarakani lakini halitoshi kuelezea kutishwa kwa Chama kizima na kuwafanya wawe kama wanapigwa na ubaridi. Ninajiuliza kwa kadiri siku zinavyokwenda yawezekana watawala wakalazimika kuanza kutumia mbinu za wazi za vitisho kama walivyofanya miaka ile walipoanza kuonesha filamu za mauaji ya kimbari ya Rwanda.

  Lakini mbinu hiyo wameanza kuhisi haiwezi kufanikiwa kwani walitegemea wakihubiri juu ya umwagikaji damu basi watu wataanza kukwepa mikutano ya Slaa. Kinyume chake imekuwa kweli kwani watu wanachosema ni kuwa "hatudanganyiki".

  Lakini ukweli bado unabakia kuwa kuna hofu ambayo haieleweki kwani siyo wana CCM tu bali hata taasisi nje ya CCM zinaanza kuonesha wazi kabisa kuhofia ajenda kali ya mabadiliko chini ya Dr. Slaa ambayo inavutia watu wengi zaidi (popular agenda).

  Kilichowashangaza zaidi CCM kwa mujibu wa ka'nzi ni jinsi ambavyo wasomi (mijini) na wananchi wa vijijini wanavyokubaliana katika kumkubali Dr. Slaa. Huko nyuma watawala walitegemea utengano kati ya makundi hayo mawili huku baadhi ya kundi la wasomi likiiunga mkono CCM. Wanachofurahia hata hivyo ambayo inawapa matumaini kidogo ni kuwa bado CCM ni chama kinachokubaliwa na kupendwea na baadhi ya wafanya biashara ambao wanaamini katika chini ya CCM maslahi yao yanalindwa.


  yangu macho...
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hahaaaa ccm wanatamani uchaguzi usogezwe mbele.na pangekuwa na mdahalo tu nod ingekuwa kwisha
   
 3. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  Wasiojua wajue, na hata kama hawataki kujua walazimishwe kujua, na ccm pia wajue, kuwa chadema ipo juu na watu wanataka mabadiliko.
   
 4. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji,

  CCM hawakutegemea Slaa kuwa mgombea wa CHADEMA (walihofia lakini hawakutegemea). Wao walijua mgombea atakuwa Baregu (au anayefanana naye - Mkumbo upooooo). Calculation zao zote zimekutana na surprise ambayo mpaka sasa wameshindwa wafanye nini kucounter wave yake.

  Sina hakika sana na kitakachotokea Oct 31 ila nimejawa na hofu kubwa sana kwa nchi yangu.
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  mwanakijiji endelea kushangaa, kwangu nayaona hayo kuwa ni sehemu ya mkondo wa mabadiliko ambao kuuzuia ya kutaka uwe mgonjwa wa akili ama ujitoe akili kama ambavyo Daily News, Rai, Mtanzania na Habari leo wamejitoa.
  vyovyote iwavyo siasa za Tanzania hazitakua sawa kuanzia October 31 mwaka huu, naamini mkondo wa mabadiliko umefika.
  kundi lililokua linaiamini sana ccm limegeuka, hili ni kundi la wakulima na watu duni , wameanza kung'amua adui yao halisi, nimebahatika kuhudhulia kampeni na movements kadhaa za kisiasa huku kanda ya ziwa, hali ni ngumu kwao.
  naamini lipo jambo linakuja, Tusilale mpaka kieleweke.
   
 6. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nina wasi wasi mkubwa sana na mara nyingi nikiwa nahofia kitu basi jambo baya hutokea. Naomba isiwe hivyo safari hii.
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hwa jamaa wanatumia nguvu sana kumnadi Kikwete! Ni kama wanamsindikiza askari mlemavu wa akili kwenda vitani! Pamoja na mbwe mbwe zote hawana imani maana upepo umegeuka sana. Nimepokea sms ikiwa na ujumbe wa kumkashfu Dr Slaa..... kama wengine kutoka "+3588108226" Nimepiga haipatikani nimetext sms haijawa delivered (Niweka matusi na kuwaambia sidanganyiki)

  Kwa kweli Kinana na timu yake wanashangazwa!
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  uchaguzi ukisogezwa mbele ndo itakula kwao vibaya sana.manake watu wengi zaidi watapata elimu na kufunguka macho!
  Yaani Dr akiingia madarakani,kuna watu watakimbia hii nchi!Na tunawataka washughulikiwe kwa kutufanya sie majuha,sio kwa vita bali kwa kufikishwa mahakamani na kuwajibishwa.
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Yaani wanaposikia Dr. Slaa presha zinawapanda. Kinachowaumiza kichwa ni kuwa kila mbinu wanayotumia ili kumchafua Slaa, inapuuzwa na wananchi na mbinu hiyo inatumika kumpandisha chati Slaa, wataisoma mwaka huu.
   
 10. C

  Chumvi1 Senior Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji
  Hao lazima wasome namba mwaka huu, I cant wait that day ambapo DR SLAA atakuwa annapishwa kwa kweli kuna watu watakimbia nchi hii tumeburuzwa sana na tumefanywa wajinga muda mrefu na kingine ninachotaka kusema watanzania wengi sana wanasali kimoyomoyo hawa jamaa mungu atuwezeshe waondoke maana bila mkono wa mungu hawa ni ujasusi ndio utakaotumika kuiba kura zetu na kuchakachua matokea maaana naona wameshaanza kuwa busy.
  Mungu ibariki Tanzania
   
 11. O

  Ogah JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kwa mara nyingine napenda kumshauri Dr. Slaa & Co......................kuwa wawaambie wananchi kuwa wataunda serikali ya umoja wa Kitaifa ili kuongeza confidence ya wananchi juu ya Dr. Slaa.................
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Juzi nilikuwa naongea na Kiongozi mmoja wa CCM akasema Dr. Slaa hafai kuwa Rais kwa sababu eti ni very Radical na katika Uongozi wake watu wengi sana watawajibishwa

  Sijui kwa nini kuna Baadhi ya Watanzania eti wanakipigania chama cha Mapinduzi eti kisife, mimi nasema Kife tu maana Uwepo wake ni kwa manufaa ya Wachache

  Kwa Kweli kuna Hofu kubwa sana imetanda ndani ya Watawala, natamani Watanzania wote wangeiona hii hofu nadhani ingeweza kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi

  Ukweli ni Kwamba Dr. Slaa Anawatisha sana
   
 13. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kama Dr. Slaa ataapishwa baada ya Tar 31 Oct Amin Amin nawaambia Watu wengi watatoroka hii nchi
   
 14. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  "Try to relax and enjoy the crisis.
   
 15. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  CCM Pressure inapanda, Pressure inashuka, Pressure inapanda, Pressure inashuka....!!

  CHADEMA ikichukua nchi lazima watu wapate high blood pressure, heart attack, diabetes, stroke.....watakaokuwa na nguvu lazima wakimbie nchi!
   
 16. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji,

  Ni rahisi sana kwa mtoto kuchezea matiti ya mama yake, lakini si rahisi kuchezea korodani za Baba yake. Kipindi hiki CCM imeshikwa pabaya. Inashindwa kupumua, taratibu inakata roho. Tarehe 31.10.10 tunaipeleka makaburini na kuizika.
   
 17. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Slaa alisha sema atafanya kazi na Dk Mwakyembe kama akikubali masharti aliyompa,kama haitoshi alisha mnadi mgombea ubunge wa chama kingine hapo kabla,Hiyo inaonesha kuwa yupo tayari kufanya kazi na watu waadilifu wasio na unafiki.
   
 18. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kikwete alisema kuwa hayuko tayari ccm impasukie mikononi mwake,hivyo aliamua kuzinyamazia kashfa za ufisadi ilimradi chama kisonge mbele.Pia alisema hayuko tayari muungano uvunjike chini yake hivyo akawa mpole kutoa msimamo wake hata pale baraza la wawakilishi lilipopitisha miswada inayotia shaka,ilimradi kuwaridhisha.Kwa sasa hivi hayuko tayari ccm ipoteze dola chini yake hivyo atafanya afanyalo ilimradi dola ibaki kwa ccm bila kujali kuwa kwa ahadi nyingi anazotoa anakuwa anaichimbia ccm kaburi kwani iwapo ataingia madarakani hawezi zitekeleza,hivyo hakuna mtu ataichagua ccm tena 2015 hata za kuiba hawatazipata.Lakini hofu kubwa ni ukweli usiopingika kuwa Dk Slaa akiingia madarakani hakuna aliyefisadi nchi atakaye pona,hiyo ni pamoja na yeye JK.Mbali na hilo wamestushwa kuona jinsi umma ulivyomkubali Dk. Slaa.
  Kwa namna hiyo basi nguvu nyingi za aina tofauti zitatumika ilimradi abakie madarakani.
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mwafirika,
  Mie sioni haja ya kuona hofu. Sisi m iko ukingoni. Na vitisho vyote vitayeyuka vyenyewe. Mungu wetu ni mkubwa kuliko sisi m.
  Kwa kuwa rais aliapa na wote tulimsikia, akisema ataheshimu katiba na sheria za nchi na kuzilinda, sitegemei huyo huyo kuzivunja na kuanzisha vagi. Najua ataondoka vizuri na mabadiliko rasmi yataanza. Tuachan e na vitisho vyake.
  Tulimkabidhi nchi kwa amani aturudishie nchi kwa amani. Hakuna damu itakayomwagwa kama anavyojaribu kuhubiri.
   
 20. O

  Ogah JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  .......hii ilitokea only in isolated occasions...............inatakiwa atamke BOLDLY kuwa ataunda serikali itakayojumuisha watu makini toka vyama vingine pia
   
Loading...