Elections 2010 Kwanini Dr. Slaa anawakosesha raha?

Hwa jamaa wanatumia nguvu sana kumnadi Kikwete! Ni kama wanamsindikiza askari mlemavu wa akili kwenda vitani! Pamoja na mbwe mbwe zote hawana imani maana upepo umegeuka sana. Nimepokea sms ikiwa na ujumbe wa kumkashfu Dr Slaa..... kama wengine kutoka "+3588108226" Nimepiga haipatikani nimetext sms haijawa delivered (Niweka matusi na kuwaambia sidanganyiki)

Kwa kweli Kinana na timu yake wanashangazwa!

Wozoza hiyo namba hata mimi nilifanya hivyo ila sasa imekula kwao kwani ni wao wao wanaomwaga damu sasa.
 
Mwanakijiji,

CCM hawakutegemea Slaa kuwa mgombea wa CHADEMA (walihofia lakini hawakutegemea). Wao walijua mgombea atakuwa Baregu (au anayefanana naye - Mkumbo upooooo). Calculation zao zote zimekutana na surprise ambayo mpaka sasa wameshindwa wafanye nini kucounter wave yake.

Sina hakika sana na kitakachotokea Oct 31 ila nimejawa na hofu kubwa sana kwa nchi yangu.

Wadau, hizi habari nazotaka kusema ni za kweli kabisa. Katika mahojianao miezi michache iliyopita, Frederick Sumaye aliwahi kumwambia mwandishi mmoja wa habari in confidence (na alimuomba hiyo iwe off record, yaani asichapishe) kwamba laiti JK angejua Slaa atachukuwa fomu za kugombea urais, basi yeye (JK) angejifikiria mara mia naye kuchukua fomu, na pengine asingechukuwa kabisa.
 
Watu kama Magufuli,Mwakyembe,Mwandosya ni majembe ya kuyatumia Slaa akiingia madarakani.
CCM wanahema kama funza.
Hao wanaosema ni radical haki yao but kwa jinsi nchi ilivyo twaitaji mtu radical for ten years ili turudi kwenye mstali
 
Kama Dr. Slaa ataapishwa baada ya Tar 31 Oct Amin Amin nawaambia Watu wengi watatoroka hii nchi

Hahahaha watu watakula kona shaaaaaaaa wanakimbilia kwa Mseven hapo.

Slaa kwakweli anakubalika mm nimepita vijijini huko wanamkubali
 
mwambieni jay k achague initial kati ya hizi, X-PRESIDENT,FORMER PRESDENT or LATE PRESDENT.
 
CCM haina haja ya kuogopa. Kwa kuwa madudu tuyajuayo waiyafanya wenyewe, basi kiungwana wawe tayari kuyakabili tu!!!

Vote out CCM!!!
 
HIVI WANOIPENDA NA KUISHABIKIA CCM NI WATANZANIA?
ccm huwa wanaamini katika siasa za kuwanyamzisha watz ambao sasa wamewasoma kwa undanio k=na kuijua ccm na kwamba watz hawa sio wale lazima ccm ielewe hivyo...............hatudanganyiki na wala hatutadanganyika kwa namna yoyote ile ni wakati wa mabadiliko................HATUKO KUONA RAIS DHAIFU KM KIKWETE AKIENDELEA KUIVURUGA NCHI KWA KUWALINDA WEZI NA KUIGEUZA IKULU MRADI WA KIFAMILIA.......HATUKO TAYARI KUMUONA KIONGOZI WA NCHI AKIWASAFISHA MAFISADI MBELE YA WAT NA BILA AIBU YOYOTE KUWA NI AWATU SAFI............"HII KWELI NI NCHI YA KUDADIKIKA, NDIVYO CCM WANAVYOAMINI"
 
Mwitikio wa CCM, makada wake na wapenzi wake dhidi ya Dr. Slaa umenishangaza sana. Toka alipotangazwa zimetumika mbinu mbalimbali za kumharibu kisiasa hata kibinafsi na nusura kidogo zifanikiwelakini zilipojibiwa kimahiri ikawa ni kama wao CCM wanamtengeneza shujaa mbele ya macho yetu. Ka nzi kalikopita sehemu mbalimbali mwishoni mwa juma kamejikuta kanashindwa kutoa taarifa ya sababu ya mwitikio huu.

Hata hivyo kanadokeza kuwa kati ya vitu vyote vinavyowatisha ni masuala ya EPA na Meremeta. Masuala haya mawili hawataki kabisa yaangukie chini ya mtu kama Dr. Slaa ambaye tayari amejionesha kuwa licha ya kwamba hana madaraka kuwatolea uvivu watuhumiwa wa uhalifu bila woga jambo ambalo limemshinda mtu aliyeko madarakani.

Lakini japo hilo linaelezea kutishwa kwa waliko madarakani lakini halitoshi kuelezea kutishwa kwa Chama kizima na kuwafanya wawe kama wanapigwa na ubaridi. Ninajiuliza kwa kadiri siku zinavyokwenda yawezekana watawala wakalazimika kuanza kutumia mbinu za wazi za vitisho kama walivyofanya miaka ile walipoanza kuonesha filamu za mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Lakini mbinu hiyo wameanza kuhisi haiwezi kufanikiwa kwani walitegemea wakihubiri juu ya umwagikaji damu basi watu wataanza kukwepa mikutano ya Slaa. Kinyume chake imekuwa kweli kwani watu wanachosema ni kuwa "hatudanganyiki".

Lakini ukweli bado unabakia kuwa kuna hofu ambayo haieleweki kwani siyo wana CCM tu bali hata taasisi nje ya CCM zinaanza kuonesha wazi kabisa kuhofia ajenda kali ya mabadiliko chini ya Dr. Slaa ambayo inavutia watu wengi zaidi (popular agenda).

Kilichowashangaza zaidi CCM kwa mujibu wa ka'nzi ni jinsi ambavyo wasomi (mijini) na wananchi wa vijijini wanavyokubaliana katika kumkubali Dr. Slaa. Huko nyuma watawala walitegemea utengano kati ya makundi hayo mawili huku baadhi ya kundi la wasomi likiiunga mkono CCM. Wanachofurahia hata hivyo ambayo inawapa matumaini kidogo ni kuwa bado CCM ni chama kinachokubaliwa na kupendwea na baadhi ya wafanya biashara ambao wanaamini katika chini ya CCM maslahi yao yanalindwa.

yangu macho...
Ukwepaji kodi na biashara haramu zinalindwa
 
kutokana na hali halisi ni kweli dr slaa anakubalika na watanzania wengi ndio maana ccm wanahanya,lakini napata hofu sana juu ya uchakachuaji matokeo pamoja na wizi wa kura na mbinu nyingi walizozipznga mafisadi kuhakikisha kwamba wanarudi jamvini tena

wana jf tumwombe mungu uchaguzi uwe huru na wa haki maana sijui tanzania itakuwa vipi bila slaa
 
Magazeti, redio, Tvs, IT people, jeshi, tapeli Yahya, SMSs, zimeshindwa na hujuma zote ziendelee kushindwa na kulegea.. Dr. Slaa, Chadema, wanaopenda mabadiliko wote be lifted higher..! Thz time HATUDANGANYIKI..
 
Mungu yuko nyuma ya wanyonge,hakika mwaka huu ni vita kati ya mwanga na giza,uhadilifu na ufisadi.
 
mimi sina wasiwasi na hilo ila kama unavyowajua watanzania ni watu watulivu tusubiri kura itaamua hiyo tarehe 31 octoba 2010
 
Jana Mlimani TV walinikosha sana kwa kumuonyesha Mwalimu akizungumza na Waandishi wa Habari pale Kilimanjaro Hotel mwaka 1995. Ukiisikiliza hiyo hotuba yake ama kuisoma kwenye kijitabu kinachoitwa NYUFA kwa kweli utaamini kwamba Mzee yule alikuwa anaona mbali na alikuwa mtabiri wa kweli wa hatma ya Tanzania si kama yule mzee wa majini pale Magomeni Mikumi! Mwalimu alisema Tanzania imeanza kuwa na nyufa kwa kukiuka misingi mizuri iliyokuwa imewekwa huko nyuma. Alizungumzia hatari za rushwa, ukabila na udini. Akasema nchi inanuka rushwa, Watanzania ni vulnerable ukabila haujaisha upo chini tu ya ngozi zao kwa hiyo usipoendelea kudhibitiwa ukabila utarudi. Akawaomba Watanzania wasiendekeze udini maana vyote hivyo ni hatari kubwa kwa mustakabali wa nchi.

Mwalimu alizungumzia kwa kina kuhusu rushwa na jinsi inavyohitaji utashi na uongozi thabiti kushughulikia tatizo hilo. Akaeleza jinsi rushwa ilivyokuwa ikishughulikiwa kwa nguvu zote katika utawala wake. Wale waliokamatwa wakitoa ama kula rushwa walipelekwa mahakamani na walipohukumiwa Serikali ilikuwa imeishaweka adhabu ya kufungwa jela miaka 2 na kupigwa viboko 24! Mwalimu alitania kwamba hivyo viboko 12 mla rushwa/mtoa rushwa anapigwa anapoingia jela na 12 anapotoka jela akamuonyeshe mkewe! Akahadithia kwamba katika awamu yake aliwahi kukamatwa hata Mgiriki mmoja raia wa Cyprus corrupt mtoa rushwa ambaye alikuwa akitamba kwamba alikuwa ameiweka Serikali mfukoni. Alikamatwa, akapelekwa mahakamani, Akafungwa jela kama Watanzania wengine. Watu chungu nzima akiwemo Rais Kenyatta wa Kenya walijaribu kumuomba Mwalimu amuachie mgiriki yule, lakini Mwalimu akakataa kata-kata akisema mtu huyo ni mshenzi, alikuwa na mfuko mkubwa kiasi gani kuweza kuiweka Serikali yote mfukoni mwake?!! Hatimaye aliachiwa baada ya Askofu Mkuu Makarios wa Cyprus kutuma ujumbe kumuomba Mwalimu amsemehe mgiriki huyo. Mwalimu akakubali kwa masharti kwamba asionekane tena sio nchini tu bali Afrika Mashariki yote! Hivyo ndivyo rushwa ilivyokuwa ikishughulikiwa katika kipindi cha uongozi wa Mwalimu.

Sasa inavyoelekea Dr. Slaa ambaye ameonyesha dhahiri kuchukizwa na ufisadi ana mwelekeo wa kufuata nyayo za Mwalimu Nyerere katika kurekebisha makosa kadha wa kadha yaliyofanywa na utawala wa CCM yanayohatarisha sana mstakabali wa Taifa letu. Kwa sababu hiyo lazima CCM waogope kwa kuwa endapo Dr. Slaa atafanikiwa itakuwa ni mwanzo wa mwisho wa mafisadi nchini mwetu!
 
Wamejaribu kila aina za mbinu za kimafia ila wanashindwa na pia wataona kila kitu na kuna mabadiliko makubwa sana yanakuja sasa
 
WAO CCM NDIO WATAYALETA YA SUDAN, WAO NA TBC1 (kama ikikubali kuingia mkenge), wataleta ya Rwanda, wao ndio wanaotaka kuifanya Tanzania kuwa Somalia (maana wanao Wasomali wengi ndani yao).... CCM wao ndio wanataka kuleta machafuko na si yeyote yule..... Mungu ITABIRI TANZANIA MUNGU TULINDE WATOTO WA TANZANIA.

N.B. Kuna mtu anasema mtu anayesema mwenzake ni mgovi ndiye mgomvi mwenyewe. Mutamsikia ama kumsoma soon
 
Kikwete alisema kuwa hayuko tayari ccm impasukie mikononi mwake,hivyo aliamua kuzinyamazia kashfa za ufisadi ilimradi chama kisonge mbele.Pia alisema hayuko tayari muungano uvunjike chini yake hivyo akawa mpole kutoa msimamo wake hata pale baraza la wawakilishi lilipopitisha miswada inayotia shaka,ilimradi kuwaridhisha.Kwa sasa hivi hayuko tayari ccm ipoteze dola chini yake hivyo atafanya afanyalo ilimradi dola ibaki kwa ccm bila kujali kuwa kwa ahadi nyingi anazotoa anakuwa anaichimbia ccm kaburi kwani iwapo ataingia madarakani hawezi zitekeleza,hivyo hakuna mtu ataichagua ccm tena 2015 hata za kuiba hawatazipata.Lakini hofu kubwa ni ukweli usiopingika kuwa Dk Slaa akiingia madarakani hakuna aliyefisadi nchi atakaye pona,hiyo ni pamoja na yeye JK.Mbali na hilo wamestushwa kuona jinsi umma ulivyomkubali Dk. Slaa.
Kwa namna hiyo basi nguvu nyingi za aina tofauti zitatumika ilimradi abakie madarakani.
Afichaye ugonjwa, kifo kinamuumbua!
 
Jana Mlimani TV walinikosha sana kwa kumuonyesha Mwalimu akizungumza na Waandishi wa Habari pale Kilimanjaro Hotel mwaka 1995. Ukiisikiliza hiyo hotuba yake ama kuisoma kwenye kijitabu kinachoitwa NYUFA kwa kweli utaamini kwamba Mzee yule alikuwa anaona mbali na alikuwa mtabiri wa kweli wa hatma ya Tanzania si kama yule mzee wa majini pale Magomeni Mikumi! Mwalimu alisema Tanzania imeanza kuwa na nyufa kwa kukiuka misingi mizuri iliyokuwa imewekwa huko nyuma. Alizungumzia hatari za rushwa, ukabila na udini. Akasema nchi inanuka rushwa, Watanzania ni vulnerable ukabila haujaisha upo chini tu ya ngozi zao kwa hiyo usipoendelea kudhibitiwa ukabila utarudi. Akawaomba Watanzania wasiendekeze udini maana vyote hivyo ni hatari kubwa kwa mustakabali wa nchi.

Mwalimu alizungumzia kwa kina kuhusu rushwa na jinsi inavyohitaji utashi na uongozi thabiti kushughulikia tatizo hilo. Akaeleza jinsi rushwa ilivyokuwa ikishughulikiwa kwa nguvu zote katika utawala wake. Wale waliokamatwa wakitoa ama kula rushwa walipelekwa mahakamani na walipohukumiwa Serikali ilikuwa imeishaweka adhabu ya kufungwa jela miaka 2 na kupigwa viboko 24! Mwalimu alitania kwamba hivyo viboko 12 mla rushwa/mtoa rushwa anapigwa anapoingia jela na 12 anapotoka jela akamuonyeshe mkewe! Akahadithia kwamba katika awamu yake aliwahi kukamatwa hata Mgiriki mmoja raia wa Cyprus corrupt mtoa rushwa ambaye alikuwa akitamba kwamba alikuwa ameiweka Serikali mfukoni. Alikamatwa, akapelekwa mahakamani, Akafungwa jela kama Watanzania wengine. Watu chungu nzima akiwemo Rais Kenyatta wa Kenya walijaribu kumuomba Mwalimu amuachie mgiriki yule, lakini Mwalimu akakataa kata-kata akisema mtu huyo ni mshenzi, alikuwa na mfuko mkubwa kiasi gani kuweza kuiweka Serikali yote mfukoni mwake?!! Hatimaye aliachiwa baada ya Askofu Mkuu Makarios wa Cyprus kutuma ujumbe kumuomba Mwalimu amsemehe mgiriki huyo. Mwalimu akakubali kwa masharti kwamba asionekane tena sio nchini tu bali Afrika Mashariki yote! Hivyo ndivyo rushwa ilivyokuwa ikishughulikiwa katika kipindi cha uongozi wa Mwalimu.

Sasa inavyoelekea Dr. Slaa ambaye ameonyesha dhahiri kuchukizwa na ufisadi ana mwelekeo wa kufuata nyayo za Mwalimu Nyerere katika kurekebisha makosa kadha wa kadha yaliyofanywa na utawala wa CCM yanayohatarisha sana mstakabali wa Taifa letu. Kwa sababu hiyo lazima CCM waogope kwa kuwa endapo Dr. Slaa atafanikiwa itakuwa ni mwanzo wa mwisho wa mafisadi nchini mwetu!

Ndio nipo naitizam hapa kwa Desktop Hii DVD ya Hotuba ya Mwalimu na kujiuliza Mwl. Nyerere aliona mbali sana na anasikitika sana na hapati jibu kwanini Azimio la Arusha lilivunjika haoni jibu kabisa na haelewi wapi palikuwa na makosa.

Mwl.Nyerere aliona lama za nyakati na alijua Changes zinakuja na haziko mbali saana ila hawa viongozi walioachiwa madaraka walikuwa wanalao jambo tu rohoni na tokea mwalimu achukuliwe na Mungu basi tena watanzania wanamkumbuka sana hata kama alikuwa na mapungufu kwani nae alikuwa binadamu ila aliweka maslahi ya Nchi mbele kwa ajili ya wananchi anaye waongoza

MDAHALO MDAHALO MDAHALO PLEASE! CCM kugomea ni DHARAU kubwa kwa jamii yetu ya Tanzania, Yaani makamba anastahili viboko hadharani:A S 13:
 
Wadau, hizi habari nazotaka kusema ni za kweli kabisa. Katika mahojianao miezi michache iliyopita, Frederick Sumaye aliwahi kumwambia mwandishi mmoja wa habari in confidence (na alimuomba hiyo iwe off record, yaani asichapishe) kwamba laiti JK angejua Slaa atachukuwa fomu za kugombea urais, basi yeye (JK) angejifikiria mara mia naye kuchukua fomu, na pengine asingechukuwa kabisa.
Ushamuuza huyo mwandishi maana naamini Sumaye anamkumbuka ni nani aliyemhoji hapo private. lol
 
Wamejaribu kila aina za mbinu za kimafia ila wanashindwa na pia wataona kila kitu na kuna mabadiliko makubwa sana yanakuja sasa

Mbinu nyingine ni chafu kabisa kama hii ilivyoelezwa hapa chini niliyoinasa kwenye thread moja iliyoanzishwa mchana huu humu JF kabla ya kufutwa kwa haraka. Ni onyesho tosha ya kule tunakokwenda:

Idara ya usalama wa taifa na zoezi la uchakachuaji kura

Poleni na harakati za kuikomboa nchi yetu!

Leo napenda kuwajulisha mikakati michafu ya kupora na kuzuia maamuzi ya umma yanayofanywa na ccm kwa uratibu wa usalama wa taifa. Baada ya ku...baini dalili za kuanguka vibaya katika uchaguzi wa mwaka huu idara ya usalama wa taifa imeandaa mikakati ya kuiba kura ili kuzuia chadema msiingie ikulu. Mikakati hii inaeleweka vizuri kwa tume ya taifa ya uchaguzi ambayo inashirikiana bega kwa bega na idara ya usalama wa taifa kumtengenezea jk ushindi bandia wa 80%.

Wana hakika watanzania watagundua wizi huo na watakataa matokeo ndiyo maana kwanza waliwatumia viongozi wa dini waliotembelea makao makuu ya chadema wawasihi chadema wakubali matokeo yatakapotangazwa na juzi wamelitumia jeshi kutisha wananchi watakaoamua kupinga matokeo ya kupikwa yanayoandaliwa na nec/usalama wa taifa. Majid kikula ambaye ni government security officer ndiye mratibu wa zoezi la kuiba kura, ni mtaalamu aliyebobea katika kazi za aina hii aliratibu vizuri zoezi kama hilo mwaka 2005. Pia mwaka 2007 alitumwa kenya kwenda kumsaidia kibaki kupora ushindi wa odinga.

Kikula anatumia muda wake mwingi hivi sasa ofisi za tume ya uchaguzi kwa ajili ya uratibu wa uvurugaji daftari la kudumu la wapiga kura akiifanya kazi hiyo kwa karibu na baadhi ya watendaji wa nec na maafisa kadhaa wa usalama wa taifa kutoka kurugenzi ya IT ya idara ya usalama (DITA) ambao wako ndani ya nec kwa zaidi ya miezi sita sasa, nitawapatia majina yao. Pia kuna vijana wataalamu wa IT waliochukuliwa kutoka maeneo mbalimbali wamepewa nyumba upanga mtaa wa undali shughuli kubwa wanayofanya ni kuandaa utaratibu wa ku-access remotely daftari la kudumu la wapiga kura.

Hawa wanafanya kazi chini ya salva rweyemamu na mindi kasiga kutoka kurugenzi ya mawasiliano ikulu. Wapo vijana kadhaa leo nawapa majina ya wawili; maharage chande na edgar masatu wanafanya kazi kwa karibu na nzowa wa idara ya usalama ambaye ndiye aliyeratibu shambulio la kumwagiwa tindikali kubenea.

Pia kuna kundi linalojumuisha wataalamu wa printing wa kiwanda cha uchapaji cha usalama wa taifa kilichopo MALINDI ambao hivi karibuni walikuwa mjini tanga kwa semina fupi ya jinsi ya kughushi kura kupitia fake ballot paper, timu hii inaongozwa na ndg SINYAU.

Kwa hiyo utaona kwamba imeandaliwa mikakati mingi kuufanikisha uovu huo ili mmoja ukikwama basi mwingine utatumika ila wameamua ni lazima jk ashinde kwa 80%. Ndani ya idara ya usalama wa taifa maafisa wengi wamechoshwa na uongozi mbovu wa ccm hivyo wanataka mabadiliko ya uongozi idara imechukua hatua kadhaa kuhakikisha maafisa wote wa idara wanampigia kura jk, wote wameagizwa kuwasilisha vitambulisho vyao vya kupigia kura ili vinakiliwe namba ili atakayepigia upinzani afukuzwe kazi baada ya uchaguzi.

Fuatilieni kwa karibu haya niliyowaeleza nimeyapata kwa nafasi yangu ndani ya tiss. Huyu KIKULA mfuatilieni kwa karibu ni hatari.

HAKIKISHENI DUNIA NA WATANZANIA WOTE WANAJUA MAPEMA HILA HIZI. Jambo la kujiuliza maafisa usalama wa taifa wanafanya nini ndani ya tume ya uchaguzi wakati huu
 
Back
Top Bottom