Kiby
JF-Expert Member
- Nov 16, 2009
- 6,933
- 4,706
Ni kweli kabisa nchi zenye mwamko wa kimageuzi yanaanzia katika miji mikuu yake tafauti na Tz. Mi nafikiri kwa upande wa tanzania vilaza wengi wapo jijini Dar. Ukitaka kufahamu hayo ninayosema, jaribu kutembelea kwenye mikusanyiko mingi na hasa vijue mahali ambapo inafanyika mijadala mbali mbali. Utakuta pale kuna watu nadhafu sana hata wanaweza kukuogopesha kama unakawaida ya kutizama sura. Lakini ukisikiliza michango yao ndipo utakapogundua kua ni mizigo. Uvivu mwingi na uswahili umesababisha watu wengi jijini kutegemea ndugu zao kwa kila hali na hivyo wengi wa hawa vijana hawana kauli yao ila siku zote wanaiimba chorus ya kile anachoambiwa na mfazili wake. Anaweza kua ni mjomba, baba, dada, shangazi, mpwa nk. Ccm ni wataalamu wa kuchakachua na hivyo wamefanikiwa kupata bidhaa ya kuchakachua na siku zote mtu mvivu wa hata kazi za kujipatia kipato mwenyewe hana kauli. Atanunuliwa hata kwa sh. elfu mbili tu. Kwa mtizamo wangu pia Dar inawezakuwa na watu wengi wasiojua kusoma na kuandika kuliko mikoa mingine. Hivyo japokuwa ni kituvu cha vyanzo vya habari lakini uwingi wa habari zinazotolewa hawana habari nazo kama wale walio nje ya jiji. Kwa siasa za tanzania na uswahili wa mswahili tusitarajie mageuzi kuanzia katika miji ya mwambao. Yataanzia vijijini na kuja kuwaamsha hawa vilaza wa jijini. Hiyo ndio habari yenyewe.