Kwanini Dar siyo ngome kuu ya upinzani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Dar siyo ngome kuu ya upinzani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 16, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Karibu nchi zote duniani ambazo zimekuwa na mwamko wa kisiasa na upinzani uliokomaa zimefanya hivyo baada ya kuteka mji wake wake mkuu au mji mashuhuri. Ni katika miji mikubwa ya nchi ndipo upinzani umeonekana kukomaa

  Zambia - Lusaka
  Kenya - Nairobi
  Irani - Tehran
  Thailand - Bangkok
  Ukraine - Kiev
  Uingereza - London


  n.k

  Lakini kwa Tanzania, Dar-es-Salaam jiji kubwa zaidi, lenye watu wengi zaidi na lenye kufikiwa na vyombo vya habari vingi zaidi siyo ngome ya upinzani Tanzania. Zaidi ya watu kujitokeza kushangilia na kuonesha kukerwa na serikali ya chama tawala mara kwa mara ni hao hao watu wa Dar ndio wanaipa nguvu CCM na sitoshangaa (natumaini isiwe) upinzani unaweza usinyakue mbunge tena Dar.

  Ni kitu gani kinafanya Da isiwe ngome ya upinzani? Kwa mfano kushindwa kuchukua halmashauri hata moja, kushindwa kutoa mameya, madiwani wengi wakiwa bado ni CCM na wabunge bado ni CCM licha ya madudu yote. Na hasa ukizingatia kuwa Dar ndiyo yaweza kudaiwa kuwa ina wasomi wengi zaidi!!!!

  Yawezekana lawama ziiangukie CCM au pongezi kwa kuweza kuchakachua nguvu za upinzani Dar? Kwa sababu hata kwenye kura za maoni utaona wana CCM Dar wanaonekana kuchangamka zaidi kuliko wale wa upinzani. Au mimi siangalii vitu kwa usahihi maana hata CUF haina nguvu Dar mahali ambapo tungetarajia kuwa na nguvu ya aina fulani.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Daresalaam ndio jiji ambalo
  money talks kuliko kwingine....

  Mwisho wa siku watu huamua kumtumikia kafiri ili mambo yaende...........

  Na idadi kubwa ya wasiopiga kura wapo dar pia.......
   
 3. K

  KGM Senior Member

  #3
  Aug 16, 2010
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  DSM watu wengi wanaendesha maisha kwa "kuchakachua", na CCM ndio mabingwa kwa kuchakachua. Sasa wachakachuaji wanaogopa mageuzi. Khabari ndio hiyo.
   
 4. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Waganga njaa hawawezi kuleta mabadiliko zaidi ya kulalamika kwa sana
   
 5. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asilimia 70 ya wakaazi wa Dar ni wafuata upepo...kuna majuha wengi (per population) Dar kuliko mkoa wowote Tanzania..!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Aug 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo, tunaweza kutabiri vizuri kama ilivyotokea kwenye kura za maoni vijijini kuwa mwamko wa kisiasa kwa kweli uko vijijini kuliko mijini!? Angalia ni wapi wabunge wengi wa CCM wameanguka?
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Aug 16, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Kweli una hoja, mimi kwa uzooefu wangu nadhani haya yanachangia
  1. Wakazi wa Dar wakipato cha chini pengine na upungufu wa elimu huuza hata kura zao kwa 20,000 [mtumikie kafiri]
  2. Benki kuu na benki zote kubwa zipo hapa Dar, fikiria! hapa si Polisi wala wakala wa uchaguzi anaweza nunuliwa tu.
  3. Tume Nec,msajili wapo hapa, sasa watamuudhi mzee kweli! si unakumbuka 1995, boksi la kura kufika magomeni saa 9 mchana.
  4. Seriakli[ccm] kuvuruga, si unajua vyuo vikuu vimefungwa hadi baada ya uchaguzi, hii ni kuzuia Dar kutekwa na wasomi.
  5. Wapinzani wamekata tamaa, hawajiamini na hukimbilia maporini.
   
 8. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Aloo unapaswa kutuheshimu sisi wa miji mingine ha wa vijijini. Siyo uungwana kutuita watu wa porini. Sasa ninyi wa mjini mna faida gani kama mmelala usingizi wa pono. Tumia maneno ya staha bana.
   
 9. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  wakaazi wa asili wa dar ndio wapiga kura na wengi ni watu wanaokaa uswahilini na wenye kipato cha chini na rahisi kushawishika kwa rushwa
  ilhali watu wenye elimu na wenye mwamko wengi hawapigi kura kwani muda huo huwa wako kwenye biashara zao na mishemishe nyingine za mjini hata hivyo kufungwa kwa chuo kikuu cha dar na wanafunzi kurejea baada ya uchaguzi nako kunapunguza kura za ngome ya upinzani
   
 10. M

  Masonjo JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 2,725
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ukiona hivyo ujue kuwa muda wa Mama Tanzania kuzaa mabadiliko bado haujafika.

  Pindi majira na wakati utakapotimia upinzani wa dhati dhidi ya CCM utaanzia Dar es Salaam kuelekea pande zote za nchi.
   
 11. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,529
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  Dar-es-Salaam, Tanzania ni kama Bogota, Colombia
  Dar-es-Salaam, Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya ni miji iliyokumbwa na balaa la Mass Media (Vyombo vya Habari) kuwafanya wakazi wa miji hiyo ama kubweteka au kuogopa mabadiliko au huhadaiwa na halaiki inayojaa ktk mikutano ya vyama vya upinzani na kuamini kutakuwa hakuna rafu za kisiasa toka chama tawala. Mfano mzuri ni hii makala ya jinsi vyombo vya habari nchini Colombia vinavyofanya kazi wakati wa Uchaguzi na labda jibu kwa wanaotaka Dar wafanye nini ili iwe mikononi mwa wapinzani:

  Colombia's election and the media Colombia's election and the media - LISTENING POST - Al Jazeera English
  On The Listening Post this week, we look at the media's role in the Colombian election and The Washington Post's two-year investigation into what they call "Top Secret America".
  When a country votes for a new president there is usually an interesting media angle in it for us. That was certainly the case in the election of Colombia's Juan Manuel Santos. President Santos comes from a family that has a major say in what gets said in the Colombian media. There are two major news channels and two major newspapers in the country and the Santos family controls one of each.

  It almost seemed too convenient that unfavourable stories about opposition candidates started popping up in the country's media just before voters went to the polls. The election was also portrayed as a neck and neck race but after the ballots were counted we learned that it was anything but.

  So with all the speculation and misreporting that went on, critics now argue that the media was used as a pawn in a well planned election campaign. Our News Divide this week looks at some of the coverage in the lead up to the election and tries to assess whether or not there was a political agenda in the media.
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Aug 16, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Mheshimiwa Babuyao, nimelitumia neno kama msemo tu, sidhani Arusha,Mwanza au Mbeya ni porini.
  Lakini kwa vile limeleta utata, basi NAOMBA RADHI kwa wale waliokwaza kwani ndio uungwana.
  Ahsante
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwanza kabisa pengine nisikubaliane nawe kusema Dar siyo ngome ya upinzani. Unamaananisha wa chama kimoja? Au upinzani kwa ujumla? Kama ni wa chama kimoja nadhani ni sahihi usemavyo, lakini kama ni kwa ujumla, inawezekana Dar ni ngome ya upinzani. Kukubalika kwa sasa kwa Chadema na ufuasi mkubwa wa CUF (ambao sidhani kama umeyeyuka sana sasa hivi) nadhani kwa pamoja ni zaidi wa ule CCM.

  Kama kigezo ni uwingi wa watu katika mikutano ya vyama, basi weka katika hali kufirika endapo sasa hivi CUF na Chadema waitishe mkutano wa pamoja hapa Dar (Jangwani) na hasa iwapo (tena katika kufikirika) mgombea wa CUF, Prof Lipumba atangaze kabla kwamba katika mkutano huo atatangaza kujitoa na kumwachia Dr Slaa!

  Halafu linganisha uwingi wa watu wa mkutano wa CCM hapo hapo Jangwani endapo nao waitishe siku inayofuata!

  Kama itakumbukwa hali kama hii ilijitokeza katika mikutano ya kampeni ya CUF na CCM mwaka 2000 hapo hapo Jangwani. Ule wa CUF ulihudhuriwa na wingi wa watu kuliko wa CCM.

  Lakini mwaka 1995 wakati wa moto wa NCCR na Mrema, Dar hakika ilikuwa ngome ya upinzani na kuwapa hofu kubwa CCM – hasa katika matokeo ya kura ya urais kwani ilielekea kuwapo kwa run-off baina ya Mkapa na Mrema (wakati ule Katiba iliruhusu runoff iwapo mgombea hatapata asilimia 50 au zaid.

  Sote twajua kilichotokea. NEC (chini ya huyu huyu Makame) ilivuruga uchaguzi mkoa wa Dar kwa kile kilichoonekana kimakusudi tu. Bila maelezo ya kuridhisha, vifaa havikupelekwa vituoni kwa wakati wake, vituo vingine vilipelekwa mchana.

  Iliszemekana wakati ule Watu wapatao laki 9 walikuwa wamejiandikisha hapa Dar na iliaminika kwamba Mrema angezoa zaidi ya laki 6. Kuvurugwa kwa uchaguzi mkoa wa Dar (ambao baadaye uliahirishwa kwa wiki tatu hivi) kulilenga kuisaidia CCM kuondokana na uwezekano wa run-off kwani idea ilikuwa ni kutizama kwanza Mkapa ana-fare vipi kutokana na matokeo ya kura za urais mikoani.

  Kuahirishwa uchaguzi kuliiathiri sana NCCR kwani wapiga kura wengi walipandwa na hasira na kuchana shahada zao za kupigia kura – na NEC ilichelewa na pia haikupanga utaratibu mzuri wa watu kujiandikisha tena (wale walizozirarua shahada).

  Hali kadhalika mgogoro uliozuka baina ya viongozi wa juu wa NCCR kuhusu ushiriki au la wa marudio ya uchaguzi, na pia kutokana na kushindwa kwa kesi iliyopelekwa Mahakama Kuu iliyotaka kufuta uchaguzi nchi nzima na kurudia wote upya.

  Hivyo siku ya kupiga kura ilipofika, ni watu takriban laki nne na uchee ndiyo waliopiga kura. Ni dhahiri wafuasi wengi wa NCCR hawakupiga kura na hiyo iliwezesha
  CCM kuzoa majority of the votes na viti sita kati ya saba vya ubunge mkoani Dar.

  Kwa hiyo utaona kwamba ngome ya upinzani iko hapa Dar sema tu CCM ilianza kuifinya kwa mabavu tangu uchaguzi wa mwanzo.


   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Aug 16, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kumbe madai ya kwamba wananchi hawana elimu (ya uraia) ya kutosha ni bogus!! Maana wakazi wa Dar wana access na mambo mengi sana kuwafanya wawe sophisticated kuliko wale wa vijijini. Mweeeeee
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Aug 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  of course ni madai bogus.. kwa sababu tangu nikiwa kijijini kabisa nilikuwa nasikiliza bbc, DW, na VOA na kuja mengi yanayoendelea. Nadhani hao wakazi wa vijijini wana more balanced view ya siasa kuliko wa mjini kwa sababu wanapata habari from more independent media kuliko hizi za kwetu.
   
 16. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2010
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  dar hakuna ttizo , watu wengi wamesoma ama wamesafiri nje ya nchini kwa kiwango fulani wanaelewa ipi pumba na upimchele wapichori...kwa ufupi hakuna chama chengine chenye uwezo wa kuunda serikali pamoja na uwezo wa kuendesha serikali bila ya matatizo yoyote zaidi ya ccm.
  ukiangalia vyama vikuu vya upinzani CUF NA CHADEMA vyote vina nguvu sana wanakotoka vingozi wao...sio siri CUF inapendwa sana Zanzibar tu...haina zaidi ya Professor Lipumba kwa upande wa pili wa muungao...sio chama ambacho mwana Dar mwenye kuwamakini kukipa kura yake.lipumba peke yake hawezikuunda serikali hata kama walioko nje ya Dar wampe kura hauwezekani.....

  na CHADEMA nao wamejikita Uchagani zaidi. wanakotoka viongozi wao ..chadema haina zaidi ya Mboe na Padri Slaa.....haina anaekishabikia Zanzibar.....hawawezi kuunda serikali....kama watu wa nje ya DAr wampe kura zote basi maana yake ni mwisho wa muungano.....

  SASA UKWELI UTABAKI KUWA HAKUNA ZAIDI YA CCM ..WANA MATATIZO YAO..WAPO MAFISADI NDANI...YAKE LAKINI NI CHAMA KILICHOSHEHENI WASOMI NA WATAALAM KARIBU WOTE......KINA KILASABABU YA KUNDESHA NCHI NA KUSHINDA NA WANA DAR WANA SABABU YA KUKUSHABIKIA.......
  LABDA CHA KUJIULIZA NINI KIMEFANYA HALI HII HAPA TANZANIA ...TOFAUTI NA WENZETU?
  KWANZA KATIBA......
  • KATIBA HAITOI FURSA SAWA KWA VYAMA VYA SIASA.
  • TULITOKA KWENYE MFUMO WA CHAMA KIMOJA ..MFUMO AMBAO KILAMTU ALIKUA TANU NA BAADAE CCM.....
  • MFUMO ULOKUWEPO HAPA NI WA CCMKUSHIKA HATAMU....YAANI SERIKALI ILIFATA MAAMUZI YA CCM
  • WATU WOTE TULICHANGIA KUIMARISHA MFUMO HUUKWA MICHANGO MBALILI.
  • CCM IKAWA CHAMA CHENYE NGUVU SANA KULIKO HATA MANAGER WA MASHIRIKA YA UMMA WAKATI HUO
  • NA WAKATI MWALIMU ANANGATUKAKAZIKUBWA ALOFANYA NI KUZUNGUKANCHI NZIMA KATIKAMRADI WAKUIMAISHA CHAMA
  • ALIKUTANA NA VIONGOZI WA DINI ZOTE HASA WAKATOLIKI KUHUSU KUSHIKAMANA NA CCM WASIKIACHE
  • HIVYO SIO RAHISI VIONGOZI WA KIKATOLIKI KUICHA CCM KUSHABIKIA VYAMA VILIVOPO VYA UPINZANI
  • BAKWATA NAO PIA WAMEWEKWA SAWA....WAMO CCM
  KOSA KUBWA NI KUKUBALI KUINGIA KATIKA MFUMO HUU ULIOPO WA VYAMA VINGI WAKATI CCM NI KAMA JABALI NA WENGINE HAWANA UBAVU WA KUSHINDANA NACHO.
  MFUMO WA VYAMA VINGI HAUKUA NA NIA NZURI....UMELETWA KUHAKIKISHA UNAIBAKISHA CCM MADARAKANI KWA MUDA MREFU......
  DEMOCRSIA YA VYAMA VINGI INA FAIDA SANA KAMA UTAKUA KAMA WENZETU UNAVO WASAISIA KUENDESHA NCHI ZAO...TATIZO NI WAPINZANIA WENYEWE TANGIA MWANZO KUKUBALI KUSHINDANA NA JABALI BILA YA KUANGALIA MFUMO WENYEWE KAMA UNA MANUFAA AMA UNAWAFANYA KAMA WASINDIKIZAJI TU WA UCHAGUZI KILA UNAPOFIKA .

  NINI KILIKUA KIFANYIKE KABLA YA MFUMO HUU UANZE ? KITU AMBACHO KILIKUA KIFANYIKE ILI MFUMO WA SIASA UWE WA UWIANO NA WENYE KULETA FAIDA INAYOTOKANA NA DEMOCRASIA YA VYAMA VYINGI BASI ILIKUA NI KWA CCM KUKUBALI KUVUNJWA.....
  IUNDWE SERIKALI YA MPITO KUELEKEA VYAMA VINGI...
  BAADAE WATU WARUHUSIWE KUUNDWA VYAMA KWA MASHARTI MAGUMU YA KULAZIMISHA UONGOZI WA UWIANO WA KIMKOA KIDINI KATIKA UONGOZI NA WANACHAMA...

  SERIKALI YA MPITO INGEUNDA TUME HURU YA UCHAGUZI. KUSIMAMIA UCHAGUZI..
  HAPO TUNGEWEZA KUPATA SERIKALI YA KWELI YA VYAMA VINGI.....JABALI CCM INGEBAKI KATIKA HISTORIA KAMA CHAMA KILICHO PIGANIA UHURU, CHAMA KILICHO ONGOZA NCHI HII KWA AMANI TANGIA UHURU ,,,
  VIONGOZI WAKE MBALI MBALI WANGEBAKI KATIKA KUMBU KUMBU YA HISTORIA YA NCHI HII.
  OFISI ZAKE ZINGEFANYWA KUWA NI MUSEUM NA KUENZIWA NA SERIKALI YOYOTE ITAYOINGIA MADARAKANI.....
  HAPA TUNGEPATA VYAMA VINAVOTUMIKIA WANANCHI KWELI KWANI UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI NDIO UNGETUMIKA KUHAKIKISHA KUENDELEA KUCHAGULIWA.

  NA HILI CCM WANGEFANYA BASI NDIO NJIA PEKEE ITATYOFANYA HISTORIA YA NCHI KUTOPOTEA ..INGEKUBALI KUFA......LAKINI MFUMO WA SASA AMBAPO YENYEWE INASHINDANA NA VYAMA HIVI VIDUCHU WATAENDELEA KUSHINDA BILA YA TABU....NA BILA YA NCHI KUPATA FAIDA YA DEMOCRASIA YA VYAMA VINGI......LAKINI IKUMBUKE SIKU IKISHINDWA HISTORIA YA NCHI ITABADILIKA....NA CCM ITASAHAULIWA KAPA UNIP HUKO ZAMBIA NA KANU NCHINI KENYA........VYOITE HIVI NI VYAMA MUHIMU KATIKA HISTORIA YA NCHI ZAO LAKINI KOSA LAO NI KAMA HILI AMBALO CCM WAMEFANYA.....KUKUBALI MFUMO WA VYAMA VINGI KATIKA MAZINGIRA YA KUFANYA WAENDEEE KUWEPO...WANASAHAU KWAMBA WATANZANIA WENGI WALIKUA CCM.....
   
 17. M

  Masonjo JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 2,725
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135


  Kwa vigezo vyote Dar bado sio ngome ya upinzani ata ukiviunganisha vyama hivyo kwa pamoja.

  Kigezo cha idadi ya wananchi wanaohudhuria mikutano bila ya udhirikaji wa uungaji mkono wao kwenye sanduku la kura ni dhana ya kufikirika.
  Mfano halisi ni uwingi wa watu waliokuwa wakihudhuria mkutano wa Mbowe Jangwani na mitaa mbalimbali ya Jijini mwaka 2005 lakini akaishia kupata 5% tu ya kura za Mkoa wa Dar es Salaam.

  Lakini pia ukizingatia kuwa;

  (1) Wabunge wote 7 wa Dar es Salaam walitoka CCM na wote walishinda uchaguzi kwa zaidi ya 50%, hivyo ata ungejumlisha kura za wagombea wote wa upinzani zisingetosha.
  (2) Mgombea uraisi wa CCM 2005 alishinda kwa 71%.
  (3) CCM ina 91% ya viti vya serikali za mitaa mkoani DAr es Salaam ilivyoshinda kwenye uchaguzi wa mwaka jana.

  Japo nakubaliana na wewe kuhusu Dar es Salaam kuwahi kuwa ngome ya NCCR mwaka 95 kabla nuru haijazimika.
   
 18. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Umenena! Dar kuna wapinzani kweli kweli na wanapiga kura. Sikumbuki ni kipindi kipi matokeo ya hesabu za kura yametolewa Dar bila mikwara, ama kucheleweshwa au kulalamikiwa. CCM wanajua hilo na wanachunga sana Dar na ndio maana waliweza kumbeba Dr Lamwai (hivi ni kosa nikisema walimhonga) akakacha upinzania akahamia CCM
   
 19. M

  Mukubwa Senior Member

  #19
  Aug 17, 2010
  Joined: Aug 20, 2007
  Messages: 124
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  wakazi wengi wa dar hawaishi maisha halisia, hivyo hawaoni u muhimu wa kutumia haki zao za msingi na kuchagua viongozi watakao tetea maslahi ya taifa hili. Wakazi wa Dar wataamka pale watakapo lazimika kuishi maisha yao kulinga na kipato chao halisi ndipo upinzani utakapo pata nguvu maana watajua nini madhara ya kuwa na viongozi wabovu.
   
 20. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  muwawamko wa kisiasa uko zanzibar... watu wa Dar es salaam wanahitaji kuwaigiza watu wa zanzibar.
   
Loading...