Kwanini CCM Iko Matatani?

Kwanini CCM Iko Matatani?

Sasa kuna majibu ya haraka na ya pupa. Na yapo majibu yanayohitaji kutafakari kidogo. Kwa haraka mtu anaweza kusema kuwa CCM iko matatani kwa sababu CDM wanapandikiza mbegu ya chuki kwa wananchi. Mwingine (katika haraka yake) anaweza kuja na kusema CCM iko matatani kwa sababu wameshindwa kujivua "gamba". Mwingine naye katika kujaribu kuelezea kwanini CCM iko matatani anaweza kuja na kusema kwa sababu ndani yake kuna "migongano".

Naomba kupendekeza kwamba kuna jawabu la kina zaidi. Naamini vyote hivi tunavyoviona ni dalili tu ya tatizo (symptoms). Sasa kwa wale ambao mnaifahamu CCM labda tangu ikiwa TAA hadi leo hii mnaweza kutusaidia na kuwasaidia vijana wetu kuelewa kwanini CCM iko matatani leo hii? Kwanini inajitahidi kutumia nguvu sana kushinda uchaguzi wakati zamani ilikuwa rahisi sana. Kwanini kwa mfano mwaka 2005 ilifanya vizrui sana kuliko wakati mwingine wa vyama vingi na miaka mitano baadaye ikafanya vibaya kuliko wakati wowote wa historia yake?

Katika majibu yetu tujaribu kuleta yote bila kujali ukweli wake. Ieleweke siulizii majibu ya kisayansi; najaribu kufanya brain storming ambayo inaweza ikatuelewa kwanini hiki chama ambacho kiliwahi kuwa mashuhuri zaidi, kupendwa zaidi na hata kuhofiwa leo hii kinaonekana kigeni machoni pa watu?

kila zama huja na umashuhuri wake, na ni vigumu kuweza kumantaini umashauri huo. CCM pass the same way
 
Mzee MM,

Respect !

Nina mengi kichwani ila kwa kifupi niseme hivi:
Kwanza ni kweli Chama Cha Mapinduzi kiko matatani
Pili sababu hasa ni utambuzi wa watanzania kuainisha matatizo yetu na utawala (sii uongozi tena) ulipo madarakani.
Hapo awali wengi wetu tulidhani na kuamini matatizo na shida zetu ni mipango ya Mungu
Sasa tunajua kwamba ni utawala mbovu
Ni ufisadi
Ni ubinafsi na uchu uliopindukia
Ni ubabe na mazabe
Ni kiburi na makaburi ya wasio na hatia (watoto, mama wajawazito, wazee wa east african comunity nk)
Haya yoote tumeweza kuyaunganisha na utawala ulipo.

Hapo mtawala huyu lazima ashike viatu vyake mkononi, akunje suruali au kanzu tayari kwa kutimua mbio !!!!!
 
Una haki ya kutoa maoni lakini siyo kubuni maoni. Hoja yako imeshakuja na majibu hata kabla hujauliza swali. Labda ungeanza kwa kueleza kwanini unaona CCM ipo matatani.

Kwa mtazamo wangu naona chama kinchoongoza serikali ya Tanzania kinapita kwenye hali ya kawaida tu ambayo inaweza ikaikuta taasisi yoyote hasa yenye dhamana ya kuongoza kundi la watu, nchi nk.

Inakuwa rahisi sana kukosoa makosa ya CCM kuliko ya Chadema kwasababu ndicho kilichopo madarakani. Inatokea kwa Democrats ya Obama seuze CCM?

Nyani haoni kundule, hivyo nawe huoni *******.
 
Sasa kuna majibu ya haraka na ya pupa. Na yapo majibu yanayohitaji kutafakari kidogo. Kwa haraka mtu anaweza kusema kuwa CCM iko matatani kwa sababu CDM wanapandikiza mbegu ya chuki kwa wananchi. Mwingine (katika haraka yake) anaweza kuja na kusema CCM iko matatani kwa sababu wameshindwa kujivua "gamba". Mwingine naye katika kujaribu kuelezea kwanini CCM iko matatani anaweza kuja na kusema kwa sababu ndani yake kuna "migongano".

Naomba kupendekeza kwamba kuna jawabu la kina zaidi. Naamini vyote hivi tunavyoviona ni dalili tu ya tatizo (symptoms). Sasa kwa wale ambao mnaifahamu CCM labda tangu ikiwa TAA hadi leo hii mnaweza kutusaidia na kuwasaidia vijana wetu kuelewa kwanini CCM iko matatani leo hii? Kwanini inajitahidi kutumia nguvu sana kushinda uchaguzi wakati zamani ilikuwa rahisi sana. Kwanini kwa mfano mwaka 2005 ilifanya vizrui sana kuliko wakati mwingine wa vyama vingi na miaka mitano baadaye ikafanya vibaya kuliko wakati wowote wa historia yake?

Katika majibu yetu tujaribu kuleta yote bila kujali ukweli wake. Ieleweke siulizii majibu ya kisayansi; najaribu kufanya brain storming ambayo inaweza ikatuelewa kwanini hiki chama ambacho kiliwahi kuwa mashuhuri zaidi, kupendwa zaidi na hata kuhofiwa leo hii kinaonekana kigeni machoni pa watu?

Mkuu MMJ

CCM walisha poteza Dila toka KOLIMBA alipo waambia waka dharau na mzimu wake unawakula taratiiibu sana Mwl.Nyerere aliwaonya mambo mengi sana hawakuelewa nao mzimu wa mwalimu unawala pia,
Tatizo kubwa ni kuto kuwajibika kwa wananchi ndicho CCM kumewashinda kabisa na kuishi kutapatapa mara juu mara chini na hawana mipango imara ya future ya taifa hili bali ni wao CCM wananiona wao tu na sio Country First
 
Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.ccm waliokuwa wanaccm wameshazeeka na wengine wamekufa.kwa maana hiyo waliokufa wamekufa nayo na waliozeeka wamezeeka nao.ndo maana hata wale ambao wapo wanatumia siasa za mwaka 47.mia

Haipo matatani hata kidogo, wazee watakaa kando kuachia kundi la vijana wasomi linalojulikana kama CCM Republican Guards, Mpo hapo?
 
CCM kimekoma kuwa chama cha wafanyakazi na wakulima ila cha viongozi na matajiri(mafisadi) the ras. Angalia waliopo cc na nec.

Hivi unatarajia watu wenye akili wanaielewa ccm kumpigia magoti ra. Huku ni kukidhalilisha chama kupita maelezo.

Heri jimbo lichukuliwe na upinzani kuliko kujidhallsha na kulamba viatu vya ra. Kwanza wapinzani ni wtz.
Natarajia ccm hakitaendelea kujidhalilisha na kuwadhalilisha wtz. Ni vibaya. Vibaya sana. Tz kwanza, ra n coy baadaye.
 
Sasa kuna majibu ya haraka na ya pupa. Na yapo majibu yanayohitaji kutafakari kidogo. Kwa haraka mtu anaweza kusema kuwa CCM iko matatani kwa sababu CDM wanapandikiza mbegu ya chuki kwa wananchi. Mwingine (katika haraka yake) anaweza kuja na kusema CCM iko matatani kwa sababu wameshindwa kujivua "gamba". Mwingine naye katika kujaribu kuelezea kwanini CCM iko matatani anaweza kuja na kusema kwa sababu ndani yake kuna "migongano".

Naomba kupendekeza kwamba kuna jawabu la kina zaidi. Naamini vyote hivi tunavyoviona ni dalili tu ya tatizo (symptoms). Sasa kwa wale ambao mnaifahamu CCM labda tangu ikiwa TAA hadi leo hii mnaweza kutusaidia na kuwasaidia vijana wetu kuelewa kwanini CCM iko matatani leo hii? Kwanini inajitahidi kutumia nguvu sana kushinda uchaguzi wakati zamani ilikuwa rahisi sana. Kwanini kwa mfano mwaka 2005 ilifanya vizrui sana kuliko wakati mwingine wa vyama vingi na miaka mitano baadaye ikafanya vibaya kuliko wakati wowote wa historia yake?

Katika majibu yetu tujaribu kuleta yote bila kujali ukweli wake. Ieleweke siulizii majibu ya kisayansi; najaribu kufanya brain storming ambayo inaweza ikatuelewa kwanini hiki chama ambacho kiliwahi kuwa mashuhuri zaidi, kupendwa zaidi na hata kuhofiwa leo hii kinaonekana kigeni machoni pa watu?

Hapo penye Red nataka kuanzia.
watanzania walishapoteza imani yao kwa CCM toka mwaka 2005, lakini kikwete akairudisha imani iliyokuwa inapotea kwa ari, nguvu, na kasi mpya kwa kuahidi maisha bora kwa kila mtanzania. Huku taarifa ikipenyezwa kuwa Kikwete ni mpinzani ndani ya CCM. Watanzania wakamchagua kwa kwa kasi kubwa vivyo.
Viongozi wa dini hasa ya kikiristo wakatuambia kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu. Wapinzani wengi wakashawishiwa na viongozi wao, nao wakammwagia JK kura.

Pili, hoja ya ufisadi.
Kuibuliwa kwa msamiati mpya wa ufisadi 2007 na kuwataja hadharani viongozi wa juu kabisa wa serikali na ccm ilizidi kuwafanya watanzania kuichukia ccm huku ikiambatana na ugumu wa maisha ya watanzania ktk kipindi cha Mkapa na hasa kikwete kunazidi kuidhoofisha CCM.

Usanii wa Kikwete pia umechangia kuibomoa ccm kwa kuasisi mtandao ambao ameshindwa kuuvunja na sasa umeleta soko moko kubwa sana ndani ya ccm. Mbaya yeye mwenyewe hana ujasiri wa kukemea chochote ndani ya chama. Anaendesha chama kwa staili ya auto pilot.

Mwisho, Kuongezeka kwa vyombo vya habari vyenye uhuru wa kutoa maoni hata zile habari zinazoumbua ccm na za kweli kumechangia kuibomoa ccm. Hapa ninazunguzia social media zote haswa JF bila kusahau simu za mikononi.

Bila shaka nakubaliana na hoja ulizotaja mwenyewe na wachangiaji wengine pia.

Sasa kuna majibu ya haraka na ya pupa. Na yapo majibu yanayohitaji kutafakari kidogo. Kwa haraka mtu anaweza kusema kuwa CCM iko matatani kwa sababu CDM wanapandikiza mbegu ya chuki kwa wananchi. Mwingine (katika haraka yake) anaweza kuja na kusema CCM iko matatani kwa sababu wameshindwa kujivua "gamba". Mwingine naye katika kujaribu kuelezea kwanini CCM iko matatani anaweza kuja na kusema kwa sababu ndani yake kuna "migongano".

Naomba kupendekeza kwamba kuna jawabu la kina zaidi. Naamini vyote hivi tunavyoviona ni dalili tu ya tatizo (symptoms). Sasa kwa wale ambao mnaifahamu CCM labda tangu ikiwa TAA hadi leo hii mnaweza kutusaidia na kuwasaidia vijana wetu kuelewa kwanini CCM iko matatani leo hii? Kwanini inajitahidi kutumia nguvu sana kushinda uchaguzi wakati zamani ilikuwa rahisi sana. Kwanini kwa mfano mwaka 2005 ilifanya vizrui sana kuliko wakati mwingine wa vyama vingi na miaka mitano baadaye ikafanya vibaya kuliko wakati wowote wa historia yake?

Katika majibu yetu tujaribu kuleta yote bila kujali ukweli wake. Ieleweke siulizii majibu ya kisayansi; najaribu kufanya brain storming ambayo inaweza ikatuelewa kwanini hiki chama ambacho kiliwahi kuwa mashuhuri zaidi, kupendwa zaidi na hata kuhofiwa leo hii kinaonekana kigeni machoni pa watu?

Wangemsikiliza Marehemu Horace Kolimba ambaye aliongea miaka ya mwanzoni mwa tisini kuwa CCM imepoteza mwelekeo wasingekuwa hapa walipo sasa. Badala ya kusikiliza ujumbe waliamua kumshughulikia mjumbe na hawakuchukua muda kutafakari alichosema. Kimsingi chanzo cha hizi dalili za wao kutumia nguvu nyingi kushinda uchaguzi hicho alichoongea Kolimba.
 
Ufahamu wa watu pia umekuwa mkubwa, mathalani vyombo vya habari na mitandao kama hii imesaidia sana kuwapasha habari wananchi na wameweza kujua uozo wanaofanya viongozi wao hasa wa CCM. Ikumbukwe watu wengi hasa wa vijijini walikuwa hawajuia kwamba pesa zinazoibwa mfano EPA ni mali yao ila walikuwa wanajua hizo ni pesa za serikali so ilikuwa haiwasumbi sana ila now wanajua na wanafahamu kumbe CCM ndo chanzo cha matatizo yote na wao wananchi ndiyo mabosi wanakiweka kiwatawale.....so wameamua!

"Emancipate yourself from mental slavery none but ourselves can free our mind" Robert Nesta Marley
 
Mzee MM,

Respect !

Nina mengi kichwani ila kwa kifupi niseme hivi:
Kwanza ni kweli Chama Cha Mapinduzi kiko matatani
Pili sababu hasa ni utambuzi wa watanzania kuainisha matatizo yetu na utawala (sii uongozi tena) ulipo madarakani.
Hapo awali wengi wetu tulidhani na kuamini matatizo na shida zetu ni mipango ya Mungu
Sasa tunajua kwamba ni utawala mbovu
Ni ufisadi
Ni ubinafsi na uchu uliopindukia
Ni ubabe na mazabe
Ni kiburi na makaburi ya wasio na hatia (watoto, mama wajawazito, wazee wa east african comunity nk)
Haya yoote tumeweza kuyaunganisha na utawala ulipo.

Hapo mtawala huyu lazima ashike viatu vyake mkononi, akunje suruali au kanzu tayari kwa kutimua mbio !!!!!

jibu la swali ni hapo kwenye rangi ya chama chetu ccm..
 
ni kwa sababu ya kuuliwa na ahadi zake yenyewe zisizotekelezeka, jamaa kaaidi meli kumi na vivuko 10 wakati moja yenyewe mbinde,
 
CCM kuwepo matatani naichukulia in the context of the fourth wave of political changes in Africa. The third wave ya miaka ya 1990s ilikuwa dominated na demokrasia ya vyama vingi pamoja na free press, opposition parties, civil society, etc. Watu wengi walidhani kuwepo tuu kwa vyama vingi kunge improve maisha yao. Unfortunately that did not happen.

Lakini impact kubwa ya wave ya tatu kwenye miaka ya 2000s is that the African population became engaged in the changes. They now read about it, they listen to the radio, they watch it on the TV and more importantly they discuss it without any fear vijiweni, mitaani, saloon, makazini, kwenye bar and in the ever growing social media. Lakini kitu kikubwa ambacho nadhani kinaiweka katika hali ngumu sio tuu CCM bali pia vyama vikongwe vya kisiasa barani Afrika ni wananchi kuanza ku-connect dots kati ya ufisadi, rushwa, utawala mbaya na maisha yao ya kila siku.

Kwa mfano, wakati Watanzania walipoletewa bili ya umeme Januari 2008 kulikuwa na ongezeko la asilimia 30. Ongezeko hili halikuwa kwa sababu ya matumizi makubwa ya umeme bali kwa vile umeme haukuwepo. Wakati serikali "iliponunua" genereta toka Richmond ilikopa dola milioni 179 za kimarekani toka benki. The generator was never delivered and the power problem was never solved na gharama za umeme zinaendelea kupanda japokuwa umeme wenyewe hauonekani (https://www.jamiiforums.com/habari-...kwa-bei-ya-umeme-ni-kiama-kwa-watanzania.html).

Mpaka leo watu hawana umeme wa maana kitu ambacho kimechangia kwa kiasi kikubwa kupanda kwa gharama za maisha ya kila siku. Japokuwa ni asilimia ndogo sana ya Watanzania wanatumia umeme lakini ukosefu wa umeme umefanya kwa njia moja au nyingine maisha yao kuwa magumu. Huu ni mfano mdogo tuu. Mengi tumeyasikia na kuyasoma.

Suddenly, sasa Watanzania wanagundua kuwa kuna uhusiano mkubwa sana kati ya usifisadi, rushwa, bad governance na maisha yao ya kila siku. Nafikiri kitendo cha mwananchi wa kawaida kugundua the existence of a strong connection between corruption, bad governance and his/her everyday life ndiyo kinachoiweka CCM katika hali iliyopo sasa. The people of Tanzania are automatically now monitoring the government under CCM on its ability to do something about the corruption which so literally is destroying the development of their country which in practice is not poor. Kadri muda unavyokwenda CCM inaonyesha kama vile haijanotice na ku-address connection inayofanywa na wananchi kati ya ufisadi/rushwa/bad governance na maisha yao ya kila siku. And this is not doing CCM any favour.
 
Kimsingi CCM hawakujipanga kukabiliana na mfumo mpya wa vyama vingi na mfumo mzima wa kibepari ambao haukuwa umezoeleka. Tukumbuke miaka ya 1995 wafanyabiashara wengi walijikita upinzani by then NCCR mageuzi ikapata support zaidi, baada ya uchaguzi kuwawia vigumu CCM na kumpata mkapa kama Rais mpya walianza kuwapa adhabu wafanyabiashara waliounga mkono upinzani. ili kulinda maslahi wafanyabiashara hawa wakalamba miguu ya ccm wakarudi kwa kasi na kutosa upinzani ambao haukuwa na nguvu kifedha. kisha kuidhamini ccm katika chaguzi zilizofuata na hapo CCM ikawa imefunga rasmi ndoa na wafanyabiashara. ikumbukwe wafanyabiashara hawa wakiwa na maslahi yao kibiashara waligundua wamepata mteremko wa kupitishia mauzauza yao na kunufaika kibiashara kwa kuipa CCm nguvu ya kifedha. in short CCM ilipoteza uelekeo kwa kuwekeza kisiasa chini ya wafanyabiashara badala ya wananchi wa tabaka la kati na la chini ambao ndio wengi. hii imekua kansa ka CCM kwani hawawezi kuninasua tena zaidi ya kusubiri siku ya anguko kuu
 
Mbona umekwisha taja wewe Mzee Mwanakijiji? Kama waliweza kusoma alama za nyakati mapema na kujivua gamba wakabadilika kutoka TAA na kuwa TANU, then kabla wananchi hawajaishtukia wakavua tena gamba na kuwa CCM, na sasa wamejisahau kuvua gamba hadi wmeshtukiwa na bado kuvua gamba hilo limeshindikana....! Je, wadhani kwanini wasiwe matatani? Kabla wao hajajitangaza kuwa ni joka kijani, sisi tulishawashtukia....!
 
Kimsingi CCM hawakujipanga kukabiliana na mfumo mpya wa vyama vingi na mfumo mzima wa kibepari ambao haukuwa umezoeleka. Tukumbuke miaka ya 1995 wafanyabiashara wengi walijikita upinzani by then NCCR mageuzi ikapata support zaidi, baada ya uchaguzi kuwawia vigumu CCM na kumpata mkapa kama Rais mpya walianza kuwapa adhabu wafanyabiashara waliounga mkono upinzani. ili kulinda maslahi wafanyabiashara hawa wakalamba miguu ya ccm wakarudi kwa kasi na kutosa upinzani ambao haukuwa na nguvu kifedha. kisha kuidhamini ccm katika chaguzi zilizofuata na hapo CCM ikawa imefunga rasmi ndoa na wafanyabiashara. ikumbukwe wafanyabiashara hawa wakiwa na maslahi yao kibiashara waligundua wamepata mteremko wa kupitishia mauzauza yao na kunufaika kibiashara kwa kuipa CCm nguvu ya kifedha. in short CCM ilipoteza uelekeo kwa kuwekeza kisiasa chini ya wafanyabiashara badala ya wananchi wa tabaka la kati na la chini ambao ndio wengi. hii imekua kansa ka CCM kwani hawawezi kujinasua tena zaidi ya kusubiri siku ya anguko kuu
 
Naomba nijibu hivi CCM sio kila mtu anapenda kuliwa au sio kila mtu anapenda kula. Sasa wale wanaoona kuwa wanatumika ndio wanaamka wakati ni too late. Katika kufanya maamuzi amua ukijua kuna vizazi vingine sio kana kwamba wewe ndio kizazi cha mwisho. majibu ndio haya sasa
 
Pamoja na kuweka maoni yetu sanaa kwa jf naomba kila mwenye unchungu na nchi hii na umaskini na awe mbele kumweleza na mwenzie uso kwa uso ubaya wa kutawaliwa na CCM...Tumewachoka na si lazima watutawale.....Hatuweka kiapo cha kutawaliwa na CCM ...People..sssss powerrrrrrr..
 
CCM iko matatani kwasababu imeacha misingi yake mikuu "Chama cha kupigania na kutetea wanyonge WAKULIMA na WAFANYAKAZI".CCM kiliacha kwa muda mrefu kutetea maslahi ya wanyonge amabo ni wakulima na wafanyakazi.

Watanzania zaidi ya asilimia 80 ni wakulima wadogo wadogo wanaishi vijijini sera na mipango mingi ya CCM ya wakati wa Nyerere ililenga kuwakwamua wakulima kiuchumi.Vyama vya ushirika vilinunua mazao ya wakulima na kuwahakikishia bei nzuri wakulima.viwanda vya pamba vilianzishwa na kuwahakikishia wakulima soko la uhakika.Watanzania wengi walioshika madaraka makubwa ya kisiasa na kiserekali walisomeshwa kwa fedha za kahawa,pamba,korosho,katani na nk.

Wafanyakazi wa mijini wengi waliajiriwa serekalini na mashirika ya umma eg Urafiki,Kilitex,Bora,General Tyre,Mwatex,Tabotex na nk.Ajira ndani ya mashirika ya umma ilikuwa ya uhakika zaidi ulikilinganisha na hizi ajira za akina Jandu or Sunflug.Ajira za wafanyakazi zililindwa na kuheshimiwa sana.Mfanyakazi wa kitanzania alitembea kifua mbele.

Kundi la wakulima na wafanyakazi limewekwa kando ndani ya mfumo mpya wa CCM.Wafanyabiashara wezi na wabadhirifu wa mali ya umma wameshika hatamu za uongozi wa CCM mfanyakazi na mkulima hawana chao ndani ya CCM ya sasa.Kiini cha matatizo ya CCM ni kuacha misingi yake ya kuwatetea wakulima na wafanyakazi.

Wakulima na wafanyakzi wako taabani.Mkulina hana uhakika wa soko la mazao yake
wafanyabisaha wanawalalia wakulima hakuna wa kuwalinda.Mazao mengi mfano matunda yanaoza mashambani serekali imeacha uekezaji wa viwanda kwa wawekezaji uchwara.

Wafanyakazi hawana uhakika wa ajira zao walizoea ajira za mashirika ya umma bahati ajira siku hizi zimehamishiwa kwa wawekezaji [wageni] ambao hawajali maslahi ya wafanyakazi wanachoangalia ni faida tu.Ajira mpya ni chache sana ikilinganisha na ongezeko la watu serekali haitaki kuwekeza kwenye viwanda inawekeza kwenye uzalishaji wa mikoa mipyaa eti kusogeza huduma karibu na wananchi.
 
Back
Top Bottom